Gundua › Mada › Urithi na wosia
Maisha ya kila siku
Urithi na wosia katika Biblia
Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (39), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.
Mifano
- Abram asiye na mtoto: mtumishi, Eliezeri wa Dameski, atakuwa mrithi wanguMwa 15:2–3
Aya
Mwa 15:2–3Abram akasema, “Bwana Yahwe, utanipatia nini, kwa kuwa naenda bila mtoto, na mrithi wa nyumba yangu ni Eliezeri wa Dameski?” Abram akasema, “Kwakuwa hujanipatia uzao, tazama, mwangalizi wa nyumba yangu ndiye mrithi wangu.”
- Sara: mwana wa mjakazi hatarithi pamoja na IsakaMwa 21:10
Aya
Mwa 21:10Kwa hiyo akamwambia Abraham, “Mfukuze huyu mwanamke huyu mtumwa pamoja na mtoto wake: kwa kuwa mtoto huyu wa mwanamke mtumwa hawezi kuwa mrithi pamoja na mwanangu Isaka.”
- Abraham anampa Isaka vyote na kuwaondoa wana wa masuria kwa zawadiMwa 24:36, Mwa 25:5–6
Aya
Mwa 24:36Sara, mke wa bwana wangu, alimzalia mwana bwana wangu alipokuwa mzee, na amempatia mwanawe kila kitu anachomiliki.
Mwa 25:5–6Abraham akampatia Isaka vitu vyote alivyokuwa navyo. Ingawaje, wakati alipokua angali akiishi, aliwapatia zawadi wana wa masuria wake na kuwapeleka katika nchi ya mashariki, mbali na Isaka, mwanae.
- Raheli na Lea: “Je, bado tuna urithi wowote katika nyumba ya baba yetu?”Mwa 31:14–16
Aya
Mwa 31:14–16Raheli na Lea wakajibu na kumwambia, “Je kuna sehemu yoyote au urithi wetu katika nyumba ya baba yetu? Je hatutendei kama wageni? Kwa maana ametuuza na kwa ujumla ametapanya pesa zetu. Mali zote ambazo sasa Mungu amemnyang'anya baba yetu ni zetu na watoto wetu. Sasa basi, lolote Mungu alilokuambia, fanya.
- Yakobo anampa Yusufu sehemu ya nchi zaidi ya ndugu zakeMwa 48:21–22
Aya
Mwa 48:21–22Israeli akamwambia Yusufu, “Tazama, ninakaribia kufa, lakini Mungu atakuwa nanyi, na atawarudisha katika nchi ya baba zenu. Kwako wewe, kwa kuwa uko juu ya ndugu zako, ninakupa mtelemko wa mlima niliouchukuwa kutoka kwa Waamori kwa upanga wangu na upinde wangu.”
- Haki ya mzaliwa wa kwanza ya Rubeni inapita kwa wana wa Yusufu1 Nya 5:1–2
Aya
1 Nya 5:1–2Wana wa Rubeni mzaliwa wa kwanza wa Israeli - sasa Rubeni alikuwa mzaliwa wa kwanza wa Israeli, lakini haki yake ya mzaliwa wa kwanza ilipewa kwa wana wa Yusufu mwana wa Israeli kwa sababu Rubeni alinajisi kochi la baba yake. Hivyo hajanakiliwa kama mwana wa kwanza. Yuda alikuwa mwenye nguvu kuliko kaka zake, na kiongozi ata toka kwake. Lakini haki ya mzaliwa wa kwanza ilikuwa ya Yusufu -
- Binti za Zelofehadi wanapokea nchi kati ya ndugu za baba yaoHesabu 27:1–4, Yos 17:3–4
Aya
Hesabu 27:1–4Kisah wakaja kwa Musa binti wa Zelofehadi mwana wa Hefa mwana wa Gilied mwana wa Machiri mwana wa Manase, wa ukoo wa Manase mwana wa Yusufu. Hawa ndio waliokuwa binti zake: Mahala, Noha, Hogla, Milika, na Tiriza. Walisimama mbele ya Musa, Eliazari kuhani, kwa. viongozi, na mbele ya watu wote langoni mwa hema ya kukutania. Walisema, “Baba yetu alifia jangwani. Hakuwa mmoja wa wale waliompinga BWANA katika lile kundi la Kora. Alikufa kwa dhambi zake, na hakuwa na watoto wa kiume. Kwa nini jina la baba yetu liondolewe mioingoni mwa ukoo wa jamaa zake kwa sababu ya kukosa wana? Tupeni ardhi miongoni mwa ndugu wa baba zetu.”
Yos 17:3–4Basi Zelofehadi mwana wa Heferi mwana wa Gileadi mwana wa Makiri mwana wa Manase hakuwa na watoto wa kiume, bali alikuwa na watoto wa kike tu. Na majina ya binti zake yalikuwa Mahila, Noa, Hogla, Milka na Tirsa. Walimwendea Eliazeri kuhani, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi na wakasema, “Yahweh alimwagiza Musa atupatie urithi wetu pamoja na kaka zetu.” Hivyo, kwa kuzingatia agizo la Yahweh, aliwapa wanawake hao urithi miongoni mwa ndugu za baba yao.
- Yeftha ananyimwa urithi kama mwana wa mwanamke mwingineAmu 11:2
Aya
Amu 11:2Mke wa Gileadi pia alizaa wanawe wengine. Wana wa mkewe walipokua, walimlazimisha Yeftha aondoke nyumbani na kumwambia, “Huwezi kurithi chochote kutoka katika familia yetu. Wewe ni mwana wa mwanamke mwingine.”
- Boazi ananunua shamba la Elimeleki ili kulihifadhi jina la marehemuRut 4:5–6, Rut 4:9–10
Aya
Rut 4:5–6Kisha Boazi akasema, “Ile siku utakayonunua shamba kutoka mkononi mwa Naomi, yakupasa pia kumchukua Ruth Mmoabu, mjane wa mtoto wa Elimeleki, ili kuliinua jina la marehemu kama urithi wake.” Ndipo yule jamaa wa karibu akasema, “Mimi siwezi kuikomboa ardhi kwa ajili yangu bila kuleta athari kwenye urithi wangu binafsi. Nakupa wewe haki ya kuikomboa kwa ajili yako mwenyewe, kwa kuwa mimi sitoweza.”
Rut 4:9–10Ndipo Boazi akawaambia viongozi na watu wote, “Ninyi ni mashaidi kuwa nimenunua kila kilichokuwa cha Elimeleki na kila kilichokuwa na Kileoni na Mahilon kutoka kwenye mikono ya Naomi. Zaidi ya hayo kumhusu Ruth Mmoabu, mke wa Mahlon: nimempa kibali cha kuwa mke wangu, ili kuendeleza jina na urithi wa marehumu, ili kwamba jina lake lisipotee kati ya ndugu zake na lango la watu wake. Ninyi ni mashahidi leo.”
- Nabothi hataki kuuza urithi wa baba zake1 Fal 21:2–3
Aya
1 Fal 21:2–3Ahabu akamwambia Nabothi, akisema, “Nipe shamba lako, ili nilifanye kuwa bustani ya mboga, kwa sababu iko karibu na nyumba yangu. Badala yake nitakupa shamba zuri la mizabibu, au, kama ukipenda nitakulipa thamani yake kwa fedha.” Nabothi akamjibu Ahabu, “BWANA na alizuie hilo nisije nikatoa urithi wa mababu zangu kwako.”
- Yehoshafati anawapa wanawe zawadi na miji, ufalme kwa mzaliwa wa kwanza2 Nya 21:3
Aya
2 Nya 21:3Baba yao alikuwa amewapa zawadi kubwa ya fedha, dhahabu, na vitu vingine vya thamani, na miji yenye ngome katika Yuda, lakini kiti cha enzi alimpa Yehoramu, kwa sababu alikuwa mzaliwa wake wa kwanza.
- Ayubu anawapa binti zake urithi kati ya ndugu zaoAyu 42:15
Aya
Ayu 42:15Katika nchi yote hawakupatikana wanawake wazuri kama mabinti wa Ayubu. Baba yao aliwapa urithi miongoni mwa kaka zao.
- Yeremia ananunua shamba la binamu yake kwa haki ya ukomboziYer 32:7–8
Aya
Yer 32:7–8“Linunue shamba langu ambalo liko katika Anathothi kwa ajili yako, kwa maana haki ya kununua ni yako.”” Kisha, kama Yahwe alivyotangaza, Hanameli, mwana wa mjomba wangu, akaja kwangu katika uwanja wa walinzi, na akasema kwangu, 'Linunue shamba langu kwa ajili yako ambalo liko Anathothi katika nchi ya Benyamini, kwa maana haki ya urithi ni ya kwako, na haki ya kulinunua ni yako. Linunue kwa ajili yako.' Kisha nilijua kuwa hili lilikuwa neno la Yahwe.
- “Mwalimu, mwambie ndugu yangu agawane urithi nami”Lk 12:13
Aya
Lk 12:13Mtu mmoja katika kusanyiko akamwambia, “Mwalimu, mwambie ndugu yangu anigawie sehemu ya uruthi wangu.”
- Mwana mdogo anaomba fungu lake la mali (mfano)Lk 15:12–13
Aya
Lk 15:12–13yule mdogo akamwambia babaye, Baba nipe sehemu ya mali inayonistali kuirithi. Hivyo akagawanya mali zake kati yao. Siku si nyingi yule mdogo akakusanya vyote anavyomiliki akaenda nchi ya mbali, na huko akatapanya hela zake, kwa kununua vitu asivyo vihitaji, na kutapanya fedha zake kwa anasa.
- Wapangaji wanapanga kumuua mrithi na kuchukua urithi (mfano)Mk 12:7
Aya
Mk 12:7Lakini wapangaji walisemezana wao kwa wao, “Huyu ndiye mrithi. Njoni, hebu na tumwue, na urithi utakuwa wetu.”
Katika Sheria
- Bila mwana: kwa binti, kisha ndugu, wajomba, jamaa wa karibu zaidiHesabu 27:8–11
Aya
Hesabu 27:8–11Utawaambia wana wa Israeli na kusema, 'Kama mtu anakufa na hana mtoto wa kiume, basi utaufanya urithi wake wapewe binti zake. Kama hana binti, basi urithi wake atapewa kaka zake. Kama hana kaka zake basi huo urithi watapewa ndugu wa baba yake. Kama baba yake hana ndugu, basi huo urithi atapewa ndugu yake wa karibu katika ukoo, na utauchukua kuwa wake. Hii itakuwa sheria iliyoanzishwa kwa amri kwa ajili ya watu wa Israeli kama BWANA akivyoniamuru.”
- Mzaliwa wa kwanza wa mke asiyependwa bado anapata sehemu mara mbiliKum 21:15–17
Aya
Kum 21:15–17Iwapo mwanamume ana wake wawili na mmoja wao ampenda na mwingine kumchukia, na wote wamekwisha mzalia watoto –wote mwanamke mpendwa na mwanamke achukiwae – basi katika siku ambayo mwanamume atakapowarithisha mali zake wanawe, hapaswi kumfanya mwana wa mke ampendaye kuwa mzawa wa kwanza kabla ya mwana wa mke amchukiaye, ambaye ndiye mwana wa kwanza. Badala yake, anapaswa kumtambua mwana wa kwanza, mwana wa mke asiyempenda, kwa kumpatia mara mbili ya mali zake; kwa maana huyo mwana ni mwanzo wa nguvu zake; haki za mzawa wa kwanza ni zake.
- Nchi ya urithi isihame kutoka kabila moja hadi jingineHesabu 36:7–9
Aya
Hesabu 36:7–9Hakuna mgawo wa watu utakaobadilika kutoka kabila moja kwenda jingine. Kila mtu wa Israeli ataendelea na mgawo wa kabila ya baba y ake. Kila mwanamke wa watu wa Israeli aliye na mgao kwenye kabila lake lazima aolewe na mtu wa ukoo unaotoka kwenye kabila la baba yake. Hii itafanyika hivyo ili kila mtu wa wana wa Israeli aweze kuwa na urithi kutoka kwa mababa zake. Hakuna mgawo utakaobadilika kutoka kabila nyingine kwenda kabila nyingine. Kila mtu wa kabila za watu wa Israeli atalinda urithi wake.”
- Nchi inagawanywa kwa kura, zaidi kwa makabila makubwaHesabu 26:53–55
Aya
Hesabu 26:53–55Ile ardhi itagawanywa kati ya wanaume hawa kama urithi wao kwa kufuata idadi ya majina yao. Kwa zile koo kubwa utawagawia urithi mkubwa, na kwa koo ndogo ndogo utawagawia urithi kidogo. Kwa kila familia utawapa urithi kufuata idadi ya wanaume waliohesabiwa. Lakini ardhi itagawiwa kwa kupigiwa kura. Watairithi nchi kama itakavyogawiwa kwa kufuata koo za mababu.
- Haruni anaambiwa hatakuwa na urithi katika nchiHesabu 18:20
Aya
Hesabu 18:20BWANA akasema na Haruni. “hautakuwa na urithi katika ardhi ya watu, wala hautakuwa na gawio miongoni mwa watu. Mimi ndimi gawiio lenu na urithi wenu miongoni mwa watu wa Israeli.
- Zawadi ya mkuu kwa mtumishi inarudi katika mwaka wa uhuruEze 46:16–17
Aya
Eze 46:16–17Bwana Yahwe asema hivi: Kama mwana wa mfalme akitoa zawadi kwa mmoja wa watoto wake, imekuwa urithi wake. Itakuwa mali ya mtoto wake, imekuwa urithi. Lakini kama akimpatia zawadi kutoka urithi wake kwa mmoja wa watumishi wake, kisha itakuwa ya huyo mtumishi mpaka mwaka wa uhuru, na kisha itarudi kwa mwana wa mfalme. Urithi wake yamkini ukawa kwa ajili ya watoto wake.
Matakwa ya mwisho
- Yakobo anapishanisha mikono yake na kumtanguliza Efraimu mbele ya ManaseMwa 48:13–14, Mwa 48:19–20
Aya
Mwa 48:13–14Yusufu akawachukua wote wawili, Efrahimu katika mkono wake wa kulia kuelekea mkono wa kushoto wa Israeli, na Manase katika mkono wake wa kulia kuelekea mkono wa kulia wa Israeli, na akawasogeza kwake. Israeli akainua mkono wake wa kulia na kuuweka juu ya kichwa cha Efrahimu, aliyekuwa mdogo, na mkono wake wa kushoto juu ya kichwa cha Manase. Akaipishanisha mikono yake, kwani Manase ndiye alikuwa mzaliwa wa kwanza.
Mwa 48:19–20Baba yake akakataa na kusema, “Ninafahamu, mwanangu, nafahamu. Yeye naye atakuwa watu, naye pia atakuwa mkuu. Lakini mdogo wake atakuwa mkuu kuliko yeye, na uzao wake utakuwa wingi wa mataifa.” Israeli akawabariki siku hiyo kwa maneno haya, “Watu wa Israeli watatamka baraka kwa majina yenu wakisema, Mungu na akufanye kama Efrahimu na kama Manase'. “Kwa njia hii, Israeli akamweka Efrahimu mbele ya Manase.
- Yakobo anawakusanya wanawe na kumbariki kila mmoja kabla ya kufaMwa 49:1, Mwa 49:28, Mwa 49:33
Aya
Mwa 49:1Kisha Yakobo akawaita wana wake, na kusema: “Jikusanyeni pamoja, ili niwaambie yatakayowapata nyakati zijazo.
Mwa 49:28Haya ni makabila kumi na mbili ya Israeli. Hiki ndicho baba yao alichowambia alipowabariki. Aliwabariki kila mmoja kwa baraka iliyomstahili.
Mwa 49:33Yakobo alipomaliza maagizo hayo kwa wanawe, akaiweka miguu yake kitandani, akakata roho, akawaendea watu wake
- Agizo la mwisho la Daudi kwa Sulemani1 Fal 2:1–3
Aya
1 Fal 2:1–3Daudi alipokaribia kufa, alimwamuru Sulemani mwanae, akisema, “Mimi sasa ninaiendea njia ya dunia yote. Kwa hiyo, uwe imara, na ujionyeshe mwenyewe kama mwanamume. Uzilinde amri za BWANA, Mungu wako ukitembea katika njia zake, utii maaagizo yake, amari zake, maamuzi yake, na maagizo ya maagano yake, uwe mwamngalifu kufanya yale yaliyoandikwa katika sheria za Musa, ili ufanikiwe katika yote utakayoyafanya, popote kule utakakokuwa,
- Isaya kwa Hezekia: “Itengeneze nyumba yako”2 Fal 20:1
Aya
2 Fal 20:1Katika siku hizo Hezekia aliugua akawa kwenye hatari ya kufa. Hivyo Isaya mwana wa Amozi, akaja, na kumwambia, “Yahwe asema, 'Weka nyumba yako kwenye mpangilio; kwa kuwa utakufa, na hutapona.'”
- Wosia una nguvu tu baada ya kifo cha aliyeuandikaEbr 9:16–17
Aya
Ebr 9:16–17Kama kuna agano linadumu, ni lazima kuthibitishwa kwa kifo cha mtu yule aliyelifanya. Kwani agano linakuwa na nguvu mahali kunatokea mauti, kwa sababu hakuna nguvu wakati mwenye kulifanya akiwa anaishi.
- Agano la kibinadamu lililothibitishwa haliwezi kubatilishwa wala kubadilishwaGal 3:15
Aya
Gal 3:15Ndugu, ninazungumza kwa namna ya kibinadamu. Hata wakati ambapo agano la kibinadamu limekwisha kuwekwa imara, hakuna awezaye kupuuza au kuongezea.
- Mrithi aliye mtoto yuko chini ya walezi na wasimamiziGal 4:1–2
Aya
Gal 4:1–2Ninasema kwamba maadamu mrithi ni mtoto, hana tofauti na mtumwa, hata ingawa ni mmiliki wa mali yote. Badala yake, yuko chini ya waangalizi na wadhamini mpaka wakati uliowekwa na baba yake.
Misemo
- Mtumishi mwenye hekima atashiriki urithi kama mmoja wa nduguMit 17:2
Aya
Mit 17:2Mtumishi mwenye busara atatawala juu ya mwana atendaye kwa aibu na atashiriki urithi kama mmoja wa ndugu.
- Mali iliyopotea katika biashara mbaya haimwachii mwana chochoteMhu 5:13–14
Aya
Mhu 5:13–14Kuna jambo baya zaidi ambalo nimeliona chini ya jua: mali iliyowekwa akiba na mwenye nayo, inamsababishia taabu mwenyewe. Wakati tajiri anapopoteza utajiri wake kwa bahati mbaya, mwana wake, ambaye amemzaa, habakiziwi chochote mikononi mwake.
- Nyumba na mali hurithiwa kutoka kwa babaMit 19:14
Aya
Mit 19:14Nyumba na utajiri ni urithi kutoka kwa wazazi, bali mke mwenye busara hutoka kwa Yehova.
- Ni nani ajuaye kama mrithi wangu atakuwa mwenye hekima au mpumbavu?Mhu 2:18–19
Aya
Mhu 2:18–19Nikachukia yote niliyoyatimiza, ambayo nilikuwa nimekwisha yafanya chini ya jua kwa sababu ni lazima niyaache kwa mtu anaye kuja baada yangu. Na ni nani ajuaye kama atakuwa mwenye hekima au mpumbavu? Ila atakuwa msimamizi juu ya kila kitu chini ya jua ambayo kazi yangu na hekima yangu imeyajenga. Huu pia ni mvuke.
Vyanzo
Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0