Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Sikukuu za mwaka wa kanisa › Krismasi

Sikukuu za mwaka wa kanisa

Krismasi

Kuzaliwa kwa Yesu kama Mathayo na Luka wanavyosimulia, pamoja na unabii wa Isaya na mwanzo wa Injili ya Yohana, kwa ukamilifu. Makanisa ya Magharibi huadhimisha Krismasi tarehe 25 Desemba; Makanisa ya Kiorthodoksi ya kalenda ya Juliasi tarehe 7 Januari.

Tarehe

MwakaMakanisa ya MagharibiKrismasiKanisa la KiorthodoksiKuzaliwa kwa Kristo
202625 Desemba 2026Ijumaa7 Januari 2027Alhamisi
202725 Desemba 2027Jumamosi7 Januari 2028Ijumaa
202825 Desemba 2028Jumatatu7 Januari 2029Jumapili
202925 Desemba 2029Jumanne7 Januari 2030Jumatatu
203025 Desemba 2030Jumatano7 Januari 2031Jumanne

Tarehe hufungua masomo ya siku hiyo katika kalenda ya Kiorthodoksi au ya Kikatoliki.

Tarehe za Kiorthodoksi ni kwa kalenda ya Juliasi, inayofuatwa na Makanisa ya Urusi, Serbia na Georgia na Mlima Athos: sikukuu zao zisizobadilika huangukia siku 13 baadaye katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria na mengine) huadhimisha Krismasi tarehe 25 Desemba; Pasaka na siku zinazoitegemea huhesabiwa sawa katika karibu Makanisa yote ya Kiorthodoksi.

Vifungu vya Biblia

Isaya

Isa 9:2–7

2Watu wanotembeakatika giza wameona wameona mwanga mkubwa; wale waishio katika nchi ya uvuli wa mauti, mwanga umewaka juu yao. 3Umeliongeza taifa; umeongeza furaha yao. Wamefurahia mbele yako kama furaha ya kipindi cha mavuno, kama watu wanavyofurahi kugawanya nyara. 4Maana nira ya mzigo wake, boriti katika mabega yake, fimbo ya mkandamizaji, umesambaratisha ndoto kama siku ya Midiamu. 5Kila buti likanyagalo gasia na vazi limekwisha kwenye damu itachomwa, mafuta kwa moto. 6Kwetu mtoto amezaliwa, kwetu mtoto ametoka; na mtawala atakuwa kwenye mabega yake; na jina lake ataitwa mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa Amani. 7Enzi yake na amani yake haitakuwa na mwisho, maana anatawala katika kiti cha enzi cha Daudi, na juu ya ufalme wake, ataanzisha hukumu ya haki, tangu sasa na hata milele. Bidii ya Yahwenwa majeshi itafanya haya.

Mathayo

Mt 1:18–25

18Kuzaliwa kwa Yesu Kristo kulikuwa kwa namna hii. Mama yake, Mariamu, alichumbiwa na Yusufu, lakini kabla hawajakutana, alionekana kuwa na mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. 19Mume wake Yusufu, alikuwa mtu mwenye haki hakutaka kumwaibisha hadharani. Aliamua kusitisha uchumba wake naye kwa siri. 20Alipokuwa akifikiri juu ya mambo haya, Malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema,'' Yusufu mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Mariamu kama mkeo, kwa sababu mimba aliyonayo ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 21Atajifungua mtoto wa kiume na utamwita jina lake Yesu, kwa maana atawaokoa watu wake na dhambi zao.'' 22Yote haya yalitokea kutimizwa kile kilichonenwa na Bwana kwa njia ya nabii, akisema, 23“Tazama, bikira atachukua mimba na kuzaa mtoto wa kiume, na watamwita jina lake Imanueli”— maana yake, “Mungu pamoja nasi.” 24Yusufu aliamka kutoka usingizini na kufanya kama malaika wa Bwana alivyomwamuru na alimchukua kama mkewe. 25Hata hivyo, hakulala naye mpaka alipojifungua mtoto wa kiume na alimwita jina lake Yesu.

Luka

Lk 2:1–20

1Sasa katika siku hizo, ikatokea kwamba Kaisari Agusto alitoa agizo akielekeza kwamba ichukuliwe sensa ya watu wote wanaoishi duniani. 2Hii ilikuwa ni sensa ya kwanza iliyofanyika wakati Krenio akiwa gavana wa Siria. 3Hivyo kila mmoja akaenda mjini kwake kuandikishwa sensa. 4Naye Yusufu aliondoka pia katika mji wa Nazareti huko Galilaya na akasafiri Yudea katika mji wa Bethlehemu, ujulikanao kama mji wa Daudi, kwa sababu alitokea katika ukoo ya Daudi. 5Alikwenda huko kujiandikisha pamoja na Mariamu, ambaye alikuwa amemposa na alikuwa akitazamia mtoto. 6Sasa ilitokea kwamba, wakiwa kule wakati wake wa kujifungua mtoto ukawadia. 7Akajifungua mtoto wa kiume, mzaliwa wake wa kwanza, akamzungushia nguo mwilini kumkinga na baridi mtoto. Ndipo akamweka kwenye kihori cha kulishia wanyama, kwa sababu haikuwepo nafasi kwenye nyumba za wageni. 8Katika eneo hilo, walikuwapo wachungaji walioishi mashambani wakilinda makundi ya Kondoo wao usiku. 9Ghafla, malaika wa Bwana akawatokea, na utukufu wa Bwana ukang'aa kuwazunguka, na wakawa na hofu sana. 10Ndipo malaika akwaambia, “Msiogope, kwasababu nawaletea habari njema ambayo italeta furaha kuu kwa watu wote. 11Leo Mwokozi kazaliwa kwaajili yenu mjini mwa Daudi! Yeye ndiye Kristo Bwana! 12Hii ndiyo ishara ambayo mtapewa, mtamkuta mtoto amefungwa nguo na amelala kwenye hori la kulishia wanyama.” 13Ghafla kukawa na jeshi kubwa la mbinguni likaungana na malaika huyo wakamsifu Mungu, wakisema, 14“Utukufu kwa Mungu aliye juu sana, na amani iwe duniani kwa wote ambao anapendezwa nao.” 15Ikawa kwamba malaika walipokwisha kuondoka kwenda mbinguni, wachungaji wakasemezena wao kwa wao, “ Twendeni sasa kule Bethlehemu, na tukaone hiki kitu ambacho kimetokea, ambacho Bwana ametufahamisha.” 16Wakaharakisha kule, na wakamkuta Mariamu na Yusufu, na wakamuona mtoto amelala kwenye hori la kulishia wanyama. 17Na walipoona hivi, wakawajulisha watu kile walichokuwa wameambiwa kumhusu mtoto. 18Wote waliosikia habari hii wakashangazwa na kile kilichosemwa na wachungaji. 19Lakini Mariamu akaendelea kufikiri kuhusu yote aliyokwisha kuyasikia, akiyatunza moyoni mwake. 20Wachungaji wakarudi wakimtukuza na kumsifu Mungu kwa ajili ya kila kitu walichokwisha sikia na kuona, kama tu ilivyokuwa imenenwa kwao.

Mathayo

Mt 2:1–12

1Baada ya Yesu kuzaliwa katika Bethelehem ya Uyahudi katika siku za mfalme Herode, watu wasomi kutoka mashariki ya mbali walifika Yerusalemu wakisema, 2“Yuko wapi yeye ambaye aliyezaliwa Mfalme wa Wayahudi? Tuliiona nyota yake mashariki nasi tumekuja kumwabudu.” 3Pindi Mfalme herode aliposikia haya alifadhaika, na Yerusalemu yote pamoja naye. 4Herode akawakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, naye akawauliza, “Kristo atazaliwa wapi?” 5Wakamwabia, “Katika Bethelehemu ya Uyahudi, kwa kuwa hivi ndivyo ilivyoandikwa na nabii, 6Nawe Bethelehemu, katika nchi ya Yuda, si mdogo miongoni mwa viongozi wa Yuda, kwa kuwa kutoka kwako atakuja mtawala atakayewachunga watu wangu Israeli.” 7Hivyo Herode aliwaita wale wasomi kwa siri na kuwauliza ni wakati gani hasa nyota ilikuwa imeonekana. 8Akawatuma Bethelehem, akisema, “Nendeni kwa uangalifu mkamtafute mtoto aliyezaliwa. Wakati mtakapomwona, nileteeni habari ili kwamba mimi pia niweze kuja na kumwabudu.” 9Baada ya kuwa wamemsikia mfalme, waliendelea na safari yao, na nyota ile waliyokuwa wameiona mashariki iliwatangulia hadi iliposimama juu ya mahali mtoto aliyezaliwa alipokuwa. 10Wakati walipoiona nyota, walifurahi kwa furaha kuu mno. 11Waliingia nyumbani na kumuona mtoto aliyezaliwa na Mariamu mama yake. Walimsujudia na kumwabudu. Walifungua hazina zao na kumtolea zawadi za dhahabu, uvumba, na manemane. 12Mungu aliwaonya katika ndoto wasirudi kwa Herode, hivyo, waliondoka kurudi katika nchi yao kwa njia nyingine.

Yohana

Yn 1:1–14

1Mwanzoni kulikuwako Neno, na Neno alikuwa pamoja na Mungu, na Neno alikuwa Mungu. 2Huyu, Neno, Mwanzoni alikuwa pamoja na Mungu. 3Vitu vyote vilifanyika kupitia yeye, na pasipo yeye hakuna hata kitu kimoja kilichokuwa kimefanyika. 4Ndani yake kulikuwa uzima, na huo uzima ulikuwa nuru ya wanadamu wote. 5Nuru yang'aa gizani, wala giza halikuizimisha. 6Palikuwa na mtu aliyetumwa kutoka kwa Mungu, ambaye jina lake alikuwa Yohana. 7Alikuja kama shahidi kushuhudia kuhusu ile nuru, ili kwamba wote waweze kuamini kupitia yeye. 8Yohana hakuwa ile nuru, bali alikuja ili ashuhudie kuhusu ile nuru 9Hiyo ilikuwa nuru ya kweli ambayo ilikuwa inakuja katika dunia nayo humtia nuru kila mmoja 10Alikuwa katika dunia, na dunia iliumbwa kupitia yeye, na dunia haikumjua. 11Alikuja kwa vitu vyake, na watu wake hawakumpokea. 12Bali kwa wale wengi waliompokea, ambao waliamini jina lake, kwa hao aliwapa haki ya kuwa wana wa Mungu, 13Ambao walizaliwa, sio kwa damu, wala kwa mapenzi ya mwili, wala kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu mwenyewe. 14Naye Neno alifanyika mwili na akaishi miongoni mwetu, tumeuona utukufu wake, utukufu kama wa mtu pekee wa kipekee aliyekuja kutoka kwa Baba, amejaa neema na kweli.

Katika sanaa

Kazi zote

Sikukuu nyingine

Sikukuu za mwaka wa kanisa

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki