Maumbile
Milima katika Biblia
Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (41), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.
- “Milima mirefu ni kwa ajili ya mbuzi wa porini”Zab 104:18
Aya
Zab 104:18Mbuzi mwitu huishi kwenye milima mrefu; na urefu wa milima ni kimilio la wibari.
- Milima inauzunguka YerusalemuZab 125:2
Aya
Zab 125:2Kama milima inavyo izunguka Yerusalemu, hivyo ndivyo Yahwe anavyo wazunguka watu wake sasa na hata milele.
- Nchi ambayo vilima vyake vinaweza kuchimbwa shabaKum 8:9
Aya
Kum 8:9Ni nchi ambayo mtakula mkate bila kupungukiwa, na ambapo mtaenda bila chochote; nchi ambayo mawe yametengenezwa kwa chuma, na kutokana na milima mtaweze kuchimba shaba.
- Mchimbaji hupiga jiwe gumu na kupindua milima kwenye misingi yakeAyu 28:9
Aya
Ayu 28:9Mtu huchimba mwamba mgumu; hupindua milima katika vyanzo vyake.
- Mlima humomonyoka na kubomokaAyu 14:18
Aya
Ayu 14:18Lakini hata milima huanguka na kuwa si chochote; hata miamba huhamishwa kutoka mahali pake;
- Vilele vya Lebanoni: Amana, Seniri, Hermoni, mapango ya simba na chuiWim 4:8
Aya
Wim 4:8Njoo nami kutoka Lebanoni, bibi arusi wangu. Njoo nami kutoka Lebanoni; njoo kutoka juu ya Amana, kutoka juu ya Seneri na Herimoni, kutoka shimoni mwa simba, kutoka mashimo ya milima ya chuwi.
- Sulemani alikuwa na wachonga mawe 80,000 milimani1 Fal 5:15
Aya
1 Fal 5:15Sulemani alikuwa na watu elfu sabini waliokuwa wabeba mizigo na watu elfu themanini wa kukata mawe milimani,
- Kwa sababu ya Midiani, Israeli walijifanyia maficho milimani na mapangoniAmu 6:2
Aya
Amu 6:2Uwezo wa Midiani uliwanyanyasa Israeli. Kwa sababu ya Midiani, watu wa Israeli walitengeneza makao wenyewe kutoka kwenye mabwawa katika milima, mapango, na ngome.
- Bendera iliyoinuliwa juu ya kilima kilicho wazi ilikuwa isharaIsa 13:2, Isa 18:3
- “Walio Uyahudi wakimbilie milimani”Mt 24:16
Aya
Mt 24:16ndipo walioko Yuda wakimbilie milimani.
- Mahali pa ibada juu ya vilima chini ya miti yenye kivuliHos 4:13, Kum 12:2
Aya
Hos 4:13Wanatoa sadaka juu ya milima na kuteketeza uvumba kwenye milima, chini ya mialoni, milibua na miela, kwa sababu kivuli ni nzuri. Basi binti zenu hufanya uasherati, na binti zenu wanazini.
Kum 12:2Hakika mtaharibu maeneo yote ambapo mataifa mtakayofukuza miungu yao walioabudu, kwenye milima mirefu, kwenye vilima, na chini ya kila mti wa kijani.
Milima katika masimulizi
- Safina ilitua juu ya milima ya AraratiMwa 8:4
Aya
Mwa 8:4safina ikatulia katika mwezi wa saba, siku ya kumi na saba ya mwezi, juu ya milima ya Ararati.
- Vilele vya milima vilionekana siku ya kwanza ya mwezi wa kumiMwa 8:5
Aya
Mwa 8:5Maji yakaendelea kuzama chini hadi mwezi wa kumi. Siku ya kwanza ya mwezi, vilele vya milima vikaonekana.
- Abraham alitumwa mlimani katika nchi ya MoriaMwa 22:2
Aya
Mwa 22:2Kisha Mungu akasema, “Mchukue mwanao, mwanao wa pekee, umpendaye, Isaka, na uende katika nchi ya Moria. Mtoe kama sadaka ya kuteketezwa mahali pale juu ya moja ya milima hiyo, ambayo nitakwambia.”
- Musa alifika na kundi Horebu, mlima wa MunguKut 3:1
Aya
Kut 3:1Wakati huu Musa aliendelea kuchunga mifugo ya Yethro baba mkwe wake, kuhani wa Midiani. Musa aliliongoza kundi la mifugo kuelekea upande wa mbali wa jangwa mpaka kufika Horebu, mlima wa Mungu.
- Mpaka uliwazuia watu wasiuguse Mlima SinaiKut 19:12
Aya
Kut 19:12Lazima uweke mipaka kote kuzunguka mlima kwa ajili ya watu. Uwaambie, 'Kuweni waangalifu msiende juu ya mlima au kushika mipaka yake. Yeyote atakaye shika mlima ata uawa.'
- Sinai ulitoa moshi kama tanuru na kutetemeka sanaKut 19:18
Aya
Kut 19:18Mlima Sina ulijwa kabisa na moshi kwasababu Yahweh alishuka na moto na moshi. Moshi ulipanda juu kama moshi wa tanuru, na mlima wote ulitikisika kwa vurugu.
- Musa alikaa mlimani siku arobaini mchana na usikuKut 24:18
Aya
Kut 24:18Musa akaingia kwenye wingu na kwenda juu ya mlima. Alikuwa mlimani siku arobaini na usiku arobaini.
- Haruni alikufa juu ya kilele cha Mlima HoriHesabu 20:27–28
Aya
Hesabu 20:27–28Musa akafanya kama BWANA alivyomwamuru. Wakaenda juu y a Mlima Hori na watu wote wakiona. Musa akamvulisha Haruni yale mavazi ya kikuhani na kumvalisha Mwanaye Eliazari. Haruni akafa pale juu ya Mlima Hori. Kisha Musa na Eliazari wakashuka.
- Kutoka Mlima Nebo, kilele cha Pisga, Musa aliiona nchiKum 34:1
Aya
Kum 34:1Musa aliondoka kutoka nyanda za Moabu mpaka mlima wa Nebo, hadi kilele cha Pisga, kilicho mkabala na Yericho. Huko Yahwe alimwonyesha nchi yote ya Gileadi kutoka umbali wa Dani,
- Makabila sita walisimama juu ya Mlima Gerizimu na sita juu ya Mlima EbaliKum 27:12–13
Aya
Kum 27:12–13“Makabila haya yanapaswa kusimama katika mlima Gerizimu kuwabariki watu baada ya nyinyi kuvuka Yordani; Simeoni, Lawi, Judah, Isakari, Yusufu na Benyamini. Haya ni makabila ambayo lazima yasimame juu yam lima Ebali kutamka laana: Rubeni, Gadi, Asheri, Zabuloni, Dan na Naftali.
- Yothamu alipaza sauti hadithi yake kutoka kilele cha Mlima GerizimuAmu 9:7
Aya
Amu 9:7Yotamu alipoambiwa juu ya jambo hilo, akaenda, akasimama juu ya Mlima Gerizimu. Alipiga kelele akawaambia, 'Sikilizeni, enyi viongozi wa Shekemu, ili Mungu awasikilize.
- Baraka alikusanya watu elfu kumi kwenye Mlima TaboriAmu 4:6
Aya
Amu 4:6Akamtuma Baraka mwana wa Abinoamu kutoka Kedeshi huko Naftali. Akamwambia, Bwana, Mungu wa Israeli, anakuamuru, Nenda katika mlima wa Tabori, uende pamoja nawe watu elfu kumi kutoka Naftali na Zabuloni.
- Sauli na Daudi pande mbili za mlima mmoja1 Sam 23:26
Aya
1 Sam 23:26Sauli akaenda akawa upande mmoja wa mlima, na Daudi na watu wake walikuwa wakienda upande mwingine wa mlima. Daudi kwa haraka akatoweka akae mbali na Sauli. Kwa sababu Sauli na watu wake walikuwa wakimzunguka Daudi na watu wake wawakamate,
- Sauli na wanawe watatu walianguka juu ya Mlima Gilboa1 Sam 31:8
Aya
1 Sam 31:8IKawa katika siku iliyofuata, Wafilisti wakafika kuchukua nyara za waliokufa, ndipo wakamuona Sauli na wanawe watatu wameanguka juu ya mlima wa Gilboa.
- Eliya aliwakusanya Israeli na manabii wa Baali juu ya Mlima Karmeli1 Fal 18:19–20
Aya
1 Fal 18:19–20Kwa hiyo sasa, Tuma neno na unikusanyie Israeli yote katika mlima Kameli, pamoja na manabii 450 wa Baali na wale manabii 400 wa Ashera wanaokula kwenye meza ya Yezebeli.” Kwa hiyo Ahabu akatuma neno kwa watu wote wa Israeli na akawakusanya manabii wote kwenye mlima Kameli.
- Juu ya kilele cha Karmeli Eliya aliweka uso wake kati ya magoti yake1 Fal 18:42
Aya
1 Fal 18:42Kwa hiyo Ahabu akaenda akala na knywa. Kisha Eliya akaenda juu ya mlima Kameli, akasudu chini na akaweka uso wake katikati ya magoti.
- Mwanamke Msamaria: “Baba zetu waliabudu katika mlima huu”Yn 4:20
Aya
Yn 4:20Baba zetu waliabudu katika mlima huu. Lakini ninyi mwasema ya kuwa Yerusalemu ndiyo sehemu ambayo watu wanapaswa kuabudu.”
- Yesu alipanda mlimani akaketi kufundishaMt 5:1
Aya
Mt 5:1Yesu alipo uona umati, akaondoka na kuelekea Mlimani. Alipokuwa ameketi chini, wanafunzi wake wakaja kwake.
- Yesu alipanda mlimani peke yake kuombaMt 14:23, Lk 6:12
- Yesu aligeuka sura juu ya mlima mrefuMt 17:1–2
Aya
Mt 17:1–2Siku sita baadaye Yesu aliwachukua pamoja naye Petro, na Yakobo, na Yohana nduguye, na akawachukua mpaka juu ya mlima mrefu wao wenyewe. Alibadilishwa mbele yao. Uso wake ukang'aa kama jua, na nguo zake zilionekana zenye kung'aa kama nuru.
- Nazareti ilikuwa juu ya kilima chenye genge pembeniLk 4:29
Aya
Lk 4:29Walisimama na kumsukumizia nje ya mji, na kumwongoza mpaka kwenye ukingo wa mlima wa mji ambapo mji wao ulijengwa juu yake, ili waweze kumtupa chini.
- Yesu alikaa jioni zake katika Mlima wa MizeituniLk 21:37
Aya
Lk 21:37Hivyo wakati wa mchana alikuwa akifundisha hekaluni na usiku alitoka nje, na kwenda kukesha katika mlima unaoitwa wa Mzeituni.
- Mlima wa Mizeituni: mwendo wa siku ya Sabato kutoka YerusalemuMdo 1:12
Aya
Mdo 1:12Ndipo wakarudi Yerusalemu kutoka kwenye mlima wa mizeituni, ambao uko karibu na Yerusalemu, mwendo wa siku ya Sabato.
Misemo
- “Kama Tabori kati ya milima na kama Karmeli kando ya bahari”Yer 46:18
Aya
Yer 46:18Kama niishivyo - hili ni tamko la mfalme - Yahwe wa majeshi kwa jina, kuna mtu atakuja aliye kama Mlima Tabori na Mlima Karmeli kando ya bahari.
- Imani inayoweza kuuambia mlima huu uhameMt 17:20, Mt 21:21
Aya
Mt 17:20Yesu akawaambia, “Kwa sababu ya imani yenu ndogo. Kweli nawaambieni, kama mtakuwa na imani hata ndogo kama punje ya mbegu ya haradali, mtaweza kuuambia mlima huu, hama kutoka hapa uende kule, nao utahama na hakutakuwa na kitu chochote cha kushindikana kwenu.
Mt 21:21Yesu akajibu na kuwaambia, “Kweli nawaambieni, kama mkiwa na imani na bila wasiwasi, hamtafanya kile kilichofanyika kwa huo mtini tu, lakini mtauambia hata huo mlima, ' uchukuliwe na ukatupwe baharini, 'na itafanyika.
- “Nitayainua macho yangu kuvielekea vilima”Zab 121:1
Aya
Zab 121:1Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu. Nitayainua macho yangu nitazame milimani. Msaada wangu utatoka wapi?
Vyanzo
Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0