Gundua › Mada › Mierezi ya Lebanoni
Maumbile
Mierezi ya Lebanoni katika Biblia
Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (32), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.
- Sulemani alinena juu ya miti, toka mwerezi wa Lebanoni hadi hisopo ukutani1 Fal 4:33
Aya
1 Fal 4:33Aliifafanua mimea, kuanzia mierezi iliyoko Lebanoni hadi Hisopo imeao ukutani. Aliwafafanua wanyama, ndege, vitu vitambaavyo na samaki. Watu walikuja kutoka mataifa yote kuisikia hekima ya Sulemani.
- Zaburi: mierezi ya Lebanoni hushibaZab 104:16
Aya
Zab 104:16Miti ya Yahwe hupata mvua nyingi; Mierezi ya Lebanoni aliyoipanda.
- Siku za Sulemani mierezi ilikuwa mingi kama mikuyu ya nchi ya chini1 Fal 10:27, 2 Nya 1:15
Aya
1 Fal 10:27Mfalme alikuwa na fedha kule Yerusalemu, pamoja na mawe ardhini. Alitengeneza miti ya mierezi kuwa mingi kama mikuyu iliyo katika nyanda za chini.
2 Nya 1:15Mfalme akatengeneza fedha na dhahabu kuwa vitu vya kawaida kama mawe katika Yerusalemu, na mbao za mierezi kuwa kama miti ya mikuyu iliyomo katika nyanda za chini.
- Watu wangebadilisha mikuyu iliyokatwa kwa miereziIsa 9:10
Aya
Isa 9:10Matofali yameanguka, lakini tutajenga tena kwa jiwe la patasi; mkuyu umekatwa chini, lakini tutaotesha mierezi katika eneo lao.
- Mwerezi kutoka Lebanoni ulifanywa mlingoti wa meli ya TiroEze 27:5
Aya
Eze 27:5Wametengeneza mbao nene na pana kwa mvinje kutoka Mlima Hermoni; wamechukua mkangazi kutoka Lebanoni kuufanya mlingoti.
- Mti wa mwerezi, hisopo na uzi mwekundu vilitumika katika ibada za utakasoLaw 14:4, Hesabu 19:6
Aya
Law 14:4Ndipo kuhani ataamuru kwamba mtu mwenye kutakaswa lazima achukue ndege safi wawili, waliohai, mti wa mwerezi, kitani nyekundu na hisopo.
Hesabu 19:6Yule kuhani atachukua mti wa mwerezi, na hisopo na sufu na kivitupa katikati ya huyo ng'ombe anayechomwa.
Ujenzi kwa mwerezi
- Hiramu wa Tiro alimtumia Daudi magogo ya mwerezi, maseremala na waashi kwa jumba lake2 Sam 5:11
Aya
2 Sam 5:11Kisha Hiramu mfalme wa Tiro akatuma wajumbe kwa Daudi, na miti ya mierezi, mafundi seremala na wajenzi. Wakamjengea Daudi nyumba.
- Daudi: “Ninaishi katika nyumba ya mwerezi, lakini sanduku liko hemani”1 Nya 17:1
Aya
1 Nya 17:1Ikawa baada ya mfalme kuwa katika nyumba yake, akasema kwa Nathani yule nabii, “Angalia, nina ishi katika nyumba iliyo jengwa na mierezi, lakini sanduku la agano la Yahweh lipo kwenye chini ya hema.”
- Sulemani alimwomba Hiramu mierezi; hakuna aliyekata miti kama Wasidoni1 Fal 5:6
Aya
1 Fal 5:6Kwa hiyo sasa amuru wakate mierezi kutoka Lebanoni kwa ajili yangu. Watumishi wangu wataungana na watumishi wako, nami nitakulipa kwa ajili ya watumishi wako ili kwamba upate malipo mazuri kwa kila kitu utakchokubali kukifanya. Kwa kuwa unajua kuwa hakuna mtu mioingoni mwetu anayejua kukata miti kama Wasidoni.”
- Magogo yalikokotwa hadi baharini na kuelea kama matezi1 Fal 5:8–9, 2 Nya 2:16
Aya
1 Fal 5:8–9Hiramu akatuma neno kwa Sulemani, akisema, “Nimeupata ujumbe ule ulionitumia. Nitatoa miti yote ya mierezi na miti ya miberoshi ambayo unahitaji. Watumishi wangu wataileta miti kutoka Lebanoni hadi baharini, nami nitaiendesha baharini mpaka mahali utakaponielekeza. Nitaigawa pale, nawe utaichukua. Utafanya kile ninachohitaji kwa kuwapa chakula watumishi wangu.”
2 Nya 2:16Tutakata mbao kutoka Lebanoni, mbao nyingi kadri unavyohitaji. Tutazileta kwako kama mitumbwi kupitia bahari kwenda Yafa, na utazibeba hadi Yerusalemu.”
- Wakataji miti wa Hiramu walilipwa ngano, shayiri, divai na mafuta ya zeituni2 Nya 2:10
Aya
2 Nya 2:10Angalia, nitawapa watumishi wako, watu watakaozikata mbao, kori ishirini elfu za ngano ya aridhini, kori ishirini elfu za shayiri, bathi ishirini elfu za mvinyo, na bathi ishirini elfu za mafuta.” (Maandishsi ya kale yanasema: “kori ishirini elfu za ngano kama chakula”).
- Waisraeli 30,000 walifanya kazi Lebanoni kwa zamu za mwezi za 10,0001 Fal 5:13–14
Aya
1 Fal 5:13–14Mfalme Sulemani akaandaa wafanya kazi kutoka Israeli yote. Idadi ya watenda kazi walioandaliwa ilikuwa wanaume elfu thelathini. Aliwatuma kwenda Lebanoni, aliwatuma kwa zamu ya watu elfu kumi kila mwezi. Kwa mwezi mmoja walienda Lebanoni na miezi miwili walikaa nyumbani. Adoniramu ndiye aliyekuwa msimamizi wa watenda kazi.
- Sulemani alimpa Hiramu miji ishirini huko Galilaya kwa ajili ya mwerezi na msonobari1 Fal 9:11
Aya
1 Fal 9:11Basi Hiramu, mfalme wa Tiro, alikuwa amemletea Sulemani mbao za mierezi na miboreshi, pamoa na dhahabu; vitu vyote ambavyo Sulemani alitamani. Kwa hiyo mfalme Sulemani akampatia Hiramu miji ishirini huko Galilaya.
- Hekalu lilisakafiwa juu kwa boriti na mbao za mwerezi1 Fal 6:9–10
Aya
1 Fal 6:9–10Kwa hiyo Sulemani akalijenga hekalu mpaka akalimaliza, akalifunika hekalu kwa boriti na mbao za mwerezi. Akajenga vyumba vya pembeni mwa hekalu, kila upande mita 2. 3 kwenda juu. Navyo vikaunganishwa na hekalu kwa mbao za mierezi.
- Ndani, mwerezi uliochongwa maboga na maua; hakuna jiwe lililoonekana1 Fal 6:15, 1 Fal 6:18
Aya
1 Fal 6:15Kisha akajenga kuta za ndani za hekalu kwa mbao za mwerezi. Kuanzia sakafu ya hekalu hadi boriti za juu, kwa ndani akazifunika kwa miti, na akaifunika sakafu kwa mbao za miberoshi.
1 Fal 6:18Zote zilikuwa za mierezi kwa ndani. Hapakuonekana chochote ndani kilichokuwa kimetengenezwa kwa mawe.
- Ua wa ndani: safu tatu za mawe yaliyochongwa na moja ya boriti za mwerezi1 Fal 6:36
Aya
1 Fal 6:36Akalijengs Korido la ndani kwa safu tatu za mawe ya kuchongwa na safu moja ya mhimili wa mierezi.
- Nyumba ya Msitu wa Lebanoni ilisimama juu ya safu nne za nguzo za mwerezi1 Fal 7:2–3
Aya
1 Fal 7:2–3Aliijenga ikulu iliyoitwa mwitu wa Lebanoni. Urefu wake ulikuwa mita 46, na upanawake ulikuwa mita 23, na kimo chake kilikuwa mita 14. Nayo ilikuwa na safu nne ya nguzo za mierezi na mithili ya mwerezi juu ya nguzo. Paa la ikulu lilikuwa la mwerezi ambalo lilikaa juu ya mihimili. Mihili hiyo ilikuwa imeshikiliwa na nguzo. Kulikuwa na mihimili arobaini na tano, ambayo ilikuwa katika safu kumi na tano.
- Waliorudi kutoka uhamishoni walisafirisha magogo ya mwerezi kutoka Lebanoni hadi YafaEzr 3:7
Aya
Ezr 3:7Hivyo wakatoa fedha kwa wahunzi na fundi wa mkono, na wakawapa chakula, vinywaji na mafuta kwa watu wa Sidoni na Tiro, ili kwamba walete miti ya mierezi kupitia baharini kutoka Lebanoni mpaka Yafa, na kama walivyo ruhusiwa na mfalme Koreshi wa Uajemi.
- Mfalme anaifunika nyumba yake kwa mwerezi na kuipaka rangi nyekunduYer 22:14
Aya
Yer 22:14Ole mtu yeyote atakayesema, 'Nitajenga nyumba ndefu na vyumba vya juu vipana, na hujenga madirisha mapana, na kuta zenye mwerezi, na huipaka rangi nyekundu.'
- “Boriti za nyumba yetu ni mierezi”Wim 1:17
Aya
Wim 1:17Nguzo za nyumba yetu ni za matawi ya mierezi, na dari letu ni la matawi ya miberoshi.
Misemo na hadithi
- Hadithi ya Yehoashi: mbigili unamwomba mwerezi binti yake2 Fal 14:9
Aya
2 Fal 14:9Lakini Yehoashi mfalme wa Israeli akawatuma wajumbe kurudi kwa Amazia mfalme wa Yuda, akisema, “Mbaruti uliokuwa Lebanoni ulituma kwa mwerezi katika Lebanuni, kusema, 'Mpatie mwanangu binti yako amuoe; lakini hayawani aliyekuwako Lebanoni akaukanyaga chini ule mbaruti.
- Hadithi ya Yothamu: moto kutoka mti wa miiba unateketeza miereziAmu 9:15
Aya
Amu 9:15Miti ya miiba ikaiambia miti, 'Ikiwa unataka kunipaka mafuta niwe mfalme juu yako, njoo na upate usalama chini ya kivuli changu. Ikiwa sivyo, basi moto lazima uondoke kwenye mchanga na uiteketeze mierezi ya Lebanoni. '
- Mwamori, mrefu kama mierezi na hodari kama mialoniAmo 2:9
Aya
Amo 2:9Bado nimemwangamiza Mwamori mbele yao, ambaye urefu wake ulikuwa kama urefu wa mierezi; alikuwa na nguvu kama mialoni. Kisha nikaharibu matunda yake juu na mizizi yake chini.
- Zaburi: “atakua kama mwerezi wa Lebanoni”Zab 92:12
Aya
Zab 92:12Wenye haki watastawi kama mtende; watakua kama mwerezi wa Lebanoni.
- “Sauti ya Bwana huivunja mierezi”Zab 29:5
Aya
Zab 29:5Sauti ya Yahwe huivunja mierezi; Yahwe huivunja vipande vipande mierezi ya Lebanon.
- “Mwenye fahari kama mierezi”Wim 5:15
Aya
Wim 5:15Miguu yake ni nguzo za marimari, iliyo ekwa juu ya dhahabu safi; muonekano wake ni kama Lebanoni, mizuri kama mierezi.
- Mierezi inafurahi: “hakuna mkata miti anayekuja juu yetu”Isa 14:8
Aya
Isa 14:8Hata mti wa mseprasi inafuhaia pamoja mierezi ya Lebanoni; inasema, Tangu ulipoweka chini, hakuna mkata kuni aliyekuja kutungusha sisi,
- “Omboleza, ewe msonobari, kwa maana mwerezi umeanguka”Zek 11:2
Aya
Zek 11:2Omboleza, enyi miti ya misonobari, kwani mierezi imeanguka! Kilichokuwa cha fahari kimeteketezwa! Ombolezeni, enyi mialoni ya Bashani, kwani msitu wenye nguvu umeshushwa.
Vyanzo
Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0