Bible Explorer

Gundua › Mada › Kilimo

Maisha ya kila siku

Kilimo katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (37), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

  • Mtu anawekwa Edeni ili kuilima na kuitunzaMwa 2:15
    Aya
    Mwa 2:15Yahwe Mungu alimtwaa mtu na kumweka ndani ya bustani ya Edeni kuilima na kuitunza.
  • Kaini ni mkulima wa ardhi; Habili anachunga kondooMwa 4:2
    Aya
    Mwa 4:2Kisha akazaa ndugu yake Habili. Sasa Habili akawa mchungaji, lakini Kaini alilima udongo.
  • Nuhu, mtu wa ardhi, anapanda shamba la mizabibuMwa 9:20
    Aya
    Mwa 9:20Nuhu akaanza kuwa mkulima, na akapanda mizabibu.
  • Isaka anapanda na kuvuna mara mia mwaka huoMwa 26:12
    Aya
    Mwa 26:12Isaka akapanda mazao katika nchi hiyo na kuvuna mwaka huo vipimo mia, kwa kuwa Yahwe alimbariki.
  • Ruth anaokota nyuma ya wavunaji: karibu efa moja ya shayiriRut 2:2–3, Rut 2:17
    Aya
    Rut 2:2–3Ruth, Mmoabu, alimwambia Naomi, “Ngoja niende nikakusanye mabaki ya chakula katika shamba. Nitamfuata yeyote ambaye nitapata kibali machoni pake.” Hivyo naomi akamwambia, “Nenda, mwanangu.” Ruth alienda kuvuna kwenye shamba akiwafuata kwa nyuma wavunaji. Na kumbe ile sehemu ya shamba ilikuwa ni mali ya Boazi, aliyekuwa na mahusiano na Elimeleki.
    Rut 2:17Kwa hiyo alivuna mpaka jioni. Kisha akatenganisha nafaka na majani ambayo amevuna, nazo nafaka zilikuwa kama efa moja ya shairi.
  • Boazi anapepeta shayiri usiku katika uwanja wa kupuriaRut 3:2
    Aya
    Rut 3:2Naye Boazi, mtu ambaye umekuwa pamoja na wasichana wake wa kazi, yeye si jamaa yetu? Tazama, jioni hii atakuwa akikung'uta shairi katika sakafu ya kupuria.
  • Gideoni anapura ngano katika shinikizo la divai ili kuificha MidianiAmu 6:11
    Aya
    Amu 6:11Basi malaika wa Bwana akaja na kukaa chini ya mwaloni huko Ofra, uliokuwa wa Yoashi (Mwabiyezeri), wakati Gidioni, mwana wa Yoashi, akitenganisha ngano katika sakafu, katika kikapu cha divai-kuificha toka kwa Wamidiani.
  • Watu wa Beth Shemeshi wanavuna ngano bondeni1 Sam 6:13
    Aya
    1 Sam 6:13Nao watu wa Beth Shemeshi walikuwa wakivuna ngano yao katika bonde. Waliponyanyua macho yao juu na kuliona sanduku, wakafurahi.
  • Waisraeli wanakwenda kwa Wafilisti kunoa majembe na mundu1 Sam 13:19–21
    Aya
    1 Sam 13:19–21Hakuna hata mhunzi aliyeonekana katika nchi yote ya Israeli, kwa sababu Wafilisti walisema, “ Waebrania wasije wakajitengenezea mapanga au mikuki.” Lakini Waisraeli wote huwa wakiteremka kwa Wafilisti, kila mtu kunoa jembe lake, sululu yake, shoka lake na mundu wake. Gharama za kunoa ncha za majembe, sululu, mashoka na kunyoosha michokoo ilikuwa theluthi moja ya shekeli.
  • Elisha analima kwa jozi kumi na mbili za ng’ombe1 Fal 19:19
    Aya
    1 Fal 19:19Kwa hiyo Eliya akaondoka mahali pale na akamkuta Elisha mwana wa Shafati, akilima na jozi za makisai kumi na mbili mbele yake, na yeye mwenyewe alikuwa akilima na ile jozi ya kumi na mbili. Eliya akaenda mpaka kwa Elisha akamtupia vazi lake juu yake.
  • Maafisa wa Daudi juu ya mashamba, mizabibu, mizeituni na makundi1 Nya 27:26–31
    Aya
    1 Nya 27:26–31Ezri mwana wa Kelubi alikuwa juu ya mashamba, hao walio lima ardhi. Shimei kutoka Rama alikuwa juu ya mashamba ya mizabibu, na Zabdi kutoka Shefamu alikuwa juu ya mizabibu na mhifadhi wa mvinyo. Mwangalizi wa miti mizeituni na miti ya mikuyu iliyo kuwa bondeni alikuwa Baali Hanani kutoka Gederi, na juu ya nyumba za ghala za mafuta alikuwa Yoashi. Juu ya mifugo iliyo kuwa inalishwa huko Sharoni alikuwa Shitrai kutoka Sharoni, na juu ya mifugo iliyo kuwa mabondeni alikuwa Shafati mwana wa Adlai. Msimamizi wa ngamia alikuwa Obili Mishimaeli, na juu ya punda wakike alikuwa Yehideia kutoka Meronothi. Juu ya mifugo alikuwa Yazizi Mhagri. Hawa wote walikuwa wasimamizi wa mali za Mfalme Daudi.
  • Uzia, mpenda ardhi, ana wakulima na watunza mizabibu2 Nya 26:10
    Aya
    2 Nya 26:10Akajenga minara ya ulinzi katika nyika na akachimba mabwawa, kwa maana alikuwa na ng'ombe wengi, katika visiwa vya chini na katika nchi tambarare. Alikuwa na wakulima na wapandaji wa zabibu katika mwinuko wa nchi na katika mashamba yenye rutuba, kwa maana alipenda kulima.
  • Sulemani anapanda mashamba ya mizabibu na bustani na kujenga mabwawaMhu 2:4–6
    Aya
    Mhu 2:4–6Nilitimiza mambo makubwa. Nilijenga nyumba kwa ajili yangu na kupanda miti ya mizabibu. Nilitengeneza bustani na viwanja; nikapanda aina zote za matunda ndani yake. Nikatengeneza mabwawa ya maji ili kumwagilia msitu mahali miti ilikuwa imepandwa.
  • Kulima, kupanda kwa mistari, na kupura kila zao kwa njia yakeIsa 28:24–28
    Aya
    Isa 28:24–28Je mkulima anayelima siku zote kwa ajili ya kupanda, analima tu kwenye aridhi? Je anaendelea kulima shamba lake pasipo kupanda? Pindi anapolindaa shamba lake, Je hatawanji jira ya mbegu, anapanda jira, anaweka ngano katika mstari, shairi katika mahali pake, na yameandikw sehemu mbili? Mungu wake amemuelekeza; anamfuundisha yeye kwa busara. Zaidi ya hayo, jira zile hazipuruliwi kwa chombo kikali; wala gurudumu la kukatia linalozunguka juu ya jira; lakini jira linapigwa kwa fimbo, na jira kwa fimbo. Nafaka ni mwanzo mkate lakini ni laini sana, japo gurudumu la gari lake na farasi wamezitawanya, na farasi wake hawajaiponda ponda.
  • Mkulima anangoja mvua za vuli na za masikaYak 5:7
    Aya
    Yak 5:7Kwa hiyo vumilieni, ndugu, mpaka ujio wa Bwana, kama mkulima husubiri mavuno ya thamani toka katika nchi, akisubiri kwa uvumilivu kwa ajili yake, mpaka mvua za kwanza na zile za mwisho zikinyesha.
  • Wanafunzi wanachuma masuke wakipita mashambaniMt 12:1
    Aya
    Mt 12:1Wakati huo Yesu alienda siku ya sabato kupitia mashambani. Wanafunzi wake walikuwa na njaa na wakaanza kuyavunja masuke na kuyala.
  • Mbegu njiani, mwambani, kati ya miiba, katika udongo mzuri (mfano)Mt 13:3–8
    Aya
    Mt 13:3–8Kisha Yesu alisema maneno mengi kwa mifano, Alisema, “Tazama, mpanzi alienda kupanda. Alipokuwa akipanda baadhi ya mbegu zilianguka kando ya njia na ndege walikuja wakazidonoa. Mbegu zingine zilianguka juu ya mwamba, ambapo hazikupata udongo wa kutosha. Ghafla zilichipuka kwa sababu udongo haukuwa na kina. Lakini jua lilipo chomoza zilichomwa kwa sababu hazikuwa na mizizi, na zilikauka. Mbengu zingine zilianguka kati ya miti yenye miiba. Miti yenye miiba ilirefuka juu ikaisonga. Mbegu zingine zilianguka kwenye udongo mzuri na kuzaa mbegu, zingine mara mia moja zaidi, zingine sitini na zingine thelathini
  • Wafanyakazi walioajiriwa shambani mwa mizabibu kwa dinari moja kwa siku (mfano)Mt 20:1–2
    Aya
    Mt 20:1–2Kwa maana ufalme wa mbinguni unafanana na mmliki wa shamba, aliyeamka asubuhi na mapema ili kuajiri wafanyakazi katika shamba lake la mizabibu. Baada ya kuwa amekubaliana na wafanyakazi dinari moja kwa kutwa, aliwatuma kwenda katika shamba lake la mizabibu.

Katika Sheria

  • Panda miaka sita; mwaka wa saba nchi inapumzikaKut 23:10–11, Law 25:3–5
    Aya
    Kut 23:10–11Kwa miaka sita utapanda mbegu kwenye nchi yako na kukusanya mazao yake. Lakini katika mwezi wa saba utaacha hakujalimwa, ili kwamba maskini miongoni mwenu wale. Wanacho acha, wanyama wa porini watakula. Utafanya hivyo na mashamba yenu ya mizabibu na ya mizaituni.
    Law 25:3–5Ni lazima mtapanda mazao yenu kwa miaka sita, na kwa miaka sita mtaikatia matawi mizabibu yenu na kukusanya mazao yake. Lakini katika mwaka wa saba, Sabato ya pumziko la utulivu kwa nchi itashikwa, ni Sabato kwa Yahweh. Hamtapanda mashamba yenu wala kuikatia mizabibu yenu matawi yake. Hamtasimamia mavuno yoyote ya mazao ya mizabibu iliyojiotesha yenyewe katika mashamba yenu ya mizabibu isiyokatiwa matawi. Huu utakuwa mwaka wa pumziko lenye utulivu kwa ardhi.
  • Pumzika siku ya saba, hata wakati wa kulima na kuvunaKut 34:21
    Aya
    Kut 34:21Utafanya kazi kwa siku sita, lakini siku ya saba utapumzika. Ata wakati wakilimo na wa mavuno, lazima upumzike.
  • Acha pembe za shamba na zabibu zilizoanguka kwa ajili ya maskiniLaw 19:9–10
    Aya
    Law 19:9–10Unapovuna mavuno ya ardhi yako, usivune hata pembezo mwa shamba lako kabisa, wala hutakusanya mabaki ya mavuno yako yote. Usikusanye kila zabibu kutoka katika mizabibu yako, wala usiziokote dhabibu zilizoanguka chini katika shamba la mizabibu. Ni lazima uziache kwa ajili ya masikini na kwa ajili ya wageni. Mimi ndimi Yahweh Mungu wako.
  • Mganda uliosahaulika unaachwa kwa mgeni, yatima na mjaneKum 24:19–21
    Aya
    Kum 24:19–21Utakapovuna zao lako shambani mwako, na ukasahau kipande cha mbegu shambani, haupaswi kurudi na kukichukua; kinapaswa kuwa cha mgeni, cha yatima, au cha mjane, ili Yahwe Mungu wako akubariki katika kazi ya mikono yako. Utakapotikisa mti wako wa mzeituni, haupaswi kupanda juu ya matawi tena; itakuwa kwa ajili ya mgeni, kwa yatima na kwa mjane. Utakapokusanya mizabibu shambani mwako, haupaswi kukusanya masazo yake tena. Kinachobaki kitakuwa cha mgeni, cha yatima na cha mjane.
  • Si aina mbili za mbegu; si ng’ombe na punda katika nira mojaLaw 19:19, Kum 22:9–10
    Aya
    Law 19:19Shika amri zangu. Usiwazalishe wanyama wako kwa kutumia wanyama wa aina nyingine tofauti. Usichanganye aina mbili tofauti za mbegu unapopanda shamba lako. Usivae vazi lililofumwa kwa kutumia nyuzi za rangi mbili tofauti zilizochanganywa pamoja.
    Kum 22:9–10Haupaswi kupanda shamba lako la mizabibu kwa mbegu mbili, ili kwamba mavuno yote yasichukuliwe na sehemu takatifu, mbegu uliyoipanda pamoja na matunda ya mzabibu. Haupaswi kulimia ng’ombe na punda kwa pamoja.
  • Matunda ya mti uliopandwa karibuni hayaliwi kwa miaka mitatuLaw 19:23–25
    Aya
    Law 19:23–25Mtakapoingia katika nchi na kupanda aina zote za miti kwa chakula, kisha mtayahesabu matunda yatakayozaliwa kuwa yamekatazwa kuliwa. Tunda litakatazwa kwako kwa miaka mitatu. Halitaliwa. Lakini katika mwaka wa nne matunda yote yatakuwa matakatiifu, matoleo ya sifa kwa Yahweh. Katika mwaka wa tano unaweza kula tunda, ambalo umelisubiri ili kwamba mti uweze kuzaa zaidi. Mimi ndimi Yahweh Mungu wako.
  • Kulipa fidia kwa mifugo iliyopotea au moto shambaniKut 22:5–6
    Aya
    Kut 22:5–6Kama mwanaume akiwapeleka malishoni mifugo yake au shamba la mizabibu na akawaachia wanyama wake, na kawa wanakula shambani mwa mwanaume mwengine, lazima afanye malipo bora kutoka shambani mwake na shamba lake la mizabibu. Kama moto ukitokea na kusambaa kwenye miba hadi mbegu, au mimea, au shamba kuteketezwa, yeye aliye anzisha moto lazima afanye malipo.
  • Kula na kushiba katika shamba la mizabibu la jirani, lakini usijaze kikapuKum 23:24–25
    Aya
    Kum 23:24–25Utakapokwenda katika shamba la mizabibu la jirani yako, unatakiwa kula mizabibu idadi yoyote unayotaka, lakini hautakiwi kuhifadhi yoyote katika kikapu chako. Utakapokwenda katika shamba la zao lililoiva la jirani yako, unaweza kuvuna kichwa cha mavuno kwa mkono wako, lakini haupaswi kutumia mundu kuvuna zao lililoiva la jirani yako.
  • Usimfunge ng’ombe kinywa anapopura nafakaKum 25:4
    Aya
    Kum 25:4Haupaswi kumfunga punda wako pua na mdomo anapokuwa akilima shamba lako.
  • Mtu ambaye bado hajafurahia shamba lake jipya la mizabibu anarudi nyumbani kutoka vitaniKum 20:6
    Aya
    Kum 20:6Kuna yeyote ambaye amepanda mzabibu na hajafurahia matunda yake? Acha aende nyumbani, ili kwamba asife vitani na mtu mwingine afurahie matunda yake.

Misemo

  • Alimaye shamba lake atakuwa na chakula teleMit 12:11
    Aya
    Mit 12:11Yule atendaye kazi katika shamba lake atapata chakula tele, bali anayesaka miradi duni hana akili.
  • Shamba la mvivu limemea miiba, ukuta wake wa mawe umebomokaMit 24:30–31
    Aya
    Mit 24:30–31Nilikwenda jirani na shamba la mtu mvivu, nikapita kwenye shamba la mzabibu la mtu asiye na akili. Miiba imeota kila sehemu, ardhi ilikuwa imefunikwa kwa upupu, na ukuta wake wa mawe ulikuwa umebomoka.
  • Panda mbegu zako asubuhi; jioni usiache mikono yako ipumzikeMhu 11:6
    Aya
    Mhu 11:6Asubuhi panda mbegu yako; hadi jioni, fanya kazi kwa mikono yako kama inavyo hitajika kwa kuwa haujui ni ipi itafanikiwa, jioni au asubuhi, au hii au ile au zote zitakuwa nzuri.
  • Ijue hali ya makundi yako ya kondoo na ng’ombeMit 27:23–27
    Aya
    Mit 27:23–27Hakikisha unajua hali ya makundi yako na ujishughulishe juu ya makundi yako, maana utajiri haudumu daima. Je taji hudumu kwa vizazi vyote? Majani huondoka na ukuaji mpya huonekana na milima ya chakula cha mifugo hukusanywa ndani. Wanakondoo watakupatia mavazi yako na mbuzi watakupatia gharama ya shamba. Kutakuwa na maziwa ya mbuzi kwa chakula chako- chakula kwa kaya yako- na chakula kwa watumishi wako wasichana.
  • Apandaye haba atavuna haba2 Kor 9:6
    Aya
    2 Kor 9:6Wazo ni hili: mtu apandaye haba pia atavuna haba, na yeyote apandaye kwa lengo la baraka pia atavuna baraka.
  • Mkulima anayefanya kazi kwa bidii anapaswa kuwa wa kwanza kupata mazao2 Tim 2:6
    Aya
    2 Tim 2:6Ni Muhimu kwamba mkulima mwenye bidii awe wa kwanza kupokea mgao wa mazao yake.

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0