Bible Explorer

Biblia › Zaburi › 129

ULB · Sura 129 / 150

Zaburi 129

1Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu. “Mara nyingi tangu ujana wangu wamekuwa wakinishambulia,” Israeli na iseme.

2“Mara nyingi tangu ujana wangu wamekuwa wakinishambulia, lakini hawajanishinda.

3Wakulima wamekuwa wakilima mgonngoni kwangu; wametengeneza matuta yao marefu.

4Yahwe ni mwenye haki; amezikata kamba za waovu.”

5Wote waaibishwe na kurudishwa nyuma, wale wachukiao Sayuni.

6Na wawe kama nyasi juu ya paa ambayo hunyauka kabla hayajakua,

7ambayo hayawezi kujaza mkono wa mvunaji wala kifua cha mfunga miganda.

8Wale wapitao karibu wasiseme, “Baraka za Mungu na ziwe juu yako; Tunakubariki katika jina la Yahwe.”

Swahili Unlocked Literal Bible (ULB, 2019) · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 (maandiko bila mabadiliko; bila maelezo ya chini na vichwa) · eBible.org