Bible Explorer

Gundua › Mada › Nyoka

Maumbile

Nyoka katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (28), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

  • Mwanzo: nyoka alikuwa mwerevu kuliko mnyama yeyote wa poriniMwa 3:1
    Aya
    Mwa 3:1Sasa nyoka alikuwa mwerevu kuliko myama mwingine yeyote wa kondeni ambaye Yahwe Mungu alikuwa amemuumba. Akamwambia mwanamke, “Je ni kweli Mungu amesema, 'Msile matunda kutoka kwenye mti wowote bustanini'?”
  • Mwanzo: nyoka atatambaa kwa tumbo lake na kula mavumbiMwa 3:14
    Aya
    Mwa 3:14Yahwe Mungu akamwambia nyoka, “ kwa sababu umefanya jambo hili, umelaaniwa wewe mwenyewe miongoni mwa wanyama wote wa kufugwa na wanyama wote wa mwituni. Itakuwa kwa tumbo lako utakwenda, na mavumbi utakula kwa siku zote za maisha yako.
  • “Njia ya nyoka juu ya mwamba” — moja ya mambo manne ya ajabu mnoMit 30:18–19
    Aya
    Mit 30:18–19Kuna vitu vitatu ambavyo vinanishangaza, vinne ambavyo sivifahamu: njia ya tai angani; njia ya nyoka juu ya mwamba; njia ya meli kwenye moyo wa bahari; na njia ya mtu pamoja mwanake kijana.
  • Nyoka ukutani: abomoaye ukuta au kuuegemea anaweza kuumwaMhu 10:8, Amo 5:19
    Aya
    Mhu 10:8Yeyote anayechimba shimo anaweza kutumbukia yake, na popote mtu anayevunja ukuja, nyoka anaweza kumuuma.
    Amo 5:19kama wakati mtu anamkimbia simba na kukutana na dubu, au aliingia katika nyumba na kuweka mkono wake kwenye ukuta na kung'atwa na nyoka.
  • Waganga wa nyoka: hakuna faida ikiwa nyoka anauma kabla ya kulogwaMhu 10:11
    Aya
    Mhu 10:11Kama nyoka akiuma kabla hajafurahi, hivyo hakuna faida kwa mfurahishaji.
  • Fira anayeziba masikio yake asisikie sauti ya mgangaZab 58:4–5
    Aya
    Zab 58:4–5Sumu yao ni kama sumu ya nyoka; wako kama fira kiziwi azibaye masikio yake, ambaye hasikilizi sauti ya waganga, haijalishi ustadi walio nao.
  • Nyoka wenye sumu wasioweza kulogwaYer 8:17
    Aya
    Yer 8:17Hebu tazama, ninawatuma nyoka kati yenu, fira ambao hawawezi kuzuiliwa kwa uganga. Watawauma - asema BWANA,.”
  • Nyoka kando ya njia huuma visigino vya farasi, na mpanda farasi huangukaMwa 49:17
    Aya
    Mwa 49:17Dani atakuwa nyoka kando ya njia, nyoka mwenye sumu aumaye visigino vya farasi katika njia, hivyo aongozaye farasi huanguka nyuma.
  • Jangwa lilikuwa na nyoka wenye sumu na ngeKum 8:15
    Aya
    Kum 8:15Usimsahau yeye aliyewaongoza kupitia jangwa kuu na la kutisha, ambako ndani yake kulikuwa na nyoka wa moto na nge, na pitia nchi yenye kiu ambako hapakuwa na maji, ambaye yeye alileta maji toka kwenye mwamba wa jiwe.
  • Negevi: nchi ya simba, nyoka na nyoka wa moto arukayeIsa 30:6
    Aya
    Isa 30:6Tamko kuhusu mnyama wa Negevi: kupitia kwenye mlango wa mateso na hatari, wa simba jike na simba dume, nyoka na nyoka wa moto aneyepaa, wamebeba utajiri wao kwenye mgongo wa punda, na hazina yao katika mabega ya ngamia, kwa watu ambao hawana msaada kwao.
  • Ukivunja yai la nyoka, nyoka hutokaIsa 59:5
    Aya
    Isa 59:5Wanetotoa mayai ya nyoka wenye sumu na hufuma mtandao wa buibui. Yeyote alaye mayai yake atakufa, na ikiwa yai litavunjika, litatotoa nyoka mwenye sumu.

Katika masimulizi

  • Fimbo ya Musa iligeuka nyoka; alimkimbia, kisha akamshika mkiaKut 4:3–4
    Aya
    Kut 4:3–4Yahwe akasema, “Itupe chini.” Musa akaitupa chini ile fimbo, nayo ikageuka na kuwa nyoka. Musa akarudi nyumba. Yahwe akamwambia Musa, “Mchukue kwa kumshikia mkia wake.” Hivyo alimchukua yule nyoka. Mara ikaggeuka na kuwa fimbo mkononi mwake tena.
  • Fimbo ya Haruni iligeuka nyoka na kumeza fimbo za wagangaKut 7:10–12
    Aya
    Kut 7:10–12Kisha Musa na Aruni wakaenda kwa Farao, na wakafanya kama Yahweh alivyo waamuru. Aruni akarusha chini gongo lake mbele ya Farao na watumishi wake, na likageuka nyoka. Kisha naye Farao akawaita wazee wenye hekima na wachawi. Wakafanya jambo hilo hilo kwa uchawi wao. Kila mtu akarusha chini gongo lake, na magongo yakawa nyoka. Lakini gongo la Aruni lilimeza nyoka zao.
  • Nyoka wenye sumu waliwauma Waisraeli jangwani, na wengi wakafaHesabu 21:6
    Aya
    Hesabu 21:6Basi Mungu akatuma nyoka wa sumu kati yao. Wale nyoka wakawauma wale watu; watu wengi walikufa.
  • Musa alifanya nyoka wa shaba juu ya mti; walioumwa waliomtazama waliishiHesabu 21:8–9
    Aya
    Hesabu 21:8–9BWANA akamwambia Musa, “Tengeneza nyoka na umweke kwenye nguzo. Na itakuwa kila anayeumwa, akimwangalia huyo nyoka atapona,” Kwa hiyo Musa akatengeneza nyoka wa shaba naye akamweka juu ya nguzo. Na kila mtu alipoumwa na nyoka na kumwangalia huyo nyoka alipona.
  • Hezekia alimvunja nyoka huyo wa shaba, Nehushtani, kwa kuwa walimfukizia uvumba2 Fal 18:4
    Aya
    2 Fal 18:4Alipaondoa mahali pa juu, akaiharibu nguzo ya jiwe, akaikata hiyo nguzo ya Ashera. Akavunja vipande vipande ile nyoka ambayo Musa aliyokuwa ameifanya, kwa sababu siku zile wana wa Israeli walikuwa wakichoma ubani katika hiyo; ilikuwa inaitwa “Nehushtani.”
  • Huko Malta nyoka, aliyefukuzwa na joto la moto, alijishika mkononi mwa PauloMdo 28:3–4
    Aya
    Mdo 28:3–4Lakini Paulo alipokuwa amekusanya mzigo wa kuni na kuuweka motoni, nyoka mdogo mwenye sumu akatoka kwenye zile kuni kwa sababu ya lile joto, na akajizungusha kwenye mkono wake. Watu wenyeji wa pale walipoona mnyama ananing'inia kutoka kwenye mkono wake, wakasemezana wao kwa wao, “Mtu huyu hakika ni muuaji ambaye ametoroka baharini, lakini haki haimuruhusu kuishi.”
  • Paulo alimkung’uta; wenyeji walingoja avimbeMdo 28:5–6
    Aya
    Mdo 28:5–6Lakini yeye akamtupia huyo mnyama katika moto na hakupata madhara yoyote. Wao walimngojea avimbe kwa homa au aanguke ghafla na kufa. Lakini baada ya kumwangalia kwa muda mrefu na kuona kwamba hakuna jambo ambalo si la kawaida kwake, walibadilisha mawazo yao na kusema alikuwa mungu.
  • Yesu anawapa wanafunzi wake mamlaka ya kukanyaga nyoka na ngeLk 10:17, Lk 10:19
    Aya
    Lk 10:17Wale sabini walirudi kwa furaha, wakisema, “Bwana, hata mapepo wanatutii katika jina lako.”
    Lk 10:19Tazama, nimewapa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za adui, na hapana chochote kwa njia yoyote kitakachowadhuru.

Misemo

  • “Kuweni na busara kama nyoka na wapole kama njiwa”Mt 10:16
    Aya
    Mt 10:16Angalia, ninawatuma kama kondoo katikati ya mbwa mwitu, kwa hiyo iweni na werevu kama nyoka na wapole kama njiwa.
  • Ni baba gani atampa mwanawe nyoka akimwomba samaki?Mt 7:10, Lk 11:11
    Aya
    Mt 7:10Au ikiwa atamwomba samaki, na yeye atampa nyoka?
    Lk 11:11Ni baba yupi miongoni mwenu, mwanaye akimuomba samaki atampa nyoka badala yake.?
  • Divai “huuma kama nyoka na kuchoma kama fira”Mit 23:31–32
    Aya
    Mit 23:31–32Usiutazame mvinyo ukiwa mwekundu, wakati unametameta kwenye kikombe na kutelemka kwa uraini. Mwisho wake unauma kama nyoka na sumu yake kama kifutu.
  • “Wananoa ndimi zao kama nyoka”Zab 140:3
    Aya
    Zab 140:3Ndimi zao zinajeruhi kama nyoka; sumu ya fira imo midomoni mwao. Selah
  • “Watalamba mavumbi kama nyoka”Mik 7:17
    Aya
    Mik 7:17Watalamba vumbi kama nyoka, kama viumbe vitaambavyo juu ya nchi. Watatoka nje kwenye maficho kwa hofu; watakuja kwako kwa hofu, Yahwe Mungu wetu, na wataogopa kwa sababu yako.
  • Misri “itatoa sauti kama nyoka akimbiaye”Yer 46:22
    Aya
    Yer 46:22Misri anatoa sauti kama ya nyoka na kuondoka kwa kutambaa. maana adui yake anajiandaa kinyume chake. Wanamkabili kama mkata miti aliye na shoka.

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0