Bible Explorer

Biblia › Isaya › 15

ULB · Sura 15 / 66

Isaya 15

1Tamko kuhusu Moabu, Kweli, kwa usiku mmoja Ari ya Moabu imeharibiwa kabisa na kuangamizwa; kweli, kwa usiku mmoja Kira ya Moabu itaharibiwa na kuangamizwa.

2Wamenda juu hekaluni, watu wa Diboni wamenda juu kuomboleza; Moabu wanaomboleza juu ya Nebo na juu ya madeba. Vichwa vyao vimenyolewa viko wazi na na ndevu zao zimenyolewa.

3Wamevaa nguo za magunia katka mitaa yao; juu ya dari zao na kila kona ya mitaa yao, kuyeyuka kwa kumwaga machozi.

4Hishiboni na Elealehi wanalia wakihitaji msaada; Sauti zao zinasikika mpaka Jahazi. Hivyo basi vijana wa vita wa Moabu wanalia wakihitaji msaada; wanatetemeka wao wenyewe.

5Moyo wangu unalia juu ya Moabu; watuhumiwa wamekimbilia Zoari na Elgathi Shelishiyahi. Wanapaa juu ya Luhithi wakilia; katika barabara ya kwenda Horonaimu wanapiga kelele ole juu ya uharibifu.

6Maji ya Nimrimu yamekauka; majani yamepooza na majani yanyochikia yanakufa; hakuna ukijani hata kidogo.

7Hivyo basi vitu vingi vimekuwa na hifadhi wameipeleka juu ya kijito maarufu.

8Kilio kimezunguka katika himaya ya Moabu; malalamiko yamefika hata Eglaimu na Beer-Elimu.

9Maana maji ya Dimoni imejaa damu; Simba atawavamia wale waliokimbia kutoka Moabu pia na walbakia katika nchi.

Swahili Unlocked Literal Bible (ULB, 2019) · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 (maandiko bila mabadiliko; bila maelezo ya chini na vichwa) · eBible.org