Bible Explorer

Gundua › Mada › Wazazi

Maisha ya kila siku

Wazazi katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (42), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

Wapendwa zaidi

  • Isaka anampenda Esau; Rebeka anampenda YakoboMwa 25:28
    Aya
    Mwa 25:28Kisha Isaka akampenda Esau kwa sababu alikula wanyama ambao alikuwa anawinda, lakini Rebeka akampenda Yakobo.
  • Rebeka anapanga kumpatia Yakobo baraka ya IsakaMwa 27:6–10
    Aya
    Mwa 27:6–10Rebeka akaongea na Yakobo mwanawe na kumwambia, “Tazama, nimemsikia baba yako akiongea na Esau ndugu yako. Akasema, 'Niletee mnyama na unitengenezee chakula kitamu, ili nikile na kukubariki mbele za Yahwe kabla ya kufa kwangu.' Kwa hiyo sasa, mwanangu, usikilize sauti yangu kama ninavyokuagiza, Nenda kundini, na uniletee wanambuzi wawili; nami nitaandaa chakula kitamu kutokana nao kwa ajili ya baba yako, kwa namna aipendayo. Utakipeleka kwa baba yako, ili kwamba akile, na kukubariki kabla hajafa.”
  • Yakobo hataki kumtuma Benjamini, kwa hofu ya madharaMwa 42:4, Mwa 42:38
    Aya
    Mwa 42:4Lakini Benjamini, ndugu wa Yusufu, Yakobo hakumtuma na ndugu zake, kwani alihofu kwamba madhara yaweza kumpata.
    Mwa 42:38Yakobo akasema, “Mwanangu atashuka pamoja nanyi. Kwani ndugu yake amekufa na yeye peke yake amebaki. Ikiwa madhara yatampata katika njia mnayoiendea, ndipo mtakapozishusha mvi zangu kaburini kwa huzuni.”

Upendo na malezi

  • Hagari anakaa umbali wa mtupo wa mshale, asiweze kumtazama mtoto wake akifaMwa 21:15–16
    Aya
    Mwa 21:15–16Maji yalipokwisha kwenye kiriba akamtelekeza kijana katika moja ya vichaka. Kisha akaondoka, na akakaa umbali kidogo na yule kijana, umbali kama wa kutupa mshale, kwa vile alisema, “Na nisitazame kifo cha mtoto.” Alipokuwa amekaa kumkabili, akapaza sauti yake akalia.
  • Mama na kaka wa Rebeka wanaomba akae nao siku kumi zaidiMwa 24:55
    Aya
    Mwa 24:55Kaka yake na mama yake wakasema, mwache binti abaki nasi kwa siku chache zingine, angalau siku kumi. baada ya hapo anaweza kwenda.”
  • Yakobo anapata nguvu tena akisikia kwamba Yusufu yu haiMwa 45:26–28
    Aya
    Mwa 45:26–28Wakamwambia “Yusufu bado yu hai, na ndiye mtawala juu ya nchi yote ya Misri.” Na moyo wake ulishikwa na ushangao, kwani hakuwaamini. Wakamwambia maneno yote ya Yusufu aliyokuwa amewambia. Yakobo alipoona mikokoteni Yusufu aliyokuwa amepeleka kuwabeba, roho ya Yakobo baba yao ikafufuka. Israeli akasema, “Inatosha. Yusufu mwanangu yu hai. Nitakwenda nikamwone kabla sijafa.”
  • Mama wa Musa anamficha miezi mitatu, kisha anamweka katika kikapuKut 2:2–3
    Aya
    Kut 2:2–3Yule mwanamke akapata mimba na kuzaa mtoto wa kiume. Alipoona ya kuwa alikuwa mtoto mwenye afaya, alimficha kwa miezi mitatu. Lakini alipokuwa hawezi kuendelea kumficha tena, alichukua kikapu cha manyasi akakipaka sifa na lami. Akamtia mtoto ndani yake na kukiweka juu ya maji katika majani kando ya mto.
  • Manoa anauliza jinsi ya kumlea mvulana atakayezaliwaAmu 13:8
    Aya
    Amu 13:8Ndipo Manoa akamwomba Bwana, akasema, Ee Bwana, tafadhali mruhusu mtu wa Mungu uliyemtuma arudi kwetu ili atufundishe kile tutakachotendea kwa mtoto atakayezaliwa hivi karibuni.
  • Wazazi wa Samsoni wanapinga mke MfilistiAmu 14:2–3
    Aya
    Amu 14:2–3'Nimemwona mwanamke huko Timna, mmojawapo wa binti za Wafilisti. Sasa mkanichukulie awe mke wangu. Baba yake na mama yake wakamwambia, “Je, hakuna mwanamke kati ya binti za ndugu zako, au kati ya watu wetu wote? Je! Utachukua mke kutoka kwa Wafilisti wasiotahiriwa?” Samsoni akamwambia baba yake, “Nichukulie kwa ajili yangu, kwa maana wakati nilipomwangalia, alinipendeza.'
  • Naomi anawabusu wakwe zake na kuwarudisha nyumbaniRut 1:8–9
    Aya
    Rut 1:8–9Naomi aliwaambia wake wa watoto wake, “Nendeni, mrudi, kila mmoja wenu, kwenye nyumba ya mama yake. na Mungu aonyeshe wema juu yenu, kama mlivyo onyesha wema kwao waliokufa na kwangu. Mungu awajalie ninyi kupata pumziko, kila mmoja wenu katika nyumba ya mme mwingine.” Kisha akawabusu, na wakapaza sauti zao na kulia.
  • Ayubu anaamka mapema kutoa sadaka za kuteketezwa kwa kila mtoto wakeAyu 1:5
    Aya
    Ayu 1:5Baada ya siku za karamu zilipokuwa zimetimia, Ayubu hutuma kwao na kuwatakasa. Aliamka asubuhi na mapema na kutoa sadaka za kuteketezwa kwa kila mtoto wake, kwa kusema, “Yawezekana kwamba wanangu wamefanya dhambi na kumkufuru Mungu mioyoni mwao.” Siku zote Ayubu alifanya hivi.
  • Daudi anatamani kwenda kwa Absalomu2 Sam 13:39
    Aya
    2 Sam 13:39Moyo wa mfalme Daudi ukatamani kwenda kumwona Absalomu, kwa maana alikuwa amefarijika kwa habari ya kifo cha Amnoni.
  • Daudi: “Mtendeeni kijana Absalomu kwa upole kwa ajili yangu”2 Sam 18:5
    Aya
    2 Sam 18:5Mfalme akawaagiza Yoabu, Abishai, na Itai kusema, “Mmtendee huyo kijana, Absalomu, kwa upole kwa ajili yangu.” Watu wote wakasikia jinsi mfalme alivyowaagiza maakida kuhusu Absalomu.
  • Rispa analinda miili ya wanawe dhidi ya ndege na wanyama2 Sam 21:8, 2 Sam 21:10
    Aya
    2 Sam 21:8Mfalme akawachukua wana wawili wa Rispa binti Ayia aliomzalia Sauli, hawa wana wawili waliitwa Armoni na Mefiboshethi; na pia Daudi akawachukua wana watano wa Mikali binti Sauli, aliomzalia Adrieli mwana wa Berzilai Mmeholathi.
    2 Sam 21:10Kisha Rispa, binti Aiya, akachukua nguo ya gunia na akajitanda mwenyewe juu ya mlima kando ya miili ya waliokufa tangu mwanzo wa mavuno mpaka wakati mvua ilipoanza kunyesha. Hakuruhusu ndege wa angani kutua juu ya miili mchana wala ayawani wa mwituni wakati wa usiku.
  • Mama halisi angependa kumtoa mtoto wake kuliko kumwona akiuawa1 Fal 3:26
    Aya
    1 Fal 3:26Yule mwanamke mwenye mtoto aliyekuwa hai akamwambia mfalme, kwa kuwa moyo wake ulikuwa na huruma sana kwa mwanae, akasema, “Aa, bwana wangu, mpatie huyu mtoto aliye hai, na usimwue kamwe.” Lakini yule mwanamke mwingine akasema, “Hatakuwa wangu wala wako. Mgawe.”
  • Sulemani anaagiza kiti cha enzi kiletwe kwa ajili ya mama yake1 Fal 2:19
    Aya
    1 Fal 2:19Kwa hiyo Bathisheba akaenda kumwambia, mfalme Sulemani kwa niaba ya Adoniya. Mfalme akainuka kumlaki na akapiga magoti mbele yake. Kisha akaa kwenye kiti chake cha enzi na kulikuwa na kiti kingine cha enzi kilicholetwa kwa ajili ya mama wa mfalme. Naye akaa mkono wa kuume wa mfalme.
  • Mariamu na Yusufu wanamtafuta kijana Yesu kwa wasiwasiLk 2:48
    Aya
    Lk 2:48Walipomwona, walistaajabu. Mama yake akamwambia, “Mwanangu, kwa nini umetutendea hivi? Sikiliza, baba yako na mimi tumekuwa tukikutafuta kwa wasiwasi mkubwa.”
  • Mama wa Yesu anasimama karibu na msalabaYn 19:25
    Aya
    Yn 19:25Askari walifanya mambo haya. Mama yake Yesu, dada wa mama yake, Mariamu mke wa Kleopa na Mariamu Magdalena - wanawake hawa walikuwa wamesimama karibu na msalaba wa Yesu.
  • Yairo anamsihi kwa ajili ya binti yake mdogoMk 5:23
    Aya
    Mk 5:23Akamsihi zaidi na zaidi, akisema, “ Binti yangu mdogo anakaribia kufa. Ninakusihi, njoo na uweke mikono yako juu yake ili kwamba aweze kupata afya na kuishi.”
  • Afisa wa mfalme: “Shuka kabla mtoto wangu hajafa”Yn 4:49
    Aya
    Yn 4:49Kiongozi akasema, “ Bwana shuka chini kabla mwanangu hajafa.”
  • Baba wa mvulana: “Naamini; nisaidie kutoamini kwangu!”Mk 9:24
    Aya
    Mk 9:24Ghafla baba wa mtoto alilia na kusema, “ Naamini! Nisaidie kutokuamini kwangu.”
  • Mama wa wana wa Zebedayo anaomba nafasi za heshima kwa ajili yaoMt 20:20–21
    Aya
    Mt 20:20–21Kisha mama wa wana wa Zebedayo alikuja kwa Yesu na wana wake. Alipiga magoti mbele yake na kumwomba kitu kutoka kwake. Yesu akamwambia, “Unataka nini?” Akamwambia, ''Amuru kuwa hawa wanangu wawili wakae, mmoja mkono wako wa kulia na mmoja mkono wako wa kushoto katika ufalme wako.''
  • Wazazi wa mtu aliyezaliwa kipofu: “Ni mtu mzima. Mwulizeni”Yn 9:20–23
    Aya
    Yn 9:20–23Hivyo wazazi wake wakamjibu, “Tunajua kuwa huyu ni mtoto wetu na kwamba alizaliwa kipofu. Jinsi gani sasa anaona, hatujui, na yeye aliyemfumbua macho yake, hatumjui. Mwulizeni yeye. Ni mtu mzima. Anaweza kujieleza mwenyewe.” Wazazi wake walisema mambo haya, kwa sababu waliwaogopa Wayahudi. Kwa vile Wayahudi walikuwa wamekubaliana tayari kuwa, ikiwa yeyote atakiri kuwa Yesu ni Kristo, atatengwa na Sinagogi. Kwa sababu hii, wazazi wake walisema, “Ni mtu mzima, mwulizeni yeye.”

Wapole kupita kiasi

  • Eli hakuwazuia wanawe1 Sam 3:13
    Aya
    1 Sam 3:13Nimemwambia kwamba niko tayari kuhukumu nyumba yake mara moja kwa ile dhambi aliyoifahamu, kwa sababu watoto wake walijiletea laana juu yao wenyewe na hakuwazuia.
  • Daudi hakumkemea Adoniya hata mara moja1 Fal 1:6
    Aya
    1 Fal 1:6Baba yake alikuwa hajawahi kumsumbua, kwa kusema, “kwa nini umefanya hili na lile?” Adoniya allikuwa mwanamume mzuri sana aliyezaliwa baada ya Absalomu.

Katika Sheria

  • Waheshimu baba yako na mama yakoKut 20:12
    Aya
    Kut 20:12Waheshimu baba na mama yako, ili uweze kuishi miaka mingi duniani Yahweh Mungu wako ametoa.
  • Kifo kwa kumpiga au kumlaani baba au mamaKut 21:15, Kut 21:17
    Aya
    Kut 21:15Yeyote atakaye mpiga baba au mama yake lazima auawe.
    Kut 21:17Yeyote atakaye mlaani baba au mama yake lazima auawe.
  • Wazazi wanawaeleza watoto wao maana ya PasakaKut 12:26–27, Kut 13:8
    Aya
    Kut 12:26–27Watoto wako watakapo kuuliza, 'Hili tendo la ibada lina maana gani?' kisha lazima useme, 'Ni sadaka ya Pasaka ya Yahweh, kwasababu Yahweh kapita nyumba za Waisraeli Misri alipo washambulia Wamisri. Aliweka nyumba zetu huru.”' Kisha watu wakamsujudia Yahweh.
    Kut 13:8Hiyo siku utasema kwa watoto wako, 'Hii ni kwasababu ya kile Yahweh alichofanya kwangu nilipo taka Misri.'
  • Wazazi wote wawili wanamleta mwana mkaidi na mwasi kwa wazeeKum 21:18–20
    Aya
    Kum 21:18–20Iwapo mwanamume ana mwana mkaidi na muasi ambaye hatatii sauti ya baba yake au sauti ya mama yake, ambaye, hata baada ya kurekebishwa, hatawasikia; basi baba yake na mama yake wanapaswa kumshika na kumleta mbele ya wazee wa mji na kwenye malango ya mji. Wanapaswa kuwaambia wazee wa mji, “Huyu mwanetu ni mkaidi na muasi; hataki kusikia sauti zetu; ni mwasherati na pia ni mlevi’.

Katika Mithali kuhusu wazazi

  • Sikiliza mafundisho ya baba yako na maagizo ya mama yakoMit 1:8
    Aya
    Mit 1:8Mwanangu, sikia fundisho la baba yako na wala usiziache kanuni za mama yako;
  • Mwana mwenye hekima humfurahisha baba yakeMit 10:1
    Aya
    Mit 10:1Mithali za Sulemani. Mwana mwenye hekima humfurahisha baba yake lakini mwana mpumbavu huleta majonzi kwa mama yake.
  • Mtu mwema huwaachia wajukuu wake urithiMit 13:22
    Aya
    Mit 13:22Mtu mwema huacha urithi kwa wajukuu wake, bali mali ya mwenye dhambi huwekwa akiba kwa yule atendaye haki.
  • Usimdharau mama yako akiwa mzeeMit 23:22
    Aya
    Mit 23:22Msikilize baba yako ambaye alikuzaa na usimdharau mama yako wakati akiwa mzee.
  • Baba yako na mama yako na wafurahiMit 23:24–25
    Aya
    Mit 23:24–25Baba yake mwenye haki atafurahia sana, na yule amzaaye mtoto mwenye busara atamfurahia. Mfurahishe baba yako na mama yako na yule aliyekuzaa afurahie.
  • Watoto wake huinuka na kumwita heriMit 31:28
    Aya
    Mit 31:28Watoto wake huinuka na kumwita heri na mume wake humsifia, akisema,

Katika nyaraka

  • Wazazi huwawekea watoto akiba, si watoto kwa wazazi2 Kor 12:14
    Aya
    2 Kor 12:14Tazama! mimi niko tayari kuja kwenu kwa mara ya tatu. Sitakuwa mzigo kwenu, kwa kuwa sitaki kitu kilicho chenu. Nawataka ninyi. Kwa kuwa watoto hawapaswi kuweka akiba kwa ajili ya wazazi. Badala yake, wazazi wanapaswa kuweka akiba kwa ajili ya watoto.
  • Akina baba, msiwachokoze watoto wenuEfe 6:4, Kol 3:21
    Aya
    Efe 6:4Na ninyi akina baba, msiwakwaze watoto na kuwasababishia hasira, badala yake, waleeni katika maonyo na maagizo ya Bwana.
    Kol 3:21Akina baba msiwachokoze watoto wenu, ili kwamba wasije wakakata tamaa.

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0