Bible Explorer

Gundua › Mada › Kiangazi na baridi

Maumbile

Kiangazi na baridi katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (40), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

  • Kupanda na kuvuna, baridi na joto, kiangazi na majira ya baridi havitakomaMwa 8:22
    Aya
    Mwa 8:22Wakati nchi isaliapo, majira ya kupanda mbegu na mavuno, baridi na joto, kiangazi na majira ya baridi, mchana na usiku havitakoma.”
  • Mianga angani ili kuonyesha majira, siku na miakaMwa 1:14, Zab 104:19
    Aya
    Mwa 1:14Mungu akasema, “kuwe na mianga katika anga kutenganisha mchana na usiku. Na ziwe kama ishara, kwa majira, kwa siku na miaka.
    Zab 104:19Aliuchagua mwezi kuweka alama ya majira; jua latambua kuchwa kwake.
  • Zaburi: “Wewe ulifanya kiangazi na majira ya baridi”Zab 74:17
    Aya
    Zab 74:17Umeiweka mipaka ya nchi; umeumba majira ya joto na majira ya baridi.
  • Mvua kwa wakati wake: mvua za vuli na za masikaKum 11:14, Yoe 2:23, Yer 5:24
    Aya
    Kum 11:14kwamba nitawapa mvua nchi yenu kwa majira yake, mvua za awali na mvua za badaye, ili kwamba mweze kukusanya nafaka zenu, mvinyo wenu mpya, na mafuta yenu.
    Yoe 2:23Furahini, enyi watu wa Sayuni, na kufurahi katika Bwana, Mungu wenu. Kwa maana atakupa mvua ya vuli kwa kiasi na kuleta mvua kwa ajili yenu, mvua ya vuli na mvua ya masika kama hapo awali.
    Yer 5:24Kwa kuwa hawasemi mioyoni mwao, “basi na tumche BWANA, Mungu wetu, yeye aletaye mvua za awali na mvua za vuli - kwa wakati wake, ambaye hutuzna majuma ya mavuno kwa ajili yetu.”
  • Wakati wa masika, wafalme waendapo vitani2 Sam 11:1
    Aya
    2 Sam 11:1Ikawa wakati wa majira ya kipupwe, wakati ambapo kwa kawaida wafalme huenda vitani, Daudi akamtuma Yoabu, mtumishi wake, na jeshi lote la Israeli. Wakaliaribu jeshi la Amoni na kuuhusuru Raba. Lakini Daudi akakaa Yerusalemu.
  • Kupura hadi mavuno ya zabibu, mavuno ya zabibu hadi wakati wa kupandaLaw 26:5
    Aya
    Law 26:5Upuraji wenu utaendelea hata wakati wa mavuno ya zabibu, na mavuno ya zabibu yataendelea mpaka majira ya kupada mbegu. Nanyi mtakula mkate na kushiba na kuishi salama mahali mtakapofanya mji wenu katika nchi.
  • Ruth alifika mwanzoni mwa mavuno ya shayiri akaokota hadi mwisho wa nganoRut 1:22, Rut 2:23
    Aya
    Rut 1:22Kwa hivyo Naomi na Ruth Mmoabu, mke wa mtoto wake, walirudi kutoka nchi ya Moabu. walirudi Bethrehemu mwazo wa mavuno ya shairi.
    Rut 2:23Kwa hiyo alikaa karibu na wafanyakazi wa kike ili avune mpaka mwisho wa mavuno ya shayiri na mavuno ya ngano. Na alikuwa akiishi pamoja na mama mkwe wake.
  • Samweli aliomba radi na mvua wakati wa mavuno ya ngano1 Sam 12:17–18
    Aya
    1 Sam 12:17–18Je, leo si mavuno ya ngano? Nitamwomba BWANA, naye ataleta ngurumo na mvua. Ndipo mtajua na kuona kwamba uovu wenu ni mwingi, mlioufanya machoni pa BWANA, kujiombea mfalme wenu ninyi wenyewe.” Hivyo Samweli akamwomba BWANA; na siku iyo hiyo BWANA akatuma ngurumo na mvua. Ndipo watu wote wakamwogopa sana BWANA pamoja na Samweli.
  • Miaka ya Yakobo: joto mchana na baridi kali usikuMwa 31:40
    Aya
    Mwa 31:40Nilikuwepo wakati wote; mchana joto lilinipata, na baridi wakati wa usiku; na sikupata usingizi.

Kiangazi

  • Egloni aliketi katika ubaridi wa chumba chake cha juuAmu 3:20, Amu 3:24
    Aya
    Amu 3:20Ehudi akaja kwake. Mfalme alikuwa amekaa peke yake, peke yake katika chumba cha juu cha baridi. Ehudi akasema, 'Nina ujumbe kutoka kwa Mungu kwa ajili yeko.' Mfalme akasimama kutoka katika kiti chake.
    Amu 3:24Baada ya Ehudi kuondoka, watumishi wa mfalme wakaja; wakaona milango ya chumba cha juu imefungwa, kwa hiyo wakafikiri, 'Hakika atakuwa anajitoa mwenyewe katika hali ya baridi ya chumba cha juu.'
  • Nyumba za majira ya baridi na nyumba za kiangaziAmo 3:15
    Aya
    Amo 3:15Nitaiharibu nyumba ya baridi pamoja na nyumba ya hari. Nyumba za pembe zitaangamia, na nyumba kubwa zitatoweka, -hivi ndivyo Yahwe asemavyo.”
  • Siba alimletea Daudi matunda mia moja ya kiangazi2 Sam 16:1–2
    Aya
    2 Sam 16:1–2Daudi alipokuwa amekwenda kitambo juu ya kilele cha kilima, Siba mtumishi wa Mefiboshethi akaja kumlaki akiwa na punda wawili waliokuwa wamebeba vipande mia mbili vya mikate, vishada mia moja vya mizeituni, vishada mia moja vya tini na mfuko wa ngozi uliojaa mvinyo. Mfalme akamuliza Siba, “Kwa nini umeleta hivi vitu?” Siba akajibu, “punda ni kwa ajili ya familia yako kupanda, mikate na matunda ni kwa ajili ya matumizi ya askari wako, na mvinyo ni kwa ajili kunywa watakaozimia nyikani.”
  • Gedalia: kusanyeni divai, matunda ya kiangazi na mafuta katika mitungiYer 40:10, Yer 40:12
    Aya
    Yer 40:10Na tazama, Ninaishi Mizpa kukutana pamoja na Wakaldayo waliokuja kwetu. Basi vuna mvinyo, matunda ya kiangazi, na mafuta na viweke kwenye vyombo vyako. Uishi katika miji ambayo umechukua.”
    Yer 40:12Basi Wayahudi wote walirudi toka kila eneo ambako walikuwa wametawanyika. Walirudi kwenye nchi ya Yuda, kwa Gedalia huko Mizpa. Walivuna mvinyo na matunda ya kiangazi kwa wingi.
  • Chungu huweka akiba ya chakula chake wakati wa kiangaziMit 6:6–8, Mit 30:25
    Aya
    Mit 6:6–8Wewe mtu mvivu, mwangalie mchwa, zitafakari njia zake ili kupata busara. Hana akida, afisa au mtawala, lakini huandaa chakula chake wakati wa joto na wakati wa mavuno huweka hazina ili kula baadaye.
    Mit 30:25mchwa ni viumbe ambao sio imara, lakini huandaa chakula chao wakati wa hari,
  • Makapi ya uwanja wa kupuria wakati wa kiangazi, yanachukuliwa na upepoDan 2:35
    Aya
    Dan 2:35Kisha chuma, udongo, fedha, na dhahabu zilivunjwa katika vipande vipande kwa wakati mmoja na yakawa kama makapi yaliyo katika sakafu za kupuria kipindi cha kiangazi. Upepo huyapeperushia mbali na hakuna alama inayoachwa. Lakini jiwe lililoipiga sanammu likawa mlima mkubwa na kuijaza dunia yote.
  • Mtini unapotoa majani, kiangazi kiko karibuMt 24:32
    Aya
    Mt 24:32Jifunzeni somo kutokana na mti mtini. Mara tu tawi linapochipuka na kutoa majani, mnajua kwamba kiangazi kinakaribia.
  • “Nguvu zangu zilikauka kama katika joto la kiangazi”Zab 32:4
    Aya
    Zab 32:4Mchana na usiku mkono wako ulinielemea. nguvu zangu zilikauka wakati wa kiangazi. Selah

Majira ya baridi

  • “Majira ya baridi yamepita; mvua imekwisha na kwenda zake”Wim 2:11–13
    Aya
    Wim 2:11–13Angalia, baridi imepita; mvua imeisha na kwenda. Maua yametokeza juu ya nchi; wakati wa kupunguza matawi na kuimba kwa ndege umekuja, na sauti za hua zimesikika nchini kwetu. Mti wa tini umepevusha tini zake za kijani, na mizabibu imestawi; yatoa marashi yake. Inuka, mpenzi wangu, mzuri wangu, na uje nami.
  • Mwezi wa tisa mfalme aliketi katika nyumba ya baridi karibu na motoYer 36:22
    Aya
    Yer 36:22Sasa mfalme alikuwa amesimama kwenye nyumba ya majira ya baridi katika mwezi wa tisa, na mkaa ulikuwa unawaka mbele yake.
  • Wakati wa mvua watu walitetemeka uwanjani katika mvua kubwaEzr 10:9, Ezr 10:13
    Aya
    Ezr 10:9Hivyo watu wote wa Yuda na Benjamini wakakusanyika Yerusalem kwa siku tatu. Ilikuwa ni mwezi wa tisa na siku ya ishirini ya mwezi. watu wote wakasimama mbele ya nyumba ya Mungu na wakatetemeka kwa sababu ya neno na mvua.
    Ezr 10:13haijalishi, kuna watu wengi na ni kipindi cha mvua. Hatuna nguvu ya kusimama nje na hii si siku moja au mbili za kufanya kazi, kwa kuwa tumekosea katika jambo hili.
  • Sikukuu ya Kuweka Wakfu wakati wa baridi; Yesu alitembea katika ukumbi wa SulemaniYn 10:22–23
    Aya
    Yn 10:22–23Ndipo ikaja Sikukuu ya Kuwekwa Wakfu Yerusalemu. Ulikuwa wakati wa baridi, na Yesu alikuwa akitembea hekaluni katika ukumbi wa Selemani.
  • “Ombeni kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi”Mt 24:20
    Aya
    Mt 24:20Ombeni kwamba kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato.
  • Kusafiri baharini kulikuwa hatari baada ya Mfungo; walitafuta bandari ya kukaa wakati wa baridiMdo 27:9, Mdo 27:12
    Aya
    Mdo 27:9Tulikuwa tumechukua muda mwingi sana, na muda wa mfungo wa Kiyahudi ulikuwa umepita pia, na sasa ilikuwa ni hatari kuendelea kusafiri. Hivyo Paulo akatuonya,
    Mdo 27:12Kwa sababu bandari haikuwa sehemu rahisi kukaa wakati wa baridi, mabaharia wengi wakashauri tusafiri kutoka pale, ili kwa namna yoyote tukiweza kuufikia mji wa Foinike, tukae pale wakati wa baridi. Foinike ni bandari huko Krete, na inatazama kaskazini mashariki na kusini mashariki.
  • Meli ya Iskanderia ilikuwa imekaa kisiwani wakati wa baridiMdo 28:11
    Aya
    Mdo 28:11Baada ya miezi mitatu, tulisafiri ndani ya meli ya Iskanda ambayo ilikuwa imepigwa baridi hapo kisiwani, ambayo viongozi wake walikuwa ndugu wawili mapacha.
  • Paulo aliamua kukaa Nikopoli wakati wa baridiTit 3:12
    Aya
    Tit 3:12Nitakapomtuma kwako Artemi au Tikiko, harakisha uje kwangu huku Nikopoli ambapo nimeamua kukaa kipindi cha baridi.
  • Paulo kwa Timotheo: “Jitahidi kuja kwangu kabla ya majira ya baridi”2 Tim 4:21
    Aya
    2 Tim 4:21Fanya hima uje kabla ya kipindi cha baridi. Eubulo anakusalimu, pia Pude, Lino, Claudia na ndugu wote.
  • Theluji iliyotandazwa kama sufu, jalidi iliyotawanywa kama majivuZab 147:16
    Aya
    Zab 147:16Huifanya theluji kama sufu, huitawanya barafu kama majivu.

Katika Mithali

  • “Akusanyaye wakati wa kiangazi ni mwana mwenye hekima”Mit 10:5
    Aya
    Mit 10:5Mwana mwenye busara hukusanya mazao wakati wa kiangazi, bali ni aibu kwake alalaye wakati wa mavuno.
  • “Kama theluji wakati wa kiangazi na mvua wakati wa mavuno”Mit 26:1
    Aya
    Mit 26:1Kama theluji wakati wa joto au mvua kwenye mavuno, ndivyo mpumbavu asivyostahili heshima.
  • “Kama baridi ya theluji wakati wa mavuno”Mit 25:13
    Aya
    Mit 25:13Kama baridi ya theluji wakati wa mavuno ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwa wenye kumtuma; huyahifadhi maisha ya mabwana wake.
  • Mvivu halimi kwa wakati wakeMit 20:4
    Aya
    Mit 20:4Mtu mvivu halimi majira ya kipupwe; hutafuta mazao wakati wa mavuno lakini hapati kitu.

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0