Bible Explorer

Gundua › Mada › Kulungu na swala

Maumbile

Kulungu na swala katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (19), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

  • Kulungu na swala wanaweza kuliwa na aliye safi na asiye safi piaKum 12:15, Kum 14:5
    Aya
    Kum 12:15Hata hivyo, mtaweza kuua na kula wanyama ndani ya malango yenu, kama mnavyotaka, kupokea baraka ya Yahwe Mungu wenu kwa ajili ya yote amewapa; na watu wasio safi na safi wote wanaweza kula, wanyama kama vile paa na kulungu.
    Kum 14:5kulungu, paa, kulungu wa kiume, mbuzi wa mwituni, paa mweupe na pofu na kondoo wa mlimani
  • Kulungu, swala na paa waliletwa kwa meza ya Sulemani1 Fal 4:22–23
    Aya
    1 Fal 4:22–23Mahitaji ya Sulemani kwa siku moja yalikuwa ni Kori thelathini za unga mzuri na kori unga wa ngano, makisai kumi walionona, na fahari ishirini wa malisho, na kondoo mia moja, nje ya ayala, paa, na kulungu na kuku walionona.
  • Ayubu: kulungu jike huinama kuzaa mtoto wake; watoto hukua kondeniAyu 39:1–4
    Aya
    Ayu 39:1–4Je unajua ni wakati gani mbuzi mwitu huzaa watoto wao katika miamba? Je waweza kuwangalia paa wakati wanapozaa watoto wao? Waweza kuhesabu miezi ya kuchukua mimba? Je unaujua muda ambao huzaa watoto wao? Wanainama chini na kuzaa watoto wao, na kisha maumivu yao ya uzazi yanaishi. Watoto wao huwa na nguvu na kukua katika uwanda wa wazi; hutoka nje na hawarudi tena.
  • Wakati wa ukame kulungu jike humwacha mtoto wake mchanga kwa kuwa hakuna majaniYer 14:5
    Aya
    Yer 14:5Kwa maana hata kunguru huwaacha wanawe katika mashamba, kwa maana hakuna nyasi.
  • “Kama vile kulungu aoneavyo shauku vijito vya maji”Zab 42:1
    Aya
    Zab 42:1Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya wana wa Korah Kama ayala ayatamanivyo maji ya mto. ndivyo hivyo ninakiu yako, Mungu.
  • Kulungu wasiopata malisho hukosa nguvu za kumkimbia mwindajiOmb 1:6
    Aya
    Omb 1:6Uzuri umemwacha binti wa Sayuni. Watoto wa mfalme wamekuwa kama ayala ambaye haoni malisho, na wanaenda bila uwezo kwa wanao wakimbiza.
  • Swala hujiokoa kutoka mkononi mwa mwindajiMit 6:5
    Aya
    Mit 6:5Jiokoe mwenyewe kama swala kutoka katika mkono wa mwindaji, kama ndege kutoka katika mkono wa mwinda ndege.

Misemo

  • Asaheli alikuwa mwepesi wa miguu kama swala wa porini2 Sam 2:18
    Aya
    2 Sam 2:18Wana watatu wa Seruya walikuwepo pale: Yoabu, Abishai na Asaheli.
  • Mashujaa wa Gadi walikuwa wepesi kama swala milimani1 Nya 12:8
    Aya
    1 Nya 12:8Baadhi ya Wagadi walijiunga na Daudi katika ngome iliyo nyikani. Walikuwa wanaume wapiganaji, waliofundishwa kwa mapambano, walioweza kumudu ngao na mkuki; ambao nyuso zao zilikuwa kali kama za simba. Walikuwa wepesi kwenye milima kama swala.
  • “Huifanya miguu yangu kama ya kulungu” mahali pa juu2 Sam 22:34, Zab 18:33, Hab 3:19
    Aya
    2 Sam 22:34Huifanya myepesi miguu yangu kama kurungu na kuniweka katika vilima virefu.
    Zab 18:33Yeye hunifanya miguu yangu kuwa myepesi kama mbawala na kuniweka mahali pa juu!
    Hab 3:19Bwana Yahwe ni nguvu yangu na anaifanya miguu yangu kama ya kulungu. Ananifanya mimi niende mbele mahali pangu pa juu. - kufuata maelekezo ya muziki, katika vyombo vyangu vya nyuzi.
  • “Kulungu jike apendezaye, paa mwenye neema”Mit 5:19
    Aya
    Mit 5:19Maana ni ayala apendezaye na kulungu mwenye uzuri. Matiti yake na yakujaze furaha muda wote; daima na utekwe na upendo wake.
  • Mpendwa, kama swala au mwana kulungu milimaniWim 2:9, Wim 2:17, Wim 8:14
    Aya
    Wim 2:9Mpenzi wangu ni kama swala au mtoto mdogo wa paa; angalia, amesimama nyuma ya ukuta wetu, akishangaa kupitia dirishani, akichungulia wavuni.
    Wim 2:17Enenda zako, mpenzi wangu, kabla pepo za jioni hazija vuma na vivuli kutoweka. Nenda zako; kuwa kama ayala au mtoto mdogo wa paa katika milima mawe mengi.
    Wim 8:14Harakisha, mpenzi wangu, na uwe kama paa au mtoto wa paa kwenye milima ya manukato.
  • “Nawaapisha kwa swala na kwa kulungu jike wa porini”Wim 2:7
    Aya
    Wim 2:7Ninataka muhaidi, mabinti wa Yerusalemu, kwa swala na paa wa porini, kwamba hamtavuruga mapenzi yetu hadi yatakapo isha yenyewe. Mwanamke akizungumza mwenyewe.
  • “Naftali ni kulungu jike aliyeachwa huru”Mwa 49:21
    Aya
    Mwa 49:21Naftali ni dubu jike asiyefungwa; atakuwa na watoto wa dubu walio wazuri.

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0