Maisha ya kila siku
Barua katika Biblia
Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (38), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.
Wafalme na maafisa
- Daudi anamtuma Uria akibeba barua inayoamuru kifo chake2 Sam 11:14–15
Aya
2 Sam 11:14–15Hivyo asubuhi Daudi akamwandikia Yoabu barua, naye akaituma kwa mkono wa Uria. Ndani ya barua Daudi aliandika hivi, “Mweke Uria mbele ya vita vikali sana, na kisha, mmwache, ili apigwe na afe.
- Yezebeli anaandika barua kwa jina la Ahabu, zilizotiwa muhuri wake1 Fal 21:8–11
Aya
1 Fal 21:8–11Kwa hiyo Yezebeli akaandika barua kwa jina la Ahabu, akaitia muhuri wake, akazituma kwa wazee na kwa watu tajiri alioketi nao kwenye vikao, na ambao pia waliishi karibu na Nabothi. Katika ile barua aliyoandika, ilisema hivi, “Pigeni mbiu ya kufunga mkamkalishe Nabothi juu mbele ya watu. Pia mwaweke watu wawili wasiokuwa waaminifu pamoja naye na wale watu watoe ushahidi kinyume naye, waseme, 'Ulimlaani Mungu na mfalme.”Halafu mchukueni nje mkampige kwa mawe mpaka afe. Kwa hiyo watu wa mji wake, wazee na watu tajiri waishio kwenye huo mji, wakafanya kama Yezebeli alivyowaeleza, kama ilivyoandikwa kwenye zile baraua ambazo alikuwa amewatumia.
- Mfalme wa Shamu anamtuma Naamani na barua2 Fal 5:5–7
Aya
2 Fal 5:5–7Kisha mfalme wa Shamu akase, “Nenda sasa, na nitatuma barua kwa mfalme wa Israeli.” Naamani akaondoka na kuchukua talanta zake kumi za fedha, vipande elfu sita vya dhahabu, na nguo kumi za kubadilisha. Pia alichukua barua ya kumpelekea mfalme wa Israeli inayosema, “Sasa wakati hii barua itakapoletwa kwako, utaona kwamba nimemtuma mtumishi wangu Naamani kwako, hivyo basi utamponya ukoma wake.” Wakati mfalme wa Israeli alipoisoma ile barua, alichana mavazi yake na kusema, “Je mimi ni Mungu, niue na nirudishe uhai, kwamba huyu mtu anataka nimponye mtu ukoma wake? Inaonekana anatafuta mashindano na mimi.”
- Yehu anawaandikia walezi wa wana sabini wa Ahabu2 Fal 10:1–7
Aya
2 Fal 10:1–7Basi Ahabu alikuwa na watoto sabini katika Samaria. Yehu akaandika barua na kuzituma kwenda Samaria, kwa watawala wa Yezreeli, pamoja na wazee na walinzi wa wana wa Ahabu akisema, “Wana wa bwana wako wako pamoja na wewe, na wewe pia una magari ya farasi na farasi na kuimarisha mji dhidi ya maadui na silaha. Hivyo basi, haraka iwezekanavyo barua hii ikufikiapo, mchagueni aliye bora na anayestahili miongoni mwa mtoto wa bwana wenu na kumuweka kwenye kiti cha kifalme cha baba yake, na kupigania ufalme wa bwana wenu.” Lakini waliogopa na kusema miongoni mwao, “Tazama, wafalme wawili hawatasimama mbele ya Yehu. Hivyo tutasimamaje?” Kisha yule mtu ambaye alikuwa kiongozi kwenye nyumba ya mfalme, na wale waliowalea watoto, wakatuma ujumbe kwa Yehu, kusema, “Sisi ni watumishi wako. Tutafanya chochote utakacho tuamuru. Hatutamfanya mtu yeyote kuwa mfalme. Fanya lile lililojema machoni pako.” Kisha Yehu akaandika barua mara ya pili, akisema, “Kama mko upande wangu, na kama mtasikiliza sauti yangu, mtachukua vichwa vya watu wa wana wa mabwana wenu, na mje kwangu Yezreeli kesho mda kama huu.” Ndipo wana wa wafalme, sabini kwa hesabu, waliokuwa watu muhimu huko mjini, ambao walikuwa wakiwaleta. Hivyo barua ilipokuja kwao, waliwachukua wana wa wafalme na kisha kuwaua, watu sabini, wakaweka vichwa vyao kwenye vikapu, na kuivituma kwa Yehu katika Yezreeli.
- Hezekia anaikunjua barua ya mfalme wa Ashuru mbele ya Yahwe2 Fal 19:14, Isa 37:14
Aya
2 Fal 19:14Hezekia akapokea hii barua kutoka wale wajumbe na kuisoma. Kisha akapanda hata kwenye nyumba ya Yahwe na kuukunjua mbele yake.
Isa 37:14Hezekia alipokea barua hii kutoka mikononi mwa mjumbe na kisoma. Halafu akaenda juu kwenye nyumba ya Yahwe na kuusoma mbele yake.
- Mfalme wa Babeli anamtumia Hezekia barua na zawadi2 Fal 20:12, Isa 39:1
Aya
2 Fal 20:12Katika kipindi hicho Merodak Baladani mfalme wa Babeli alituma barua na zawadi kwa Hezekia, kwa kuwa alisikia kwamba Hezekia alikuwa anaumwa.
Isa 39:1Katika mda ule Merodaki mtoto wa Baladani, mfalme wa Babeli, alituma zawadi na barua kwa Hezekia; maana alisikia Hezekia alikuwa anaumwa na amepona.
- Barua kutoka kwa Eliya inamfikia Mfalme Yehoramu2 Nya 21:12
Aya
2 Nya 21:12Barua kutoka kwa nabii Eliya ikaja kwa Yerohamu. Ilisema, “Hivi ndivyo Yahwe, Mungu wa Daudi, babu yako, anasema: Kwa sababu hujatembea katika njia za Yehoshafafati, baba yako, wala katika njia za Asa, mfalme wa Yuda,
- Matarishi wanapeleka mwaliko wa Pasaka wa Hezekia katika Israeli yote2 Nya 30:1, 2 Nya 30:6
Aya
2 Nya 30:1Hzekia akatuma wajumbe kwa Israeli wote na Yuda, na pia akawaandikia barua Efraimu na Manase, kwamba waje kwenye nyumba ya Yahwe katika Yerusalemu, kusherekea Pasaka ya Yahwe, Mungu wa Israeli.
2 Nya 30:6Hivyo matarishi wakaenda na barua kutoka kwa mfalme na viongozi wake katika Israeli na Yuda yote, kwa agizo la mfalme. wakasema, “Ninyi watu wa Israeli, rudini kwa Yahwe, Mungu wa Abrahamu, Isaka na Israeli, ili kwamba aweze kuwarudia masalia wenu ninyi mlipona kutoka kwenye mkono wa wafalme wa Ashuru.
- Barua dhidi ya Yerusalemu, kwa Kiaramu, kwa ArtashastaEzr 4:7–8, Ezr 4:11
Aya
Ezr 4:7–8Ilikuwa siku za Ahasuero ambazo Artashasta, Mithredathi, na Tabeeli na wenzake wakamwandikia Ahasuero. Barua iliandikwa Kiaramu na kutafsiliwa. Rehumu jemedari na Shimshai mwandishi wakaandika hivi kwa Artashasta kuhusu Yerusalem.
Ezr 4:11Hii ni nakala waliotuma kwa Artashasta: “Watumishi wako, watu wa mji ngambo ya mto, waandika hivi:
- Taarifa ya liwali Tatenai kwa Mfalme DarioEzr 5:6–7
Aya
Ezr 5:6–7Hii ni nakala ya barua kwa Tatenai, mkuu wa mji ngambo ya mto, na Shethar - Bozenai na wenzao katika mji ngambo ya Mto, ambao waliwatuma kwa mfalme Dario. Wakatuma ujumbe, wakiandika kwa mfalme Dario, “Amani tele iwe kwako”
- Nehemia anaomba barua za kupita salama na za mbaoNeh 2:7–9
Aya
Neh 2:7–9Ndipo nikamwambia mfalme, “Ikiwa itampendeza mfalme, nipe barua kwa ajili ya wakuu ng'ambo ya Mto, ili wapate kuniruhusu nipite katika maeneo yao njiani kwenda Yuda. Pia iwepo barua kwa Asafu, mlinzi wa msitu wa mfalme, ili anipe miti ya kufanya mihimili ya malango ya ngome karibu na hekalu, na kwa ukuta wa mji, na kwa nyumba ambayo Nitaishi.” Kwa hiyo kwa sababu mkono mzuri wa Mungu ulikuwa juu yangu, mfalme alinipa hitaji langu. Nilifika kwa wakuu ng'ambo ya Mto, na kuwapa barua za mfalme. Basi mfalme alikuwa amepeleka maofisa wa jeshi na wapanda farasi pamoja nami.
- Sanbalati anamtumia Nehemia barua iliyo waziNeh 6:5–7
Aya
Neh 6:5–7Sanbalati alimtuma mtumishi wake kwangu kwa njia ile ile mara ya tano, na barua iliyo wazi mkononi mwake. Imeandikwa, “Inaripotiwa kati ya mataifa, na Geshemu pia anasema, kwamba wewe na Wayahudi mna mpango wa kuasi, kwa sababu hiyo ndio mnajenga ukuta. Kutokana na taarifa hizi, unakaribia kuwa mfalme wao. Nawe umewachagua manabii kutangaza habari zako juu ya Yerusalemu, wakisema, “Kuna mfalme huko Yuda!” Unaweza kuwa na hakika mfalme atasikia ripoti hizi. Basi, hebu njoo tuzungumze.
- Barua za Hamani zinapelekwa na matarishi katika kila jimboEst 3:13
Aya
Est 3:13Barua hizi za kutaka kuwakatilia mbali Wayahudi wote zilizambazwa katika majimbo yote ya Mfalme Ahusiero, kuangamiza, kuua na kuwaharibu Wayahudi wote, tangu mdogo hadi mkubwa, watoto na wanawake, ndani ya siku moja katika siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili (ambao ni mwezi wa Adari) na kuteka mali zo.
- Mordekai anatia barua muhuri kwa pete ya mfalme; matarishi wanapanda farasi wepesiEst 8:10
Aya
Est 8:10Modekai akaandika kwa jina la Mfalme Ahusiero na akazipiga muhuri kwa pete ya mfalme. Akapeleka nyaraka kwa matarishi, akawapandisha kwenye farasi waendao kwa haraka waliotumika kwa huduma ya mfalme, waliozaliwa kwa mfalme.
- Barua za Mordekai kuhusu Purimu kwa Wayahudi wa karibu na wa mbaliEst 9:20
Aya
Est 9:20Modekai akaweka mambo haya na akatuma nyaraka kwa Wayahudi wote waliokuwa katika utawala wa Mfalme Ahusiero,
- Barua ya Yeremia kwa mateka huko BabeliYer 29:1
Aya
Yer 29:1Haya ni maneno katika waraka ambao Yeremia nabii alituma kutoka Yerusalemu kwa wazee waliosalia miongoni mwa mateka na makuhuni, manabii, na watu wote ambao Nebukadreza aliwapeleka utumwani kutoka Yerusalemu hadi Babeli.
- Jemadari Klaudio Lisia anamwandikia liwali FelikiMdo 23:25–30
Aya
Mdo 23:25–30Akaandika barua kwa namna hii, Klaudio Lisia kwa Liwali mtukufu Feliki, salamu. Mtu huyu alikamatwa na wayahudi wakawa karibu kumwua, ndipo nikaenda pamoja na kikosi cha askari nikamwokoa, nilipopata habari ya kuwa yeye ni raia wa kirumi. Nilitaka kujua kwa nini wamemshtaki, hivyo nikampeleka kwenye baraza. Nikaona kwamba alikuwa ameshitakiwa kwa ajili ya maswali ya sheria yao, wala hakushitakiwa neno lolote la kustahili kuuawa wala kufungwa. Kisha ikajulikana kwangu kwamba kuna njama dhidi yake, hivyo kwa haraka nikamtuma kwako, na kuwaagiza wanaomshitaki pia walete mashitaka dhidi yake mbele yako. Wakaagana.”
Katika kanisa la kwanza
- Luka anaandika habari kwa mpangilio kwa ajili ya TheofiloLk 1:3, Mdo 1:1
- Sauli anaomba barua kwa masinagogi ya DameskiMdo 9:2
Aya
Mdo 9:2na kumwomba barua kwa ajili ya masinagogi huko Dameski, ili kwamba akimpata mtu aliye katika Njia ile, awe mwanaume au mwanamke, awafunge na kuwaleta Yerusalemu.
- Barua ya baraza la Yerusalemu inasomwa AntiokiaMdo 15:23, Mdo 15:30
- Ndugu wanaandika ili Apolo akaribishwe AkayaMdo 18:27
Aya
Mdo 18:27Alipotamani kuondoka kwenda Akaya, ndugu walimtia moyo na kuwaandikia barua wanafunzi walioko Akaya ili wapate kumpokea. Alipowasili, kwa neema aliwasaidia sana wale waliomini.
- Viongozi wa Wayahudi wa Roma: “Hatujapokea barua yoyote kukuhusu”Mdo 28:21
Aya
Mdo 28:21Kisha wakamwambia, “Hatujawahi kupokea barua kutoka Yudea kukuhusu wewe, wala hakuna ndugu aliyekuja na kutoa taarifa au kusema neno lolote baya kuhusu wewe.
- Tertio aliandika barua kwa WarumiRum 16:22
Aya
Rum 16:22Mimi, Tertio, niliyeuandika waraka huu, nawasalimu katika jina la Bwana.
- Paulo anataja barua ya awali kwa Korintho1 Kor 5:9
Aya
1 Kor 5:9Niliandika katika barua yangu kuwa msichangamane na wazinzi.
- Barua za kumtambulisha mtu2 Kor 3:1
Aya
2 Kor 3:1Je, tumeanza kujisifia wenyewe tena? Hatuhitaji barua ya mapendekezo kwenu au kutoka kwenu, kama baadhi ya watu, je twahitaji?
- “Angalieni jinsi nilivyowaandikia kwa herufi kubwa… kwa mkono wangu mwenyewe!”Gal 6:11
Aya
Gal 6:11Angalieni ukubwa wa barua nilizowaandikia kwa mkono wangu mwenyewe.
- Salamu kwa mkono wa Paulo mwenyewe ni alama ya kila barua2 The 3:17
Aya
2 The 3:17Hii ni salam yangu, Paulo, kwa mkono wangu mwenyewe, ambayo ni alama katika kila waraka. Hivi ndivyo niandikavyo.
- Jihadharini na barua “inayoonekana kutoka kwetu” tu2 The 2:2
Aya
2 The 2:2kwamba msisumbuliwe wala kutabishwa kwa urahisi, kwa roho, au kwa ujumbe au kwa barua inayoonkana kuwa imetoka kwetu, ikisema ya kuwa siku ya Bwana tayari imekuja.
- Kolosai na Laodekia wanapaswa kubadilishana baruaKol 4:16
Aya
Kol 4:16Barua hii itakapokuwa imesomwa miongoni mwenu, isomwe pia kwa kanisa la walaodekia, nanyi pia hakikisheni mnaisoma ile barua kutoka Laodekia.
- Paulo anamwandikia Filemoni kuhusu OnesimoFlm 1:1, Flm 1:10
- Petro: baadhi ya mambo katika barua za Paulo ni magumu kuelewa2 Pet 3:16
Aya
2 Pet 3:16Paulo anaongelea hayo yote katika barua zake, kuna vitu ambavyo ni vigumu kuvielewa. Watu wasio na adabu na uimara wameviharibu vitu hivyo, Na kama wanavyofanya kwa maandiko. Kuelekea maangamizi yao.
Vyanzo
Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0