Maisha ya kila siku
Ndugu katika Biblia
Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (42), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.
- Abram anamwambia mpwa wake Lutu, “Sisi ni ndugu”Mwa 12:5, Mwa 13:8
Aya
Mwa 12:5Abram akamchukua Sarai mkewe, Lutu, mtoto wa ndugu yake, na vyote walivyomiliki ambavyo wamevikusanya, na watu ambao wamewapata wakiwa huko Harani. Wakatoka kwenda katika nchi ya Kanaani, wakafika nchi ya Kanaani.
Mwa 13:8Kwa hiyo Abram akamwambia Lutu, “Pasiwe na ugomvi kati yako na mimi, na kati ya wachunga wanyama wako na wachunga wanyama wangu; licha ya hayo sisi ni familia.
- Kaini anamuua Habili: “Je, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?”Mwa 4:8–9
Aya
Mwa 4:8–9Kaini akamwambia Habili ndugu yake. Hata wakati walipokuwa shambani, Kaini aliinuka dhidi ya Habili ndugu yake na akamuua. (Katika tafsiri za kale zinasema, Kaini alimwambia Habili ndugu yake, “ twende mashambani.” Na wakati walipokuwa shambani, Kaini alimuinukia Habili ndugu yake na kumuua). Kisha Yahwe akamuuliza Kaini, “Ndugu yako Habili yuko wapi?” Akasema, “sijui. Je mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?”
- Esau anamwuzia Yakobo haki yake ya mzaliwa wa kwanza kwa mchuziMwa 25:29–34
Aya
Mwa 25:29–34Yakobo akapika mchuzi. Esau akaja kutoka nyikani, akiwa dhaifu kutokana na njaa. Esau akamwambia Yakobo, “Nilishe mchuzi mwekundu. Tafadhari, nimechoka!” Na hii ndiyo sababu jina lake aliitwa Edomu. Yakobo akasema, “Kwanza uniuzie haki yako ya mzaliwa wa kwanza.” Esau akasema, “Tazama, nakaribia kufa. Ni nini kwangu haki ya mzaliwa wa kwanza?” Yakobo akasema, “Kwanza uape kwangu mimi,” kwa hiyo Esau akaapa kiapo na kwa njia hii akawa ameuza haki yake ya mzaliwa wa kwanza kwa Yakobo. Yakobo akampatia Esau mkate pamoja na mchuzi wa dengu. Akala na kunywa, kisha akainuka na akaenda zake. Kwa njia hii Esau akawa ameidharau haki yake ya mzaliwa wa kwanza.
- Esau anapanga kumuua Yakobo baada ya kifo cha baba yaoMwa 27:41
Aya
Mwa 27:41Esau akamchukia Yakobo kwa sababu ya baraka ambayo baba yake alimpa. Esau akajisemea moyoni, “Siku za maombolezo kwa ajili ya baba yangu zinakaribia; baada ya hapo nitamwua Yakobo ndugu yangu.”
- Yakobo anamwogopa Esau na watu wake mia nneMwa 32:6–7
Aya
Mwa 32:6–7Wajumbe wakarudi kwa Yakobo na kusema, “Tulikwenda kwa Esau ndugu yako. Anakuja kukulaki, na watu mia nne pamoja naye.” Ndipo Yakobo alipoogopa sana na kutaabika. Hivyo akagawanya watu aliokuwa nao katika kambi mbili, na kondoo pia, mbuzi na ngamia.
- Esau anakimbia kumkumbatia Yakobo, nao wanalia wote wawiliMwa 33:4
Aya
Mwa 33:4Esau akakimbia kumlaki, akamkumbatia, akakumbatia shingo yake na kumbusu. Kisha wakalia.
- Simeoni na Lawi wanamlipizia kisasi dada yao DinaMwa 34:25, Mwa 34:31
Aya
Mwa 34:25Katika siku ya tatu, walipokuwa katika maumivu bado, wawili wa wana wa Yakobo (Simoni na Lawi, kaka zake Dina), wakachukua kila mmoja upanga wake na kuushambulia mji ambao ulikuwa na uhakika wa ulinzi wake, nao wakauwa wanamme wote.
Mwa 34:31Lakini Simoni na Lawi wakasema, “Je Shekemu alipaswa kumtendea dada yetu kama kahaba?”
- Rubeni anajaribu kumwokoa Yusufu kutoka shimoniMwa 37:21–22, Mwa 37:29
Aya
Mwa 37:21–22Rubeni alilisikia hilo na kumwokoa kutoka katika mikono yao. Alisema, “Tusiuondoe uhai wake.” Rubeni aliwambia, “Msimwage damu. Mtupeni katika shimo hili lililopo nyikani, lakini msiweke mikono yenu juu yake” - ili kwamba aweze kumwokoa katika mikono yao na kumrudisha kwa baba yake.
Mwa 37:29Rubeni akarudi kwenye shimo, na, tazama, Yusufu hakuwemo shimoni. Akararua mavazi yake.
- Yuda: “Tumwuze … kwa maana ni ndugu yetu”Mwa 37:26–27
Aya
Mwa 37:26–27Yuda akawambia ndugu zake, “Ni faida gani kama tutamwua ndugu yetu na kufunika damu yake? Haya, na tumwuze kwa Waishmaeli na wala tusiweke mikono yetu juu yake. Kwani yeye ni ndugu yetu, nyama yetu.” Ndugu zake wakamsikiliza.
- “Watumishi wako ni ndugu kumi na wawili … na mmoja hayupo”Mwa 42:13
Aya
Mwa 42:13Wakasema, “Sisi watumishi wako tupo ndugu kumi na wawili, wana wa baba mmoja katika nchi ya Kanaani. Tazama, mdogo yupo na baba yetu, na mwingine hayupo hai tena.”
- Yusufu anaingia chumbani kulia anapomwona BenjaminiMwa 43:30
Aya
Mwa 43:30Yusufu akaharakisha kutoka chumbani, kwani aliguswa sana kuhusu nduguye. Akatafuta mahali pa kulia. Akaingia chumbani mwake na kulia umo.
- Yuda anajitolea kubaki mtumwa badala ya BenjaminiMwa 44:33–34
Aya
Mwa 44:33–34Kwa hiyo sasa, tafadhari mwache mtumishi wake akae kama mtumwa kwa bwana wangu badala ya kijana, na umwache kijana aende na ndugu zake. Kwa maana nitakwenda jinsi gani kwa baba yangu ikiwa kijana hayupo nami? Ninaogopa kuona mabaya yatakayompata baba yangu.”
- “Mimi ni Yusufu, ndugu yenu, mliyemwuza Misri!”Mwa 45:3–4
Aya
Mwa 45:3–4Yusufu akawambia ndugu zake, “Mimi ni Yusufu. Je baba yangu ni mzima bado? Ndugu zake hawakuweza kumjibu, kwani walitishwa na uwepo wake. Kisha Yusufu akawambia ndugu zake, “Nikaribieni, tafadhari.” Nao wakasogea. Akawambia, “Mimi ni Yusufu ndugu yenu, mliyemwuza Misri.
- Yusufu anamkumbatia Benjamini na kuwabusu ndugu zake woteMwa 45:14–15
Aya
Mwa 45:14–15Akaikumbatia shingo ya Benjamini ndugu yake na kulia, na Benjamini akalia shongoni mwake. Akawabusu ndugu zake wote na kulia kwa ajili yao. Baada ya hayo ndugu zake wakaongea naye.
- Yusufu: “Msigombane njiani!”Mwa 45:24
Aya
Mwa 45:24Hivyo akawaruhusu ndugu zake nao wakaondoka. Akawambia, “Angalieni msijemkagombana njiani.”
- Baada ya kifo cha Yakobo Yusufu anawatuliza ndugu zake walioogopaMwa 50:15–21
Aya
Mwa 50:15–21Nduguze Yusufu walipoona kwamba baba yao amekufa, wakasema, “Itakuwaje ikiwa Yusufu atatukasirikia na akataka kutulipa kikamilifu kwa ajili ya uovu tuliomtenda?” Hivyo wakamwagiza Yusufu, kusema, “Baba yako alitoa maelekezo kabla hajafa, kusema, 'Mwambieni hivi Yusufu, “Tafadhari samehe makosa ya ndugu zako na dhambi yao uovu waliokutenda.” Basi wasamehe watumishi wa Mungu wa baba yako.” Yusufu akalia walipomwambia. Ndugu zake pia wakaenda na kuinamisha nyuso zao mbele zake. Wakasema, “Tazama, sisi ni watumishi wako.” Lakini Yusufu akawajibu, “Msiogope, Je mimi ni badala ya Mungu? Lakini kwenu, mlikusudia kunidhuru, lakini Mungu alikusudia mema, kuhifadhi maisha ya watu wengi, kama mwonavyo leo. Hivyo basi msiogope. Nitawahudumia ninyi na watoto wenu wadogo.” Kwa njia hii aliwatia moyo na kuongea na mioyo yao kwa upole.
- Haruni atanena na watu kwa niaba ya ndugu yake MusaKut 4:14–16
Aya
Kut 4:14–16Kisha Yahwe akamkasirikia Musa. Akasema, “Vipi kuhusu Aroni kaka yako yule Mlawi? Najua ya kuwa anaweza kuongea vizuri. Hata hivyo, anakuja kukutana na wewe, na atakapokuona moyo wake utajawa na furaha. Wewe utaongea naye na utaweka maneno ya kusema kinywani mwake. Nami nitakiongoza kinywa chako na kinywa chake pia, nami nitaonesha ninyi nyote yawapasayo kutenda. Yeye ataongea na watu kwa niaba yako. Yeye atakuwa msemaji wako, na wewe utakuwa kama Mungu kwake.
- Abimeleki anawaua ndugu zake; mdogo kabisa, Yothamu, anajifichaAmu 9:5
Aya
Amu 9:5Abimeleki akaenda nyumbani kwa baba yake huko Ofra; na juu ya jiwe moja akawaua ndugu zake sabini, wana wa Yerubaali. Yotamu ndiye aliyebaki, mwana mdogo kabisa wa Yerubaali, kwa kuwa alijificha.
- Ndugu za Yeftha wanamfukuza kutoka nyumba ya baba yaoAmu 11:2–3
Aya
Amu 11:2–3Mke wa Gileadi pia alizaa wanawe wengine. Wana wa mkewe walipokua, walimlazimisha Yeftha aondoke nyumbani na kumwambia, “Huwezi kurithi chochote kutoka katika familia yetu. Wewe ni mwana wa mwanamke mwingine.” Basi Yeftha akaondoka toka kwa ndugu zake, akaishi katika nchi ya Tobu. Watu wasiokuwa na sheria waliungana na Yeftha na wakaja na kwenda pamoja naye.
- Wana wa Yese: Daudi ni wa saba1 Nya 2:13–15
Aya
1 Nya 2:13–15Yese akawa baba wa mzaliwa wake wa kwanza Eliabu, wa pili Abinadabu, wa tatu Shama. Nethaneli wa nne, Radai wa tano. Ozemu wa sita, na Daudi wa saba.
- Eliabu, mkubwa kabisa, anamkaripia ndugu yake Daudi1 Sam 17:28
Aya
1 Sam 17:28Kaka yake mkubwa Eliabu, alisikia wakati akisema na watu. Hasira ya Eliabu ikawaka moto dhidi ya Daudi, naye akamuuliza, “Kwa nini umekuja hapa? Wale kondoo wachache umewaacha na nani huko nyikani? Nakijua kiburi chako, na utundu wa moyo wako; maana umekuja hapa ili uweze kuona mapigano.”
- Yoabu, Abishai na Asaheli, wana watatu wa Seruya2 Sam 2:18
Aya
2 Sam 2:18Wana watatu wa Seruya walikuwepo pale: Yoabu, Abishai na Asaheli.
- Absalomu anamwua Amnoni kwa kumwaibisha dada yao Tamari2 Sam 13:22, 2 Sam 13:28–29
Aya
2 Sam 13:22Absalome hakusema chochote kwa Amnoni, kwa maana Absalome alimchukia kwa kile alichokifanya, kumdhalilisha Tamari, dada yake.
2 Sam 13:28–29Absalomu akawaamuru watumishi wake kusema, “Sikilizeni kwa makini. Amnoni atakapokuwa amelewa mvinyo, na nitakapowambia, 'Mpigeni Amnoni,' msiogope mwueni. Je siyo mimi niliyewamru? Mwe jasiri na hodari.” Hivyo watumishi wa Absalome wakamtendea Amnoni kama walivyoamriwa. Kisha wana wote wa mfalme wakainuka na kila mmoja akapanda nyumbu wake akakimbia.
- Sulemani anaamuru kaka yake Adoniya auawe1 Fal 2:22–25
Aya
1 Fal 2:22–25Mfalme Sulemani akamjibu mama yake, “Kwa nini unamwombea Adoniya huyo Abishagi Mshunami? Kwa nini usimwombee ufalme pia, kwa kuwa ni ndugu yangu mkubwa? - au kwa Abiathari kuhani, au Yoabu mwana wa Seruya?” Kisha mfalme Sulemani akaapa kwa BWANA, akisema, “Mungu wangu na anifanyie hivyo, na zaidi pia, kama Adoniya hajayasema haya kinyume na maisha yake. Sasa basi kama BWANA aishivyo, ambaye ndiye alinifanya mimi kuwepo na kunipa kiti cha enzi cha Daudi baba yangu, na ambaye amenifanyia nyumba kwa ahadi yake, hakika Adoniya lazima auawe leo.” Kwa hiyo mfalme Sulemani akamtuma Benaya mwana wa Yehoyada naye akamkuta Adoniya na kumwua.
- Yehoramu anawaua ndugu zake wote kwa upanga2 Nya 21:4
Aya
2 Nya 21:4Sasa Yehoramu alipokuwa ameinuka katika ufalme wa baba yake na kujiimarisha mwenyewe kama mfalme, akawaua ndugu zake wote kwa upanga, na pia viongizi wengine mbali mbali wa Israeli.
- Jozi mbili za ndugu wavuvi kando ya Bahari ya GalilayaMt 4:18, Mt 4:21
Aya
Mt 4:18Alipokuwa akitembea kandokando ya Bahari ya Galilaya, aliwaona ndugu wawili, Simoni aliyekuwa akiitwa Petro, na Andrea kaka yake, wakitega nyavu baharini, kwa kuwa walikuwa wavuvi wa samaki.
Mt 4:21Na Yesu alipokuwa akiendelea kutoka hapo aliwaona ndugu wawili wengine, Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana kaka yake. Walikuwa katika mtumbwi pamoja na Zebedayo baba yao wakishona nyavu zao. Akawaita,
- Andrea kwanza anampata ndugu yake Simoni na kumleta kwa YesuYn 1:40–42
Aya
Yn 1:40–42Mmoja wa wale wawili waliomsikia Yohana akiongea na kisha kumfuata Yesu alikuwa ni Andrea, ndugu yake Simoni Petro. Akamwona ndugu yake Simoni na akamwambia, “Tumempata Masihi” (ambayo inatafsiriwa Kristo). Akamleta kwa Yesu. Yesu akamtazama na akasema, “Wewe ni Simoni mwana wa Yohana” utaitwa Kefa,” (maana yake 'Petro').
- Martha na Mariamu: “Ndugu yangu asingalikufa”Yn 11:21, Yn 11:32
- Ndugu za Yesu: Yakobo, Yose, Yuda na SimoniMk 6:3
Aya
Mk 6:3“Je huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu na ndugu yao kina Yakobo, Yose, Yuda na Simioni? Je dada zake si wanaishi papa hapa pamoja nasi?” Na hawakufurahishwa na Yesu.
- Ndugu zake hawakuamini, lakini baadaye waliomba pamoja na wanafunziYn 7:5, Mdo 1:14
Katika Sheria na misemo
- Usimchukie ndugu yako moyoni mwakoLaw 19:17
Aya
Law 19:17Usimchukie ndugu yako moyoni mwako. Mkemee jirani yako kwa heshima ili kwamba usishiriki katika dhambi kwa sababu yake.
- Mrudishie ndugu yako ng’ombe au kondoo wake aliyepoteaKum 22:1–2
Aya
Kum 22:1–2Hautakiwi kumtazama ng’ombe au kondoo wa Muisraeli mwenzako akikosea njia na ukajificha kwao; hakika unapaswa kuwarejesha kwake. Iwapo Muisraeli mwenzako hayupo karibu nawe, au kama haumfahamu, basi unapaswa kumleta mnyama huyo nyumbani kwako, na lazima uwe naye mpaka pale mwenyewe atakapomtafuta, na kisha lazima umrejeshee mwenyewe.
- Ni vyema jinsi gani ndugu wakaapo pamoja kwa umojaZab 133:1
Aya
Zab 133:1Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu, wa Daudi. Tazama, jinsi ilivyo vema na yakupendeza ndugu waishi pamoja, kwa umoja!
- Ndugu aliyekosewa ni mgumu kumpata kuliko mji wenye ngomeMit 18:19
Aya
Mit 18:19Ndugu aliyechukizwa ni mgumu kushawishiwa kuliko mji wenye nguvu, na kugombana ni kama makomeo ya ngome.
- Kwanza patana na ndugu yako, kisha utoe sadaka yakoMt 5:23–24
Aya
Mt 5:23–24Hivyo kama unatoa sadaka yako katika madhabahu na unakumbuka kuwa ndugu yako ana jambo lolote dhidi yako, iache sadaka mbele ya madhabahu, kisha shika njia yako. Kapatane kwanza na ndugu yako, na kisha uje kuitoa sadaka yako.
Vyanzo
Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0