Maisha ya kila siku
Ulevi katika Biblia
Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (30), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.
Misemo
- Divai ni mwenye dhihaka, kileo ni mgomviMit 20:1
Aya
Mit 20:1Divai ni dhihaka na kinywaji kikali ni mgomvi; anayepotea kwa kunywa hana busara.
- Ni nani mwenye macho mekundu? Wale wakaao sana kwenye divaiMit 23:29–35
Aya
Mit 23:29–35Nani mwenye taabu? Nani mwenye huzuni? Nani mwenye mapigano? Nani mwenye malalamiko? Nani mwenye majeraha bila sababu? Nani mwenye macho mekundu? Ni wale ambao huzengea kwenye mvinyo, wale wanaojaribu kuchanganya mvinyo. Usiutazame mvinyo ukiwa mwekundu, wakati unametameta kwenye kikombe na kutelemka kwa uraini. Mwisho wake unauma kama nyoka na sumu yake kama kifutu. Macho yako yataona vitu vigeni na moyo wako utatamka vitu vya ukaidi. Utakuwa kama anayelala kwenye bahari au anayelala juu ya mlingoti. “ Wamenipiga,” utasema, “ lakini sikuumia. Wamenichapa, lakini sikuwa na hisia. Nitaamka lini? Nitatafuta kinywaji kingine.”
- Mlevi na mlafi watakuwa maskiniMit 23:20–21
Aya
Mit 23:20–21Usishirikiane pamoja na walevi, au pamoja na walaji wa nyama walafi, maana mlevi na mlafi wanakuwa masikini na usingizi utawavika kwa matambara.
- Si kwa wafalme kunywa divaiMit 31:4–7
Aya
Mit 31:4–7Lemueli, kunywa divai, siyo kwa ajili ya wafalme, wala kwa watawala kuuliza, “ kileo kikali kiko wapi?” Kwa sababu kama watakunywa, watasahau sheria ni nini, na kupotosha haki za wote walioonewa. Wape kileo kikali watu wanaopotea na mvinyo kwa wale wenye kutaabika kwa uchungu. Atakunywa na kusahau umasikini wake na hataikumbuka taabu yake.
- Ole wao waamkao asubuhi na mapema kufuata kileoIsa 5:11–12
Aya
Isa 5:11–12Ole wao wanaoamka asubuhi na mapema kutafuta pombe kali, wale wanaokaa usiku wa manane mpaka pombe inawaka moto. Wanasherekea kwa kinubi, kinanda, kigoma, filimbi, na mvinyo, lakini hawazitambui kazi za Yahwe, wala hawaziangalii kazi za mikono yake.
- “Mashujaa wa kunywa divai na hodari wa kuchanganya kileo”Isa 5:22
Aya
Isa 5:22Ole wao ambao ni washindi kwa kunjwa mvinyo, na wazoefu wa kuchanganya pombe kali;
- Makuhani na manabii wanayumbayumba kwa kileoIsa 28:7–8
Aya
Isa 28:7–8Lakini wale wanaoyumbayumba kwa ajili ya mvinyo, na wanojikongoja kwa ajili ya pombe kali. Kuhani na nabii watayumbayuma kwa ajili ya pombe kali, na watamezwa na mvinjo. Watajikongoja kwa ajili ya pombe kali, Kujikongoja katika maono na kuyumbayuma katika maamuzi. Hakika, meza zote zimejaa matapishi. Hivyo basi hakuna sehemu iliyosafi.
- “Kesho itakuwa kama leo, tena bora zaidi sana!”Isa 56:12
Aya
Isa 56:12''Njooni, ''Tunywe mvinyo na pombe. Kesho itakuwa kama leo, siku kubwa zaidi ya kipimo.''
- Divai huondoa ufahamuHos 4:11
Aya
Hos 4:11Wanapenda uasherati, divai, na divai mpya, ambayo imechukua uelewa wao.
- Kunywa divai kwa mabakuliAmo 6:6
Aya
Amo 6:6Wanakunywa mvinyo kutoka kwenye bakuli na kujipaka mafuta wenyewe kwa mafuta ya marahamu, lakini hawahuzuniki juu ya mateso ya Yusufu.
- Ole wake anayewalevya jirani zakeHab 2:15
Aya
Hab 2:15'Ole wake yule anayemfanya jirani yake alewe, wewe ambaye unaye ongeza sumu uwafanye walewe ili uweze kutazama uchi wao.
- Walevi hulewa usiku1 The 5:7
Aya
1 The 5:7Kwa kuwa wanaolala hulala usiku na wanao lewa hulewa usiku.
- Msilewe kwa divaiEfe 5:18, Rum 13:13, Lk 21:34
Aya
Efe 5:18Msilewe kwa mvinyo, huongoza kwenye uharibifu, badala yake mjazwe na Roho Mtakatifu.
Rum 13:13Na tuenende sawa sawa, kama katika nuru, si kwa sherehe za uovu au ulevi. Na tusienende katika zinaa au tamaa isiyoweza kudhibitiwa, na si katika fitina au wivu.
Lk 21:34Lakini jiangalieni wenyewe, ili kwamba mioyo yenu isije ikalemewa na ufisadi, ulevi, na mahangaiko ya maisha haya. Kwa sababu ile siku itawajia ghafla
Katika Sheria
- Wazazi wanaweza kumshtaki mwana mbele ya wazee: “mlafi na mlevi”Kum 21:20
Aya
Kum 21:20Wanapaswa kuwaambia wazee wa mji, “Huyu mwanetu ni mkaidi na muasi; hataki kusikia sauti zetu; ni mwasherati na pia ni mlevi’.
- Makuhani hawanywi divai wanapoingia katika hema la kukutaniaLaw 10:9
Aya
Law 10:9“Msinywe mvinyo wala kinywaji kikali, wewe, au wanao wanaobaki pamoja nawe, ili kwamba mtakapoingia kwenye hema ya kukutania msije mkafa. Hii itakuwa amri ya kudumu katika vizazi vyote vya watu wenu,
- Mnadhiri anajiepusha na divai na kileoHesabu 6:3
Aya
Hesabu 6:3Asinywe kileo kitokanacho na siki au kilevi. Asinywe maji ya divai yeyote au kula zabibu mbichi wala zilizokauka.
Mifano
- Nuhu anapanda shamba la mizabibu na kulewaMwa 9:20–21
Aya
Mwa 9:20–21Nuhu akaanza kuwa mkulima, na akapanda mizabibu. Akanywa sehemu ya divai na akalewa. Akawa amelala hemeani uchi.
- Binti za Lutu wanamlevya baba yaoMwa 19:32–33
Aya
Mwa 19:32–33Njoo na tumnyweshe baba yetu mvinyo na tulale naye ili kwamba tuendeleze uzao wa baba yetu.” Kwa hiyo wakamnywesha baba yako mvinyo usiku ule. Kisha yule wa kwanza akaingia na akalala na baba yake; Baba yake hakujua ni wakati gani alikuja kulala, wala wakati alipo amka.
- Nabali, amelewa sana karamuni mwake, hasikii lolote hadi asubuhi1 Sam 25:36–37
Aya
1 Sam 25:36–37Abigaili akarudi kwa Nabali; tazama, alikuwa akifanya sherehe katika mji wake, kama sherehe ya mfalme; na moyo wa Nabali ulifurahi ndani yake, kwa sababu alikwa amelewa sana. Kwa hiyo hakumwambia chochote kabisa hadi kulipopambazuka Ikawa asubuhi, divai ilipokuwa imemtoka Nabali, basi mkewe akamwambia mambo hayo; moyo wake ukafa ndani yake, na akawa kama jiwe.
- Daudi anamlevya Uria, lakini Uria haendi nyumbani2 Sam 11:13
Aya
2 Sam 11:13Daudi alipomwita, alikula na kunywa pamoja naye, Daudi akamfanya alewe. Wakati wa jioni Uria akaenda kulala kitandani pake pamoja na watumish wa bwana wake; hakushuka nyumbani kwake.
- Absalomu anasubiri hadi moyo wa Amnoni ufurahi kwa divai2 Sam 13:28
Aya
2 Sam 13:28Absalomu akawaamuru watumishi wake kusema, “Sikilizeni kwa makini. Amnoni atakapokuwa amelewa mvinyo, na nitakapowambia, 'Mpigeni Amnoni,' msiogope mwueni. Je siyo mimi niliyewamru? Mwe jasiri na hodari.”
- Mfalme Ela anauawa na Zimri wakati analewa1 Fal 16:9–10
Aya
1 Fal 16:9–10Mtumishi wake Zimri, mkuu wa nusu ya magari yake akatengeneza hila dhidi yake. Wakati huo Ela alikuwa Tirza, akinywa na kulewa kwenye nyumba ya Arza, ambaye alikuwa mkuu wa watumishi wa nyumbani huko Tirza. Zimri akaiingia ndani, akamshambulia na kumwua, katika mwaka wa ishirini na saba wa Asa mfalme wa Yuda, naye akawa mfalme mahali pake.
- Beni Hadadi na wafalme 32 wanakunywa hemani mwao adhuhuri1 Fal 20:16
Aya
1 Fal 20:16Nao wakatoka wakati wa adhuhuri. Naye Beni Hadadi alikuwa akinywa na kulewa hemani mwake, yeye na wale wafalme wadogo thelathini na mbili waliokuwa wakimsaidia.
- Ahasuero, akifurahi kwa divai, anamwita malkia VashitiEst 1:10–11
Aya
Est 1:10–11katika siku ya saba moyo wa mfalme ulipokuwa na furaha kwa sababu ya mvinyo, aliwaagiza Mehumani, Biztha, Harbona, Bigtha, Abagtha, Zethari na Karkas (hawa saba ndio waliohudumu mbele ya mfalme) kumleta Malkia Vashiti akiwa katika mavazi yake ya kimalkia. Akiwa na lengo la kuwaonyesha watu na maakida urembo wake, maana alikuwa mrembo.
- Belshaza anakunywa kwa vyombo vya hekalu la YerusalemuDan 5:1–4
Aya
Dan 5:1–4Mfalme Belshaza alifanya sherehe kubwa kwa kwa ajili ya wakuu wake wa kuheshimiwa wapatao elfu moja, na alikunywa divai mbele yao wote watu elfu moja. Wakati Belshaza alipokuwa akionja divai, alitoa agizo la kuleta vyombo vilivyotengenezwa kwa dhahabu au kwa fedha ambavyo Nebukadneza baba yake alikuwa amevichukua kutoka katika hekalu huko Yerusalemu, ambavyo yeye, na wakuu wake, na wake zake, na masuria waliweza kuvinywea. Watumishi walivileta vyombo ya dhahabu vilivyokuwa vimechukulia katika hekalu, nyumba ya Mungu huko Yerusalemu. Mfalme na wakuu wake, na wake zake na masuria walivinywea. Walikunywa divai na kuzisifu sanamu zao zilizotengenezwa kwa dhahabu na fedha, shaba, chuma, mbao na mawe.
Walidhaniwa wamelewa
- Eli anadhani Hana, anayeomba kimya, amelewa1 Sam 1:13–15
Aya
1 Sam 1:13–15Hana aliongea moyoni mwake. Midomo yake ilitikisika, lakini sauti yake haikusikika. Hivyo Eli alimdhania kuwa amelewa. Eli akamwambia, “Utakuwa mlevi mpaka lini? Weka mbali divai yako.” Hana akajibu, “Sivyo bwana wangu, mimi ni mwanamke mwenye roho ya huzuni. Sijanywa divai wala kinywaji chochote cha kulevya, bali nimekuwa nikiimimina nafsi yangu mbele za BWANA.”
- Yesu anaitwa “mlafi na mlevi”Mt 11:19
Aya
Mt 11:19Mwana wa Adamu alikuja akila na kunywa na wakasema 'Angalia, ni mtu mlaji na mlevi, rafiki wa watoza ushuru na wenye dhambi!' Lakini hekima inadhihirishwa kwa matendo yake.''
- Siku ya Pentekoste: “Wamejazwa kwa mvinyo mpya!”Mdo 2:13–15
Aya
Mdo 2:13–15Lakini wengine walidhihaki wakisema, “Hawa wamejazwa kwa mvinyo mpya.” Lakini Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti, akawaambia, “Watu wa Yudea na wote mnaoishi hapa Yerusalemu, hili lijulikane kwenu, sikilizeni kwa makini maneno yangu. Watu hawa hawajalewa kama mnavyodhani, sababu saa hizi ni asubuhi saa tatu.
Vyanzo
Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0