Gundua › Mada › Mazishi na makaburi
Maisha ya kila siku
Mazishi na makaburi katika Biblia
Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (42), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.
- Wafu walizikwa haraka, mara nyingi siku ileileKum 21:23, Mdo 5:6, Mdo 5:10
Aya
Kum 21:23basi mwili wake haupaswi kubaki usiku kucha juu ya mti. Badala yake, unapaswa kuhakikisha unamzika siku hiyo; kwa maana yeyote anyongwaye amekwisha laaniwa na Mungu. Tii amri hii ili kwamba usitie najisi nchi ambayo Yahwe Mungu wako anawapatia kama urithi.
Mdo 5:6Vijana wakaja mbele na kumtia katika sanda, na kumpeleka nje na kumzika.
Mdo 5:10Ghafla akadondoka miguuni pa Petro, akakata roho, na wale vijana wakaja ndani wakamkuta ameshakufa. Wakambeba kumpeleka nje, na kumzika karibu na mmewe.
- Manukato yalichomwa kwa heshima ya wafalme waliokufaYer 34:5
Aya
Yer 34:5Utakufa katika amani. Kama kwenye mafukizo ya babu zako, wafalme waliokuwepo kabla yako, watauchoma mwili wako. Watasema, 'Ole, bwana!” Watakuomboleza. Sasa nimesema—hili ni tangazo la Yahwe.”
- Mfalme Daudi anatembea nyuma ya jeneza la Abneri na kulia kaburini pake2 Sam 3:31–32
Aya
2 Sam 3:31–32Daudi akamwambia Yoabu na wote waliokuwa pamoja naye, “Rarueni mavazi yenu, jivikeni nguo za magunia, na muomboleze mbele ya mwili wa Abneri.” Na mfalme Daudi akaufuata mwili wa Abneri wakati wa mazishi. Wakamzika Abneri huko Hebroni. Mfalme akalia kwa sauti katika kaburi la Abneri, na watu wote pia wakalia.
- Huko Naini umati mkubwa unamsindikiza mwana pekee wa mjane kwenda kuzikwaLk 7:12
Aya
Lk 7:12Alipofika karibu na Lango la jiji tazama, mtu aliyekufa alikuwa amebebwa, na ni mtoto wa pekee kwa mama yake. aliyekuwa mjane, na umati wa wawakilishi kutoka kwenye jiji walikuwa pamoja naye.
Mazishi
- Wazee wa Farao, magari na wapanda farasi wanapanda kumzika YakoboMwa 50:7–9
Aya
Mwa 50:7–9Yusufu akaenda kumzika baba yake. Maofisa wa Farao wote wakaenda pamoja naye - washauri wa nyumba yake, maofisa waandamizi wote wa nchi ya Misri, pamoja na nyumba yote ya Yusufu na ndugu zake, na nyumba yote ya baba yake. Lakini watoto wao, kondoo wao na makundi ya mbuzi wao yaliachwa katika nchi ya Gosheni. Vibandawazi na wapanda farasi pia walikwenda pamoja naye. Lilikuwa kundi kubwa sana la watu.
- Isaka na Ishmaeli wanamzika Abraham; Esau na Yakobo wanamzika IsakaMwa 25:9, Mwa 35:29
- Israeli wote wanamwombolezea Samweli na kumzika nyumbani kwake Rama1 Sam 25:1, 1 Sam 28:3
Aya
1 Sam 25:1Basi Samweli akafariki. Waisraeli wote wakakusanyika pamoja na kumwomboleza, na wakamzika nyumbani kwake huko Rama. Kisha Daudi akainuka na akashuka hadi jangwa la Parani.
1 Sam 28:3Samweli alikuwa amefariki; Waisraeli wote walimwomboleza na kumzika huko Rama, katika mji wake mwenyewe. Wakati huo Sauli alikuwa amewafukuza kutoka nchini wote walioongea na wafu au pepo.
- Watu wa Yabeshi wanasafiri usiku kucha kuuchukua mwili wa Sauli1 Sam 31:11–13
Aya
1 Sam 31:11–13Na wenyeji wa Yabeshi Gileadi waliposikia kile Wafilisti walichomfanyia Sauli, wapiganaji wote wakainuka na kwenda usiku wote na wakauondoa mwili wa Sauli na miili ya wanawe kutoka ukuta wa Bethi Shani. Nao wakaenda Yabeshi na wakaichoma moto hiyo miili huko. Kisha wakachukua mifupa yao na kuizika chini ya mti wa mkwaju huko Yabeshi, na wakafunga siku saba.
- Daudi anahamisha mifupa ya Sauli na Yonathani hadi kaburi la Kishi2 Sam 21:12–14
Aya
2 Sam 21:12–14Hivyo Daudi akaenda na kuchukua mifupa ya Sauli na mifupa ya Yonathani mwanawe kutoka kwa watu wa Yabeshi Gileadi, waliokuwa wameiiba kutoka katika eneo la jumuiya la Beth Shani, Wafilisti walipokuwa wamewatundika baada ya Wafilisti kumwua Sauli katika Gilboa. Daudi akaiondoa pale mifupa ya Sauli na mifupa ya Yonathani mwanawe, na wakakusanya pia mifupa ya wale watu saba waliotundikwa. Wakaizika mifupa ya Sauli na Yonathani mwanawe huko Zela katika nchi ya Benjamini, katika kaburi la Kishi babaye. Wakafanya kila alichoagiza mfalme. Ndipo Mungu akajibu maombi yao kwa ajili ya nchi.
- Watu wamchao Mungu wanamzika Stefano na kumwombolezea sanaMdo 8:2
Aya
Mdo 8:2Watu wachamungu walimzika Stefano na kufanya maombolezo makubwa juu yake.
Matakwa kuhusu mazishi
- Yakobo anaomba azikwe pamoja na baba zake, si MisriMwa 47:30, Mwa 49:29–32
Aya
Mwa 47:30Nitakapolala na baba zangu, utanitoa Misri na kunizika katika eneo la kuzikia la baba zangu.” Yusufu akasema, “Nitafanya kama ulivyosema.”
Mwa 49:29–32Kisha akawaelekeza na kuwaambia, “Ninakaribia kwenda kwa watu wangu. Mnizike pamoja na babu zangu katika pango lililoko katika shamba la Efroni Mhiti, katika pango lililo katika shamba la Makpela, karibu na Mamre katika nchi ya Kanaani, shamba Ibrahimu alilolinunua kwa Efron Mhiti kwa ajili ya eneo la kuzikia. Pale walimzika Ibrahimu na Sara mkewe; pale wakamzika Isaka na Rebeka mkewe; na pale nikamzika Lea. Shamba na pango lililomo lilinunuliwa kutoka kwa watu wa Hethi.”
- Yusufu anawaapisha wana wa Israeli kuibeba mifupa yake kutoka MisriMwa 50:25
Aya
Mwa 50:25Kisha Yusufu akawaapisha watu wa Israeli kwa kiapo. Akasema, “Bila shaka Mungu atawajilia. Wakati huo mtachukuwa mifupa yangu kutoka hapa.”
- Barzilai anataka kufa karibu na kaburi la baba yake na mama yake2 Sam 19:37
Aya
2 Sam 19:37Tafadhari mruhusu mtumishi wako arudi nyumbani, ili kwamba nife katika mji wangu katika kaburi la baba na mama yangu. Lakini tazama, huyu hapa mtumishi wako Kimhamu. Haya yeye na avuke na bwana wangu mfalme na umfanyie lolote lipendezalo kwako.”
- Nabii mzee anaomba azikwe kando ya mtu wa Mungu1 Fal 13:30–31
Aya
1 Fal 13:30–31Akaulaza mwili kwenye kaburi lake, nao wakamwombolezea, wakisema, “Aa! ndugu yangu!” Kisha baada ya kumzika, yule nabii mzee akawaambia wanawe, akasema, “Nitakapokufa, mtanizika kwenye kaburi ambalo tumemzika mtu wa Mungu. Mtalaza mifupa yangu pembeni mwa mifupa yake.
Makaburi na mahali pa kuzikia
- Abraham ananunua pango la Makpela kwa shekeli mia nne za fedhaMwa 23:16–20
Aya
Mwa 23:16–20Abraham akamsikiliza Efroni na akampimia Efroni kiwango cha fedha alizosema mbele ya wana wa Helthi wakisikiliza, shekeli mia nne za fedha, kwa mujibu wa viwango vya vipimo vya kibiashara. Kwa hiyo shamba la Efroni, lililokuwa katika Makpela, mbele ya Mamre, shamba pamoja na pango lililokuwamo ndani yake na miti yote iliyokuwamo ndani ya shamba na iliyokuwa mpakani ikatolewa kwa Abraham kwa njia ya manunuzi mbele ya wana wa Hethi, na mbele ya wote waliokuja malangoni pa mji wake. Baada ya haya, Abraham akamzika Sara mkewe katika pango la shamba la Makpela, lililo mbele ya Mamre, ambayo ni Hebroni, katika nchi ya Kanaani. Kwa hiyo shamba pamoja na pango likatolewa na wana wa Hethi kwa Abraham kama milki na eneo la kuzikia.
- Yakobo anasimamisha nguzo juu ya kaburi la Raheli njiani kwenda BethlehemuMwa 35:19–20
Aya
Mwa 35:19–20Raheli akafa na kuzikwa katika njia iendayo Efrathi (ndio Bethlehemu). Yakobo akaweka nguzo katika kaburi lake. Ndiyo alama ya kaburi la Raheli hata leo.
- Walizikwa chini ya miti: Debora chini ya mwaloni, Sauli chini ya mkwajuMwa 35:8, 1 Sam 31:13
Aya
Mwa 35:8Debora, mlezi wa Rebeka, akafa. Akazikwa chini kutoka Betheli chini ya mwaloni, hivyo ikaitwa Aloni Bakuthi.
1 Sam 31:13Kisha wakachukua mifupa yao na kuizika chini ya mti wa mkwaju huko Yabeshi, na wakafunga siku saba.
- Wafalme wa Yuda walizikwa katika Mji wa Daudi1 Fal 2:10, 2 Nya 32:33
Aya
1 Fal 2:10Ndipo Daudi alipolala na mababu zake na alizikwa kwenye mji wa Daudi.
2 Nya 32:33Hezekia akalala pamaoja na babu zake, na wakamzika katika mlima wa makaburi ya vizazi vya Daudi. Yuda wote na wakaaji wa Yerusalemu wakamheshimu katika kifo chake. Manase mwanaye akawa mfalme katika nafasi yake.
- Kuhani Yehoyada anazikwa pamoja na wafalme2 Nya 24:16
Aya
2 Nya 24:16Wakamzika katika aamji wa Daudi miongoni mwa wafalme, kwa sababu alikuwa amefanya mema katika Israeli, kwa Mungu, na kwa ajili ya nyumba ya Mungu,
- Yoashi na Yehoramu wanazikwa, lakini si katika makaburi ya wafalme2 Nya 24:25, 2 Nya 21:20
Aya
2 Nya 24:25Katika muda ambao Waaramu walikuwa wameondoka, Yoashi alikuwa amejeruhiwa vikali. Watumishi wake wakapanga njama dhidi yake kwa sababu ya mauaji ya wana wa Yehoyada, yule kuhani. Wakamuua katika kitanda chake, na akafa; wakamzika katika mji wa Daudi, lakini siyo katika makaburi ya wafalme.
2 Nya 21:20Alikuwa ameanza kutawala alipokuwa na umrai wa miaka thelatahini na mbaili; akatawala katika Israeli kwa miaka minane, na alikufa bila kuaombolezwa. Wakamzika katika mji wa Daudi, lakini siyo katika makaburi ya kifalme.
- Uzia, mwenye ukoma, anazikwa shambani karibu na makaburi ya kifalme2 Nya 26:23
Aya
2 Nya 26:23Kwa hiyo Uzia akalala pamoja na babu zake; walimzka pamoja na babu zake katika uwanja wa maziko wa Mfalme, kwa maana walisema, “Ni mwenye ukoma”. Yothamu, mwanaye, akawa mfalme katika nafasi yake.
- Manase na Amoni wanazikwa katika bustani ya Uza2 Fal 21:18, 2 Fal 21:26
Aya
2 Fal 21:18Manase akalala pamoja na babu zake na alizikwa kwenye bustani ya nyumba yake, katika bustani ya Uza. Amoni mwanawe akawa mfalme katika sehemu yake.
2 Fal 21:26Watu wakamzika kwenye kaburi lake katika bustani ya Uza, na Yosia mwanawe akawa mfalme katika sehemu yake.
- Yoabu anazikwa nyumbani kwake nyikani1 Fal 2:34
Aya
1 Fal 2:34Kisha Benaya mwana wa Yehoyada akaenda akamvamia Yoabu na kumwua. Alizikwa kwenye nyumba yake kule jangwani.
- Yosia anaona makaburi kwenye mteremko wa kilima na mnara juu ya moja2 Fal 23:16–17
Aya
2 Fal 23:16–17Yosia alipotazama kwenye lile eneo, akagundua kwamba yale makaburi yalikuwa juu ya mlima. Akawatuma watu kuichukua mifupa kutoka kwenye yale makaburi; kisha akaichoma kwenye madhabahu, akainajisi. Hii ilitokana na neno la Yahwe ambalo mtu wa Mungu aliliongea, yule mtu aliyekuwa ameongea haya mambo kabla. Kisha akasema, “Ni ukumbusho wa nani ule ninao uona?” Mtu wa ule mji akamwambia, “Lile ni kaburi la mtu wa Mungu ambaye alikuja kutoka Yuda na kuongea kuhusu haya mambo ambayo ameyafanya dhidi ya madhabahu ya Betheli.”
- Yesu analazwa katika kaburi jipya bustanini karibu na mahali pa msalabaYn 19:41–42
Aya
Yn 19:41–42Mahali ambapo Yesu alisulibiwa kulikuwa na bustani; ndani ya ile bustani kulikuwa na kaburi jipya ambalo hakuna mtu alikuwa amawahi kuzikwa humo. Basi, kwa kuwa ilikuwa siku ya maandalio kwa Wayahudi, na kwa vile lile kaburi lilikuwa karibu, basi wakamlaza Yesu ndani yake.
- Wanawake wanajiuliza nani atalivingirisha jiwe kubwa kutoka kaburiniMk 16:3–4
Aya
Mk 16:3–4Wakisemezana wao kwa wao, “Nani ataliviringisha jiwe kwa ajili yetu ili tuingie kaburini?” Wakati walipotazama, walimuona mtu amekwisha kulivingirisha jiwe, ambalo lilikuwa kubwa sana.
- Shamba la mfinyanzi linanunuliwa kuwa mahali pa kuzikia wageniMt 27:7
Aya
Mt 27:7Walijadiliana kwa pamoja na fedha ikatumika kununulia shamba la mfinyazi la kuzika wageni.
- Mwili wa Uria unatupwa katika makaburi ya watu wa kawaidaYer 26:23
Aya
Yer 26:23Wakamtoa Uria nje kutoka Misiri na kumleta kwa Mfalme Yehoyakimu. Kisha Yehoyakimu akamuua kwa upanga na kumpeleka nje kwenye makaburi ya watu wa kawaida.
- Absalomu anatupwa shimoni chini ya rundo kubwa la mawe2 Sam 18:17
Aya
2 Sam 18:17Wakamchukua Absalomu na kumtupa katika shimo kubwa msituni; wakaufukia mwili wake chini ya rundo kubwa la mawe, wakati Israeli wote walipokimbia kila mtu nyumbani kwake.
- Hakuna anayejua kaburi la Musa liko wapiKum 34:6
Aya
Kum 34:6Yahwe alimzika katika bonde katika nchi ya Moabu mkabala na Beth-peori, lakini hakuna ajuaye kaburi lake lilipo hadi leo hii.
- Mtu mwenye pepo anaishi makaburiniMk 5:3, Lk 8:27, Mt 8:28
Aya
Mk 5:3Mtu huyu aliishi makaburini. Hakuna aliyeweza kumzuia zaidi, hakuna hata kwa minyororo.
Lk 8:27Yesu aliposhuka na kukanya kwenye ardhi, mtu fulani kutoka mjini, akakutana naye, na huyu mtu alikuwa na nguvu za giza. Kwa muda mrefu alikuwa havai nguo, na alikuwa haishi kwenye Nyumba, lakini aliishi kwenye makaburi.
Mt 8:28Wakati Yesu alipokuwa amekuja upande mwingine wa nchi ya Magadala, wanaume wawili waliotawaliwa na pepo walikutana naye. Walikuwa wakitokea makaburini na walikuwa wakifanya vurugu sana, kiasi kwamba hakuna msafiri angeweza kupita njia ile.
Vyanzo
Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0