Bible Explorer

Gundua › Mada › Uzee

Maisha ya kila siku

Uzee katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (42), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

Misemo

  • Simama mbele ya wazee; waheshimu wazeeLaw 19:32
    Aya
    Law 19:32Ni lazima usimame mbele za mtu mwenye mvi na uheshimu uwepo wa mzee. Yakupasa umwegope Mungu wako. Mimi ndimi Yahweh.
  • Hekima hupatikana kwa wazeeAyu 12:12
    Aya
    Ayu 12:12Kwa wazee mna hekima; katika wingi wa siku mna ufahamu.
  • Mvi ni taji ya utukufuMit 16:31, Mit 20:29
    Aya
    Mit 16:31Mvi ni taji ya utukufu; hupatikana kwa kuishi katika njia ya haki.
    Mit 20:29Utukufu wa watu vijana ni nguvu zao na fahari ya watu wazee ni mvi zao.
  • Wajukuu ni taji ya wazeeMit 17:6
    Aya
    Mit 17:6Wajukuu ni taji ya wazee na wazazi huleta heshima kwa watoto wao.
  • Miaka sabini, au themanini tukiwa na nguvuZab 90:10
    Aya
    Zab 90:10Miaka yetu ni sabini, au themanini tukiwa na afya; lakini hata hivyo miaka yetu mizuri imetiwa alama ya taabu na huzuni. Ndiyo, inapita haraka, kisha tunatoweka.
  • “Usinitupe wakati wa uzee wangu”Zab 71:9, Zab 71:18
    Aya
    Zab 71:9Usinitupe katika siku za miaka ya uzee wangu; usiniache wakati nguvu zangu zitakapoisha.
    Zab 71:18Hakika, hata niwapo mzee na mvi kichwani, Mungu, usiniache mimi, kama ambavyo nimekuwa nikitanga nguvu yako kwa vizazi vijavyo, na uweza wako kwa yeyote ajaye.
  • Hata katika uzee watazaa matundaZab 92:14
    Aya
    Zab 92:14Wao huzaa matunda hata uzeeni; hukaa safi na wenye afya,
  • “Nilikuwa kijana na sasa ni mzee”Zab 37:25
    Aya
    Zab 37:25Nilikuwa kijana na sasa ni mzee; sijawahi kumuona mtu mwenye haki ametelekezwa wala watoto wake kuombaomba mkate.
  • “Hata uzeeni mwenu… hata mtakapokuwa na mvi nitawachukua”Isa 46:4
    Aya
    Isa 46:4Hata kwa njie wazee Mimi ndiye, mpaka mmeshapata mvi nitawachukua. Nimewaumba ninyi na nitawabeba ninyi; Nitwachukua nyie na nitawakomboa nyie.
  • Uzee unaelezwa: siku ambazo hutapata furaha ndani yakeMhu 12:1–5
    Aya
    Mhu 12:1–5Pia mkumbuke Muumba wako katika siku za za ujana, kabla ya siku za ugumu hazijaja, na kabla ya miaka haijafika utakapo sema, “Mimi sina furaha katika hizo,” fanya hivi kabla ya nuru ya jua na mwezi na nyota havijawa giza, na mawingu kurudi baada ya mvua. Huo utakuwa wakati ambapo mlinzi wa ikulu atatetemeka, na wanaume imara wameinama, na wanawake wanao saga kukoma, kwa sababu ni wachache, na wale wanao chungulia dirishani hawaoni vizuri tena. Huo utakuwa wakati ambao milango imefungwa katika mtaa, na mlio wa kusanga kukoma, wakati wanaume watasitushwa kwa mlio wa ndege, na wimbo wa sauti ya wasichana kukoma. Utakuwa wakati ambapo watu wataogopa vilivyoinuka na hatari iliyoko barabarani, na wakati ambapo mlozi utachanua maua, na wakati panzi watakapokokotana wenyewe, na wakati ambapo hamu za asili zitakaposhindwa. Kisha mtu aenda katika nyumba yake ya milele na waombolezaji watelemka mitaani.
  • Wazee wa kiume na wa kike wataketi mitaani mwa Yerusalemu, fimbo mkononiZek 8:4
    Aya
    Zek 8:4Yahwe wa majeshi asema hivi: Kwa mara nyingine tena kutakuwa na vikongwe katika mitaa ya Yerusalemu, na kila mtu ataitaji mkongojo mkononi mwake kwa vile alivyo mzee.
  • Utakapokuwa mzee, mwingine atakuvikaYn 21:18
    Aya
    Yn 21:18Amini, amini, nakuambia, ulipokuwa kijana ulizoea kuvaa nguo mwenyewe na kwenda kokote ulikotaka; lakini utakapokuwa mzee, utanyosha mikono yako, na mwingine atakuvalisha nguo na kukupeleka usikotaka kwenda.”
  • Wazee wa kiume na wazee wa kike kanisaniTit 2:2–3
    Aya
    Tit 2:2–3Wazee wawe na kiasi, heshima, busara, imani safi, katika upendo, na katika uvumilivu. Vilevile wanawake wazee lazima daima wajioneshe wao wenyewe kama wenye kujiheshimu, na sio wasengenyaji. Lazima wasiwe watumwa wa pombe.

Mifano

  • Abraham anaahidiwa uzee mwema na anakufa mzee, ameridhikaMwa 15:15, Mwa 25:8
    Aya
    Mwa 15:15Lakini utakwenda kwa baba zako kwa amani, na utazikwa katika uzee mwema.
    Mwa 25:8Abraham akapumua pumzi ya mwisho na akafa katika uzee mwema, mzee aliye shiba siku, na akakusanywa kwa watu wake.
  • Sara mzee anacheka kwa ahadi ya mwanaMwa 18:11–12, Mwa 21:7
    Aya
    Mwa 18:11–12Abraham na Sara walikuwa wazee, umri wao ulikuwa umeendelea sana, na Sara alikuwa amepita umri ambao mwanamke anaweza kuzaa watoto. Kwa hiyo Sara akajicheka mwenyewe, akijisemesha mwenyewe, “baada ya kuwa nimechakaa na bwana wangu ni mzee, je ni tapata furaha hii?”
    Mwa 21:7Pia akasema, “Nani angesema kwa Abraham kwamba Sara atalea mtoto, na sasa kweli nimemzalia mtoto wakiume katika uzee wake!”
  • Isaka, mzee na karibu kipofu, anamwita EsauMwa 27:1–2
    Aya
    Mwa 27:1–2Isaka alipozeeka na macho yake kuwa mazito kiasi cha kutokuona, alimwita Esau, mwanawe mkubwa, na akamwambia, “Mwanangu. Yeye akasema, “Mimi hapa.” Akamwambia, “Tazama, mimi nimezeeka. Sijui siku ya kufa kwangu.
  • Yakobo mbele ya Farao: “Safari zangu zimekuwa miaka 130”Mwa 47:9
    Aya
    Mwa 47:9Yakobo akamwambia Farao, “Miaka ya safari zangu ni mia moja na thelathini. Miaka ya maisha yangu imekuwa mifupi na ya maumivu. Siyo kama miaka ya baba zangu.”
  • Yakobo mzee haoni vizuri wana wa YusufuMwa 48:10
    Aya
    Mwa 48:10Basi macho ya Israeli yalikuwa yanashindwa kwa ajili ya umri wake, hivyo hakuweza kuona. Hivyo Yusufu akawasogeza karibu yake, na akawabusu na kuwakumbatia.
  • Musa akiwa na miaka 120: macho hayakufifia, nguvu hazikupunguaKum 34:7
    Aya
    Kum 34:7Musa alikuwa na umri wa miaka mia moja na ishirini alipokufa; macho yake hayakufifia, wala nguvu asili zake hazikupungua.
  • Kalebu akiwa na miaka themanini na mitano: “bado nina nguvu kama zamani”Yos 14:10–11
    Aya
    Yos 14:10–11Tazama! sasa, Yahweh amenihifadhi hai kwa miaka hii arobaini na tano, kama alivyosema - tangu kipindi kile Yahweh alivyomwambia Musa neno hili, wakati huo Waisraeli walikuwa wakitembea jangwani. Tazama! sasa katika siku hii ya leo nina miaka themanini na mitano. Bado hata siku hii ya leo nina nguvu kama nilivyokuwa katika siku ile ambayo Musa alinituma. Nguvu zangu za sasa ni sawa na nguvu zangu za kipindi kile, kwa ajili ya vita na kwa kwenda na kwa kuja.
  • Yoshua mzee anawaita Israeli woteYos 13:1, Yos 23:1–2
    Aya
    Yos 13:1Sasa Yoshua alikuwa mzee wakati Yahweh alipomwambia, “Umekuwa mzee, lakini bado kuna nchi kubwa ya kuteka.
    Yos 23:1–2Na baada ya siku nyingi, kipindi ambacho Yahweh alikuwa ameipa Israeli pumziko kutoka maadui zao waliowazunguka, Joshua alikuwa mzee sana. Yoshua aliwaita Waisraeli wote, na wazee wao, na viongozi, na waamuzi, na kwa maafisa, na kisha akawaambia, “Mimi nimezeeka sana.
  • Eli, mwenye miaka tisini na minane na mzito, anaanguka kitini1 Sam 4:15, 1 Sam 4:18
    Aya
    1 Sam 4:15Basi Eli alikuwa na umri wa miaka tisini na nane; macho yake yamepofuka, na hakuweza kuona.
    1 Sam 4:18Alipotamka sanduku la Mungu, Eli alianguka chali kutoka kwenye kiti chake karibu na mlango. akavunjika shingo lake, na kufariki, kwa sababu alikuwa mzee tena mzito. Naye alikuwa mwamuzi wa Israeli kwa miaka arobaini.
  • Samweli anazeeka na kuwaweka wanawe kuwa waamuzi1 Sam 8:1, 1 Sam 8:5
    Aya
    1 Sam 8:1Samweli alipozeeka, aliwaweka watoto wake wawe waamuzi juu ya Israeli.
    1 Sam 8:5Wakamwambia, “Angalia, wewe umekuwa mzee, na watoto wako hawaenendi katika njia zako. Tuchagulie mfalme wakutuamua kama yalivyo mataifa yote.”
  • Barzilai, mwenye miaka themanini, anakataa kwenda ikulu pamoja na Daudi2 Sam 19:32–37
    Aya
    2 Sam 19:32–37Basi Berzilai alikuwa mzee sana mwenye umri wa miaka themanini. Alikuwa amemsaidia mfalme kwa mahitaji alipokuwako Mahanaimu kwani alikuwa na mali nyingi. Mfalme akamwambia Berzilai, njoo pamoja nami, nami nitaandaa kwa ajili yako huko Yerusalemu.” Berzilai akamjibu mfalme, “Kwani kuna siku ngapi zilizosalia maishani mwangu, hata niende na mfalme huko Yerusalemu? Nina umri wa miaka themanini. Je naweza kutofautisha mema na mabaya? Je mtumishi wako anaweza kuonja ninachokula au kunywa? Je naweza kusikia sauti zaidi za wanaume na wanawake waimbao? Kwa nini basi mtumishi wako awe mzigo kwa bwana wangu mfalme? Mtumishi wako angependa tu kuvuka Yordani pamoja na mfalme. Kwa nini mfalme anilipe kwa thawabu kama hiyo? Tafadhari mruhusu mtumishi wako arudi nyumbani, ili kwamba nife katika mji wangu katika kaburi la baba na mama yangu. Lakini tazama, huyu hapa mtumishi wako Kimhamu. Haya yeye na avuke na bwana wangu mfalme na umfanyie lolote lipendezalo kwako.”
  • Mfalme Daudi mzee hapati joto hata chini ya mablanketi1 Fal 1:1–4
    Aya
    1 Fal 1:1–4Mfalme Daudi alipokuwa mzee sana, walimfunika kwa nguo, lakini hakupata joto. Kwa hiyo watumishi wake wakamwambia, “Na tutafute msichana bikra kwa ajili ya mfalme bwana wetu. Ili amtumikie na kumtunza. Naye atalala kwenye mikono yake ili bwana mfalme wetu apate joto. Kwa hiyo wakatafuta msichana mrembo katika mipaka yote ya Israeli. Wakampata Abishagi Mshunami wakamlte kwa mfalme. Yule msichana alikuwa mrembo sana. Naye akamtumikia mfalme na kumtunza, Lakini mfalme hakumjua.
  • Rehoboamu anakataa shauri la wazee1 Fal 12:6–8
    Aya
    1 Fal 12:6–8Mfalme Rehoboamu akatafuta ushauri kwa wazee waliokuwa wamesimama mbele ya Sulemani baba yake wakati wa uhai wake, naye akasema, “mnanishauri niwajibuje hawa watu?” Nao wakamwambia, “Kama wewe utakuwa mtumishi wa hawa watu na akawatumikia, na akawapa majibu ya maneno mema, ndipo watakapokuwa watumishi wako daima.” Lakini Rehoboamu akapuuzia ushauri aliopewa na wazee na akaenda kuomba ushauri kwa vijana ambao alikua pamoja nao wakasimama mbele yake.
  • Nabii Ahiya, macho yake yamefifia kwa uzee1 Fal 14:4
    Aya
    1 Fal 14:4Mke wa Yeroboamu akafanya hivyo; akaenda Shilo mpaka kwenye nyumba ya Ahiya. Wakati huo Ahiya alikuwa hawezi kuona, kwa kuwa macho yake yalikuwa yameishiwa nguvu kwa sababu ya umri wake.
  • Yehoyada anakufa akiwa na miaka 130, mzee na mwenye siku nyingi2 Nya 24:15
    Aya
    2 Nya 24:15Yehoyada akazeeka na alaaikuwa amejaa siku, na kisha akafa; alikuwa na umri wa mika 130 alipokufa.
  • Elihu anasubiri kunena kwa sababu wengine ni wazee kuliko yeyeAyu 32:6–7
    Aya
    Ayu 32:6–7Ndipo Elihu mwana wa Barakeli Mbuzi alinena na kusema, “Mimi ni mdogo, na ninyi ni wazee. Hii ndio sababu nilijizuia na sikuthubutu kuzungumza mawazo yangu mwenyewe. Nilisema, “Urefu wa siku utazungumza; na wingi wa miaka utatufundisha hekima.
  • Ayubu anaishi kuona vizazi vinneAyu 42:16–17
    Aya
    Ayu 42:16–17Baada ya haya, Ayubu aliishi miaka 140; aliwaona wana wake na wana wa wanawe, hata kizazi cha nne. Basi Ayubu alifariki, akiwa mzee na akijawa na siku nyingi.
  • Mjukuu wa Naomi atamtunza katika uzee wakeRut 4:15
    Aya
    Rut 4:15Na awe kwako mrutubishaji wa maisha na mwenye ruzuku uzeeni mwako, kwa kuwa mtoto wako mkwe, ambaye anakupenda, ambaye ni bora kwako kuliko watoto wa kiume saba, amemzaa.
  • Zakaria na Elizabeti, wote wawili wazee sanaLk 1:7, Lk 1:18
    Aya
    Lk 1:7Lakini hawakuwa na mtoto, kwasababu Elizabethi alikuwa tasa, na kwa wakati huu wote wawili walikuwa wazee sana.
    Lk 1:18Zakaria akamwambia malaika, “Nitawezaje kujua hili? Kwasababu mimi ni mzee na mke wangu miaka yake imekuwa mingi sana.”
  • Ana, mjane wa miaka themanini na minneLk 2:36–37
    Aya
    Lk 2:36–37Nabii mwanamke aliyeitwa Ana pia alikuwako hekaluni. Yeye alikuwa binti wa Fanueli kutoka kabila la Asheri. Alikuwa na miaka mingi sana. Naye aliishi na mume wake kwa miaka saba baada ya kuoana, na ndipo akawa mjane kwa miaka themanini na minne. Naye hakuwahi kuondoka hekaluni na alikuwa akiendelea kumwabudu Mungu pamoja na kufunga na kuomba, usiku na mchana.
  • Paulo: “Mimi Paulo, sasa ni mzee”Flm 1:9
    Aya
    Flm 1:9lakini kwa sababu ya upendo, badala yake nakusihi - mimi, Paulo niliye mzee, na sasa ni mfungwa kwa ajili ya Kristo Yesu.

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0