Maisha ya kila siku
Kufunga katika Biblia
Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (40), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.
Katika maombolezo na huzuni
- Watu wa Yabeshi wanazika mifupa ya Sauli na kufunga siku saba1 Sam 31:13
Aya
1 Sam 31:13Kisha wakachukua mifupa yao na kuizika chini ya mti wa mkwaju huko Yabeshi, na wakafunga siku saba.
- Daudi na watu wake wanafunga hadi jioni kwa ajili ya Sauli na Yonathani2 Sam 1:12
Aya
2 Sam 1:12Walilia, wakaomboleza na kufunga mpaka jioni kwa ajili ya Sauli, Yonathani mwanawe, watu wa Yahwe, na kwa ajili ya nyumba ya Israeli kwa maana wameanguka kwa upanga.
- Daudi anakataa kula hadi jua lizame baada ya kifo cha Abneri2 Sam 3:35
Aya
2 Sam 3:35Watu wote wakaja kumtaka Daudi ale wakati kungali mchana, lakini Daudi akaapa, “Mungu na anifanyie hivyo, na kuzidi, ikiwa nitaonja mkate au chochote kabla jua halijazama.”
- Daudi anafunga kwa ajili ya mtoto mgonjwa na anakula mtoto anapokufa2 Sam 12:16–23
Aya
2 Sam 12:16–23Kisha Daudi akamwomba Mungu kwa ajili ya kijana. Daudi akafunga naye akaingia ndani na kulala usiku wote juu ya sakafu. Wazee wa nyumba yake wakainuka na kusimama kando yake, ili wamwinue kutoka sakafuni. Lakini hakuinuka, na hakula pamoja nao. Ikawa siku ya saba mtoto akafa. Watumishi wa Daudi wakaogopa kumwambia kwamba mtoto amekufa, kwa maana walisema, “Tazama, wakati mtoto alipokuwa hai tuliongea naye, lakini hakuisikiliza sauti yetu. Atakuwaje ikiwa tutamwambia kwamba kijana amekufa?!” Daudi alipoona kwamba watumishi wake walikuwa wakinong'onezana, Akatambua kwamba mtoto amekufa. Akawauliza, “Je mtoto amekufa?” Wakajibu, “Amekufa.” Kisha Daudi akainuka kutoka sakafuni naye akaoga, akajipaka mafuta, na kubadili mavazi yake. Akaenda katika hema la kukutania na akaabudu pale, kisha akarudu katika kasri lake. Akataka chakula kiletwe, wakamwandalia, naye akala. Ndipo watumishi wake walipomwambia, “Kwa nini umefanya jambo hili? Ulifunga na kulia kwa ajili ya mtoto wakati alipokuwa hai, lakini mtoto alipokufa, ukainuka na kula.” Daudi akajibu, “Wakati mtoto alipokuwa hai nilifunga na kulia. Nilisema, Ni nani ajuaye kwamba Yahwe angeweza kunihurumia mtoto akaishi au sivyo? Lakini sasa amekufa, hivyo nifungie nini? Je naweza kumrudisha tena? Nitakwenda kwake, lakini yeye hawezi kunirudia.”
- Nehemia anaomboleza siku nyingi, akifunga, kwa habari za YerusalemuNeh 1:4
Aya
Neh 1:4Na mara tu niliposikia maneno haya, nikakaa na kulia, na kwa siku niliendelea kuomboleza na kufunga na kuomba mbele ya Mungu wa mbinguni.
- Ezra hali chakula wala hanywi maji, akiombolezaEzr 10:6
Aya
Ezr 10:6Ndipo Ezra akainuka kutoka mbele ya nyumba ya Mungu na kwenda kwenye chumba ya Yehohanani mtoto wa Eliashibu, Yeye hakula mkate au kunywa maji. Tangu alipokuwa akiomboleza kuhusiana na wale wenye imani haba waliokuwa uhamishoni.
- Mtunga zaburi alifunga akivaa gunia wengine walipokuwa wagonjwaZab 35:13
Aya
Zab 35:13Lakini, walipokuwa akiugua, nilivaa magunia; nilifunga kwa ajili yao huku kichwa changu kikiinamia kifuani kwangu.
Katika hatari na dhiki
- Esta: “Msile wala msinywe kwa siku tatu”Est 4:16
Aya
Est 4:16“Nenda, uwakusanyea Wayahudi wote wanaoishi katika mji wa Shushani, na wafunge kwa ajili yangu. Wasile wala kunywa kwa muda wa siku tatu. Mimi na watumishi watumishi wangu wa kike tutafunga kwa siku hizo. Na kisha nitaenda mbele ya mfalme kinyume cha sheria. Na kama nitakufa na nife.
- Yehoshafati anatangaza kufunga katika Yuda yote2 Nya 20:3
Aya
2 Nya 20:3Yehoshafati akaogopa na akajipanga kumtafuta Yahwe. Akatangaza haraka katika Yuda yote.
- Ezra anatangaza kufunga kando ya mto Ahava kwa safari salamaEzr 8:21–23
Aya
Ezr 8:21–23Tena nikatangaza kufunga mto Ahava ili kujinyenyekeza mbele za Mungu, kutafuta njia iliyoonyoka kutoka kwake kwa ajili yetu, watoto wetu na mali zetu, Niliona aibu kumwomba mfalme kwa ajili ya jeshi au mpandafarasi kwa ajili ya kutulinda tunapokuwa njiani, tangu tumemwambia mfalme “mkono wa Mungu uko pamoja na wote wanaomtafuta kwa mazuri. lakini uweza wake na ghazabu yake ni juu ya wale wote wanaomwasi yeye. Hivyo tulifunga na kumsihi Mungu kwa jambo hilo.
- Israeli wanalia na kufunga Betheli wakati wa vita na BenjaminiAmu 20:26
Aya
Amu 20:26Basi askari wote wa Israeli na watu wote wakaenda Betheli, wakalia, wakakaa mbele za Bwana; nao wakafunga siku hiyo hata jioni, wakatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Bwana.
- Huko Mispa watu wanamwaga maji na kufunga1 Sam 7:6
Aya
1 Sam 7:6Wakakusanyika Mispa, wakateka maji na kuyamwaga chini mbele za BWANA. Siku hiyo walifunga na kusema, “Tumemfanyia BWANA dhambi.” Hapo Mispa ndipo Samweli aliwaamu na kuwaongoza watu wa Iraeli. -8
- Israeli wanakusanyika wakifunga, wamevaa magunia, na mavumbi vichwaniNeh 9:1
Aya
Neh 9:1Siku ya ishirini na nne ya mwezi huo huo watu wa Israeli walikusanyika, nao walikuwa wamefunga, nao walikuwa wamevaa magunia, nao wakaweka vumbi juu ya vichwa vyao.
- Ahabu anararua mavazi yake, anavaa gunia na kufunga1 Fal 21:27
Aya
1 Fal 21:27Ahabu aliposikis maneno haya, Akachana mavazi yake na akavaa magunia kwenye mwili wake na akfaunga, na akalala kwenye magunia na akahuzunika sana.
- Kufunga kunatangazwa Yerusalemu wakati wa YehoyakimuYer 36:9
Aya
Yer 36:9Ilikuja tokea katika mwaka wa tano na mwezi wa tisa kwa Yehoyakimu mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, kwamba watu wote Yerusalemu na watu waliotoka Yerusalemu toka miji ya Yuda walitangaza kufunga kwa kumheshimu Yahwe.
- Mfalme Dario anakesha usiku akifunga wakati Danieli yuko na simbaDan 6:18
Aya
Dan 6:18Basi mfalme alienda kwenye ikulu yake na usiku ule alikuwa na mfungo. Hakuna starehe yoyote iliyoletwa mbele yake, nao usingizi ulimkimbia.
- Danieli anaomba kwa kufunga, akivaa gunia na kujipaka majivuDan 9:3
Aya
Dan 9:3Niliugeuza uso wangu kumwelekea Bwana Mungu, ili kumtafuta yeye kwa sala na maombi, kwa kufunga, na kuvaa nguo za magunia na kukaa katika majivu.
- Danieli hali chakula kitamu, nyama wala divai kwa wiki tatuDan 10:2–3
Aya
Dan 10:2–3Katika siku hizo, mimi Danieli, nilikuwa katika maombolezo kwa wiki tatu. Sikula chakula kizuri, sikula nyama, sikunywa divai, na sikujipaka mafuta mwenyewe mpaka ukamilifu wa wiki tatu nzima.
- Ninawi wanafunga wakivaa magunia — hata ng’ombe na kondooYon 3:5–8
Aya
Yon 3:5–8Watu wa Ninawi walimwamini Mungu na wakatangaza kufunga. Wote hwakavaa nguo za magunia, kutoka aliyemkubwa hata mdogo. Mapema habari zilimfikia mfalme wa Ninawi. Akasimama kutoka kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akajivika magunia, akaketi katika majivu. Alitoa tangazo ambalo lilsemalo, “katika mji wa Ninawi, kwa mamlaka ya mfalme na wakuu wake, msiruhusu mtu wala mnyama, ng'ombe wala kundi, asionje kitu chochote. Wao wasile wala kunywe maji. Lakini watu na wanyama wawe wamefunikwa kwa magunia na walie kwa sauti kubwa kwa Mungu. Kila mtu ageuke na kuacha njia yake mbaya na kutoka katika udhalimu uliyopo mikononi mwake.
- Sauli anawakataza askari wake kula kabla ya jioni1 Sam 14:24
Aya
1 Sam 14:24Siku hiyo watu wa Israeli walifadhaika kwa sababu Sauli aliwaweka watu chini ya kiapo akasema, “Na alaaniwe mtu atakaye kula chakula kabla ya jioni na kabla sijalipiza kisasi kwa maadui zangu.” Hivyo hakuna hata mmoja kati ya watu wote aliyeonja chakula.
- Maadui wa Paulo wanaapa kutokula mpaka wamuueMdo 23:12
Aya
Mdo 23:12Kulipokucha, baadhi ya Wayahudi walifanya agano na kuita laana juu yao wenyewe: walisema ya kwamba hawatakula wala kunywa chochote mpaka watakapomuua Paulo.
Siku arobaini
- Musa siku arobaini mchana na usiku bila mkate wala majiKut 34:28, Kum 9:9, Kum 9:18
Aya
Kut 34:28Musa alikuwa huko na Yahweh kwa siku arobaini na usiku; hakula chakula chochote wala kunywa maji yeyote. Aliandika katika mbao maneno ya agano, Amri kumi.
Kum 9:9Wakati nilipoenda juu ya mlima kupokea mbao za mawe, mbao za agano ambalo Yahwe alifanya nanyi, Nilibaki kwenye mlima kwa siku arobaini na usiku arobaini; Wala sikula mkate wala kunywa maji.
Kum 9:18Tena nilala kifudifudi mbele ya Yahwe kwa siku arobaini na usiku arobaini; wala sikula mkate wala kunywa maji, kwa sababu dhambi zenu zote ambazo mlikuwa mmefanya, kwa kufanya hivyo ambavyo ilikuwa ni mbaya machoni pa Yahwe, ili kwamba kumchochea yeye katika hasira.
- Eliya anatembea siku arobaini kwa nguvu ya mlo mmoja1 Fal 19:8
Aya
1 Fal 19:8Kwa hiyo akainuka na kula na kunywa, naye akasafiri kwa nguvu ya chakula hicho kwa siku arobaini mchana na usiku hata akafika Horebu, mlima wa Mungu.
- Yesu anafunga siku arobaini mchana na usikuMt 4:2
Aya
Mt 4:2Alipokuwa amefunga kwa siku arobaini mchana na usiku alipata njaa.
Desturi
- Siku ya Upatanisho: “mtajinyenyekeza wenyewe”Law 16:29
Aya
Law 16:29Hii itakuwa sharti kwaajili yenu kwamba katika mwezi wa saba, kwenye siku ya kumi ya mwezi, mtanyenyekea wenyewe na msifanye kazi, iwe mwenyeji wa kuzaliwa au mgeni anayeishi kati yenu.
- Kufunga katika mwezi wa nne, wa tano, wa saba na wa kumiZek 7:5, Zek 8:19
Aya
Zek 7:5“Ongea na watu wote wa nchi na makuhani uwaambie, “Mlipofunga na kuomboleza katika mwezi wa tano na wa saba katika hii miaka sabini, je kweli mlifunga kwa ajili yangu?
Zek 8:19“Yahwe wa majeshi asema hivi: Mifungo ya mwezi wa nne, mwezi wa tano, mwezi wa saba na mwezi wa kumi itakuwa nyakati za furaha ya kila aina, kwa nyumba ya Yuda! Kwa hiyo pendeni kweli na amani!
- Isaya: kufunga kunakoenda pamoja na kuwatendea wafanyakazi hakiIsa 58:3–7
Aya
Isa 58:3–7Kwa niini tulifunga; walisema, 'Lakini hamkuona hilo? Kwa nini tulijinyenyekeza wenywe, lakini hakutambua?' Tazama, siku ya kufunda kwanu utatafuta furaha yanu mwenyewe na kuwanyanyasa wafanyakazi wenu wote. Tazama, ninyi mnafunga ili muwe wepesi wa kugombana na kupigana, na kupiga kwa ngumi ya uovu wako; haujafunga leo kuifanya sauti yako isikike juu. Kwa uhalisi aina ya mfungo huu ndio ambao ninauhitaji: Siku ambayo kila mtu hunyenyekea mwenyewe, huinamisha kichwa chake chini kama mwanzi, na hutawanya mavazi ya magunia na majivu chini yake? Je kweli unauita huu ni mfungo, siku ya kumfurahisha Yahwe.? Hii sio mfungo ambao niliuchagua mimi: kufungua vifungo vya waovu, kufungua kamba za nira, kuwaweka huru walioangamizwa, na kuharibu kila nira? Sio kwamba kula mkate na wenye njaa na kuwaleta masikini na kuwaleta wasio na makazi katika nyuma yako?'' Unapomuana mtu yuko uchi, unatakiwa vumvishe mavazi; na usijifiche mwenyewe na ndugu zako.
- Ana aliabudu usiku na mchana, akifunga na kuombaLk 2:37
Aya
Lk 2:37na ndipo akawa mjane kwa miaka themanini na minne. Naye hakuwahi kuondoka hekaluni na alikuwa akiendelea kumwabudu Mungu pamoja na kufunga na kuomba, usiku na mchana.
- Farisayo: “Mimi hufunga mara mbili kwa wiki”Lk 18:12
Aya
Lk 18:12Nafunga mara mbili kila wiki. Natoa zaka katika mapato yote ninayopata. '
- Kwa nini wanafunzi wa Yohana hufunga, lakini wanafunzi wa Yesu hawafungi?Mt 9:14–15
Aya
Mt 9:14–15Ndipo wanafunzi wa Yohana wakaja kwake na kusema, “Kwa nini sisi na mafarisayo tunafunga, lakini wanafunzi wako hawafungi?” Yesu akawaambia, Je wasindikizaji wa arusi wanaweza kuwa na huzuni pindi Bwana arusi anapokuwa pamoja nao? Lakini siku zinakuja ambapo Bwana arusi atachukuliwa kutoka kwao, na ndipo watakapofunga.
- Yesu: mnapofunga, osheni nyuso zenuMt 6:16–18
Aya
Mt 6:16–18Zaidi ya yote, unapokuwa umefunga, usioneshe sura ya huzuni kama wanafiki wanavyofanya, kwa kuwa wanakunja sura zao ili kwamba watu wawatambue wamefunga. Kweli ninakuambia, wamekwisha kupokea thawabu yao. Lakini wewe, unapokuwa umefunga, paka mafuta kichwa chako na uoshe uso wako. Hivyo haitakuonesha mbele ya watu kuwa umefunga, lakini tu itakuwa kwa Baba yako aliye sirini. Na Baba yako aonaye sirini, atakupa thawabu yako.
- Sauli wa Tarso hali wala hanywi kwa siku tatuMdo 9:9
Aya
Mdo 9:9Kwa siku tatu haoni, hali, wala hanywi.
- Kanisa la Antiokia linafunga kabla ya kuwatuma Barnaba na SauliMdo 13:2–3
Aya
Mdo 13:2–3Walipokuwa wakimwabudu Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu alisema, “Niteengeeni pembeni Barnaba na Sauli, waifanye kazi niliyo waitia.” Baada ya Kanisa kufunga, kuomba, na kuweka mikono yao juu ya watu hawa, wakawaacha waende.
- Wazee wanachaguliwa kwa maombi na kufungaMdo 14:23
Aya
Mdo 14:23Walipo wateua kwa ajili yao wazee wa kila kusanyiko la waaminio, na wakiwa wameomba na kufunga, waliwakabidhi kwa Bwana, ambaye wao walimwamini.
- Paulo mara nyingi alikuwa bila chakula2 Kor 11:27
Aya
2 Kor 11:27Nimekuwa katika kazi ngumu na katika maisha magumu, katika usiku mwingi wa kutolala, katika njaa na kiu, mara nyingi katika kufunga, katika baridi na uchi.
- Kusafiri baharini kulikuwa hatari baada ya “Kufunga”Mdo 27:9
Aya
Mdo 27:9Tulikuwa tumechukua muda mwingi sana, na muda wa mfungo wa Kiyahudi ulikuwa umepita pia, na sasa ilikuwa ni hatari kuendelea kusafiri. Hivyo Paulo akatuonya,
- Wasafiri wenzake Paulo wanakaa siku kumi na nne bila chakulaMdo 27:33
Aya
Mdo 27:33Wakati mwanga wa asubuhi ulipokuwa unajitokeza, Paulo akawasihi wote angalau wale kidogo. Akasema, “Hii ni siku ya kumi na nne mnasuburi bila kula, hamjala kitu.
Vyanzo
Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0