Bible Explorer

Gundua › Mada › Bahari

Maumbile

Bahari katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (32), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

  • Maji yaliyokusanyika yaliitwa “bahari”Mwa 1:9–10
    Aya
    Mwa 1:9–10Mungu akasema, “maji yaliyo chini ya mbingu yakusanyike pamoja mahali pamoja, na ardhi kavu ionekane.” Ikawa hivyo. Mungu aliita ardhi kavu “nchi,” na maji yaliyo kusanyika akayaita “bahari.” Akaona kuwa ni vyema.
  • Viumbe wakubwa wa baharini waliumbwa siku ya tanoMwa 1:21–23
    Aya
    Mwa 1:21–23Mungu akaumba viumbe wakubwa wa baharini, pamoja na kila kiumbe hai cha aina yake, viumbe waendao na wanaojaa kila mahali majini, na kila ndege mwenye mabawa kwa aina yake. Mungu akaona kuwa ni vyema. Mungu akavibariki, akisema, “zaeni na muongezeke, na mjae majini katika bahari. Ndege waongezeke juu nchi.” Ikawa jioni na asubuhi, siku ya tano.
  • Bahari, kubwa na pana, imejaa viumbe, ambako meli hupitaZab 104:25–26
    Aya
    Zab 104:25–26Kule kuna bahari, yenye kina kirefu na pana, ikiwa na viume vingi visivyo hesabika, vyote vidogo na vikubwa. Meli husafili humo, na ndimo alimo Lewiathani uliye muumba acheze baharini.
  • Mito yote huingia baharini, lakini bahari haijaiMhu 1:7
    Aya
    Mhu 1:7Mito yote hutiririka katika bahari, lakini bahari haijai. Mahali mito inakoenda, ndiko inakoenda tena.
  • Mchanga ni mpaka ambao mawimbi hayawezi kuuvukaYer 5:22, Ayu 38:8–11
    Aya
    Yer 5:22Je, hamnihofu mimi - asema BWANA - au kutetemeka mbele ya uso wangu? Nimeweka mpaka wa mchanga kwenye bahari, ambao ni agizo la kudumu ambalo halibomoki - hata kama bahari ina kupwa na kujaa, bado hauwenzi kubomoka. Hata kama mawimbi yake yanaunguruma, hayawezi kuvuka.
    Ayu 38:8–11Ni nani huifunga bahari kwa milango wakati inapofurika, kana kwamba inatoka katika tumbo, wakati nilipoyafanya mawingu kuwa ni mavazi yake, na giza nene kuwa mkanda wake wa kujifungia? Hapo ilikuwa wakati nilipoweka bahari mpaka wangu, na nilipoweka makomeo yake na milango, na wakati nilipoiambia, 'Unaweza kuja hapa kutoka mbali, lakini si zaidi; na hapa ndipo nitauweka mpaka kwa fahari ya mawimbi yako.'
  • Mabaharia juu ya mawimbi hupanda hadi mbinguni na kushuka hadi vilindiniZab 107:23–27
    Aya
    Zab 107:23–27Baadhi husafiri baharini katika meli na kufanya biashara juu ya bahari. Hawa huona matendo ya Yahwe na maajabu yake baharini. Kwa maana aliamuru na alivumisha upepo wa dhoruba ambao uliyainua juu mawimbi ya baharini. Walipanda juu mawinguni na kushuka vilindini. Nafsi zao ziliyeyuka katika dhiki. Waliyumba-yumba na kupepesuka kama walevi na hawakujua la kufanya.

Bahari za nchi

  • Bahari Kuu ilikuwa mpaka wa magharibiHesabu 34:6, Yos 1:4
    Aya
    Hesabu 34:6Mpaka wa Magharibi utakuwa pwani ya bahari kuu. Huu ndio utakuwa mpaka wenuwa Magharibi.
    Yos 1:4kuanzia jangwani na Lebanoni, hadi mto mkubwa wa Frati, nchi yote ya Wahiti, na hata Bahari kuu, ambako jua huzama, itakuwa nchi yenu.
  • Bahari ya Chumvi, mahali lilipokuwa Bonde la SidimuMwa 14:3
    Aya
    Mwa 14:3Hawa wafalme watano wa mwisho waliungana pamoja katika bonde la Sidim (pia likiitwa bahari ya chumvi).
  • Maji ya Yordani kwenda Bahari ya Chumvi yalikatika Israeli walipovukaYos 3:16
    Aya
    Yos 3:16maji yote yaliyotiririka kutoka juu yalisimama katika chuguu kimoja. Maji yakakoma kutiririka kutoka katika umbali mrefu. Maji yaliacha kutiririka kutoka Adam, mji ulio karibu na Zarethani, hadi bahari ya Negevu, Bahari ya Chumvi. Na watu walivuka ng'ambo karibu na Yeriko.
  • Mipaka kutoka Bahari ya Shamu hadi Bahari ya WafilistiKut 23:31
    Aya
    Kut 23:31Nitatengeneza mipaka yako kutoka Bahari ya Shamu hadi Bahari ya Wafilisti, na kutoka nyikani hadi Mto Frati. Nitakupa ushindi juu ya wakazi wote wa nchi. Utawaondoa kutoka kwako mwenyewe.
  • Sulemani alijenga merikebu huko Ezioni Geberi pwani ya Bahari ya Shamu1 Fal 9:26
    Aya
    1 Fal 9:26Tena Sulemani alitengeneza merikebu kule Ezioni Geberi, ambayo iko karibu na Elathi katika ufukwe wa bahari ya shamu, katika nchi ya Edomu.
  • Petro na Andrea walitupa nyavu katika Bahari ya GalilayaMt 4:18
    Aya
    Mt 4:18Alipokuwa akitembea kandokando ya Bahari ya Galilaya, aliwaona ndugu wawili, Simoni aliyekuwa akiitwa Petro, na Andrea kaka yake, wakitega nyavu baharini, kwa kuwa walikuwa wavuvi wa samaki.

Katika masimulizi

  • Upepo wa mashariki uliirudisha bahari; Israeli walivuka katika nchi kavuKut 14:21–22
    Aya
    Kut 14:21–22Musa akanyoosha mkono wake kuelekea bahari. Yahweh akasogeza bahari nyuma kwa upepo mkali wa mashariki usiku huo wote na kufanya bahari nchi kavu. Kwa namna hii maji yaligawanyika. Waisraeli walienda katikati ya bahari kwa nchi kavu. Maji yaliunda ukuta mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto.
  • Kulipopambazuka bahari ilirudi na kufunika magari ya FaraoKut 14:27–28
    Aya
    Kut 14:27–28Hivyo Musa akanyoosha mkono wake kuelekea bahari, na ikarudi kwenye hali yake ya kawaida palipo pambazuka. Wamisri walikimbilia ndani ya bahari, na Yahweh akawaingiza Wamisri katikati ndani yake. Maji yakarudi na kufunika magari ya farasi ya Farao, wapanda farasi, na jeshi lake lote lililo fuata magari ya farasi kwenye bahari. Hakuna aliyepona.
  • Mabaharia wa Yona walitupa mizigo baharini kuipunguzia meli uzitoYon 1:4–5
    Aya
    Yon 1:4–5Lakini Bwana akatuma upepo mkubwa juu ya bahari, ikawa tufani juu ya bahari. Hivi karibuni ikaonekana kwamba meli ilikuwa inataka kuvunjika. Wale baharia waliogopa sana na kila mtu alilia kwa mungu wake mwenyewe. Wakatupa mizigo bahari iliyokuwa merikebuni ili kuifungua. Yona alikuwa ameshuka hapa pande za ndani ya melikebu, naye alikuwa amelala huko usingizi.
  • Yona alipotupwa baharini, bahari iliyochafuka ikatuliaYon 1:15
    Aya
    Yon 1:15Basi wakamchukua Yona wakamtupa baharini, nayo bahari ikaacha kuchafuka.
  • Samaki mkubwa alimmeza YonaYon 1:17
    Aya
    Yon 1:17Bwana alikuwa ameandaa samaki mkubwa kummeza Yona, na Yona alikuwa ndani ya tumbo lasamaki siku tatu na usiku wa tatu.
  • Yesu alilala juu ya mto katika shetri huku mawimbi yakiipiga mashuaMk 4:37–39
    Aya
    Mk 4:37–39Na upepo mkali wa dhoruba na mawimbi yalikuwa yakiingia ndani ya mtumbwi na mtumbwi tayali ulikuwa umejaa. Lakini Yesu mwenyewe alikuwa kwenye shetri, amelala kwenye mto. Wakamwamsha, wakisema, “Mwalimu, haujali sisi tunakufa?” Na akaamka, akaukemea upepo na akaiambia bahari, “'Iwe shwari, amani”. Upepo ukakoma, na kulikuwa na utulivu mkubwa.
  • Yesu alitembea juu ya bahari katika zamu ya nne ya usikuMt 14:25–26
    Aya
    Mt 14:25–26Katika usiku wa zamu ya nne Yesu aliwakaribia, akitembea juu ya maji. Wakati wanafunzi wake walipomwona akiitembea juu ya bahari, walihofu na kusema, “Ni mzuka,'' na kupaaza sauti katika hali ya uoga.
  • Petro alishuka kutoka mashua akatembea juu ya majiMt 14:28–29
    Aya
    Mt 14:28–29Petro alimjibu kwa kusema, “Bwana, kama ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji.'' Yesu akasema, “Njoo.'' Hivyo Petro akatoka ndani ya mashua na akatembea juu ya maji kwenda kwa Yesu.
  • Sarafu katika kinywa cha samaki wa kwanza aliyevuliwaMt 17:27
    Aya
    Mt 17:27Lakini tusije tukawafanya watoza ushuru wakatenda dhambi, nenda baharini, tupa ndoano, na umtwae yule samaki ajaye kwanza. Baada ya kuufungua mdomo wake, utakuta mle shekeli moja. Ichukue na uwape watoza ushuru kwa ajili yangu na wewe.
  • Samaki wakubwa 153, na wavu haukupasukaYn 21:11
    Aya
    Yn 21:11Basi Simon Petro akapanda na kuukokota ule wavu uliokuwa umejaa samaki wakubwa, kiasi cha samaki 153; japo walikuwa wengi, ule wavu haukuchanika.
  • Nguruwe wapatao elfu mbili walikimbia kwenye mteremko wakaingia bahariniMk 5:13
    Aya
    Mk 5:13Hivyo aliwaruhusu; roho wachafu waliwatoka na kuingia ndani ya nguruwe, nao walikimbilia chini ya kilima mpaka baharini, na karibia nguruwe elfu mbili walizama baharini.
  • Vipimo vya kina katika Adria: maji yanazidi kupungua kinaMdo 27:27–28
    Aya
    Mdo 27:27–28Ulipofika usiku wa kumi na nne, tulipokuwa tukiendeshwa huko na huko kwenye bahari ya Adratik, kama usiku wa manane hivi, mabaharia walifikiri kwamba wamekaribia nchi kavu. Walitumia milio kupima kina cha maji na wakapata mita thelathini na sita, baada ya muda mfupi wakapima tena wakapata mita ishirini na saba.

Bahari ya hekaluni

  • Bahari ya chuma cha kuyeyushwa ya Sulemani: birika kubwa la mviringo1 Fal 7:23
    Aya
    1 Fal 7:23Tena akafanya bahari ya kusubu ya, yenye mita 2. 3 kutoka ukingo hadi ukingo, kimo chake kilikuwa mita 4. 6, mziingo wake ulikuwa mita 13. 7.
  • Ilisimama juu ya ng’ombe kumi na wawili, watatu wakielekea kila upande1 Fal 7:25
    Aya
    1 Fal 7:25Bahari ikakaa juu ya makisai kumi na mbili, tatu, zilitazama kaskazini, tatu zikitazama magharibi, tatu zikitazama kusini na tatu zikitazama kaskazini. Ile bahari iliwekwa juu yao, na pande zao zote za nyuma zilikuwa ndani.

Misemo

  • Uzao “kama mchanga wa pwani ya bahari”Mwa 22:17, Mwa 32:12
    Aya
    Mwa 22:17hakika nitakubariki na nitakuzidishia uzao wako kama nyota za angani, na kama mchanga ulioko kwenye ufukwe wa bahari; na uzao wakowatamiliki lango la adui zao.
    Mwa 32:12Lakini ulisema, 'hakika nitakufanya ufanikiwe. Nitaufanya uzao wako kuwa kama mchanga wa bahari, ambao hauwezi kuhesabika kwa hesabu yake.”
  • Ufahamu wa Sulemani “kama mchanga wa pwani ya bahari”1 Fal 4:29
    Aya
    1 Fal 4:29Mungu alimpa Sulemani hekima kubwa, ufahamu, na upana wa uelewa kama mchanga wa baharini.
  • Bahari iliyochafuka haiwezi kutulia; mawimbi yake hutoa matopeIsa 57:20
    Aya
    Isa 57:20Lakini waovu ni kama bahari iliyochafuka, haiwezi kutulia, na maji yake yametanda juu ya matope.

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0