Maisha ya kila siku
Fedha katika Biblia
Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (41), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.
Fedha iliyopimwa
- Abraham anapima shekeli 400 za fedha kwa pango la MakpelaMwa 23:15–16
Aya
Mwa 23:15–16“Tafadhari bwana wangu, nisikilize. Kipande cha ardhi kinathamani ya shekeli mia nne za fedha, na hiyo ni kitu gani kati yangu mimi na wewe? wazike wafu wako.” Abraham akamsikiliza Efroni na akampimia Efroni kiwango cha fedha alizosema mbele ya wana wa Helthi wakisikiliza, shekeli mia nne za fedha, kwa mujibu wa viwango vya vipimo vya kibiashara.
- Yakobo ananunua shamba Shekemu kwa vipande mia moja vya fedhaMwa 33:19
Aya
Mwa 33:19Kisha akanunu sehemu ya ardhi alipokuwa ameweka hema yake kutoka kwa wana wa Hamori, baba wa Shekemu, kwa vipande mia vya fedha.
- Yusufu anauzwa kwa shekeli ishirini za fedhaMwa 37:28
Aya
Mwa 37:28Wafanyabiashara wa Kimidiani wakapita. Ndugu zake wakamwinua na kumtoa Yusufu shimoni. Wakamwuza Yusufu kwa Waishmaeli kwa vipande ishirini vya fedha. Waishmaeli wakamchukua Yusufu mpaka Misri.
- Ndugu wanakuta fedha yao imerudishwa magunioni mwaoMwa 42:25, Mwa 42:35, Mwa 43:21
Aya
Mwa 42:25Kisha Yusufu akaagiza watumishi kujaza mifuko yao kwa nafaka, na kurudisha pesa ya kila mmoja katika gunia lake, nakuwapa mahitaji kwa safari. Wakatendewa hivyo.
Mwa 42:35Ikawa walipoyafungua magunia yao, na tazama, kila mfuko wa fedha wa mmojawao ulikuwa katika gunia lake. Wakati wao na baba yao walipoona mifuko yao ya fedha, wakaogopa.
Mwa 43:21Ikawa, tulipofika katika eneo la kupumzikia, tukafungua magunia yetu, na, tazama, pesa ya kila mtu ilikuwa katika gunia lake, pesa yetu kwa kiasi kamili. Tumeileta katika mikono yetu.
- Yusufu anakusanya fedha yote ya Misri na Kanaani kwa nafakaMwa 47:14–16
Aya
Mwa 47:14–16Yusufu akakusanya pesa yote iliyokuwa katika nchi ya Misri na nchi ya Kanaani, kwa kuwauzia wakaaji wake chakula. Kisha Yusufu akaleta ile pesa katika kasri la Farao. Pesa yote ya nchi za Misri na Kanaani ilipokwisha, Wamisri wote wakaja kwa Yusufu wakisema, “Tupe chakula! Kwa nini tufe mbele zako kwa maana pesa yetu imekwisha?” Yusufu akasema, “Ikiwa pesa yenu imekwisha, leteni wanyama wenu nami nitawapa chakula badala ya wanyama wenu.”
- Kila mkuu wa Wafilisti anamwahidi Delila fedha kwa siri ya nguvu zakeAmu 16:5
Aya
Amu 16:5Wale wakuu wa Wafilisti wakamwendea, wakamwambia, “mdanganye Samsoni ili uone mahali zilipo nguvu zake kuu, na kwa namna gani tunaweza kumshinda, ili tumfunge na kumtesa. Fanya hili, na kila mmoja wetu atakupa vipande 1,100 vya fedha.”
- Mika anamrudishia mama yake shekeli 1,100 alizomchukuliaAmu 17:2–4
Aya
Amu 17:2–4Akamwambia mama yake, “Shilingi 1,100 za fedha ambazo zilichukuliwa kutoka kwako, ambazo ulizungumza kwa kiapo, na kuniambia-tazama hapa! Ninazo fedha pamoja nami. Nimeziiba.” Mama yake akasema, 'Na Bwana atakubariki, mwanangu!' Alirejesha vipande 1,100 vya fedha kwa mama yake na mama yake akasema, “Nimeweka fedha hii kwa Bwana, kwa ajili ya mwanangu kuifanya na kuchonga takwimu za chuma. Kwa hiyo sasa, ninawarejesha.” Alipokuwa amrudishia mama yake fedha, mama yake alichukua vipande mia mbili za fedha na akawapa mfanyakazi wa chuma ambaye aliwafanya kuwa sanamu na kuchonga takwimu za chuma, na wakawekwa ndani ya nyumba ya Mika.
- Ahabu anamtolea Nabothi fedha kwa shamba lake la mizabibu1 Fal 21:2
Aya
1 Fal 21:2Ahabu akamwambia Nabothi, akisema, “Nipe shamba lako, ili nilifanye kuwa bustani ya mboga, kwa sababu iko karibu na nyumba yangu. Badala yake nitakupa shamba zuri la mizabibu, au, kama ukipenda nitakulipa thamani yake kwa fedha.”
- Naamani anafunga talanta mbili za fedha katika mifuko miwili kwa Gehazi2 Fal 5:23
Aya
2 Fal 5:23Naamani akajibu, “Ninafuraha kubwa kukupatia talanta mbili.” Naamani akamsihi Gehazi na kujaribu talanta mbili za fedha kwenye mifuko miwili ya kubebea, pamoja na nguo mbili za kubadilisha, na kutandaza kwa wafanyakazi wake wawili, ambao walikuwa wamebebea ile mifuko miwili ya fedha mbele ya Gehazi.
- Sanduku lenye tundu kifunikoni linakusanya fedha za hekalu2 Fal 12:9–11
Aya
2 Fal 12:9–11Badala yake, Yehoyada yule kuhani akachukua kasha, akatoboa tundu kwenye kifuniko chake, na kuliweka karibu na madhabahu, upande wa kulia kama mtu anaingia kwenye madhabahu ya Yahwe. Makuhani ambao walikuwa wakilinda mlango wa hekalu wakatumbukiza pesa zote ambazo zilizokuwa zimeletwa kwenye nyumba ya Yahwe. Ikawa walipoona kwamba kulikuwa na pesa za kutosha kwenye kasha, mwadishi wa mfalme na kuhani mkuu wakaja na kuweka pesa kwenye mifuko na kisha kuhesabu, pesa ikaonekana kwenye nyumba ya Yahwe. Wakawapa pesa ambayo ilikuwa imepimwa kwenye mikono ya watu ambao waliokuwa wanatunza nyumba ya Yahwe. Wakawalipa mafundi seremala na wajenzi ambao walikuwa wemefanya kazi kwenye nyumba ya Yahwe,
- Menahemu anachukua shekeli hamsini kwa kila tajiri kwa ajili ya Ashuru2 Fal 15:20
Aya
2 Fal 15:20Menahemu akatoza hii pesa kutoka Israeli kwa kumtaka kila mtu tajiri alipe shekeli hamsini za fedha kwake kumpatia mfalme wa Ashura. Hivyo mfalme wa Ashuru akarudi na hakukaa pale katika ile nchi.
- Daudi anamlipa Orinani shekeli 600 za dhahabu kwa mahali pale1 Nya 21:25
Aya
1 Nya 21:25Hivyo Daudi akalipa shekeli mia sita ya dhahabu kwa hilo eneo.
- Yeremia anapima shekeli kumi na saba na kutia sahihi hati iliyotiwa muhuriYer 32:9–10
Aya
Yer 32:9–10Kwa hiyo nililinua shamba katika Anathothi kutoka kwa Hanameli, mwana wa mjomba wangu, na nilipima fedha kwa ajili yake, shekeli kumi na saba katika uzito. Kisha niliandika katika barua na kuitia muhuri, na kulikuwa na mashadi wakaishuhudia. Kisha nikampa fedha katika mizani.
- Wafanyabiashara wanapunguza efa na kuongeza shekeliAmo 8:5
Aya
Amo 8:5wakisema, “Wakati mwezi mpya utakapoisha, hivyo tunaweza kuuza mazao tena? Wakati siku ya Sabato itakapoisha, ili kwamba tuuze ngano? Tutafanya kipimo kidogo na kuongeza bei, tukidanganya kwa mizani za udanganyifu.
- Vipande thelathini vya fedha vinapimwa kama ujiraZek 11:12–13
Aya
Zek 11:12–13Nikawaambia, “Ikiwa itawapendeza, nilipeni ujira wangu. Kama sivyo, msifanye hivyo.” Hivyo wakapima ujira wangu - vipande thelathini vya fedha. Kisha Yahwe akaniambia, “Weka fedha katika hazina, thamani nzuri zaidi ambayo walikupa!” Hivyo nikachukua vipande thelathini vya fedha na kuviweka katika hazina ndani ya nyumbani Yahwe.
Katika Sheria
- Ng’ombe anayemchoma mtumwa: shekeli thelathini za fedhaKut 21:32
Aya
Kut 21:32Kama ng'ombe akimpiga mtumishi wa kiume au wakike, mmiliki wa ngombe lazima alipe shekeli thelathini za fedha, na ng'ombe lazima apigwe mawe.
- Kila aliyehesabiwa analipa nusu shekeliKut 30:13–16
Aya
Kut 30:13–16Kila mtu apitaye kwa wale waliohesabiwa atatoa nusu shekeli kwa kuiandama shekeli ya mahali patakatifu; (shekeli ni gera ishirini). Nusu shekeli kwa sadaka ya Yahweh. Kila mtu apitaye kwa wale waliohesabiwa tangu huyo ambaye umri wake ni miaka ishirini, au zaidi, atatoa hiyo sadaka kwangu. Watu watakapo leta hii sadaka kwangu kufanya upatananisho, matajiri hawataleta zaidi, wala maskini hawataleta kilichopungua katika hiyo nusu shekeli. Nawe utapokea hizo fedha za upatanisho mikononi mwa hao wana wa Israeli, na kuziweka kwa ajili ya utumishi wa hema ya kukutania. Ili kwamba ziwe ukumbusho kwa ajili ya wana wa Israeli mbele yangu ili kufanya upatanisho kwa ajili ya roho zenu.
- Usimkopeshe ndugu maskini fedha kwa ribaLaw 25:37
Aya
Law 25:37Hutampa mkopo wa fedha na kumtoza riba, wala hutamuuzia chakula chako ili kupata faida.
- Zaka inabadilishwa kwa fedha na kutumiwa sikukuuniKum 14:25–26
Aya
Kum 14:25–26mtabadilisha sadaka katika pesa. Fungeni pesa kwenye mkono, na nendeni kwenye eneo ambalo Yahwe Mungu wenu atachagua. Huko mtatumia pesa kwa chochote mnatamani kwa ng'ombe au kondoo, au kwa mvinyo, au kwa kinywaji imara, au kwa chochote mnatamani; mtakula hapo mbele ya Yahwe Mungu wenu, na mtafurahi, nyie na nyumba zenu.
Katika Injili na Matendo
- Dinari moja kwa kazi ya siku moja shambani mwa mizabibuMt 20:2
Aya
Mt 20:2Baada ya kuwa amekubaliana na wafanyakazi dinari moja kwa kutwa, aliwatuma kwenda katika shamba lake la mizabibu.
- Sarafu ya kodi ina sura ya KaisariMt 22:19–21
Aya
Mt 22:19–21Nionesheni pesa itumikayo kulipia kodi.” Ndipo wakamletea dinari. Yesu akawauliza, “Sura na jina hili ni vya nani?” Wakamjibu, “Vya Kaisari.” Ndipo Yesu akawaambia, “Mpeni Kaisari vitu vilivyo vyake na vya Mungu mpeni Mungu.”
- Sarafu kinywani mwa samakiMt 17:27
Aya
Mt 17:27Lakini tusije tukawafanya watoza ushuru wakatenda dhambi, nenda baharini, tupa ndoano, na umtwae yule samaki ajaye kwanza. Baada ya kuufungua mdomo wake, utakuta mle shekeli moja. Ichukue na uwape watoza ushuru kwa ajili yangu na wewe.
- Mtumishi anaficha fedha ya bwana wake ardhiniMt 25:18, Mt 25:27, Lk 19:23
Aya
Mt 25:18Lakini mtumwa aliyepokea talanta moja, alienda zake, akachimba shimo ardhini, na kuificha fedha ya bwana wake.
Mt 25:27Kwahiyo ulipaswa kuwapa fedha yangu watu wa benki, na wakati wa kurudi kwangu ningeipokea ile yangu pamoja na faida.
Lk 19:23Basi, mbona hukuweka fedha yangu katika benki, ili nikirudi niichukue pamoja na faida?
- Mwanamke anafagia nyumba kutafuta moja ya sarafu kumi za fedhaLk 15:8–9
Aya
Lk 15:8–9Au kuna mwanamke gani mwenye sarafu kumi za fedha, akipotewa na sarafua moja, hata washa taa na kufagia nyumba na kutafuta kwa bidii hadi atakapoipata? Na akiisha kuiona huwaita rafiki zake na jirani zake akawaambia furahini pamoja nami, kwa kuwa nimeipata tena sarafu yangu niliyokua nimeipoteza.
- Yesu anapindua meza za wabadili fedhaMt 21:12, Yn 2:14–15
Aya
Mt 21:12Kisha Yesu akaingia katika hekalu la Mungu. akawafukuza nje wote waliokuwa wakinunua na kuuza hekaluni. Pia alipindua meza za wabadilishaji wa fedha na viti vya wauza njiwa.
Yn 2:14–15Akawakuta wauzaji wa ng'ombe, kondoo, na njiwa ndani ya Hekalu. Pia na wabadilisha fedha walikuwa wameketi ndani ya Hekalu. Yesu akatengeneza mjeledi wenye vifundo, akawatoa wote walikuwemo katika hekalu, ikijumuisha ng'ombe na kondoo. Akamwaga fedha za wabadili fedha na kuzipindua meza zao.
- Wanafunzi wanatumwa bila fedha mikanda mwaoMt 10:9, Mk 6:8
- Sarafu mbili ndogo za shaba za mjane maskiniMk 12:41–42
Aya
Mk 12:41–42Kisha Yesu aliketi chini karibu na sanduku la sadaka ndani ya eneo la hekalu; alikuwa akitazama watu waliokuwa wakitia pesa zao ndani ya sanduku. Watu wengi matajiri waliweka kiasi kikubwa cha pesa. Kisha mwanamke mjane maskini alikuja na kutia vipande viwili, thamani ya senti.
- Yuda anarudisha vipande thelathini vya fedha; shamba linanunuliwaMt 27:3–7
Aya
Mt 27:3–7Kisha wakati Yuda, ambaye alikuwa amemsaliti, aliona kwamba Yesu amekwisha kuhukumiwa, alijuta na kurudisha vipande thelathini vya fedha kwa mkuu wa makuhani na wazee, na akasema, “Nimefanya dhambi kwa kuisaliti damu isiyo na hatia.” Lakini wakajibu, “Inatuhusu nini sisi? Yaangalie hayo mwenyewe.” Kisha alivirusha chini vile vipande vya fedha katika hekalu, na kuondoka zake na kujinyonga mwenyewe. Mkuu wa makuhani alivichukua vile vipande vya fedha na kusema, “Si halali kuiweka fedha hii katika hazina, kwa sababu ni gharama ya damu.” Walijadiliana kwa pamoja na fedha ikatumika kununulia shamba la mfinyazi la kuzika wageni.
- Askari wanapewa kiasi kikubwa cha fedhaMt 28:12
Aya
Mt 28:12Nao makuhani walipokuwa wamekutana na wazee na kulijadili jambo hilo pamoja nao, walitoa kiasi kikubwa cha pesa kwa wale askari
- Petro: “Fedha na dhahabu sina”Mdo 3:6
Aya
Mdo 3:6Lakini Petro akasema, “fedha na dhahabu mimi sina, lakini kile nilichonacho nitatoa kwako. Katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth, tembea.”
- Simoni mchawi anawapa mitume fedhaMdo 8:18–20
Aya
Mdo 8:18–20Wakati Simoni alipoona kwamba Roho Mtakatifu ametolewa kupitia kuwekewa mikono na mitume; akataka kuwapa pesa, Akasema, “Nipeni hii nguvu, ili kila nitakayemwekea mikono apokee Roho Mtakatifu.” Lakini Petro akamwambia; pesa yako pamoja na wewe ipotelee mbali, kwa sababu umedhani kuwa karama ya Mungu inapatikana kwa pesa.
Misemo
- “Fedha hujibu mambo yote”Mhu 10:19
Aya
Mhu 10:19Watu huandaa chakula kwa kicheko, divai huleta furaha maishani, na fedha hutimiza hitaji kwa kila kitu.
- Apendaye fedha hatashiba fedhaMhu 5:10
Aya
Mhu 5:10Yeyote apendaye fedha hatatosheka na fedha, na yeyote apendaye utajiri mara zote hutaka zaidi. Huu pia ni mvuke.
- Hekima, kama fedha, ni kingaMhu 7:12
Aya
Mhu 7:12Kwa kuwa hekima hutoa ulinzi kama vile fedha inavyoweza kutoa ulinzi, lakini faida ya maarifa ni kwamba hekima humpa uhai kwa yeyote aliye nayo.
- Kupenda fedha ni shina la maovu ya kila namna1 Tim 6:10
Aya
1 Tim 6:10Kwa kuwa kupenda fedha ni chanzo cha aina zote za uovu. Watu ambao hutamani hiyo, wamepotoshwa mbali na imani na wamejichoma wenyewe kwa huzuni nyingi.
Vyanzo
Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0