Bible Explorer

Biblia › Zaburi › 133

ULB · Sura 133 / 150

Zaburi 133

1Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu, wa Daudi. Tazama, jinsi ilivyo vema na yakupendeza ndugu waishi pamoja, kwa umoja!

2Ni kama mafuta mazuri kichwani yashukayo ndevuni. Ndevu za Haruni, na yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake.

3Ni kama umande wa Hermoni uangukao milimani pa Sayuni. Maana huko ndiko Bwana alipoamuru baraka, naam uzima milele na milele.

Swahili Unlocked Literal Bible (ULB, 2019) · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 (maandiko bila mabadiliko; bila maelezo ya chini na vichwa) · eBible.org