Bible Explorer

Biblia › Zaburi › 128

ULB · Sura 128 / 150

Zaburi 128

1Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu. Amebarikiwa kila mtu amchaye Yahwe, atembeaye katika njia zake.

2Kazi ya mikono yako, wewe utaifurahia; utabarikiwa na kufanikiwa.

3Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaao katika nyumba yako; wanao watakuwa kama miche ya mimea ya mizeituni wakaapo kuzunguka meza yako.

4Ndiyo, hakika, mtu anaye muheshimu Yahwe atabarikiwa.

5Mungu na akubariki toka Sayuni; na uweze kuona mafanikio ya Yerusalemu siku zote za maisha yako.

6Uishi uwaone wana wa wanao. Amani iwe na Israli.

Swahili Unlocked Literal Bible (ULB, 2019) · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 (maandiko bila mabadiliko; bila maelezo ya chini na vichwa) · eBible.org