Bible Explorer

Gundua › Mada › Mapango

Maumbile

Mapango katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (30), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

Makazi na maficho

  • Lutu na binti zake wawili waliishi pangoni milimaniMwa 19:30
    Aya
    Mwa 19:30Lakini Lutu akapanda juu kutoka Soari na kwenda kuishi katika milima akiwa pamoja na binti zake wawili, kwa sababu aliogopa kuishi Soari. Kwa hiyo akaishi pangoni, yeye na binti zake wawili.
  • Eliya alilala usiku pangoni huko Horebu1 Fal 19:8–9
    Aya
    1 Fal 19:8–9Kwa hiyo akainuka na kula na kunywa, naye akasafiri kwa nguvu ya chakula hicho kwa siku arobaini mchana na usiku hata akafika Horebu, mlima wa Mungu. Akaingia kwenye pango akakaa humo. Kisha neno la BWANA likamjia likimwambia, “Unafanya nini hapa, Eliya?”
  • Alijifunika uso kwa joho lake akasimama mlangoni pa pango1 Fal 19:13
    Aya
    1 Fal 19:13Naye Eliya alipoisikia sauti, akafunika uso wake kwa vazi lake, akatoka nje, akasimama kwenye lango la hilo pango. Na sauti ikaja kwake ikisema, “unafanya nini hapa?,
  • Wafalme watano walijificha katika pango la MakedaYos 10:16–17
    Aya
    Yos 10:16–17Basi wale wafalme watano walikuwa wametoroka na kujificha wao wenyewe katika pango huko Makeda. Taarifa zilimfikia Yoshua kusema, “Wafalme watano wamepatikana wamejificha katika pango huko Makeda!”
  • Yoshua aliamuru mawe makubwa yavingirishwe mlangoni pakeYos 10:18
    Aya
    Yos 10:18Yoshua akasema, “Viringisheni mawe makubwa katika mlango wa pango na muweke wanajeshi hapo ili kuwalinda.
  • Baadaye mawe yalibaki mlangoni pa pango “hadi leo”Yos 10:27
    Aya
    Yos 10:27Ilipokuwa jioni, Yoshua alitoa maagizo, nao waliwashusha chini ya miti na kisha wakawatupa katika pango ambalo walikuwa wamejificha wao wenyewe. Waliweka mawe makubwa juu ya mlango wa pango. Mawe hayo yapo pale hadi leo hii.
  • Waisraeli walijificha mapangoni, vichakani, miambani, mashimoni na visimani1 Sam 13:6
    Aya
    1 Sam 13:6Watu wa Israeli walipoona kuwa wapo katika matatizo -kwa maana watu walikata tamaa, wakajificha kwenye mapango, kwenye vichaka, kwenye miamba, kwenye visima na katika mashimo.
  • Wafilisti: “Waebrania wanatoka katika mashimo”1 Sam 14:11
    Aya
    1 Sam 14:11Kwa hiyo wote wawili wakajifunua mbele ya ngome ya Wafilisti. Wafilisti wakasema, “Angalia, Webrania wanakuja kutokea kwenye mashimo walimojificha.”
  • Obadia aliwaficha manabii mia moja, hamsini kila pango, na chakula na maji1 Fal 18:4, 1 Fal 18:13
    Aya
    1 Fal 18:4kwa kuwa wakati Yezebeli alipokuwa akiwaua manabii wa BWANA, Obadia alichukua manabii mia akawaficha katika makundi ya hamsini hamsini katika pango na akawalisha kwa mikate na maji.
    1 Fal 18:13Je, haujaambiwa, bwana wangu, nilichokifanya wakati Yezebeli alipowaua manabii wa BWANA, jinsi nilivyowaficha wale manabii mia moja wa BWANA katika makundi ya hamsini kwenye pango na kuwalisha kwa mikate na maji?
  • Samsoni alikaa katika pango la mwamba wa EtamuAmu 15:8, Amu 15:11
    Aya
    Amu 15:8Kisha akawakata vipande vipande, paja na mguu, kwa kuwauwa sana. Kisha akashuka chini akaishi katika pango katika mwamba wa Etamu.
    Amu 15:11Kisha watu elfu tatu wa Yuda wakashuka hata kwenye pango la Eatamu, wakamwambia Samsoni, “Je, hujui kwamba Wafilisti hutawala juu yetu? Je! umetutendea nini?” Samsoni akawaambia, “Kwa kadili walivyonitendea mimi, vivyo hivyo nimewatendea wao.”
  • Daudi alikimbilia pango la Adulamu; watu kama 400 walijiunga naye1 Sam 22:1–2
    Aya
    1 Sam 22:1–2Basi Daudi aliondoka hapo na akatoroka kwenda kwenye pango la Adulamu. Kaka zake na wote wa nyumba ya baba yake waliposikia hayo, wakateremka kumwendea huko. Kila mmoja aliyekuwa na mahangaiko, kila mmoja aliyekuwa na deni, na kila mmoja ambaye hakuwa na furaha moyoni-wote walijikusanya kwake, na Daudi akawa jemedari wao. Kulikuwa na wanaume wapatao mia nne waliokuwa pamoja naye.
  • Wakuu watatu walimjia Daudi katika pango la Adulamu wakati wa mavuno2 Sam 23:13, 1 Nya 11:15
    Aya
    2 Sam 23:13Watatu kati ya askari thelathini walishuka kwa Daudi nyakati za mavuno, katika pango la Adulamu. Jeshi la Wafilisti lilikuwa limepiga kambi katika bonde la Mrefai.
    1 Nya 11:15Kisha watatu wa viongozi thelathini wakashuka chini kwenye mwamba wa Daudi, katika pango la Adulamu. Jeshi la Wafilisti walieka kambi katika bonde la Refaim.
  • Sauli aliingia pango alimojificha Daudi; Daudi alikata pindo la joho lake1 Sam 24:3–4
    Aya
    1 Sam 24:3–4Akafika penye mazizi ya kondoo kando ya njia, mahali palipokuwa na pango. Sauli akaingia ndani yake kujisaidia. Wakati huo Daudi na watu wake walikuwa wamekaa mbali zaidi ndani ya pango lilelile. Watu wake Daudi wakamwambia, “Hii ndiyo siku ambayo BWANA aliisema akikuambia, 'Nitamweka adui wako mkononi mwako, ili umtendee kama unavyotaka.”' Kisha Daudi akainuka na kumnyemelea kwa mbele kimya kimya na kulikata pindo la kanzu ya Sauli.
  • Daudi alitoka pangoni akamwita Sauli1 Sam 24:8
    Aya
    1 Sam 24:8Baadaye tena, Daudi akasimama juu, akatoka pangoni, na kumwita Sauli: “Bwana wangu mfalme.” Sauli alipotazama nyuma, Daudi akasujudu hadi chini na kuonyesha heshima.
  • Vichwa viwili vya zaburi: Daudi “pangoni”Zab 57:1, Zab 142:1
    Aya
    Zab 57:1Kwa kiongozi wa muziki; seti kwenye Al Tashheth. Zaburi ya Daudi. Zaburi; wakati alipo mkimbia Sauli, pangoni. Unihurumie, Mungu, unihurumie mimi, kwa maana ninakukimbilia wewe mpaka matatizo haya yaishe. Ninakaa chini ya mbawa za zako kwa ajili ya ulinzi mpaka huu uharibifu utakapoisha.
    Zab 142:1Zaburi ya Daudi, alipokuwa pangoni; maombi. Kwa sauti yangu namlilia Yahwe anisaidie; kwa sauti yangu naomba kwa ajili ya neema ya Yahwe.
  • Waliotengwa waliishi kati ya miamba na katika mashimo ardhiniAyu 30:6
    Aya
    Ayu 30:6Hivyo walipaswa kuishi katika mabonde ya mto, katika mashimo ya ardhi na miamba.
  • Wengine walijificha mapangoni na katika mashimo ya ardhiEbr 11:38
    Aya
    Ebr 11:38(ambayo ulimwengu haukustahili kuwa nao), wakitangatanga nyikani, milimani, katika mapango na katika mashimo ya ardhini.

Mapango ya kuzikia

  • Abraham alinunua pango la Makpela kutoka kwa Efroni MhitiMwa 23:9, Mwa 23:17–20
    Aya
    Mwa 23:9Mwambieni aniuzie pango la Makpela, ambalo analimiliki, ambalo liko mwishoni mwa shamba lake. Kwa bei kamili aniuzie waziwazi mbele ya watu kama miliki ya kuzikia.”
    Mwa 23:17–20Kwa hiyo shamba la Efroni, lililokuwa katika Makpela, mbele ya Mamre, shamba pamoja na pango lililokuwamo ndani yake na miti yote iliyokuwamo ndani ya shamba na iliyokuwa mpakani ikatolewa kwa Abraham kwa njia ya manunuzi mbele ya wana wa Hethi, na mbele ya wote waliokuja malangoni pa mji wake. Baada ya haya, Abraham akamzika Sara mkewe katika pango la shamba la Makpela, lililo mbele ya Mamre, ambayo ni Hebroni, katika nchi ya Kanaani. Kwa hiyo shamba pamoja na pango likatolewa na wana wa Hethi kwa Abraham kama milki na eneo la kuzikia.
  • Isaka na Ishmaeli walimzika Abraham hukoMwa 25:9–10
    Aya
    Mwa 25:9–10Isaka na Ishmaili, wanae wakamzika katika pango la Makipela, katika shamba la Efron mwana wa Soari Mhiti, pango lililokuwa karibu na Mamre. Shamba hili Abraham alilinunua kwa watoto wa Hethi. Abraham akazikwa pale pamoja na Sara mkewe.
  • Yakobo: Abraham, Sara, Isaka, Rebeka na Lea walizikwa katika pango hiloMwa 49:29–32
    Aya
    Mwa 49:29–32Kisha akawaelekeza na kuwaambia, “Ninakaribia kwenda kwa watu wangu. Mnizike pamoja na babu zangu katika pango lililoko katika shamba la Efroni Mhiti, katika pango lililo katika shamba la Makpela, karibu na Mamre katika nchi ya Kanaani, shamba Ibrahimu alilolinunua kwa Efron Mhiti kwa ajili ya eneo la kuzikia. Pale walimzika Ibrahimu na Sara mkewe; pale wakamzika Isaka na Rebeka mkewe; na pale nikamzika Lea. Shamba na pango lililomo lilinunuliwa kutoka kwa watu wa Hethi.”
  • Wana wa Yakobo walimbeba kutoka Misri hadi MakpelaMwa 50:13
    Aya
    Mwa 50:13Wana wake wakampeleka katika nchi ya Kanaani na wakamzika katika pango katika shamba la Makpela, karibu na Mamre. Ibrahimi alikuwa amelinunua pango pamoja na shamba kwa ajili ya eneo la kuzikia. Alikuwa amelinunua kutoka kwa Efroni Mhiti.
  • Kaburi la Lazaro lilikuwa pango lenye jiwe limewekwa mlangoniYn 11:38
    Aya
    Yn 11:38Ndipo Yesu, hali akiomboleza nafsini mwake tena, alienda kwenye kaburi. Sasa lilikuwa pango, na jiwe limewekwa juu yake.
  • Kaburi la Yesu lilichongwa mwambani, jiwe likavingirishwa mlangoniMt 27:60, Mk 15:46
    Aya
    Mt 27:60na akaulaza katika kaburi jipya lake alilokuwa amelichonga mwambani. Kisha akavingirisha jiwe kubwa likafunika mlango wa kaburi na akaenda zake.
    Mk 15:46Yusufu alikuwa amenunua sanda. Akamshusha toka msalabani, akamfunga kwa sanda, na kumweka ndani ya kaburi lililochimbwa katika mwamba. Kisha akalivingirisha jiwe mlangoni mwa kaburi.

Misemo

  • “Kuweni kama njiwa ajengaye kiota mlangoni pa pango”Yer 48:28
    Aya
    Yer 48:28Jitengeni na miji na kuweka kambi katika minuko, enyi watu wa Moabu. Kuwa kama njiwa anayeatamia juu ya mlango wa tundu katika miamba.

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0