Maisha ya kila siku
Kucheza ngoma katika Biblia
Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (21), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.
- Miriamu na wanawake wanacheza kwa matari baada ya kuvuka bahariKut 15:20
Aya
Kut 15:20Miriamu nabii wa kike, dada wa Aruni, akanyanyua tari, na wanawake wote wakatoka na matari, wakicheza nae.
- Musa anaona ndama na watu wakichezaKut 32:19
Aya
Kut 32:19Hata alipoyakaribia kambini akaiona ile ndama, na watu wakicheza. Hasira ya Musa ikawaka. Akazitupa zile mbao mikononi mwake, akazivunja chini ya mlima.
- Binti wa Yeftha anatoka kumlaki akichezaAmu 11:34
Aya
Amu 11:34Yeftha alifika nyumbani kwake huko Mizpa, na binti yake akatoka kumlaki na ngoma na kucheza. Alikuwa mtoto wake pekee, na badala yake hakuwa na mwana wa kiume wala binti.
- Binti za Shilo wanacheza kwenye sikukuu ya kila mwakaAmu 21:19–21
Aya
Amu 21:19–21Wakasema, “Mnajua kuwa kuna sikukuu kwa Bwana kila mwaka huko Shilo (ambayo ni kaskazini ya Betheli, mashariki ya barabara inayopanda kutoka Betheli hadi Shekemu, na kusini mwa Lebona). Wakawaagiza wana wa Benyamini, wakisema, “Nendeni, mjifiche kwa siri, na kusubiri katika mashamba ya mizabibu. Tazama wakati ambapo wasichana kutoka Shilo watatoka kucheza, Tokeni nje ya mizabibu na kila mmoja wenu anapaswa kunyakua mke kutoka kwa wasichana wa Shilo, kisha kurudi kwenye nchi ya Benyamini.
- Wanawake wanacheza na kuimba: “Sauli ameua maelfu yake”1 Sam 18:6–7, 1 Sam 21:11
Aya
1 Sam 18:6–7Wakati wanarudi nyumbani kutoka kuwapiga Wafilisti, wanawake walitoka miji yote ya Israeli, wakiimba na kucheza, ili kukutana na mfalme Sauli, wakiwa na matowazi, wenye furaha, na wakiwa na ala za muziki. Hao wanawake waliimba kwa kupokezana huku wakicheza; Wakiimba: “Sauli ameua maelfu yake, Na Daudi ameua makumi elfu yake.”
1 Sam 21:11Mtumishi wa Akishi akamwambia, “huyu siye Daudi mfalme wa nchi hii? Je, wanawake hawakupokezana wakiimba na kucheza, 'Sauli ameua maelfu yake, na Daudi makumi elfu yake?”'
- Daudi anacheza kwa nguvu zake zote mbele ya sanduku2 Sam 6:14–16
Aya
2 Sam 6:14–16Daudi akacheza mbele ya Yahwe kwa nguvu zake zote; alikuwa amevaa naivera ya kitani pekee. Hivyo Daudi na nyumba yote ya Israeli wakalipandisha sanduku la Yahwe kwa vifijo na sauti za tarumbeta. Hata ikawa sanduku la Yahwe lilipofika mjini mwa Daudi, Mikali, binti Sauli, alichungulia dirishani. Akamwona mfalme Daudi akiruka na kucheza mbele ya Yahwe. Akamdharau moyoni mwake.
- Mikali anamwona Mfalme Daudi akicheza na kumdharau1 Nya 15:29
Aya
1 Nya 15:29Lakini sanduku la Yahweh lilivyokuja kwa mji wa Daudi, Mikali binti wa Sauli, alitazama nje ya dirisha, Akamuona Mfalme Daudi akicheza na kusherehekea. Kisha akamdharau moyoni mwake.
- Watoto wanarukaruka kwa sauti ya matari na kinubiAyu 21:11–12
Aya
Ayu 21:11–12Wanawapeleka wadogo wao kama kundi la kondoo, na watoto wao hucheza. Wanaimba kwa tari na vinubi na hufurahi kwa muziki na zomari.
- “Umegeuza maombolezo yangu kuwa kucheza”Zab 30:11
Aya
Zab 30:11Wewe umegeuza kuomboleza kwangu kuwa kucheza; wewe umeyaondoa mavazi yangu ya magunia na kunivisha furaha.
- Msifuni kwa matari na kuchezaZab 149:3, Zab 150:4
- Wakati wa kuomboleza na wakati wa kuchezaMhu 3:4
Aya
Mhu 3:4Kuna wakati wa kulia na wakati wa kucheka, wakati wa kuomboleza na wakati kucheza,
- “Ngoma ya Mahanaimu”Wim 6:13
Aya
Wim 6:13Geuka nyuma, geuka nyuma, wewe mwanamke mkamilifu; geuka nyuma, geuka nyuma iliniweze kukushangaa. Mwanamke mdogo akizungumza na mpenzi wake Kwanini wanishangaa, mwanamke mkamilifu, kana kwamba nina cheza katika ya mistari miwili ya wachezaji?
- Wanawali wanafurahi kwa kucheza, vijana na wazee piaYer 31:4, Yer 31:13
Aya
Yer 31:4Nitakujenga tena kwa hiyo utakuwa umejengwa, bikra wa Israeli..... na kwenda nje michezo ya furaha.
Yer 31:13Kisha wanawali watafurahia kwa kucheza, na vijana na wanaume wazee watakuwa pamaoja. Kwa maana nitayageuza maombolezo yao kuwa sherehe. Nitakuwa na huruma juu yao na kuwafanya kufurahi badala ya kuhuzunika.
- “Kucheza kwetu kumegeuka kuwa maombolezo”Omb 5:15
Aya
Omb 5:15Furaha ya moyo imekoma na kucheza kwetu kumegeuka kilio.
- Watoto sokoni: “Tuliwapigia filimbi, nanyi hamkucheza”Mt 11:17
Aya
Mt 11:17na kusema, 'Tuliwapigia zomari na hamkucheza. Tuliomboleza, na hamukulia.'
- Muziki na kucheza kwa ajili ya mwana anayerudiLk 15:25
Aya
Lk 15:25Basi yule mwanae mkubwa alikuwako shamba. Alipokuwa akija na kuikaribia nyumba alisikia sauti ya nyimbo na michezo.
- Binti wa Herodia anacheza katika karamu ya kuzaliwa kwa HerodeMt 14:6–7, Mk 6:22
Aya
Mt 14:6–7Lakini wakati siku ya kuzaliwa Herode ilipofika binti wa Herodia alicheza katikati ya watu na kumpendeza Herode. Katika kujibu kili aliahidi kwa kiapo kwamba atampa chochote atakachoomba.
Mk 6:22Ndipo binti wa Herodia akaingia na kucheza mbele yao, akamfurahisha Herode na wageni walioketi wakati wa chakula cha jioni. Ndipo mfalme akamwambia binti, “Niombe chochote unachotaka nami nitakupa.”
Vyanzo
Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0