Bible Explorer

Gundua › Mada › Rushwa

Maisha ya kila siku

Rushwa katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (27), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

  • Usipokee rushwa, kwa kuwa rushwa hupofusha machoKut 23:8, Kum 16:19
    Aya
    Kut 23:8Husiwai chukuwa rushwa, kwa kuwa rushwa inawapofusha wanaoona, na kupotosha maneno ya wakweli.
    Kum 16:19Haupaswi kuiondoa haki kwa nguvu; haupaswi kuonesha upendeleo wala kuchukua rushwa, kwa kuwa rushwa upofusha macho ya hekima na kupotosha maneno ya haki.
  • Amelaaniwa apokeaye rushwa ili kumuua mtu asiye na hatiaKum 27:25
    Aya
    Kum 27:25Alaaniwe mwanamume apokeaye rushwa kumuua mtu asiye na hatia’. Kisha watu wote lazima waseme, ‘Amina’.
  • Samweli: “Nimepokea rushwa mkononi mwa nani?”1 Sam 12:3
    Aya
    1 Sam 12:3Mimi niko hapa, Nishuhudieni mbele za BWANA na mbele za mtiwa mafuta wake. Nimechukua ng'ombe wa nani? Nimechukua punda wa nani? Ni nani nimemdhulumu? Nimemwonea nani? Nimepokea rushwa kutoka mikono ya nani inipofushe macho yangu? Nishuhudieni, nami nitawarudishia
  • Mfalme Yehoshafati kwa waamuzi wake: hakuna upendeleo wala rushwa2 Nya 19:7
    Aya
    2 Nya 19:7Basi sas iacheni hofu ya Mungu iwe juu yenu. Iweni waangaliafu mnapoamua, kwa maana hakuna uovu wa Yahwe Mungu wetu, wala hakuna upendeleo wala hongo.”
  • Ni nani atakayekaa kwa Mungu? Yule anayekataa rushwaZab 15:5, Isa 33:15
    Aya
    Zab 15:5Yeye habadilishi nia yake aazimapo fedha. Yeye hachukui rushwa ili kumshuhudia kinyume asiye na hatia. Yeye afanyanyaye mbambo haya hatatikisika kamwe.
    Isa 33:15Nyie mnaotembe katika haki na kuongea kw uaminifu; yeye anayedharau mapato ya ukandamizaji, yeye anayekataa kuchuka rushwa, ambaye hausiki kwenye kupanga vurugu za kihalifu, na ambaye haangali maovu-
  • Misemo ya Mithali: zawadi hufungua milango; zawadi ya siri hutuliza hasiraMit 17:8, Mit 18:16, Mit 21:14
    Aya
    Mit 17:8Rushwa ni kama jiwe la kiini macho kwa yule ambaye atoaye; yeye anayeiacha, hufanikiwa.
    Mit 18:16Zawadi ya mtu inaweza kufungua njia na kumleta mbele ya mtu muhimu.
    Mit 21:14Zawadi ya siri hutuliza hasira na zawadi ya kificho hutuliza ghadhabu kuu.
  • Achukiaye rushwa ataishiMit 15:27
    Aya
    Mit 15:27Mporaji huleta shida kwenye familia yake, bali yeye ambaye huchukia rushwa ataishi.
  • Rushwa huharibu moyoMhu 7:7
    Aya
    Mhu 7:7kweli jeuri humfanya mtu mwenye hekima kuwa mpumbavu, na rusha huharibu moyo.
  • Manabii wanawashtaki watawala na waamuzi wanaopenda rushwaIsa 1:23, Isa 5:23, Mik 3:11, Mik 7:3, Amo 5:12
    Aya
    Isa 1:23Viongozi wenu wamemgeuka Mungu wamekuwa marafiki wa wezi; yeyote anayopenda rushwa na kuikimbilia. Hawawajali yatima, wala wajane wanaokuja kuwanyenyekea mbele yao.
    Isa 5:23ambao wako huru kumpa haki mtenda maovu, na kuwanyima haki wenye haki!
    Mik 3:11Viongozi wenu huhukumu kwa rushwa, makuhani wenu hufundisha kwa hijara, na manabii wenu hufanya utabiri kwa ajili ya pesa. Hata hivyo bado mtamtegemea Yahwe na kusema, “Je hayupo Yahwe pamoja nasi? Hakuna uovu utakaokuja juu yetu.”
    Mik 7:3Mikono yao ni mizuri mno kwa kufanya madhara. watawala huuliza pesa, hakimu yuko tayari kwa rushwa, na mtu mwenye nguvu anawaambia wengine kile anachokitaka kujipatia. Hivyo ndivyo waundavyo kwa pamoja.
    Amo 5:12Kwa kuwa najua ni jinsi gani mlivyo na makosa mengi na jinsi dhambi zenu zilivyo kubwa- ninyi mnaowaonea wenye haki, chukueni rushwa, na kuwageuza wahitaji kwenye lango la mji.

Mifano

  • Wana wa Samweli wanapokea rushwa na kupotosha haki1 Sam 8:3
    Aya
    1 Sam 8:3Watoto wake hawakuenenda katika njia za baba yao, bali walipiga mbio kutafuta mapato ya udhalimu. Walipokea rushwa na na kupotosha hukumu.
  • Wakuu wa Wafilisti wanampa Delila fedha ili amsaliti SamsoniAmu 16:5
    Aya
    Amu 16:5Wale wakuu wa Wafilisti wakamwendea, wakamwambia, “mdanganye Samsoni ili uone mahali zilipo nguvu zake kuu, na kwa namna gani tunaweza kumshinda, ili tumfunge na kumtesa. Fanya hili, na kila mmoja wetu atakupa vipande 1,100 vya fedha.”
  • Asa anampelekea Beni Hadadi fedha na dhahabu ya hekalu1 Fal 15:18–19
    Aya
    1 Fal 15:18–19Kisha Asa akazichukua zile fedha na dhahabu zilizokuwa zimebaki kwenye hazina kwenye nyumba ya BWANA, na katika hazina ya ikulu ya mfalme. Akaziweka katika mikono ya watumishi wake na kuzituma kwa Beni Hadadi mwana wa Tabrimoni mwana wa Hezioni, mfalme wa Shamu ambaye alikuwa akishi Dameski. Akamwambia, “Naomba tufanye patano kati yangu na wewe, kama ilivyokuwa kati ya baba yangu na baba yako. Tazama, Nimekutumia zawadi ya fedha na dhahabu. Ili uvunje agano lako na Baasha mfalme wa Israeli, ili kwamba aniache.”
  • Ahazi anampelekea mfalme wa Ashuru fedha na dhahabu ya hekalu2 Fal 16:8
    Aya
    2 Fal 16:8Hivyo Ahazi akachukua fedha na dhahabu iliyokuwa imepatikana katika nyumba ya Yahwe na mingoni mwa waweka hazina wa nyumba ya mfalme na kuituma kama zawadi kwa mfalme wa Ashuru.
  • Washauri wanaajiriwa kuzuia ujenzi upya wa hekaluEzr 4:5
    Aya
    Ezr 4:5Pia wakawahonga washauri ili kuwachanganya katika mipango yao. Walitenda haya kipindi chote cha Koreshi na kipindi cha utawala wa Dario mfalme wa Uajemi.
  • Shemaya anaajiriwa kumtisha Nehemia ajifiche hekaluniNeh 6:10–13
    Aya
    Neh 6:10–13Nikaenda nyumbani kwa Shemaya mwana wa Delaya, mwana wa Mehetabeli, aliyefungwa nyumbani mwake. Akasema, “Hebu tukutane pamoja katika nyumba ya Mungu, ndani ya hekalu, na tufunge milango ya hekalu, kwa maana wanakuja kukuua. Usiku wanakuja kukuua.” Nikajibu, “Je! Mtu kama mimi ninaweza kukimbia? Na mtu kama mimi ninaweza kuingia hekaluni ili nipate kuishi? Sitaingia.” Niligundua kwamba sio Mungu aliyemtuma, lakini alikuwa amefanya unabii dhidi yangu. Tobia na Sanbalati walimwajiri. Walimpa kazi kunifanya niwe na hofu, ili nifanye kile alichosema na kutenda dhambi, hivyo wangeweza kunipa jina baya ili kuniaibisha.
  • Hamani anatoa talanta elfu kumi kwa amri dhidi ya WayahudiEst 3:9
    Aya
    Est 3:9Kama ikimpendeza mfalme, toa amri watu hawa wote wakatiliwe mbali, nami nitapima talanta elfu kumi za fedha katika mikono ya wale ambao ni wasimamizi wa maswala ya mfalme, ili kwamba waweke katika hazina ya mfalme.”
  • Wakuu wa makuhani wanamlipa Yuda vipande thelathini vya fedhaMt 26:15
    Aya
    Mt 26:15na kusema, “Mtanipatia nini nikimsaliti?” Wakampimia Yuda vipande thelathini vya fedha.
  • Askari wanalipwa waseme kwamba wanafunzi waliiba mwiliMt 28:12–15
    Aya
    Mt 28:12–15Nao makuhani walipokuwa wamekutana na wazee na kulijadili jambo hilo pamoja nao, walitoa kiasi kikubwa cha pesa kwa wale askari na kuwaambia, “Waambieni wengine kuwa, 'wanafunzi wa Yesu walikuja usiku wakauiba mwili wa Yesu wakati sisi tulipokuwa tumelala.' Kama taarifa hii itamfikia liwali, sisi tutamshawishi na kuwaondoleeni ninyi mashaka yote.” Kwa hiyo wale askari wakazichukua zile pesa na kufanya kama walivyokuwa wameelekezwa. Habari hii ikaenea sana kwa Wayahudi na imekuwa hivyo hadi leo.
  • Liwali Feliki anatumaini kwamba Paulo atampa rushwaMdo 24:26
    Aya
    Mdo 24:26Muda uo huo, alitegemea kwamba Paulo atampa fedha kwa hiyo alimwita mara nyingi akaongea naye.

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0