Bible Explorer

Gundua › Mada › Umande wa asubuhi

Maumbile

Umande wa asubuhi katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (22), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

  • Umande ulishuka juu ya kambi usiku, na mana pamoja naoHesabu 11:9
    Aya
    Hesabu 11:9Na umande ulipoanguka kambini usiku ule, na mana ilianguka pia.
  • Umande wa asubuhi ulipoondoka, vipande vyembamba vilikuwa juu ya ardhiKut 16:13–14
    Aya
    Kut 16:13–14Ikaja kuwa kwamba jioni kware wakaja juu na kufunika kambi. Asubui umande ulitanda kambini. Umande ulipo kwisha, pale juu ya ardhi ya nyikani kulikuwa na kama barafu iliyo ganda kwenye ardhi.
  • Umande hukaa usiku kucha juu ya matawiAyu 29:19
    Aya
    Ayu 29:19Mizizi yangu imeenea majini, na umande kukaa usiku wote katika matawi yangu.
  • Mawingu yalidondosha umandeMit 3:20
    Aya
    Mit 3:20Kwa maarifa yake vina vilipasuka na mawingu kudondosha umande wake.
  • “Ni nani aliyeyazaa matone ya umande?”Ayu 38:28
    Aya
    Ayu 38:28Je kuna baba wa mvua? Ni nani aliyeyafanya matone ya umande?
  • Mpendwa usiku: “Kichwa changu kimelowa umande”Wim 5:2
    Aya
    Wim 5:2Nilikuwa nimelala, lakini moyo wangu ulikuwa umeamka katika ndoto. Sauti ya mpenzi wangu yabisha na kusema, “Nifungulie, dada yangu, mpenzi wangu, hua wangu, wangu usiye na doa, kwa kuwa kichwa changu kimelowa na matone, nywele zangu na unyevu wa usiku.”
  • Nebukadneza alilowa kwa umande wa mbinguniDan 4:33
    Aya
    Dan 4:33Agizo hili kinyume na Nebukadneza lilitekelezwa ghafla. Aliondolewa miongoni mwa watu. Alikula majani kama ng'ombe, na mwili wake ulilowa kwa umande wa kutoka mbinguni. Nywele zake zilirefuka kama manyoa ya tai, na makucha yake yalikuwa kama makucha ya ndege.
  • Umande wa Hermoni ukishuka juu ya milima ya SayuniZab 133:3
    Aya
    Zab 133:3Ni kama umande wa Hermoni uangukao milimani pa Sayuni. Maana huko ndiko Bwana alipoamuru baraka, naam uzima milele na milele.

Katika masimulizi

  • Gideoni alikamua bakuli zima la maji kutoka kwenye ngozi ya kondooAmu 6:37–38
    Aya
    Amu 6:37–38tazameni, ninaweka ngozi ya samazi kwenye sakafu. Ikiwa kuna umande tu juu ya ngozi, na ni kavu duniani, basi nitajua kwamba utanitumia kuokoa Israeli, kama ulivyosema.” Hivi ndivyo ilivyotokea-Gideoni aliamka mapama asubuhi, akaikamua ngozi hiyo, na akatoa umande kwenye ngozi, wa kutosha kujaza bakuli kwa maji.
  • Usiku uliofuata ngozi ilikuwa kavu na umande ulifunika ardhiAmu 6:39–40
    Aya
    Amu 6:39–40Gideoni akamwambia Mungu, 'Usinikasirikie, nitasema tena kwa mara nyingine. Tafadhali niruhusu nijaribu tena kwa kutumia ngozi. Wakati huu uifanye kavu, na iwe na umande juu ya ardhi yote kuzunguka. Mungu alifanya kile alichoomba usiku huo. Ngozi ilikuwa kavu, na kulikuwa na umande katika ardhi yote iliyozunguka.
  • Eliya kwa Ahabu: hakuna umande wala mvua katika miaka hii1 Fal 17:1
    Aya
    1 Fal 17:1Eliyas Mtishibi, kutoka Tishibi ya Gileadi, akamwambia Ahabu, “Kama BWANA, Mungu wa Israeli aishivyo, ambaye ninasimama, hakutakuwa na umande wala mvua isiipokuwa kwa neno langu.”
  • Maombolezo ya Daudi: “Enyi milima ya Gilboa, msiwe na umande wala mvua”2 Sam 1:21
    Aya
    2 Sam 1:21Milima ya Gilboa, kusiwe na umande au mvua juu yenu. wala mashamba yasitoe nafaka kwa ajili ya sadaka, kwa maana hapo ngao ya mwenye nguvu imeharibiwa. Ngao ya Sauli haiwezi tena kutiwa mafuta.
  • Hagai: mbingu zilizuia umande wake na nchi mazao yakeHag 1:10
    Aya
    Hag 1:10Kwa sababu hii mbingu zimeshikiwa zisitoe umande kutoka kwako, na ardhi imeshikilia haizalishi.

Baraka

  • Baraka ya Isaka: umande wa mbinguni na unono wa nchiMwa 27:28
    Aya
    Mwa 27:28Mungu akupe sehemu ya umande wa mbinguni, sehemu ya unono wa nchi, na wingi wa nafaka na mvinyo mpya.
  • Esau angeishi mbali na umande wa mbinguniMwa 27:39
    Aya
    Mwa 27:39Isaka baba yake akajibu na kumwambia, “Tazama, mahali unapoishi patakuwa mbali na utajiri wa nchi, mbali na umande juu angani.
  • Musa: nchi ya Yusufu imebarikiwa kwa umande wa thamani kutoka mbinguniKum 33:13
    Aya
    Kum 33:13Kuhusu Yusufu, Musa akasema: Nchi yake na ibarikiwe na Yahwe na vitu vya thamani vya mbinguni, na umande, na kina kilalacho chini.
  • Nchi ya nafaka na divai mpya, ambako mbingu hudondosha umandeKum 33:28
    Aya
    Kum 33:28Israeli waliishi katika usalama. Wana wa Yakobo walikuwa salama katika nchi ya nafaka na divai mpya; hakika, mbingu na idondoshe umande juu yake.

Misemo

  • “Kama umande wa asubuhi unaotoweka”Hos 6:4, Hos 13:3
    Aya
    Hos 6:4Efuraimu, nikufanyie nini? Yuda, nikufanyie nini? Uaminifu wako ni kama wingu la asubuhi, kama umande unaoondoka mapema.
    Hos 13:3Kwa hiyo watakuwa kama mawingu ya asubuhi, kama umande unaoondoka mapema, kama makapi yanayotokana na upepo kutoka kwenye sakafu, na kama moshi utokao kwenye bomba.
  • Kibali cha mfalme “ni kama umande juu ya majani”Mit 19:12
    Aya
    Mit 19:12Ghadhabu ya mfalme ni kama muungurumo wa simba kijana, bali fadhila yake ni kama umande kwenye majani.
  • “Tutamwangukia kama umande uangukavyo juu ya ardhi”2 Sam 17:12
    Aya
    2 Sam 17:12Kisha tutampata popote atakapokuwa nasi tutamfunika kama umande uangukavyo juu ya nchi. Hatutamwachia hata mmoja aliye hai kati ya watu wake wala yeye mwenyewe.
  • “Kama wingu la umande katika joto la mavuno”Isa 18:4
    Aya
    Isa 18:4Yahwe asema hivi, ''nitachunguza kimyakimya kutoka nyumbani kwangu, kama kupika joto kwenye jua, na kama ukungu kwenye joto la mavuno.

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0