Gundua › Mada › Desturi za maombolezo
Maisha ya kila siku
Desturi za maombolezo katika Biblia
Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (55), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.
- Kurarua mavazi kwa habari mbayaMwa 37:29, Mwa 37:34, Mwa 44:13, 2 Sam 1:11, 2 Sam 13:31, Ayu 1:20, 2 Fal 2:12
Aya
Mwa 37:29Rubeni akarudi kwenye shimo, na, tazama, Yusufu hakuwemo shimoni. Akararua mavazi yake.
Mwa 37:34Yakobo akararua mavazi yake na kuvaa mavazi ya magunia katika viuno vyake. Akaomboleza kwa ajili ya mwanawe siku nyingi.
Mwa 44:13Wakararua mavazi yao. Kila mtu akapakia juu ya punda wake nao wakarudi mjini.
2 Sam 1:11Kisha Daudi akararua mavazi yake, na watu wote waliokuwa pamoja naye wakafanya vilevile.
2 Sam 13:31Kisha mfalme akainuka na kurarua mavazi yake na kujilaza juu ya sakafu; watumishi wake wote wakasimama karibu naye mavazi yao yameraruriwa.
Ayu 1:20Kisha Ayubu akainuka, akalirarua joho lake, akanyoa kichwa chake, akaanguka chini kifudifudi na kumwabudu Mungu.
2 Fal 2:12Elisha akaiona akalia kwa sauti, “Baba yangu, baba yangu, gari la kukokotwa na farasi la Israeli na waendesha farasi!'” Hakumwona Eliya tena, na akashikilia nguo zake mwenyewe na kugawanya kwenye vipande viwili.
- Gunia kiunoniMwa 37:34, 1 Fal 21:27, Est 4:1
Aya
Mwa 37:34Yakobo akararua mavazi yake na kuvaa mavazi ya magunia katika viuno vyake. Akaomboleza kwa ajili ya mwanawe siku nyingi.
1 Fal 21:27Ahabu aliposikis maneno haya, Akachana mavazi yake na akavaa magunia kwenye mwili wake na akfaunga, na akalala kwenye magunia na akahuzunika sana.
Est 4:1Modeka aliposikia kilichokuwa kimepangwa dhidi yao, alirarua mavazi yake na kuvaa maguni na majivu. Akaenda katikati mwa mji na kulia kwa sauti na uchungu mwingi.
- Mavumbi au majivu kichwaniYos 7:6, 2 Sam 13:19, 2 Sam 15:32, Ayu 2:12
Aya
Yos 7:6Basi Yoshua alizirarua nguo zake. Yeye pamoja na wazewe wa Israeli waliweka mavumbi juu ya vichwa vyao na wakainamisha vichwa vyao hadi katika nchi mbele ya sanduku la Yahweh, na walibaki pale mpaka jioni.
2 Sam 13:19Tamari akaweka majivu juu ya kichwa chake na akalirarua vazi lake
2 Sam 15:32Ikawa Daudi alipofika juu njiani mahala Mungu alipokuwa akiabudiwa, Hushai Mwarki akaja kumlaki vazi lake limeraruliwa na mavumbi kichwani pake.
Ayu 2:12Walipoinua macho yao wakiwa mbali, hawakuweza kumtambua. Wakapaza sauti zao na kulia; kila mmoja wao akararua joho lake na kurusha majivu hewani na juu ya kichwa chake.
- Kulala katika gunia na majivuEst 4:3, Yon 3:6
Aya
Est 4:3Amri hii ilipofika katika kila jimbo, kulikuwa na kilio kikubwa kwa Wayahudi, na kufunga, kulia na maombolezo. Wengi wao walilala katika magunia na majivu.
Yon 3:6Mapema habari zilimfikia mfalme wa Ninawi. Akasimama kutoka kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akajivika magunia, akaketi katika majivu.
- Kulala chini ardhini2 Sam 12:16, 2 Sam 13:31
Aya
2 Sam 12:16Kisha Daudi akamwomba Mungu kwa ajili ya kijana. Daudi akafunga naye akaingia ndani na kulala usiku wote juu ya sakafu.
2 Sam 13:31Kisha mfalme akainuka na kurarua mavazi yake na kujilaza juu ya sakafu; watumishi wake wote wakasimama karibu naye mavazi yao yameraruriwa.
- Kichwa kimefunikwa na miguu mitupu2 Sam 15:30
Aya
2 Sam 15:30Lakini Daudi akaenda bila viatu huku akilia hata Mlima wa Mizeituni, naye alikuwa amefunika kichwa chake. Kila mtu miongoni mwao waliokuwa pamoja naye akafunika kichwa chake, nao wakaenda huku wakilia.
- Kufunika uso2 Sam 19:4, Est 6:12
Aya
2 Sam 19:4Mfalme akafunika uso wake na kulia kwa sauti, “Mwanangu Absalomu, Absalomu, mwanangu, mwangangu!”
Est 6:12Baada ya hayo Modekai alirudi kwenye lango la mfalme. Huku Hamani akarudi kwa haraka nyumbani kwake, huku akiomboleza, na akiwa ameinamisha kichwa chake.
- Kung’oa nywele za kichwa na ndevuEzr 9:3
Aya
Ezr 9:3Niliposikia haya, nikachana nguo zangu na kanzu na kunyoa nywele kichwani na ndevu na nikakaa chini kutafakari.
- Kunyoa kichwaAyu 1:20, Eze 27:31
- Kuvua mapamboKut 33:4–6
Aya
Kut 33:4–6Watu walipo sikia haya maneno ya kushtua, walilia, na hakuna aliye vaa mikufu. Yahweh alisema kwa Musa, “Waambie Waisraeli, 'Ninyi ni watu wakorofi. Kama ningeenda miongoni mwenu ata kwa muda kidogo, nigewaharibu ninyi. Hivyo sasa, toa mikufu yenu ili niamue nini cha kufanya kwenu.”' Hivyo Waisraeli hawaku vaa mikufu kutoka Mlima Horebu na kwendelea.
- Bila kujipaka mafuta, na mavazi ya maombolezo2 Sam 14:2, Dan 10:3
Aya
2 Sam 14:2Hivyo Yoabu akatuma neno huko Tekoa kumleta kwake mwanamke mwelevu. Akamwambia, “Tafadhari, vaa mavazi ya uombolezaji ujifanye kuwa mwombolezaji. Usijipake mafuta, lakini uwe kama mwanamke ambaye ameomboleza kwa muda mrefu kwa ajili yake aliyekufa.
Dan 10:3Sikula chakula kizuri, sikula nyama, sikunywa divai, na sikujipaka mafuta mwenyewe mpaka ukamilifu wa wiki tatu nzima.
- Waombolezaji hutembea njianiMhu 12:5
Aya
Mhu 12:5Utakuwa wakati ambapo watu wataogopa vilivyoinuka na hatari iliyoko barabarani, na wakati ambapo mlozi utachanua maua, na wakati panzi watakapokokotana wenyewe, na wakati ambapo hamu za asili zitakaposhindwa. Kisha mtu aenda katika nyumba yake ya milele na waombolezaji watelemka mitaani.
- Wanawake stadi wa kuomboleza waliitwa kuliaYer 9:17–18
Aya
Yer 9:17–18BWANA wa majeshi asema hivi, “Yafikirini haya: Waiteni waliaji; waje. Tumeni wanawake wenye taaluma ya kuomboleza, waje. Waje haraka waimbe wimbo wa maombolezo juu yetu, ili macho yetu yatokwe na machozi na kope zetu zibubujikwe na maji.
- Wapiga filimbi na umati wenye kelele nyumbani kwa msichana aliyekufaMt 9:23
Aya
Mt 9:23Na Yesu alipofika kwenye nyumba ya afisa, naye aliwaona wapiga tarumbeta na umati wa watu ulikuwa ukipiga kelele.
- Marafiki wanakuja kuifariji familiaYn 11:19, Yn 11:31
Katika Sheria
- Usijikate mwili wala kunyoa paji la uso kwa ajili ya mfuLaw 19:28, Kum 14:1
- Kugusa maiti kulimfanya mtu najisi siku sabaHesabu 19:11, Hesabu 19:16
Aya
Hesabu 19:11Yeyote atakayegusa maiti ya mtu atakuwa najisi kwa siku saba.
Hesabu 19:16Vivyo hivyo, kwa mtu aliye nje ya hema ambaye atamgusa mtu aliyeuawa kwa upanga, au mzoga wowote, au mfupa wa mtu, au kaburi—mtu huyo atakuwa najisi kwa siku saba.
- Makuhani wanaweza kujitia unajisi kwa ndugu wa karibu tuLaw 21:1–3
Aya
Law 21:1–3Yahweh akamwambia Musa, “Zungumza na makuhani, wana wa Aroni, nawe waambie, 'hakuna hata mmoja miongoni mwenu atakayejitia unajisi kwa wale wanaokufa miongoni mwa watu wake, isipokuwa yule aliye ndugu wa karibu—mama yake, baba yake, mwanawe, bintiye, nduguye, au dada yake bikira anayemtegemea, kwa kuwa hana mume—kwake huyo anaweza kujitia unajisi.
- Kuhani mkuu hapaswi kurarua mavazi yake wala kukaribia maitiLaw 21:10–11
Aya
Law 21:10–11Mtu ambaye ni kuhani mkuu miongoni mwa nduguze, ambaye mafuta ya upako yamekwisha kumiminwa kichwani pake, na ambaye amekwisha kuwekwa wakfu ili kuvaa mavazi maalum ya kuhani mkuu, kamwe hataziacha wazi nywele zake wala hatazirarua nguo zake. Hataingia kamwe mahali popote ambapo kuna maiti na kujitia unajisi, hata kama ni maiti ya baba yake au ya mama yake.
- Haruni na wanawe hawapaswi kuwaombolezea Nadabu na AbihuLaw 10:6
Aya
Law 10:6Msiache wazi nywele za vichwa vyenu, wala msirarue nguo zenu, ili kwamba msije mkafa, na kwamba Yahweh asilikasirikie kusanyiko zima. Lakini waacheni jamaa zenu, nyumba yote ya Israeli waweze kufanya ibada za maombolezo kwa ajili ya hao ambao Yahweh amewaangamiza kwa moto.
- Hakuna chochote cha zaka kilicholiwa wakati wa maombolezoKum 26:14
Aya
Kum 26:14Sijala kati yao wakati wa maombolezo yangu, wala sijaziweka mahali pengine nilipokuwa mchafu, wala sijazitoa kati yao kwa heshima ya wafu. Nimesikiliza sauti ya Yahwe Mungu wangu; Nimetii kila kitu ulichoniamuru kukifanya.
Mifano
- Abraham anamwombolezea na kumlilia SaraMwa 23:2
Aya
Mwa 23:2Sara akafa katika Kiriathi Arba, ambayo ni Hebroni, katika nchi ya Kanaani. Abraham akaomboleza na kumlilia Sara.
- Yakobo anakataa kufarijiwa kwa ajili ya YusufuMwa 37:34–35
Aya
Mwa 37:34–35Yakobo akararua mavazi yake na kuvaa mavazi ya magunia katika viuno vyake. Akaomboleza kwa ajili ya mwanawe siku nyingi. Wanawe na binti zake wote wakainuka na kumfariji, lakini alikataa kufarijiwa. Akasema, “Hakika nitashuka kuzimu nikimwombolezea mwanangu.” Babaye akamlilia.
- Misri wanamwombolezea Yakobo siku sabini; Yusufu anaomboleza siku saba huko AtadiMwa 50:3, Mwa 50:10–11
Aya
Mwa 50:3Wakatimiza siku arobain, kwani huo ndio uliokuwa muda kamili wa kutia dawa. Wamisri wakamlilia kwa siku sabini
Mwa 50:10–11Hata walipokuja katika sakafu ya kupuria ya Atadi upande mwingine wa Yordani, wakaomboleza kwa majonzi ya huzuni kubwa. Yusufu akafanya maombolezo ya siku saba kwa ajili ya babaye pale. Wenyeji wa nchi, Wakanaani, walipoona maombolezo katika sakafu ya Atadi, wakasema, “Hili ni tukio la kuhuzunisha sana kwa Wamisri.” Ndiyo maana eneo hilo likaitwa Abeli Mizraimu, lililoko mbele ya Yordani.
- Israeli wanamwombolezea Haruni siku thelathini, na Musa thelathiniHesabu 20:28–29, Kum 34:8
Aya
Hesabu 20:28–29Musa akamvulisha Haruni yale mavazi ya kikuhani na kumvalisha Mwanaye Eliazari. Haruni akafa pale juu ya Mlima Hori. Kisha Musa na Eliazari wakashuka. Watu walipoona kuwa Haruni amekufa, taifa lote wakamlilia Haruni kwa siku arobaini.
Kum 34:8Watu wa Israeli walimuomboleza Musa katika nyanda za Moabu kwa siku thelathini, hapo ndipo siku za maombolezo ya Musa zilipotimia.
- Kilio kikubwa Misri: hakuna nyumba isiyo na mfuKut 12:30
Aya
Kut 12:30Farao akaamka usiku - yeye, watumishi wake, na Wamisri. Palikuwa na kelele za maombolezo Misri, kwa kuwa hakukuwa na nyumba ambayo hamna mtu hakufa.
- Daudi na watu wake wanalia mpaka wanaishiwa nguvu1 Sam 30:4
Aya
1 Sam 30:4Ndipo Daudi na watu aliokuwa nao wakapaza sauti zao na kulia hadi walipokuwa hawana nguvu zaidi za kulia.
- Maombolezo ya Daudi kwa Sauli na Yonathani: “Jinsi mashujaa walivyoanguka!”2 Sam 1:17–19
Aya
2 Sam 1:17–19Ndipo Daudi akaimba wimbo wa maombolezo juu ya Sauli na Yonathani mwanawe. Akawaamuru watu kuufundisha wimbo wa Bow kwa wana wa Yuda, ambao umeandikwa katika Kitabu cha Yashari. “Utukufu wako, Israel, umeondolewa, umeondolewa juu ya mahali pako pa juu! Jinsi mwenye nguvu alivyoanguka!
- Maombolezo ya Daudi kwa Abneri2 Sam 3:33–34
Aya
2 Sam 3:33–34Mfalme akamwombolea Abneri naye akaimbo, “Je ilipasa Abneri afe kama afavyo mpumbavu? Mikono yako haikufungwa. Miguu yako hakuwa imefungwa minyororo. Kama mtu aangukavyo mbele ya wana wa uovu, ndivyo ulivyoanguka.” Watu wote wakamlilia zaidi.
- “Ee mwanangu Absalomu! Mwanangu, mwanangu!”2 Sam 18:33, 2 Sam 19:4
Aya
2 Sam 18:33Ndipo mfalme alipohuzunishwa sana naye akaenda chumbani juu ya lango na kulia. Kadili alivyokwenda aliomboleza, mwanangu Absalomu, mwanangu, mwanangu Absalomu! afadhari ningekufa badala yako, Absalomu, mwanangu, mwanangu!”
2 Sam 19:4Mfalme akafunika uso wake na kulia kwa sauti, “Mwanangu Absalomu, Absalomu, mwanangu, mwangangu!”
- Bathsheba anamwombolezea Uria2 Sam 11:26–27
Aya
2 Sam 11:26–27Hivyo mke Uria aliposikia kwamba mme wake amekufa, akaomboleza sana kwa ajili yake. Huzuni yake ilipoisha, Daudi akatuma na kumchukua kwake katika kasri lake, naye akawa mkewe na akamzalia mwana. Lakini alichokifanya Daudi hakikumpendeza Yahwe.
- Waimbaji wanaume na wanawake wanaimba maombolezo kwa Yosia2 Nya 35:24–25
Aya
2 Nya 35:24–25Kwa hiyo watumishi wake wakamtoa nje ya gari, na kumuweka katika gari lake la tahadhari. Wakampeleka Yerusalemu, ambako alikufa. Alzikwa katika makaburi ya babu zake. Yuda wote na Yerusalemu wakamwomboleza. Yeremia akamwomboleza Yosia; waimbaji wote wa kiume na wa kike wakaomboleza kuhusu Yosia hata leo. Nyimbo hizi zikawa desturi katika Israeli; tazama, zimeandikwa katika nyimbo za maombolezo.
- Mordekai analia katika gunia; gunia halikuruhusiwa langoni pa mfalmeEst 4:1–2
Aya
Est 4:1–2Modeka aliposikia kilichokuwa kimepangwa dhidi yao, alirarua mavazi yake na kuvaa maguni na majivu. Akaenda katikati mwa mji na kulia kwa sauti na uchungu mwingi. Akaenda hadi langoni mwa mfalme; kwa sababu hakuna aliye ruhusiwa kuingia akiwa amevaa magunia.
Vyanzo
Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0