Maumbile
Farasi katika Biblia
Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (37), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.
- Ayubu: farasi hukwaruza bondeni, hufurahia nguvu zake na kukimbilia vitaniAyu 39:19–21
Aya
Ayu 39:19–21Je umempa farasi nguvu zake? Je umeivika shingo yake kwa manyoya? Je umemfanya aruke kama panzi? Enzi ya mlio wake ni wa kutisha. Hurarua kwa nguvu na kufurahia katika nguvu zake; hukimbia upesi kukutana na silaha.
- Huicheka hofu wala harudi nyuma mbele ya upangaAyu 39:22–23
Aya
Ayu 39:22–23Huidharau hofu na hashangazwi; huwa harudi nyuma kutoka katika upanga. Podo hugongagonga ubavuni mwake, pamoja na mkuki unaong'aa na fumo.
- Kwa sauti ya tarumbeta hawezi kusimama tuli; huinusa vitaAyu 39:24–25
Aya
Ayu 39:24–25Huimeza nchi kwa hasira na ghadhabu; katika sauti ya tarumbeta, hawezi kusimama sehemu moja. Wakati wowote tarumbeta inapolia, husema, 'Ooh! Huisikia harufu ya vita kutoka mbali - vishindo vya radi za makamanda na makelele.
- Mkoromo na mlio wa farasi wa vita ulisikika toka mbaliYer 8:16
Aya
Yer 8:16Mkoromo wa farasi wake umesikika kutoka Dani. Dunia nzima inatikisika kwa sababu ya sauti ya kukaribia kwa farasi wake wenye nguvu. Kwa kuwa watakuja kuiangamiza nchi na utajiri wake, mji na wote wakaao nadani yake.
- Lijamu vinywani mwao huwawezesha wapanda farasi kumwongoza mnyama mzimaYak 3:3
Aya
Yak 3:3Sasa kama tunaweka lijamu za farasi katika vinywa vyao wanatutii, na tunaweza kuigeuza miili yao yote.
- Farasi na nyumbu lazima wazuiliwe kwa lijamu na hatamuZab 32:9
Aya
Zab 32:9Msiwe kama farasi au kama nyumbu, ambao hawana uelewa; ni kwa hatamu na lijamu tu unaweza kuwapeleka popote utakapo wao waende.
- Shayiri na majani yaliletwa kwa ajili ya farasi wa magari1 Fal 4:28
Aya
1 Fal 4:28Na pia walileta kwenye eneo husika shayiri na majani kwa ajili ya wale farasi wa magari na kwa wale farasi wa mbio kila mmoja alileta kadri alivyoweza.
- Magurudumu ya gari na farasi walipita juu ya nafaka bila kuipondaIsa 28:28
Aya
Isa 28:28Nafaka ni mwanzo mkate lakini ni laini sana, japo gurudumu la gari lake na farasi wamezitawanya, na farasi wake hawajaiponda ponda.
Vitani
- Farasi na magari ya Farao waliwafuata Israeli hadi bahariniKut 14:9, Kut 15:19
Aya
Kut 14:9Lakini Wamisri wali wafukuzia, pamoja na farasi na magari ya farasi, wapanda farasi, na jeshi lake. Walikuta Waisraeli wameeka kambi pembezoni mwa bahari kati ya Pi Hahirothi na Baali Zefoni.
Kut 15:19Kwa kuwa farasi wa Farao walienda na magari ya farasi na wapanda farasi kwenye bahari. Yahweh alileta maji ya bahari juu yao. Lakini Waisraeli walienda juu ya nchi kavu katikati ya bahari.
- Yoshua aliwakata mishipa farasi wa adui na kuyachoma moto magari yaoYos 11:6, Yos 11:9
Aya
Yos 11:6Yahweh akamwambia Yoshua, “Usiogope mbele zao, kwa kuwa muda kama huu kesho ninawatia hao kwa Waisraeli wakiwa wafu. Utaivunja vunja miguu ya farasi zao, na utayachoma moto magari yao.”
Yos 11:9Yoshua aliwatendea kama vile Yahweh alivyomwambia. Alivunja miguu ya farasi na magari aliyachoma moto.
- Daudi aliwakata mishipa farasi wote wa magari isipokuwa mia moja2 Sam 8:4
Aya
2 Sam 8:4Daudi aliteka magari 1,700 ya farasi na askari ishirini elfu waendao kwa miguu. Daudi akawakata miguu farasi wa magari, lakini akahifadhi wakutosha magari mia moja.
- Mfalme Yehoshafati kwa Ahabu: “Farasi wangu ni farasi wako”1 Fal 22:4
Aya
1 Fal 22:4Kwa hiyo akamwambia Yehoshafati, “Je, utakwenda na mimi katika vita huko Ramothi Gileadi?” Yehoshafati akamjibu mfalme wa Israeli, “Mimi ni kama wewe, watu wangu ni kama watu wako, na farasi wangu ni kama farasi wako.”
- Dhihaka ya Waashuru: farasi elfu mbili, kama unaweza kuwapandisha wapanda farasi2 Fal 18:23
Aya
2 Fal 18:23Basi kwa hiyo, nataka kukufanyia ahadi nzuri kutoka kwa bwana wangu mfalme wa Ashuru. Nitakupatia farasi elfu mbili, kama unaweza kuwatafuta kuwaendesha kwa ajili yao.
- Wapelelezi wa Samaria walichukua magari mawili na farasi kuwafuata Washami2 Fal 7:13–14
Aya
2 Fal 7:13–14Mmoja wa wale watumishi wa mfalme akajibu na kusema, “Nakuomba, ngoja baadhi ya watu wachukue farasi watano wale waliosalia, ambao wamebaki kwenye mji. Wako kama mkutano wote wa Israeli waliobaki-wengi wamekufa; ngoja tuwatume na tuone.” Hivyo wakachukua magari mawili ya farasi pamoja na farasi, na mfalme akawatuma baada ya jeshi la Washami, akisema, “Enendeni mkaone.”
- “Watandikeni farasi; pandeni farasi; simameni mahali penu na kofia za chuma!”Yer 46:4
Aya
Yer 46:4Watieni farasi lijamu na hatamu, na mpande juu yao, ninyi wapanda farasi. Jiwekeni mahali penu, mkiwa mmevaa helmeti vichwani mwenu. Inoweni mishale yenu na kuvaa silaha zenu.
- Kwato za farasi dume wakipiga mbio na mshindo wa magariYer 47:3
Aya
Yer 47:3Kwa sauti ya kukanyaga kwa kwato za farasi wao wenye nguvu, kwa mwungurumo wa vibandawazi vyao na kelele za magurudumu yao, wazazi hawatawasaidia watoto wao kwa sababu ya udhaifu wao.
Wafalme na biashara
- Sheria: mfalme hapaswi kujikusanyia farasi wengiKum 17:16
Aya
Kum 17:16Lakini hapaswi kuzidisha farasi kwa ajili yake, wala kusababisha watu kurudi Misri ili kwamba aweze kuzidisha farasi, kwa kuwa Yahwe alikwisha sema kwako, 'Unapaswa kuanzia sasa usirudi njia hiyo tena.'
- Mabanda ya Sulemani ya farasi wa magari yake, na wapanda farasi wake1 Fal 4:26, 2 Nya 9:25
Aya
1 Fal 4:26Sulemani alikuwa na mabanda ya farasi arobaini elfu kwa ajili ya magari yake, na wapanda farasi elfu kumi na mbili.
2 Nya 9:25Selemani alikuwa na mazizi elfu nne kwa ajili ya farasi na magari, na wapanda farasi kumi na mbili elfu, ambao waliwaweka katika miji ya magari na pamoja naye katika Yerusalemu.
- Farasi kutoka Misri aligharimu shekeli 150 za fedha, gari 6001 Fal 10:28–29
Aya
1 Fal 10:28–29Sulemani alimiliiki farasi waliokuwa wamenunuliwa kutoka Misri na Kilikia. Wachuuzi wa mfalme waliwanunua kwa makundi, kila kundi kwa bei yake. Magari yalinunuliwa kutoka Misri kwa shekeli mia sita za fedha kila moja, na farasi kwa shekeli 150 kila moja. Vitu vingi katika hivi baadaye viliuzwa kwa wafalme wote wa Wahiti na Aramu.
- Farasi wa Sulemani walitoka Misri, Kue na nchi nyingine1 Fal 10:28, 2 Nya 9:28
Aya
1 Fal 10:28Sulemani alimiliiki farasi waliokuwa wamenunuliwa kutoka Misri na Kilikia. Wachuuzi wa mfalme waliwanunua kwa makundi, kila kundi kwa bei yake.
2 Nya 9:28Wakaleta farasi kutoka Misri na kutoka nchi zote kwa ajili ya Selemani.
- Beth Togarma ilifanya biashara ya farasi, farasi wa vita na nyumbu na TiroEze 27:14
Aya
Eze 27:14Beth Togarma waliandaa farasi, farasi dume, na nyumbu kama kama bidhaa zako.
- Waliorudi kutoka Babeli walikuwa na farasi 736 na nyumbu 245Ezr 2:66
Aya
Ezr 2:66Farasi wao: 736, Nyumbu wao: 245.
- Baadhi ya Yuda walikwenda Misri kutegemea farasi na magari yakeIsa 31:1
Aya
Isa 31:1Ole wao washukao Misri kuomba msaada na kutegemea farasi, kuweka imani katika magari (maana wako wengi) na (maana faras haziesabiki). Lakini hawausiani na Mtakatifu wa Israeli, wala hawamtafuti Yahwe!
- Yosia aliondoa farasi ambao wafalme wa Yuda walikuwa wamewaweka wakfu kwa jua2 Fal 23:11
Aya
2 Fal 23:11Akawachukua farasi ambao wafalme wa Yuda waliokuwa wametolewa kwa ajili ya jua. Walikuwa kwenye eneo la lango la uingilia kwenye hekalu la Yahwe, karibu na chumba cha Nathani Meleki, msimamizi mkuu wa nyumba ya mfalme. Yosia akayachoma yale magari ya farasi ya jua
- Mordekai alitembezwa mjini juu ya farasi wa mfalme mwenyeweEst 6:8–11
Aya
Est 6:8–11avikwe nguo za kifalme, mavazi ambayo mfalme amekwisha yavaa na farasi ambaye ametumiwa na mfalme na ambaye ana taji ya kifalme kichwani mwake. Nguo hizo na farasi apewe msimamizi bora kuliko wote. Na wamvike yule ambaye mfalme ampenda na kumuheshimu, na wampandishe juu ya farasi na kumpitisha katika mitaa yote ya mji. Na watangaze mbele yake, “Hivi ndivyo alivyofanyiwa mtu yule ambaye mfalme ampenda na kumuheshimu!” Kisha mfalme akamwambia, Hamani “fanya hima, mvike Modekai nguo na umpandishe kwenye farasi, na lisipungue hata jambo moja katika hayo uliyo yasema.” Kisha Hamani akachukua mavazi na farasi. Akamvika Modekai na akampandisha kwenye farasi na kumpitisha katika mitaa yote ya mji. Akatangaza mbele zake, “Hii imefanyika kwa mtu ambaye mfalme anampenda na kumuheshimu!”
- Eliya alitenganishwa na Elisha kwa gari la moto na farasi wa moto2 Fal 2:11
Aya
2 Fal 2:11Ikawa walipokuwa bado wakienda mbele na kuzungumza, gari la kukokotwa na farasi lenye moto na farasi wa moto ikatokea, ambapo iliwatenga wale watu wawili kutoka kila mmoja, na Eliya akaenda juu kwa uvumi wa upepo kwenda mbinguni.
Misemo
- “Farasi wake ni wepesi kuliko tai”Yer 4:13
Aya
Yer 4:13Tazama anavamia kama wingu, na magari yake ni kama dhoruba. Farasi wake wana mbio kuliko tai. Ole wetu kwa kuwa tutaharibiwa!
- “Farasi wao ni wepesi kuliko chui, wakali kuliko mbwa mwitu wa usiku”Hab 1:8
Aya
Hab 1:8Farasi wao pia wanambio sana kuliko chui, wepesi sana kuliko mbwa mwitu wa jioni. Farasi wao huwaseta, na wapanda farasi wao wanakuja kutoka mbali - wanapaa kama tai anayewahi kula.
- “Farasi huwekwa tayari kwa siku ya vita”Mit 21:31
Aya
Mit 21:31Farasi hutayarishwa kwa siku ya mapigano, lakini ushindi hupatikana kwa Yehova.
- Zaburi: hata nguvu nyingi za farasi haziwezi kuokoaZab 33:17
Aya
Zab 33:17Farasi sio salama kwa ajili ya ushindi; ijapokuwa nguvu zake ni nyingi, hawezi kuokoa.
- “Mjeledi kwa farasi, hatamu kwa punda”Mit 26:3
Aya
Mit 26:3Mjeledi ni kwa ajili ya farasi, hatamu kwa ajili ya punda na fimbo ni kwa ajili mgongo wa wapumbavu.
- “Je, farasi hukimbia juu ya miamba?”Amo 6:12
Aya
Amo 6:12Je farasi watakimbia juu ya mteremko wa miamba? Je mtu atalima huko na ng'ome? Bado mmegeuza haki kuwa sumu na tunda la haki kuwa uchungu.
- “Kama umekimbia na watu waendao kwa miguu … utawezaje kushindana na farasi?”Yer 12:5
Aya
Yer 12:5Bwana akasema, “Kweli, wewe, Yeremia, umetembea na askari wa miguu na wamechoka, unawezaje kushindana dhidi ya farasi? Ikiwa unashuka chini ya nchi iliyo salama, utafanyaje katika misitu karibu na Yordani?
Vyanzo
Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0