Mwanzo › Sikukuu za mwaka wa kanisa › Pentekoste
Sikukuu za mwaka wa kanisa
Pentekoste
Siku hamsini baada ya Pasaka: kushuka kwa Roho Mtakatifu juu ya wanafunzi huko Yerusalemu, kama kitabu cha Matendo kinavyosimulia, pamoja na unabii wa Yoeli anaounukuu Petro na maneno ya Yesu katika Injili ya Yohana.
Tarehe
| Mwaka | Makanisa ya MagharibiPentekoste | Kanisa la KiorthodoksiPentekoste |
|---|---|---|
| 2027 | 16 Mei 2027Jumapili | 20 Juni 2027Jumapili |
| 2028 | 4 Juni 2028Jumapili | 4 Juni 2028Jumapili |
| 2029 | 20 Mei 2029Jumapili | 27 Mei 2029Jumapili |
| 2030 | 9 Juni 2030Jumapili | 16 Juni 2030Jumapili |
| 2031 | 1 Juni 2031Jumapili | 1 Juni 2031Jumapili |
Tarehe hufungua masomo ya siku hiyo katika kalenda ya Kiorthodoksi au ya Kikatoliki.
Tarehe za Kiorthodoksi ni kwa kalenda ya Juliasi, inayofuatwa na Makanisa ya Urusi, Serbia na Georgia na Mlima Athos: sikukuu zao zisizobadilika huangukia siku 13 baadaye katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria na mengine) huadhimisha Krismasi tarehe 25 Desemba; Pasaka na siku zinazoitegemea huhesabiwa sawa katika karibu Makanisa yote ya Kiorthodoksi.
Vifungu vya Biblia
Matendo ya Mitume
1Ilipofika siku ya Pentekoste, wote walikuwa pamoja sehemu moja. 2Ghafla ikatokea muungurumo kutoka mbinguni kama upepo mkali. ukaijaza nyumba yote walimokuwa wameketi. 3Hapo zikawatokea ndimi, kama ndimi za moto zimegawanyika, zikawa juu yao kila mmoja wao. 4Wao wote wakajazwa na Roho Mtakatifu na wakaanza kusema kwa lugha zingine, kama vile Roho alivyowajalia kusema. 5Sasa walikuwapo wayahudi waliokuwa wanaishi Yerusalemu, wacha Mungu, kutoka kila taifa chini ya mbingu. 6Ngurumo hizi ziliposikiwa, kundi la watu likaja pamoja na wakiwa na wasiwasi kwa sababu kila mtu aliwasikia wakiongea kwa lugha yake mwenyewe. 7waliduwaa na kushangazwa, wao walisema, “Kweli, hawa wote wanaoongea siyo Wagalilaya? 8Kwa nini sisi tunawasikia, kila mmoja katika lugha tulizozaliwa nazo? 9Waparthia na Wamedi na Waelamu, na hao waishio Mesopotamia, Uyahudi, na Kapadokia, na katika Ponto na Asia, 10katika Frigia, Pamfilia, katika Misri, na sehemu ya Libya hata Kirene, na wageni kutoka Rumi, 11Wayahudi na waongofu, Wakrete na Waarabu, tunawasikia wakizungumza katika lugha zetu kuhusu kazi za uweza wa Mungu.” 12Wote walikuwa wameduwaa na kutatanishwa; walisemezana wao kwa wao, “Hii ina maana gani?” 13Lakini wengine walidhihaki wakisema, “Hawa wamejazwa kwa mvinyo mpya.” 14Lakini Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti, akawaambia, “Watu wa Yudea na wote mnaoishi hapa Yerusalemu, hili lijulikane kwenu, sikilizeni kwa makini maneno yangu. 15Watu hawa hawajalewa kama mnavyodhani, sababu saa hizi ni asubuhi saa tatu. 16Lakini hili lilikuwa limesemwa kupitia kwa nabii Yoeli: 17Itakuwa katika siku za mwisho; Mungu asema, nitamwaga Roho wangu kwa watu wote. Wana wenu na binti zenu watatoa unabii, vijana wenu wataona maono, na wazee wenu wataota ndoto. 18Vilevile juu ya watumishi wangu na watumishi wangu wa kike katika siku hizo, nitamwaga Roho wangu, nao watatabiri. 19Nitaonesha maajabu juu angani na ishara chini duniani, damu, moto, na mafusho ya moshi. 20Na jua litabadilishwa kuwa giza na mwezi kuwa damu, kabla haijaja siku kuu na ya ajabu ya Bwana. 21itakuwa ya kwamba kila mmoja ambaye huliitia jina la Bwana ataokoka.'
Yoeli
28Itakuwa baada ya hayo nitamimina Roho yangu juu ya wenye mwili yote, na wana wenu na binti zenu watatabiri. Wazee wenu wataota ndoto, vijana wenu wataona maono. 29Pia juu ya watumishi na watumishi wa kike, siku hizo nitaimimina Roho wangu. 30Nitaonyesha maajabu mbinguni na duniani, damu, moto na nguzo za moshi. 31Jua litakuwa giza na mwezi kuwa damu, kabla ya siku kuu na ya kutisha ya Bwana itakapokuja. 32Itakuwa kwamba kila mtu anayeita jina la Yahweh ataokolewa. Kwa maana juu ya Mlima Sayuni na Yerusalemu watakuwa na wale waliokoka, kama Bwana alivyosema, na kati ya wale walisalia, wale ambao Bwana anawaita.
Yohana
37Sasa katika siku ya mwisho, siku kubwa ya sikukuu, Yesu alisimama akapaza sauti, akisema, “Ikiwa yeyote ana kiu, na aje kwangu anywe. 38Yeye aniaminiye mimi, kama maandiko yalivyosema, kutoka ndani yake itatiririka mito ya maji ya uzima.” 39Lakini aliyasema haya kuhusu Roho, ambaye wao wamwaminio watampokea; Roho alikuwa bado hajatolewa kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa bado.
Yohana
19Na ilipokuwa jioni, siku hiyo, siku ya kwanza ya juma, na milango ikiwa imefungwa mahali wanafunzi walipokuwapo kwa kuwahofia Wayahudi, Yesu alikuja na kusimama katikati yao na kuwaambia, “Amani iwe kwenu.” 20Alipokwisha sema haya akawaonesha mikono yake na ubavu wake. Nao wanafunzi walipomwona Bwana walifurahi. 21Kisha Yesu akawaambia tena, “Amani iwe nanyi. Kama vile Baba alivyonituma mimi, vivyo hivyo nami nawatuma ninyi.” 22Yesu alipokwisha sema hayo, akawavuvia akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu. 23Yeyote mmsameheye dhambi, wamesamehewa; na wale mtakaowafungia watafungiwa.”
Katika sanaa
PentekosteDürer · karibu 1509/1510?
Kushuka kwa Roho MtakatifuGustave Doré · 1866
Mitume WakihubiriGustave Doré · 1866
PentekosteMchoraji wa Kijerumani · katikati ya karne ya 13
Kristo Awatokea MitumeRembrandt · 1656
Kristo Awatokea Katika Chumba cha Juu (Apparition du Christ au cénacle)James Tissot · 1886–1894
Sikukuu nyingine
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki