Bible Explorer

Gundua › Mada › Kondoo

Maumbile

Kondoo katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (38), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

  • Habili alikuwa mchungaji wa kondooMwa 4:2
    Aya
    Mwa 4:2Kisha akazaa ndugu yake Habili. Sasa Habili akawa mchungaji, lakini Kaini alilima udongo.
  • Habili alileta wazaliwa wa kwanza wa kundi lakeMwa 4:4
    Aya
    Mwa 4:4Habili pia, alileta sehemu ya wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona. Yahwe akamkubali Habili pamoja na sadaka yake,
  • Abraham alimwona kondoo dume amekwama kwa pembe zake kichakaniMwa 22:13
    Aya
    Mwa 22:13Abraham akatazama juu na tazama, nyuma yake kulikuwa na kondoo mume amenaswa pembe zake kichakani. Abraham akaenda akamchukua kondoo na akamtoa kama sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe.
  • Wachungaji walivingirisha jiwe kutoka kinywa cha kisima ili kunywesha makundiMwa 29:2–3
    Aya
    Mwa 29:2–3Hata alipotazama, akaona kisima kondeni, na, tazama, makundi matatu ya kondoo yalikuwa yamelala kando yake. Kwani kutoka katika hicho wangeyanywesha makundi, na jiwe juu ya mdomo wa kisima lilikuwa kubwa. Wakati makundi yote yangekusanyika pale, wachungaji wangevingirisha jiwe kutoka katika mdomo wa kisima na kuwanywesha kondoo, na kisha kurudisha jiwe juu ya mdomo wa kisima, mahali pake.
  • Raheli alikuwa mchungaji; Yakobo aliwanywesha kondoo wa baba yakeMwa 29:9–10
    Aya
    Mwa 29:9–10Wakati bado Yakobo anaongea nao, Raheli akaja pamoja na kondoo wa babaye, kwani alikuwa akiwachunga. Yakobo alipomwona Raheli, binti wa Labani, kaka wa mamaye, na kondoo wa Labani, kaka wa mama yake, Yakobo akaja juu, akalivingirisha jiwe kutoka mlangoni mwa kisima, na akawanywesha kondoo wa Labani, kaka wa mama yake.
  • Binti saba wa Yethro waliwanywesha kundi, na Musa akawasaidiaKut 2:16–17
    Aya
    Kut 2:16–17Wakati huo kuhani wa Midiani alikuwa na mabinti saba. Walikuja mtoni kuchota maji na kujaza vyombo vyao ili wawanyweshe mifuko ya baba yao. Wachungaji walikuja na kutaka kuwafukuza, lakini Musa alienda kuwasaidia. Kisha akawanywesha mifugo wao.
  • Musa alikuwa akichunga kundi la Yethro alipofika HorebuKut 3:1
    Aya
    Kut 3:1Wakati huu Musa aliendelea kuchunga mifugo ya Yethro baba mkwe wake, kuhani wa Midiani. Musa aliliongoza kundi la mifugo kuelekea upande wa mbali wa jangwa mpaka kufika Horebu, mlima wa Mungu.
  • Daudi, mwana mdogo kabisa, alikuwa akichunga kondoo1 Sam 16:11
    Aya
    1 Sam 16:11Kisha Samweli akamuulia Yese, “Je, watoto wako wote wako hapa?” Naye akajibu, “Yupo mdogo kabisa lakini anachunga kondoo.” Samweli akamwambia Yese, “Tuma watu wakamwite; maana hatutakaa chini hadi atakapofika hapa.”
  • Yakobo kama mchungaji: joto mchana, baridi kali usiku, hasara kwa wanyama wakaliMwa 31:38–40
    Aya
    Mwa 31:38–40Kwa miaka ishirini nimekuwa nawe. Kondoo wako na mbuzi wako hawakutoa mimba, wala sikula dume lolote la kondoo katika wanyama wako. Kilichoraruliwa na hayawani sikukuletea. Badala yake, nilichukua upotevu huo, kwamba wameibwa mchana au usiku. Nilikuwepo wakati wote; mchana joto lilinipata, na baridi wakati wa usiku; na sikupata usingizi.
  • Ujira wa Yakobo: wanyama wenye madoadoa, wenye mabaka na weusiMwa 30:32
    Aya
    Mwa 30:32Niache nipite kati ya kundi lako lote leo, kwa kuondoa kila kondoo mwenye milia na mabaka, na kila kondoo mweusi kati yao, na kati ya wenye mabaka na milia katika mbuzi. Hawa watakuwa ujira wangu.
  • Fimbo zake zilizobambuliwa kwenye mabirika na wana wenye miliaMwa 30:37–39
    Aya
    Mwa 30:37–39Yakobo akachukua matawi mabichi yaliyokatwa ya mipopla, mlozi na mwaramoni mbichi akatoa maganda ili michilizi myeupe ionekane, na akaifanya sehemu nyeupe ya ndani ya mti iliyokuwa ndani ya fito ionekane. Kisha akaziweka fito alizokuwa amezibambua mbele ya makundi ya kondoo, mbele ya mabirika yakunyweshea walipokuja kunywa maji. Wakashika mimba walipokuja kunywa maji. Wanyama wakapandana mbele ya fito; nao wakazaa watoto wenye milia, mabaka na wenye madoa.
  • Wachungaji walikesha wakilinda makundi yao usikuLk 2:8
    Aya
    Lk 2:8Katika eneo hilo, walikuwapo wachungaji walioishi mashambani wakilinda makundi ya Kondoo wao usiku.
  • Kondoo wanaijua sauti ya mchungaji; huwaita kwa majinaYn 10:3–4
    Aya
    Yn 10:3–4Kwake mlinzi wa mlango humfungulia. Kondoo waisikia sauti yake na huwaita kondoo zake kwa majina yao na kuwatoa nje. Atakapowatoa nje hao walio wake, huwatangulia, na kondoo humfuata, kwa sababu wanaijua sauti yake.

Sufu, maziwa na kukata manyoya

  • Maziwa ya kundi, mafuta ya wana kondoo na kondoo dume wa BashaniKum 32:14
    Aya
    Kum 32:14Alikula siagi kutoka katika kundi na kunywa maziwa kutoka katika kundi la mifugo, pamoja na mafuta ya wanakondoo, kondoo dume wa Bashani na mbuzi, pamoja na ngano safi kabisa – nawe ulikunywa divai itokayo povu iliyotengenezwa kwa juisi ya mizabibu.
  • Labani alikuwa amekwenda kukata manyoya ya kondoo wake Raheli alipochukua sanamuMwa 31:19
    Aya
    Mwa 31:19Labani alipokuwa amekwenda kuwakata manyoya kondoo wake, Raheli akaiba miungu ya nyumba ya baba yake.
  • Yuda alipanda kwa wakata manyoya ya kondoo wake huko TimnaMwa 38:12–13
    Aya
    Mwa 38:12–13Baada ya muda mrefu, binti Shua, mkewe Yuda, alikufa. Yuda akafarijika na kwenda kwa wakatao kondoo wake manyoya huko Timna, yeye na rafiki yake, Hira Mwadulami. Tamari akaambiwa, “Tazama, mkweo anakwenda Timna kukata kondoo wake manyoya.”
  • Nabali alikuwa na kondoo 3,000 na mbuzi 1,000, akiwakata manyoya huko Karmeli1 Sam 25:2
    Aya
    1 Sam 25:2Kulikuwa na mtu mmoja huko Maoni, na mali zake zilikuwa huko Karmali. Mtu huyo alikuwa tajiri sana. Alikuwa na kondoo elfu tatu na mbuzi elfu moja. Naye alikuwa akiwakata manyoya kondoo wake huko Karmeli.
  • Wakati wa kukata manyoya ulimaanisha karamu: ya Nabali na ya Absalomu1 Sam 25:11, 1 Sam 25:36, 2 Sam 13:23–24
    Aya
    1 Sam 25:11Je, nichukue mkate wangu na maji yangu na nyama yangu ambayo nimewachinjia wakata manyoya wangu, na niwape watu wanaotoka nisikokujua?”
    1 Sam 25:36Abigaili akarudi kwa Nabali; tazama, alikuwa akifanya sherehe katika mji wake, kama sherehe ya mfalme; na moyo wa Nabali ulifurahi ndani yake, kwa sababu alikwa amelewa sana. Kwa hiyo hakumwambia chochote kabisa hadi kulipopambazuka
    2 Sam 13:23–24Ikawa baada ya miaka miwili mizima Absalomu akawa na wakatao kondoo manyoya wakifanya kazi huko Baali Hazori, ulioko karibu na Efraim, naye Absalomu akawaarika wana wote wa mfalme kufika huko. Absalomu akamwendea mfalme na kusema, “Tazama sasa, mtumishi wako anao wakatao kondoo manyoya. Tafadhari, naomba mfalme na watumishi wake waende nami, mtumishi wako.”
  • Sufu ya kwanza iliyokatwa kutoka kundi ilikwenda kwa makuhaniKum 18:3–4
    Aya
    Kum 18:3–4Hii ni sababu ya makuhani kutoka kwa watu, kutoka kwa wale wanaotoa dhabihu, kama itakuwa ng'ombe au kondoo: wanapaswa kutoa kwa kuhani bega, mashavu mawili, na sehemu za ndani. Mazao ya kwanza ya nafaka zako, mvinyo wako mpya, na mafuta yako, na manyoya ya kwanza ya kondoo zako, unapaswa umpe.
  • Ayubu aliwapa maskini joto kwa manyoya ya kondoo wakeAyu 31:20
    Aya
    Ayu 31:20ikiwa moyo wake haujanibariki kwasababu amekuwa hajatiwa joto na sufu ya kondoo zangu,

Makundi kwa idadi

  • Mesha mfalme wa Moabu alilipa wana kondoo 100,000 na sufu ya kondoo dume 100,0002 Fal 3:4
    Aya
    2 Fal 3:4Basi Mesha mfalme wa Moabu alifuga kondoo. Alikuwa akimpatia mfalme wa Israeli kondoo 100,000 na manyoya ya kondoo dume 100,000.
  • Waarabu walimletea Yehoshafati kondoo dume 7,700 na beberu 7,7002 Nya 17:11
    Aya
    2 Nya 17:11Baadhi ya Wafilisti wakamletea Yehoshafati zawadi, fedha kama kodi. Waarabu pia wakamletea makundi, 7,700 kondoo waume, na mbuzi 7,770.
  • Kondoo 250,000 walitekwa kutoka kwa Wahagri1 Nya 5:21
    Aya
    1 Nya 5:21Walikamata wanya wao, pamoja na ngamia elfu hamsini, kondoo 250,000, punda elfu mbili, na wanaume 100,000.
  • Ayubu alikuwa na kondoo 7,000, na baadaye 14,000Ayu 1:3, Ayu 42:12
    Aya
    Ayu 1:3Alimiliki kondoo elfu saba, ngamia elfu tatu, jozi mia moja za maksai, na punda mia tano na idadi kubwa ya watumishi. Mtu huyu alikuwa mtu mkuu wa watu wote wa mashariki.
    Ayu 42:12Yahweh aliubarikiwa mwisho wa maisha ya Ayubu kuliko mwanzo wake; alikuwa na kondoo kumi na nne elfu, ngamia elfu sita, jozi elfu moja, na punda jike elfu moja.
  • Kedari ilifanya biashara ya wana kondoo, kondoo dume na mbuzi na TiroEze 27:21
    Aya
    Eze 27:21Arabuni na wakuu wote wa Kedari walikuwa wafanyabiashara pamoja nawe; walikuandalia wanakondoo, kondoo dume na mbuzi.
  • Sulemani alitoa kondoo 120,000 wakati wa kuweka wakfu hekalu1 Fal 8:63
    Aya
    1 Fal 8:63Sulemani akatoa sadaka ya amani, ambayo aliifanya kwa BWANA: Nayo ilikuwa makisai elfu ishirini na mbili, na kondoo 120,000. Kwa hiyo mfalme na watu wa Israeli wakaiweka wakfu nyumba ya BWANA.

Katika Sheria

  • Kondoo aliyeibiwa akachinjwa au kuuzwa: alipe kondoo wanneKut 22:1
    Aya
    Kut 22:1Kama mwanaume akiiba ng'ombe aua kondoo na kumuua au kumuuza, kisha lazima alipe ng'ombe watano au ng'ombe mmoja, na kondoo wanne kwa mmoja.
  • Kondoo aliyeraruliwa na wanyama wakali: alete mzoga kama ushahidiKut 22:10, Kut 22:13
    Aya
    Kut 22:10Kama mwanaume akimpa jirani yake punda, ng'ombe, kondoo, au mnyama yeyote kumuhifadhia, na kama akifa au kuumia au akibebwa pasipo mtu kumuona,
    Kut 22:13Kama mnyama alikatwa vipande, acha mwanaume mwengine alete huyo mnyama kama ushahidi. Hatalipa kwa ajili ya vile vipande.

Katika Yerusalemu

  • Makuhani walijenga upya Lango la KondooNeh 3:1
    Aya
    Neh 3:1Kisha Eliashibu, kuhani mkuu, akasimama pamoja na ndugu zake makuhani, wakajenga lango la kondoo. Walitakasa na kuweka milango yake. Waliweka wakfu hadi mnara wa Hamea na hadi mnara wa Hananeli.
  • Birika la Bethzatha lilikuwa karibu na Lango la KondooYn 5:2
    Aya
    Yn 5:2Na kule Yerusalemu palikuwa na birika kwenye mlango wa kondoo, lililokuwa likiitwa kwa lugha ya Kiebrania Bethzatha, nalo lina matao matano.

Misemo

  • Meno “kama kundi la kondoo waliokatwa manyoya wakipanda kutoka kuoshwa”Wim 4:2
    Aya
    Wim 4:2Meno yako ni kama kondoo walio nyolewa, wakitoka sehemu ya kuoshwa. Kila mmoja ana pacha, na hamna ata mmoja miongoni mwao aliyefiwa.
  • “Hakikisha unaijua hali ya makundi yako”Mit 27:23
    Aya
    Mit 27:23Hakikisha unajua hali ya makundi yako na ujishughulishe juu ya makundi yako,
  • “Wana kondoo watakupa mavazi”Mit 27:26
    Aya
    Mit 27:26Wanakondoo watakupatia mavazi yako na mbuzi watakupatia gharama ya shamba.
  • “Kama kondoo mbele ya wakata manyoya yake hukaa kimya”Isa 53:7
    Aya
    Isa 53:7Aliteswa; lakini alinyenyekea mwenyewe, hakufungua mdomo wake; kama kondooendae kuchinjwa, na kama kondoo mbele ya mtu anayemkata mnyoa yake taratibu, hivyo hakufungua mdomo wake.

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0