Bible Explorer

Gundua › Mada › Maua na majani

Maumbile

Maua na majani katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (35), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

Maua

  • Vichwa vya nguzo za ukumbi wa hekalu vilikuwa na umbo la maua ya yungiyungi1 Fal 7:19, 1 Fal 7:22
    Aya
    1 Fal 7:19Zile taji kwenye vile vichwa vya nguzo za ukumbi zilikuwa zimepambwa kwa maua, yenye vimo vya mita 1. 8.
    1 Fal 7:22Na juu ya zile nguzo kulikuwa na mapambo kama maua. Hivyo ndivyo zile nguzo zilivyotengenezwa.
  • Ukingo wa Bahari ya shaba ulikuwa kama ua la yungiyungi1 Fal 7:26, 2 Nya 4:5
    Aya
    1 Fal 7:26Bahari ilikuwa nene kama upana wa mkono, na ukingo wake ulikuwakama ukingo wa kikombe, kama ua la yungi huingia bathi elfu mbili za maji.
    2 Nya 4:5Bahari ilikuwa nene kama upana wa mkono, na ukingo wake ulikuwa kama ukingo wa kikombe, kama ua la yungi. Bahari ilikuwa na mabafu elfu tatu ya maji.
  • “Fikirini maua ya yungiyungi jinsi yanavyokua: hayafanyi kazi wala hayasokoti”Mt 6:28, Lk 12:27
    Aya
    Mt 6:28Na kwa nini mna kuwa na wasiwasi kuhusu mavazi? Fikiria kuhusu maua kwenye mashamba, jinsi yanavyokua. Hayafanyi kazi na hayawezi kujivisha.
    Lk 12:27Angalieni maua -yanavyomea. Hayafanyi kazi wala hayasokoti. Lakini nawaambia, hata Sulemani katika utukufu wake wote hakuvikwa kama mojawapo ya haya,
  • Hata Sulemani katika utukufu wake wote hakuvikwa kama moja ya hayoMt 6:29
    Aya
    Mt 6:29Bado ninawaambia, hata Sulemani katika utukufu wake wote hakuvikwa kama mojawapo ya haya.
  • Mchungaji analisha kundi lake kati ya mauaWim 2:16, Wim 6:3
    Aya
    Wim 2:16Mpenzi wangu ni wangu, na mimi ni wake; anakula penye nyinyoro kwa raha. Mwanamke anaongea na mpenzi wake
    Wim 6:3Mimi ni wa mpenzi wangu, na mpenzi wangu ni wangu; na kula katika nyinyoro kwa raha. Mpenzi wa mwanamke akizungumza naye
  • Mpendwa anashuka bustanini mwake kukusanya mauaWim 6:2
    Aya
    Wim 6:2Mpenzi wangu ameenda katika bustani yake, kwenye vitanda vya manukato, kwenda kula katika bustani na kukusanya nyinyoro.
  • “Ua la bondeni … kama ua kati ya miiba”Wim 2:1–2
    Aya
    Wim 2:1–2Mimi ni ua katika tambarare, nyinyoro katika bonde. Mwanaume akizungumza naye Kama nyinyoro miongoni mwa mimba, ndivyo wewe, mpenzi wangu, miongoni mwa mabinti wengine wote. Mwanamke akizungumza mwenyewe
  • “Midomo yake ni kama maua, inayodondosha manemane”Wim 5:13
    Aya
    Wim 5:13Mashavu yake ni kama vitanda vya manukato, vinavyotoa arufu ya marashi. Midomo yake nni nyinyoro, inayo tiririka udi.
  • Paa mapacha wakila kati ya mauaWim 4:5
    Aya
    Wim 4:5Maziwa yako mawili ni kama swala wawili, mapacha wa ayala, wakila miongoni mwa nyinyoro.

Majani

  • Majani huota kwa ajili ya mifugo na juu ya vilimaZab 104:14, Zab 147:8, Kum 11:15
    Aya
    Zab 104:14Huzifanya nyasi kukua kwa ajili ya mifugo na mimea kwa ajili ya binadamu kulima ili kwamba mwanadamu aweze kuzalisha chakula toka nchini.
    Zab 147:8Huzifunika mbingu kwa mawingu na huiandaa mvua kwa ajili ya nchi, akizifanya nyasi kukua juu ya milima.
    Kum 11:15Nitawapa nyasi kwenye mashamba yenu kwa ajili ya mifugo yenu, na mtakula na kushiba.
  • Mvua juu ya majani yaliyokatwa karibuniZab 72:6
    Aya
    Zab 72:6Naye apate kuja kama mvua juu ya nyasi zilizokatwa, kama manyuyu yanyunyizayo nchi.
  • Majani juu ya paa hunyauka kabla ya kukuaZab 129:6–7, 2 Fal 19:26
    Aya
    Zab 129:6–7Na wawe kama nyasi juu ya paa ambayo hunyauka kabla hayajakua, ambayo hayawezi kujaza mkono wa mvunaji wala kifua cha mfunga miganda.
    2 Fal 19:26Makazi yao, ya nguvu kidogo, imevunjwa vunjwa na aibu. Wamekuwa mimea katika shamba, majani ya kijani, majani juu kwenye dari au kwenye shamba, lililochomwa kabla halijakua.
  • Majani ya kondeni: leo yapo, kesho hutupwa jikoniMt 6:30, Lk 12:28
    Aya
    Mt 6:30Ikiwa Mungu anayavalisha majani katika mashamba, ambayo yadumu siku moja na kesho yanatupwa katika moto, je ni kwa kiasi gani atawavalisha ninyi, ninyi wenye imani ndogo?
    Lk 12:28Kama Mungu huyavika vizuri majani ya kondeni, ambayo leo yapo, na kesho hutupwa kwenye moto. Je si zaidi atawavika ninyi? enyi wa imani haba!
  • Majani makavu yanapoondolewa, majani mapya huchipukaMit 27:25
    Aya
    Mit 27:25Majani huondoka na ukuaji mpya huonekana na milima ya chakula cha mifugo hukusanywa ndani.
  • Jua kali hunyausha mmea, na ua lake huangukaYak 1:11
    Aya
    Yak 1:11Jua huchomoza na joto la kuunguza kukausha mimea, na maua huanguka na uzuri wake hufa. Vivyo hivyo watu matajiri watachakaa katikati ya kazi zao.
  • Wakati wa ukame Ahabu alitafuta majani ya farasi katika kila chemchemi na bonde1 Fal 18:5
    Aya
    1 Fal 18:5Ahabu akamwambia Obadia, “Pita katika nchi yote na katika chemichemi zote za maji na vijito. Yamkini tunaweza kupata maji na nyasi ili tuwaokoa hawa farasi na nyumbu, ili tusiwakose wanyama wote.”
  • Maji ya Nimrimu yalikauka na majani yakanyaukaIsa 15:6
    Aya
    Isa 15:6Maji ya Nimrimu yamekauka; majani yamepooza na majani yanyochikia yanakufa; hakuna ukijani hata kidogo.
  • Kiboko (Behemothi) hula majani kama ng’ombeAyu 40:15
    Aya
    Ayu 40:15Mwangalie sasa kiboko, ambaye niliwafanya kama nilivyokufanya wewe; anakula nyasi kama ng'ombe.
  • Nebukadneza alikula majani kama ng’ombeDan 4:33
    Aya
    Dan 4:33Agizo hili kinyume na Nebukadneza lilitekelezwa ghafla. Aliondolewa miongoni mwa watu. Alikula majani kama ng'ombe, na mwili wake ulilowa kwa umande wa kutoka mbinguni. Nywele zake zilirefuka kama manyoa ya tai, na makucha yake yalikuwa kama makucha ya ndege.
  • “Je, punda mwitu hulia akiwa na majani mabichi?”Ayu 6:5
    Aya
    Ayu 6:5Je punda mwitu hulia akiwa na malisho? Au ng'ombe huwa dhaifu wakati wa njaa ambapo anachakula?
  • Wale elfu tano waliketi juu ya majani mabichiYn 6:10, Mk 6:39
    Aya
    Yn 6:10Yesu akawambia, “Waketisheni watu chini” (kulikuwa na nyasi nyingi mahali pale). Hivyo wanaume wapata elfu tano wakakaa chini.
    Mk 6:39Akawaamuru watu waketi katika makundi juu ya majani mabichi.

Misemo

  • “Wote wenye mwili ni majani … majani hukauka na maua huanguka”Isa 40:6–8, 1 Pet 1:24
    Aya
    Isa 40:6–8Sauti inasema, ''Lia.'' Jibu lingine, ''Kwa nini nilie?'' ''Mwili wote ni nyasi na maagano yaliyoaminika ni kama ua kwenye shamba. Nyasi zinanyauka na maua yanaperuka pale Yehwe atakapo puliza punzi yake juu yake; hakika ubinadamu ni nyasi. Nyasi hunyauka, maua hupepea, lakini neno la Yahwe litasimama daima.''
    1 Pet 1:24Kwa maana “ miili yote ni kama majani, na utukufu wake wote ni kama ua la jani. Jani hunyauka, na ua hudondoka,
  • Majani mapya huchipuka asubuhi na kunyauka jioniZab 90:5–6
    Aya
    Zab 90:5–6Huwafagia kama vile kwa mafuliko nao hulala; na wakati wa asubuhi wako kama majani yameayo. Asubuhi yachipuka na kumea; jioni yakatika na kukauka.
  • Siku za mwanadamu ni kama majani; upepo hupita na hayapo tenaZab 103:15–16
    Aya
    Zab 103:15–16Kama ilivyo kwa mwanadamu, siku zake ni kama majani; hustawi kama ua katika shamba. Upepo hulipiga, nalo hutoweka, na hakuna hata mmoja awezaye kuelezea mahali lilipokua.
  • Maneno yanayoshuka kama umande, kama mvua nyepesi juu ya majani mabichiKum 32:2
    Aya
    Kum 32:2Acha dunia isikie maneno ya kinywa changu. Acha mafundisho yangu yamwagike chini kama mvua, acha usemi wangu udondoke kama umande, kama mvua tulivu juu ya majani laini, na kama mvua za manyunyu juu ya mimea.

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0