Maisha ya kila siku
Chakula katika Biblia
Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (38), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.
Watu walikula nini
- Maziwa ya mbuzi kwa ajili ya nyumbaMit 27:27
Aya
Mit 27:27Kutakuwa na maziwa ya mbuzi kwa chakula chako- chakula kwa kaya yako- na chakula kwa watumishi wako wasichana.
- Siagi, maziwa, mafuta ya wana-kondoo na ngano boraKum 32:14
Aya
Kum 32:14Alikula siagi kutoka katika kundi na kunywa maziwa kutoka katika kundi la mifugo, pamoja na mafuta ya wanakondoo, kondoo dume wa Bashani na mbuzi, pamoja na ngano safi kabisa – nawe ulikunywa divai itokayo povu iliyotengenezwa kwa juisi ya mizabibu.
- Vipande kumi vya jibini kwa jemadari wa jeshi1 Sam 17:17–18
Aya
1 Sam 17:17–18Kisha Yese akamwambia mwanawe Daudi, “Wapelekee kaka zako efa ya bisi na hii mikate kumi, na uzipeleke upesi kule kambini kwa ajili ya kaka zako. Pia peleka hizi jibini kumi kwa jemedari wa kikosi chao cha elfu. Ukawaangalie wako na hali gani kisha uniletee habari kuhusu wanavyoendelea vizuri.
- Ngano, shayiri, maharagwe, dengu, asali na jibini kwa watu wa Daudi2 Sam 17:28–29
Aya
2 Sam 17:28–29wakaleta magodoro na mabulangeti, mabakuri na vyungu, na ngano, unga wa shayiri, nafaka zilizokaangwa, maharage, dengu, asali, siagi, kondoo na samli, ili kwamba Daudi na watu waliokuwa pamoja naye waweze kula. Kwani walisema, “Watu wana njaa, wamechoka na wana kiu huko nyikani.”
- Abraham anaandaa mkate, ndama mwororo, siagi na maziwaMwa 18:5–8
Aya
Mwa 18:5–8Nami acha nilete chakula kidogo, ili kwamba mjiburudishe wenyewe. Ndipo baadae mwaweza kwenda zenu, kwa kuwa mmekuja kwa mtumishi wenu.” Nao wakasema, “Fanya kama ulivyo sema.” Kisha Abraham akaenda upesi hemani kwa Sara, na akasema, “Harakisha, chukua vipimo vitatu vya unga safi, uukande, na fanya mkate.” Kisha Abraham akakimbia kundini, akachukua ndama wa ng'ombe aliye laini na mzuri, na akampatia mtumishi na kwa haraka akamwandaa. Akatwaa siagi na maziwa na ndama aliye kwisha andaliwa, na akaweka chakula mbele yao, naye akasimama karibu nao chini ya mti wakati wanakula.
- Ruth anachovya mkate katika siki na kula bisiRut 2:14
Aya
Rut 2:14Wakati wa chakula Boazi alimwambia Ruth, “Njoo hapa, ule baadhi ya mikate, na uchovye kipande katika divai.” Alikaa kando ya wavunaji, na Boazi akampatia kiasi cha nafaka zilizo kaangwa. Ruth alikula mpaka alipotosheka na kusaza.
- Mkate, andazi la tende na andazi la zabibu kwa kila mmoja2 Sam 6:19
Aya
2 Sam 6:19Kisha akawagawia watu wote, umati wote wa Israeli, wanaume kwa wanawake, kipande cha mkate, nyama na keki ya zabibu. Kisha watu wote wakaondoka; kila mmoja akarudi kwake.
- Abigaili analeta mikate, divai, kondoo, zabibu kavu na mikate ya tini1 Sam 25:18
Aya
1 Sam 25:18Ndipo Abigaili akaharakisha na akachukuwa mikate mia mbili, chupa mbili za divai, kondoo watano waliokwisha andaliwa, vipimo vitano vya bisi, vishada mia moja vya zabibu, na mikate mia mbili ya tini na akavipakia juu ya punda.
- Siba anamletea Daudi mkate, zabibu kavu na matunda ya kiangazi2 Sam 16:1–2
Aya
2 Sam 16:1–2Daudi alipokuwa amekwenda kitambo juu ya kilele cha kilima, Siba mtumishi wa Mefiboshethi akaja kumlaki akiwa na punda wawili waliokuwa wamebeba vipande mia mbili vya mikate, vishada mia moja vya mizeituni, vishada mia moja vya tini na mfuko wa ngozi uliojaa mvinyo. Mfalme akamuliza Siba, “Kwa nini umeleta hivi vitu?” Siba akajibu, “punda ni kwa ajili ya familia yako kupanda, mikate na matunda ni kwa ajili ya matumizi ya askari wako, na mvinyo ni kwa ajili kunywa watakaozimia nyikani.”
- Mmisri mwenye njaa anapata nguvu kwa mkate wa tini na zabibu kavu1 Sam 30:11–12
Aya
1 Sam 30:11–12Nao walimkuta Mmisri shambani na wakamleta kwa Daudi; wakampatia mkate, na akala; wakampa maji ya kunywa; kisha walimpa kipande cha keki ya tini na vishada viwili vya zabibu. Alipomaliza kula, akapata nguvu tena, kwa kuwa alikuwa hajala mkate wala kunywa maji, siku tatu mchana na usiku.
- Samaki, matango, matikiti, mboga, vitunguu na vitunguu saumu huko MisriHesabu 11:5
Aya
Hesabu 11:5Tunakumbuka samaki tulizokula bure kule Misri, yale matango, na matikiti maji, na mboga na vitunguu na vitunguu saumu.
- Mkate na mchuzi wa denguMwa 25:34
Aya
Mwa 25:34Yakobo akampatia Esau mkate pamoja na mchuzi wa dengu. Akala na kunywa, kisha akainuka na akaenda zake. Kwa njia hii Esau akawa ameidharau haki yake ya mzaliwa wa kwanza.
- Manna ilikuwa na ladha ya maandazi yaliyopikwa kwa asaliKut 16:31
Aya
Kut 16:31Watu wa Israeli walikiita chakula kile “manna.” Ilikuwa ni nyeupe kama mbegu ya mgiligani, na ladha yake kama maandazi yaliyo pikwa na asali.
- Nafaka iliyochomwa ya nchi; kisha manna ikakomaYos 5:11–12
Aya
Yos 5:11–12Na siku iliyofuata baada ya Pasaka, walikula sehemu ya mazao ya nchi, mikate isiyotiwa chachu na nafaka iliyokaangwa katika siku hiyo iyo. Mana zilikoma siku ile walipokula mazao ya nchi. Hapakuwa tena na mana kwa watu wa Israeli, bali walikula mazao ya nchi ya Kanaani mwaka huo.
- Mkate wa ngano, shayiri, maharagwe, dengu, mtama na kusemethiEze 4:9
Aya
Eze 4:9Chukua ngano kwa ajili yako, shayiri, dengu, mtama, kusemethi; viweke kwenye chombo kimoja na tengeneza mkate kwa ajili yako kulingana na hesabu ya siku ambazo utakazo lala katika ya upande wako. Kwa siku 390 utaula.
- Danieli anaomba mboga za majani na maji tuDan 1:12
Aya
Dan 1:12Alisema, “Tafadhari tujaribuni, sisi watumishi wako kwa siku kumi. Tupatieni tu mboga mboga za kula na maji ya kunywa.
- Kunguru wanamletea Eliya mkate na nyama asubuhi na jioni1 Fal 17:6
Aya
1 Fal 17:6Nao kunguru wakamletea mkate na nyama asubuhi, na mkate na nyama jioni, naye akanywa maji ya kijito kile.
- Yohana Mbatizaji alikula nzige na asali ya mwituniMt 3:4
Aya
Mt 3:4Sasa Yohana alivaa manyoya ya ngamia na mkanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni.
- Afadhali mlo wa mboga pamoja na upendo kuliko ng’ombe aliyenonaMit 15:17
Aya
Mit 15:17Bora mlo wenye mboga kukiwa na upendo kuliko kuandaliwa ndama aliyenona kwa chuki.
- Mwana anaomba mkate au samakiMt 7:9–10
Aya
Mt 7:9–10Au kuna mtu miongoni mwenu ambaye, ikiwa mtoto wake amemwomba kipande cha mkate atampa jiwe? Au ikiwa atamwomba samaki, na yeye atampa nyoka?
- Samaki na mkate juu ya moto wa makaa kando ya ziwaYn 21:9
Aya
Yn 21:9Walipofika ufukweni, waliona moto wa mkaa pale na juu yake kulikuwa na samaki pamoja na mkate.
- Yesu aliyefufuka anakula kipande cha samaki wa kuchomaLk 24:42
Aya
Lk 24:42Wakampa kipande cha samaki aliyechomwa.
Mezani
- Rebeka anaandaa chakula kitamu cha wana-mbuzi wawiliMwa 27:9
Aya
Mwa 27:9Nenda kundini, na uniletee wanambuzi wawili; nami nitaandaa chakula kitamu kutokana nao kwa ajili ya baba yako, kwa namna aipendayo.
- Wanawake walifanya kazi ya kupika na kuoka mikate1 Sam 8:13, Mit 31:15
Aya
1 Sam 8:13Naye atawachukua binti zenu kuwa watengeneza manukato, wapishi, na waoka mikate.
Mit 31:15Huamka wakati wa usiku na kuwapa chakula watu wa kaya yake, na kugawa kazi kwa watumishi wake wa kike.
- Wamisri hawakula pamoja na WaebraniaMwa 43:32
Aya
Mwa 43:32Watumishi wakamhudumia Yusufu peke yake na wale ndugu peke yao. Wamisri pale wakala pamoja naye peke yao kwa sababu Wamisri hawakuweza kula mkate na Waebrania, kwani hilo ni chukizo kwa Wamisri.
- Shukrani zilitolewa kabla ya kuumega mkateMk 8:6, Lk 24:30, Mdo 27:35
Aya
Mk 8:6Aliuamuru umati ukae chini. Akachukua mikate saba, akamshukuru Mungu, na kuivunja. Akawapa wanafunzi wake waiweke mbele yao, nao wakaiweka mbele ya umati.
Lk 24:30Ilitokea kwamba, wakati amekaa nao kula, alichukua mkate, akaubariki, na kuuvunja, akawapa.
Mdo 27:35Alipokwisha kusema hayo, akachukua mkate akamshukuru Mungu mbele ya macho ya kila mtu. Kisha akaumega mkate akaanza kula.
- Wimbo uliimbwa baada ya Karamu ya MwishoMt 26:30
Aya
Mt 26:30Walipokuwa wamemaliza kuimba wimbo, walitoka kwenda Mlima wa Mizeituni.
Vyakula vilivyokatazwa
- Wanyama wa nchi kavu: wale tu wenye kwato zilizogawanyika wanaocheuaLaw 11:3–4
Aya
Law 11:3–4Mnaweza kula mnyama yeyote aliye na kwato zenye kugawanyika na ambaye pia hucheua. Hata hivyo, kuna baadhi ya wanyama ambao ama hawacheui au hana kwato zilizogawanyika, nanyi msiwale hao, wanyama kama ngamia, kwa sababu yeye hucheua lakini hana kwato zilizogawanyika. Kwa hiyo ngamia ni najisi kwenu.
- Viumbe wa majini: wale tu wenye mapezi na magambaLaw 11:9–10
Aya
Law 11:9–10Nao wanyama waishio majini mnaoweza kuwala ni wale wote walio na mapezi na magamba, iwe waliomo baharini au mitoni. Lakini viumbe wote hai wasio na mapezi na magamba waliomo baharini au mitoni, pamoja na wale waendao majini na viumbe hai waliomo majini —watakuwa chukizo kwenu.
- Tai, vipungu na ndege wengine waliotajwa wasiliweLaw 11:13
Aya
Law 11:13Nao ndege mtakaowachukia na msiopaswa kuwala ni hawa wafuatao: tai, furukombe, kipungu,
- Nzige, senene, parare na panzi wanaweza kuliwaLaw 11:21–22
Aya
Law 11:21–22Lakini manaweza kula wadudu wenye mabawa wanaotembea kwa miguu minne ya kurukia ardhini yenye vifundo. Na manaweza kula kula aina zote za nzige, senene, parare, au panzi.
- Damu inamwagwa na kufunikwa kwa udongoLaw 17:13–14
Aya
Law 17:13–14Na yeyote miongoni mwa watu wa Israeli, au yeyote wa Wageni aishiye miongoni mwenu ni lazima aimwage damu ya mnyama na kuifukia hiyo damu kwa mafumbi. Kwa kuwa uhai wa kila kiumbe umo katika damu yake. Ni kwa sababu hii niliwaambia watu wa Israeli, ni lazima msile damu ya kiumbe cho chote, kwa kuwa maisha ya kila kiumbe chenye uhai ni damu yake. Yeyeote ailaye ni lazima akatiliwe mbali.
- Hakuna nyama ya mnyama aliyeraruliwa na wanyama mashambaniKut 22:31
Aya
Kut 22:31Mtakuwa watu walio tengwa kwa ajili yangu. Hivyo hamtakula nyama iliyo uliwa na wanyama porini. Badala yake, uwatupie mbwa.
- Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yakeKut 23:19, Kum 14:21
Aya
Kut 23:19Lazima ulete matunda ya kwanza bora kutoka shambani mwako ndani ya nyumba yangu, nyumba ya Yahweh Mungu wako. Haupaswi kumchemsha mbuzi mtoto akiwa bado ananyonya.
Kum 14:21Hampaswi kula chochote kinachokufa chenyewe; mnaweza kumpa mgeni ambaye yuko katika mji wenu, kwamba anaweza kula au mnaweza kuuza kwa mgeni. Kwa kuwa mu taifa lilolowekwa wakfu kwa ajili ya Yahwe Mungu wenu. Hampaswi kumchemusha mbuzi kijana katika maziwa ya mama yake.
Vyanzo
Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0