Maisha ya kila siku
Taa katika Biblia
Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (28), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.
Katika maskani na hekalu
- Kinara cha dhahabu ya kufua, matawi sita na vikombe kama maua ya mloziKut 25:31–36
Aya
Kut 25:31–36Nawe fanya kinara cha taa cha dhahabu safi; hicho kinara na kifanywe cha kazi ya kufua, kitako chake, na mti wake, vikombe vyake, na matovu yake, na maua yake, vyote vitakuwa vya kitu kimoja nacho. Nacho kitakuwa na matawi sita yenye kutoka ubavuni mwake - matawi matatu ya kinara upande wake mmoja, na matawi matatu ya kinara upande wake wa pili. Tawi la kwanza lazima liwe na vikombe vitatu vilivyotengenezwa mfano wa maua ya mlozi katika tawi moja, tovu na ua na vikombe vitatu vilivyofanywa mfano wa maua ya mlozi katika tawi la pili, tovu na ua. Vivyo hivyo hayo matawi yote sita yatokayo katika kile kinara. Katika hicho kinara, lazima kuwe na vikombe vinne vilivyofanywa mfano wa maua ya mlozi, matovu yake, na maua yake. Lazima kuwe na tovu chini ya matawi - mawili la kitu kimoja nacho, na tovu chini ya matawi mawili la kitu kimoja nacho, na tovu chini ya matawi mawili la kitu kimoja nacho, kwa hayo matawi sita yatokayo katika kile kinara. Matovu yake na matawi yake yatakuwa ya kitu kimoja nacho, kiwe chote pia kazi moja ya kufua, ya dhahabu safi.
- Taa saba, na makasi na sahani za dhahabuKut 25:37–38, Kut 37:23
Aya
Kut 25:37–38Lazima nawe uzifanye hivyo vinara saba na taa zake saba, nao wataziwasha hizo taa zake, zitoe nuru mbele yake. Na makoleo yake, na visahani vyake, vyote vitakuwa vya dhahabu safi.
Kut 37:23Kisha akafanya taa zake saba na mikasi ya tambi zake na vyetezo vyake kutokana na dhahabu safi.
- Kimetengenezwa kwa talanta moja ya dhahabu safiKut 25:39, Kut 37:24
- Mafuta safi ya zeituni zilizopondwa huziwasha taa daimaKut 27:20, Law 24:2
Aya
Kut 27:20awe waamuru wana wa Israeli wakuletee mafuta ya zeituni safi ya kupondwa kwa ajili ya nuru, ili kufanya ile taa kuwaka daima.
Law 24:2“Waamru watu wa Israeli wakuletee mafuta halisi yaliyokamliwa kutokana na mizeituni ili yatumike kwenye taa, ili kwamba taa ziweze kuwaka daima na kuleta mwanga.
- Haruni anazitunza taa tangu jioni hadi asubuhiKut 27:21, Law 24:3–4
Aya
Kut 27:21Ndani ya ile hema ya kukutania, nje ya hilo pazia, lililo mbele ya huo ushuhuda, Haruni na wanawe wataitengeza tangu jioni hadi asubuhi mbele ya BWANA; itakuwa ni amri ya milele katika vizazi vyao vyote kwa ajili ya wana wa Israeli.
Law 24:3–4Nje ya pazia lililoko mbele ya sanduku la maamzi ndani ya hema la kukutania, Aroni ataiwasha daima taa mbele za Yahweh, tangu asubuhi hata jioni. Hii itakuwa amri ya kudumu katika vizazi vyote vya watu wenu. Kuhani mkuu atazifanya taa ziwake daima mbele za Yahweh, taa hizo zilizo kwenye kinara cha dhahabu safi.
- Uvumba unafukizwa taa zinapotunzwa, asubuhi na jioniKut 30:7–8
Aya
Kut 30:7–8Na Aruni atafukiza uvumba wa manukato juu yake; kila siku asubuhi. Atakapozitengeneza zile taa, ataufukiza, na Aruni atakapoziwasha zile taa wakati wa jioni, ataufukiza, uwe uvumba wa daima mbele za Yahweh katika vizazi vyenu vyote.
- Taa zinawekwa ziangaze eneo lililo mbele ya kinaraHesabu 8:2–3
Aya
Hesabu 8:2–3“Sema na Haruni umwambie, 'zile taa saba lazima zimulike mbele ya kinara utakapoziwasha,” Haruni alifanya haya. Aliziwasha zile taa juu ya kinara ili ziangaze mbele yake kama BWANA alivyomwagiza Musa.
- Kinara kinasimama kuelekea meza, upande wa kusiniKut 40:24–25
Aya
Kut 40:24–25Alieka kinara cha taa kwenye hema la kukutania, upande wa pili wa meza, kusini mwa hema la kukutani. Aliwasha taa mbele za Yahweh, kama Yahweh alivyo muamuru.
- Safarini kinafunikwa kwa kitambaa cha samawatiHesabu 4:9
Aya
Hesabu 4:9Watachukua nguo ya rangi ya samawi na kukifunika kinara, pamoja na taa zake, na koleo zake, na sahani zake na vikombe vyake vya kuwekea mafuta ya taa.
- Samweli analala kabla taa ya Mungu haijazimika1 Sam 3:3
Aya
1 Sam 3:3Ile taa ya BWANA bado ilikuwa bado inawaka, na Samweli alikuwa amelala katika nyumba ya BWANA, palipokuwa na sanduku la Mungu.
- Sulemani anatengeneza vinara kumi vya dhahabu, vitano kila upande1 Fal 7:49, 2 Nya 4:7
Aya
1 Fal 7:49Vile vinara vya dhahabu, ambavyo vitano vilikuwa upande wa kulia na vitano mkono wa kushoto, mbele ya chumba cha ndani, vilikuwa vya dhahabu safi, na maua, na taa na koleo zilikuwa za dhahabu.
2 Nya 4:7Akatengeza vinara vya taa kumi vya dhahabu ambavyo vilitengenezwa kutokana na maelekezo ya jinsi vilivyopaswa kuwa; akaviweka hekaluni, vitanao mkno wa kulia, na vitano mkono wa kushoto.
- Taa za kinara cha dhahabu zinawashwa kila jioni2 Nya 13:11
Aya
2 Nya 13:11Kila asubuhi na jioni humtolea Yahwe sadaka za kuteketezwa na uvumba mtamu. Pia hupanga mkate wa uwepo juu ya meza takatifu; pia huweka kinara cha dhahabu pamoaja na taa zake, ili watoe sadaka kila jioni. sisi huzishika sheria za Yahwe, Mungu wetu, Lakini ninyi mmemsahau.
- Hezekia: baba zetu walifunga ukumbi wa hekalu na kuzima taa2 Nya 29:6–7
Aya
2 Nya 29:6–7Kwa kuwa babu zetu walikosea na kufanya kilichokuwa uovu katika macaho ya Yahwe Mungu wetu; walimsahau, wakageuzia mbali nyuso zao kutoka sehemu ambapo Yahwe anaishi, na kuigeuzia migongo yao. Pia waliifunga milango ya ukumbi nakuziweka nje taa; hawakufukiza uvumba au kutoa sadaka za kuteketezwa katika sehemu takatifu kwa Mungu wa Israeli.
- Wababeli wanachukua vinaraYer 52:19
Aya
Yer 52:19Makalai na chetezo cha uvumba, mabakuri, vyungu, kinara cha taa, vikaango, makalai zilizotengenezwa kwa dhahabu, na zilizotengenezwa kwa dhahabu - kapteni wa mlinzi wa mfalme akazichukua pia.
Nyumbani
- Watu huweka taa juu ya kinara, si chini ya pishi wala chini ya kitandaMt 5:15, Mk 4:21, Lk 8:16, Lk 11:33
Aya
Mt 5:15Wala watu hawawashi taa na kuweka chini ya kikapu, bali kwenye kinara, nayo yawaangaza wote walio ndani ya nyumba.
Mk 4:21Yesu akawaambia, “ Je huwa unaleta taa ndani ya nyumba na kuiweka chini ya kikapu, au chini ya kitanda? Huileta ndani na kuiweka juu ya kiango.
Lk 8:16Sasa, hakuna hata mmoja, anayewasha taa na kuifunika kwa bakuli au kuiweka chini ya kitanda. Badala ya kuiweka kwenye kinara cha taa ili kwamba kila mmoja anayeingia apate kuiona.
Lk 11:33Hakuna Mtu yeyote, awashaye taa na kuiweka sehemu ya chini yenye giza isiyoonekana au chini ya kikapu, ila huwasha na kuweka juu ya kitu ili kila mtu aingiaye aweze kuona mwanga.
- Mwanamke anawasha taa na kufagia nyumba kutafuta sarafu iliyopoteaLk 15:8
Aya
Lk 15:8Au kuna mwanamke gani mwenye sarafu kumi za fedha, akipotewa na sarafua moja, hata washa taa na kufagia nyumba na kutafuta kwa bidii hadi atakapoipata?
- Taa ya mke hodari haizimiki usikuMit 31:18
Aya
Mit 31:18Huangalia ni kipi kitaleta faida nzuri kwake; usiku wote taa yake haizimishwi.
- Maandishi yanatokea ukutani mwa jumba la kifalme karibu na kinaraDan 5:5
Aya
Dan 5:5Kwa wakati huo huo vidole vya mkono wa mtu vilionekana mbele ya kinara cha taa na kuandika katika ukuta uliopigwa lipu katika ikulu ya mfalme. Mfalme aliweza kuona sehemu ya mkono ulipokuwa unaandika.
- Taa nyingi katika chumba cha juu huko TroaMdo 20:8
Aya
Mdo 20:8Kulikuwa na taa nyingi katika chumba cha juu ambapo tulikuwa tumekusanyika pamoja.
- Wanawali kumi wenye taa; watano hawaleti mafuta ya ziada (mfano)Mt 25:1–8
Aya
Mt 25:1–8Ndipo ufalme wa mbinguni utafananishwa na wanawali kumi waliochukua taa zao na kuondoka kwenda kumpokea bwana harusi. Watano miongoni mwao walikuwa wapumbavu na watano wengine walikuwa werevu. Wanawali wapumbavu walipochukua taa zao, hawakuchukua mafuta yoyote. Bali wanawali welevu walichukua vyombo vyenye mafuta pamoja na taa zao. Sasa wakati bwana harusi amechelewa kufika, wote walishikwa usingizi na wakalala. Lakini wakati wa usiku wa manane kulikuwa na yowe, 'Tazama, bwana harusi! Tokeni nje mkampokee.' Ndipo hao wanawali waliamka wote na kuwasha taa zao. Wale wapumbavu waliwaambia wale welevu, 'Mtupatie sehemu ya mafuta yenu kwa sababu taa zetu zinazimika.'
Vyanzo
Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0