Maumbile
Nge katika Biblia
Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (8), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.
- Jangwa lilikuwa na nyoka wenye sumu na ngeKum 8:15
Aya
Kum 8:15Usimsahau yeye aliyewaongoza kupitia jangwa kuu na la kutisha, ambako ndani yake kulikuwa na nyoka wa moto na nge, na pitia nchi yenye kiu ambako hapakuwa na maji, ambaye yeye alileta maji toka kwenye mwamba wa jiwe.
- Ezekieli anaambiwa asiogope, ingawa anaishi kati ya ngeEze 2:6
Aya
Eze 2:6Wewe, mwanadamu, usiwaogope au maneno yao. Usiogope, ingawa utakuwa pamoja na mitemba na miiba na ijapokuwa unaishi na nge. Usiogope maneno yao au kuvunjika moyo kwa nyuso zao, kwa kuwa ni nyumba zenye kuasi..
- Yesu anawapa wanafunzi wake mamlaka ya kukanyaga nyoka na ngeLk 10:17, Lk 10:19
Misemo
- Akiomba yai, je, baba atampa nge?Lk 11:12
Aya
Lk 11:12Au akimuomba yai atampa nge badala yake?.
- Rehoboamu: “Baba yangu aliwapiga kwa mijeledi, mimi nitawapiga kwa nge”1 Fal 12:11, 1 Fal 12:14, 2 Nya 10:14
Aya
1 Fal 12:11Kwa hiyo sasa, ingawa baba yangu aliwatwika kongwa zito, Mimi nitaiongeza kongwa lenu. Baba yangu aliwaadhibu kwa mijeredi, Lakini mimi nitawaadhibu kwa nge.'”
1 Fal 12:14Akawaambia akifuata ushauri wa wale vijana; akasema, “Baba yangu aliwatwika kongwa zito, lakini mimi nitaongeze kongwa lenu. Baba yangu aliwaadhibu kwa mijeredi, mimi nitawaadhibu kwa nge.”
2 Nya 10:14Akasema kwao akiufuata ushauri wa wanaume vijana, akisema, “ Baba yangu aliifanya nira yenu nzito, lakini mimi nitaiongeza. Baba yangu aliwaadhibu kwa mijeredi, lakini mimi nitawaadhibu kwa nge.”
Vyanzo
Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0