Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Sikukuu za mwaka wa kanisa › Epifania na Teofania

Sikukuu za mwaka wa kanisa

Epifania na Teofania

Tarehe 6 Januari makanisa ya Magharibi hukumbuka ziara ya Mamajusi; Kanisa la Kiorthodoksi huadhimisha Teofania, ubatizo wa Yesu katika Yordani — tarehe 19 Januari katika Makanisa ya kalenda ya Juliasi. Vifungu vya Injili vya zote mbili, kwa ukamilifu.

Tarehe

MwakaMakanisa ya MagharibiEpifaniaKanisa la KiorthodoksiTeofania
20276 Januari 2027Jumatano19 Januari 2027Jumanne
20286 Januari 2028Alhamisi19 Januari 2028Jumatano
20296 Januari 2029Jumamosi19 Januari 2029Ijumaa
20306 Januari 2030Jumapili19 Januari 2030Jumamosi
20316 Januari 2031Jumatatu19 Januari 2031Jumapili

Tarehe hufungua masomo ya siku hiyo katika kalenda ya Kiorthodoksi au ya Kikatoliki.

Tarehe za Kiorthodoksi ni kwa kalenda ya Juliasi, inayofuatwa na Makanisa ya Urusi, Serbia na Georgia na Mlima Athos: sikukuu zao zisizobadilika huangukia siku 13 baadaye katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria na mengine) huadhimisha Krismasi tarehe 25 Desemba; Pasaka na siku zinazoitegemea huhesabiwa sawa katika karibu Makanisa yote ya Kiorthodoksi.

Vifungu vya Biblia

Mathayo

Mt 2:1–12

1Baada ya Yesu kuzaliwa katika Bethelehem ya Uyahudi katika siku za mfalme Herode, watu wasomi kutoka mashariki ya mbali walifika Yerusalemu wakisema, 2“Yuko wapi yeye ambaye aliyezaliwa Mfalme wa Wayahudi? Tuliiona nyota yake mashariki nasi tumekuja kumwabudu.” 3Pindi Mfalme herode aliposikia haya alifadhaika, na Yerusalemu yote pamoja naye. 4Herode akawakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, naye akawauliza, “Kristo atazaliwa wapi?” 5Wakamwabia, “Katika Bethelehemu ya Uyahudi, kwa kuwa hivi ndivyo ilivyoandikwa na nabii, 6Nawe Bethelehemu, katika nchi ya Yuda, si mdogo miongoni mwa viongozi wa Yuda, kwa kuwa kutoka kwako atakuja mtawala atakayewachunga watu wangu Israeli.” 7Hivyo Herode aliwaita wale wasomi kwa siri na kuwauliza ni wakati gani hasa nyota ilikuwa imeonekana. 8Akawatuma Bethelehem, akisema, “Nendeni kwa uangalifu mkamtafute mtoto aliyezaliwa. Wakati mtakapomwona, nileteeni habari ili kwamba mimi pia niweze kuja na kumwabudu.” 9Baada ya kuwa wamemsikia mfalme, waliendelea na safari yao, na nyota ile waliyokuwa wameiona mashariki iliwatangulia hadi iliposimama juu ya mahali mtoto aliyezaliwa alipokuwa. 10Wakati walipoiona nyota, walifurahi kwa furaha kuu mno. 11Waliingia nyumbani na kumuona mtoto aliyezaliwa na Mariamu mama yake. Walimsujudia na kumwabudu. Walifungua hazina zao na kumtolea zawadi za dhahabu, uvumba, na manemane. 12Mungu aliwaonya katika ndoto wasirudi kwa Herode, hivyo, waliondoka kurudi katika nchi yao kwa njia nyingine.

Mathayo

Mt 3:13–17

13Kisha Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka mto Yorodani kubatizwa na Yohana. 14Lakini Yohana alitaka kumzuia akisema, “Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu?'' 15Yesu akajibu akasema, ''Ruhusu iwe hivi sasa, kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote.'' Kisha Yohana akamruhusu. 16Baada ya kuwa amebatizwa, mara Yesu alitoka kwenye maji, na tazama, Mbingu zikafunguka kwake. Na alimuona Roho wa Mungu akishuka kwa mfano wa njiwa na kutulia juu yake. 17Tazama, sauti ilitoka mbinguni ikisema, “Huyu ni mwanangu mpendwa. Ninaye pendezwa sana naye.''

Marko

Mk 1:9–11

9Ilitokea katika siku hizo kwamba Yesu alikuja kutoka Nazareti ya Galilaya, na alibatizwa na Yohana katika mto Yordani. 10Wakati Yesu alipoinuka kutoka majini, aliona mbingu zimegawanyika wazi na Roho akishuka chini juu yake kama njiwa. 11Na sauti ilitoka mbinguni, “Wewe ni Mwanangu mpendwa. Ninapendezwa sana na wewe.”

Yohana

Yn 1:29–34

29Siku iliyofuata Yohana alimwona Yesu akija kwake akasema, “ Tazama mwanakondoo wa Mungu aichukuae dhambi ya ulimwengu! 30huyu ndiye niliyesema habari zake nikisema, “Yeye ajaye nyuma yangu ni mkuu kuliko mimi, kwa kuwa alikuwa kabla yangu.' 31Sikumtambua yeye, lakini ilifanyika hivyo ili kwamba afunuliwe katika Israeli, kwamba nilikuja nikibatiza kwa maji.” 32Yohana alishuhudia, “Niliona Roho akishuka kutoka mbinguni mfano wa hua, na ilibaki juu yake. 33Mimi sikumtambua lakini yeye aliyenituma ili nibatize kwa maji aliniambia, 'yule ambaye utaona Roho akishuka na kukaa juu yake, Huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu.' 34Nimeona na nimeshuhudia kwamba huyu ni Mwana wa Mungu.”

Katika sanaa

Kazi zote

Sikukuu nyingine

Sikukuu za mwaka wa kanisa

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki