Maumbile
Simba katika Biblia
Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (31), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.
- Simba hunguruma juu ya mawindo yake; mwana simba hunguruma pangoni mwakeAmo 3:4
Aya
Amo 3:4Je simba huunguruma msituni wakati hakuna mawindo? Je mwana simba ataunguruma kutoka pangoni mwake kama hajakamata kitu?
- Simba jike na wana simba hujikunyata mapangoni na kuvizia vichakaniAyu 38:39–40
Aya
Ayu 38:39–40Je waweza kuwinda mawindo kwa ajili ya simba jike au kutosheleza hamu ya watoto wadogo wa simba wakati wanapokwaruza kwaruza katika pango lao na kukaa katika kificho ili kulala katika hali ya kuvizia?
- Simba aliwararua mawindo kwa ajili ya watoto wake na kujaza mapango yake mawindoNah 2:11–12
Aya
Nah 2:11–12Sasa liko wapi pango la simba, sehemu ambapo simba wadogo hula chakula, sehemu ambapo simba dume na simba jike walitembea, pamoja wana-simba, ambapo hawakuogopa kitu chochote? Simba alirarua mawindo yake vipande vipande kwa ajili ya watoto wake; aliwanyonga mawindo wake kwa ajili ya wake zake, na kulijaza pango lake mawindo, makao yake kwa mizoga iliyoraruliwa.
- Simba mzee hufa kwa kukosa mawindo; watoto wa simba jike hutawanyikaAyu 4:10–11
Aya
Ayu 4:10–11Kuunguruma kwa simba, sauti ya simba mkali, meno ya simba wadogo - yamevunjika. Simba mzee huangamia kwa kukosa wahanga; watoto wa simba jike wametawanyiko kila mahali.
- Hodari kati ya wanyama, harudi nyuma mbele ya chochoteMit 30:30
Aya
Mit 30:30simba, aliyeimara miongoni mwa wanyama- wala hajiepushi na kitu chochote;
- Simba waliishi katika vichaka vya YordaniYer 49:19, Yer 50:44, Zek 11:3
Aya
Yer 49:19Tazama, nitapanda kama simba kutoka katika misitu ya Yordani hata eneo la malisho mabichi. Maana nitaharakisha kumfanya Edomu kumkimbia, nami nitamweka mwingine atakayekuwa amechaguliwa kwa usimamizi huo. Maana ni nani aliyekama mimi, ni nani atakayeniagiza kuja? Mchungaji gani awezaye kunizuia?
Yer 50:44Tazama! Anakwenda juu kama simba atokaye katika miinuko ya Yordani kuelekea katika eneo la malisho ya uvumilivu. Maana kwa haraka nitawafanya wakimbie kutoka humo, nami nitamweka mtu aliyechaguliwa kwa uangalizi wake. Maana ni nani aliye kama mimi, na ni nani atakayeniagiza? Mchungaji gani awezaye kunizuia?
Zek 11:3Wachungaji wanapiga yowe, kwa kuwa utukufu wao umeharibiwa! Sauti ya mungurumo wa wana simba, kwa kuwa kiburi cha Mto Yordani kimeharibiwa!
- Mchungaji angeweza kunyakua kutoka kwa simba miguu miwili tu au kipande cha sikioAmo 3:12
Aya
Amo 3:12Hivi ndivyo Yahwe asemavyo,” Kama mchungaji aokoavyo miguu miwili tu kwenye mdomo wa simba, au kipande cha sikio, ndivyo wana wa Israeli watakavyookolewa wale waishio katika Samaria, pamoja na pembe ya kulalia, au pembe ya kitanda.”
- Kundi la wachungaji wakipiga kelele halikuweza kumfukuza simba kutoka mawindo yakeIsa 31:4
Aya
Isa 31:4Hivi ndivyo Yahwe alivyosema na mimi, '' kama simba, na hata mtoto wa simba, hunguruma juu ya mawindo yake, pale makundi ya wachungaji yanapoita dhidi yake, lakini hatatemeka kwa sauti zao, wala hatakwenda kwa sababu ya kelele zao, hivyo Yahwe wa majeshi atashuka kupigana kwenye mlima Sayuni, katika kilima hicho.
Makutano
- Samsoni alimrarua mwana simba kwa mikono mitupuAmu 14:5–6
Aya
Amu 14:5–6Basi Samsoni akaenda Timna pamoja na baba yake na mama yake; nao wakafika kwenye mashamba ya mizabibu ya Timna. Na, tazama, kuna simba mdogo wa alikuja na alikuwa akiunguruma. Roho wa Bwana ghafla akaja juu yake, naye akamrarua simba kwa urahisi kama ambavyo angeweza kumrarua mbuzi mdogo, naye hakuwa na kitu mkononi mwake. Lakini hakuwaambia baba au mama yake kile alichofanya.
- Baadaye alikuta nyuki na asali ndani ya mzoga wa simbaAmu 14:8–9
Aya
Amu 14:8–9Siku chache baadaye aliporudi kumwoa, akageuka na kutafuta mzoga wa simba. Na, tazama, kulikuwa na kundi la nyuki na asali katika kile kilichobaki katika mwili wa simba. Akaweka asali mikononi mwake na akaenda, akala huku akienda. Alipokuja kwa baba yake na mama yake, akawapa, nao wakala. Lakini hakuwaambia kuwa amechukua asali nje ya kile kilichobaki kwenye mwili wa simba.
- Kitendawili chake: “Katika mlaji kulitoka chakula”Amu 14:14, Amu 14:18
Aya
Amu 14:14Akawaambia, 'Kati ya mtu aliyekula alikuwa kitu cha kula; nje ya nguvu ilikuwa kitu tamu. Lakini wageni wake hawakuweza kupata jibu katika siku tatu.
Amu 14:18Na watu wa mji wakamwambia, siku ya saba kabla ya jua kuzama, 'Ni nini kilicho bora zaidi kuliko asali? Ni kitu gani chenye nguvu kuliko simba? ' Samsoni akawaambia, 'Ikiwa hamkulima na ng'ombe wangu, hamtapata jibu la kitendawili changu.'
- Daudi, kijana mchungaji, aliua simba na dubu waliochukua wana kondoo1 Sam 17:34–36
Aya
1 Sam 17:34–36Lakini Daudi akamwambia Sauli, “Mtumishi wako alikuwa akichunga kondoo za baba yake. Mara simba au dubu alikuja akamchukua mwana kondoo kutoka kundini, Nilimfukuza na kumshambulia na kumpokonya kutoka kinywani mwake. Na aliponirukia, nilimshika ndevu zake, nilimpiga, na kumuua. Mtumishi wako amekwisha kmuua simba na dubu. N huyu Mfilisti asiyetahiriwa atakuwa kama mmoja wa wanyama hao, kwa kuwa ameyadharau majeshi ya Mungu aliye hai.”
- Benaya alishuka shimoni siku ya theluji akamuua simba2 Sam 23:20
Aya
2 Sam 23:20Benaya kutoka Kabseeli mwana wa Yehoyada; alikuwa mtu hodari aliyefanya matendo makuu. Aliwauwa wana wawili wa Arieli wa Moabu. Pia alishuka shimoni na kuuwa simba wakati wa theruji.
- Simba alimuua mtu wa Mungu lakini hakumla wala kumgusa punda wake1 Fal 13:24–28
Aya
1 Fal 13:24–28Baada ya mtu wa Mungu kuondoka, akakutana na simba njiani na kumwua barabarani, na mwili wake uliachwa barabarani. Na yule punda akasimama pembeni yake, na yule simba naye akasimama pembeni ya ule mwili. Watu walipopita na kuuona ule mwili umeachwa barabarani, na yule simba akisimama karibu na ule mwili, walikuja wakaeleza habari hiyo mjini kule ambako yule nabii mzee aliishi. Yule nabii aliyemrudisha toka njiani aliposikia, akasema, “Yeye mtu wa Muugu ndiye aliyeshindwa kutii neno la BWANA. Kwa hiyo BWANA alimtoa kwa simba, ambaye amemrarua katika vipande vipande na kumwua, kama vile neno la BWANA lilivyokuwa limemwonya.” Kwa hiyo yule nabii mzee akawaamnbia wanawe, akisema, “Tandikeni punda wangu,” nao wakamtandikia. Akaenda akaukuta mwili umeachwa barabarani, punda na simba wamesimama pembeni ya ule mwili. Yule simba hakuula ule mwili, wala hakumshambulia yule punda.
- Simba alimuua mtu aliyekataa kumpiga nabii1 Fal 20:35–36
Aya
1 Fal 20:35–36Mtu mmoja, mmoja wana wa wana wa manabii, akamwambia mmoja wa wale manabii wenzake kwa neno la BWANA, “Tafadhali nipige.” Lakini yule mtu akakataa kumpiga. Kisha yule nabii akamwambia nabii mwenzake, “ Kwa sababu umekataa kutii sauti ya BWANA, mara tu utakaponiacha, simba atakuua.” na mara tu baad ya yule mtu kumwacha, simba akamkuta na kumwua.
- Simba waliwaua baadhi ya walowezi walioletwa katika miji ya Samaria2 Fal 17:25–26
Aya
2 Fal 17:25–26Ikatokea wakati walipoanza kuishi huko hawakumcha Yahwe. Hivyo Yahwe akatuma simba miongoni mwao ambao waliwaua baadhi yao. Basi wakaongea na mfalme wa Ashuru, wakisema, “Wale mataifa uliowaamisha na kuwaweka kwenye miji ya Samaria hawayajui mambo wanayotakiwa kuyafanya kutokana na mungu wa nchi. Hivyo alikuwa amewatuma simba kwenda kwao, na, tazama, wale simba walikuwa wakiwauua watu huko kwa sababu hawakufahamu yale mambo waliyokuwa wanatakiwa kuyafanya kwa mungu wa nchi.”
- Danieli alitupwa katika tundu la simba, lililotiwa muhuri kwa jiwe na pete ya mfalmeDan 6:16–17
Aya
Dan 6:16–17Ndipo mfalme alitoa agizo, na walimleta ndani Danieli, na kisha wakamtupa katika tundu la simba. Mfalme akamwambia Danieli, “Mungu wako, ambaye unamtumikia daima, na akuokoe.'' Jiwe lililetwa katika mlango wa tundu, na mfalme alilitia muhuri wa pete yake mwenyewe na pamoja na muhuri wa wakuu wake ili kwamba chochote kisiweze kubadilishwa kuhusiana na Danieli.
- Alfajiri Danieli alitolewa bila jeraha loloteDan 6:19–23
Aya
Dan 6:19–23Kisha katika mapambazuko mfalme aliamka na kwa haraka alienda kwenye tundu la simba. Na alipokaribia kwenye tundu, alimwita Danieli kwa sauti ya huzuni, akimwambia Danieli, “Danieli, mtumishi wa Mungu aliye hai, je Mungu wako ambaye anamtumkia daima ameweza kukuokoa kutoka katika simba? Ndipo Danieli akamwambia mfalme, “Mfalme, uishi milele! Mungu wangu amemtuma mjumbe na amevifunga vinywa vya simba, na hazijaweza kunidhuru. Kwa kuwa sikuwa na hatia yoyote mbele yake na pia mbele yako, ewe mfalme, na sijakufanyia jambo lolote la kukudhuru.” Basi mfalme alikuwa na furaha sana. Alitoa agizo kwamba wanatakiwa wamtoe Danieli nje ya tundu. Hivyo Danieli aliondolewa kutoka katika tundu. Hakuna dhara lolote lililoonekana kwake, kwa kuwa alikuwa amemtumainia Mungu wake.
- Washtaki wake walitupwa ndani, na simba wakawashinda kabla hawajafika chiniDan 6:24
Aya
Dan 6:24Mfalme alitoa agizo, waletwe wale watu waliomshitaki Danieli na kisha akawatupa wao katika tundu la simba - wao, na watoto wao, na wake zao. Kabla hawajafika sakafuni, simba waliwararua na kuvunjavunja mifupa yao vipande vipande.
Simba waliochongwa
- Kiti cha enzi cha Sulemani: simba kando ya kila egemeo, simba kumi na wawili ngazini sita1 Fal 10:19–20
Aya
1 Fal 10:19–20Hicho kiti kilikuwa na ngazi sita, na kitako chake kilikuwa cha mviringo. Na kilikuwa kimezungushiwa kwa mikono pande zake zote. Na simba wawili walisimama pembeni mwa ile mikono. Kulikuwa na simba kumi na wawili waliokuwa wamesimama kwenye ile ngazi. Moja katika kila upande wa ngazi hizo. Hapakuwepo na kiti kama hicho katika ufalme mwingine.
- Simba, ng’ombe na makerubi walipamba vitako vya shaba vya hekalu1 Fal 7:29, 1 Fal 7:36
Aya
1 Fal 7:29na juu ya papi na vipandio kulikuwa na simba, makisai, na makerubi. Chini na juu simba kulikuwa na masongo ya kazi ya kufuliwa.
1 Fal 7:36Juu ya mabamba na papi zake Huramu akachora makerubi, simba, na mitende ambayo ilifunika nafasi ya juu, nayo ilikuwa imezungukwa na masongo.
Misemo
- “Mbwa aliye hai ni bora kuliko simba aliyekufa”Mhu 9:4
Aya
Mhu 9:4Kwa kuwa yeyote anayeungana na wote walio hai kuna tumaini, kama vile mbwa aliye hai ni bora kuliko simba aliye kufa.
- Mvivu husema, “Kuna simba nje!”Mit 22:13, Mit 26:13
- “Hofu ya mfalme ni kama kunguruma kwa simba”Mit 20:2
Aya
Mit 20:2Kumwogopa mfalme ni kama kumwogopa simba kijana aungurumaye, yeyote anayemkasirisha hutoa fidia ya maish yake.
- Sauli na Yonathani walikuwa “wepesi kuliko tai, hodari kuliko simba”2 Sam 1:23
Aya
2 Sam 1:23Sauli na Yonathani walikuwa wakipendwa na walikuwa wenye neema maishani, hata wakati wa mauti yao walikuwa pamoja. Walikuwa na kasi kuliko tai, walikuwa na nguvu kuliko simba.
- Mashujaa wa Gadi walikuwa na nyuso kama za simba na wepesi kama swala1 Nya 12:8
Aya
1 Nya 12:8Baadhi ya Wagadi walijiunga na Daudi katika ngome iliyo nyikani. Walikuwa wanaume wapiganaji, waliofundishwa kwa mapambano, walioweza kumudu ngao na mkuki; ambao nyuso zao zilikuwa kali kama za simba. Walikuwa wepesi kwenye milima kama swala.
Vyanzo
Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0