Mwanzo › Sikukuu za mwaka wa kanisa › Kwaresima
Sikukuu za mwaka wa kanisa
Kwaresima
Siku arobaini za mfungo kabla ya Pasaka: katika makanisa ya Magharibi tangu Jumatano ya Majivu, katika Kanisa la Kiorthodoksi tangu Jumatatu Safi. Mfungo wa Yesu nyikani na maneno yake kuhusu sadaka, sala na kufunga, kwa ukamilifu.
Tarehe
| Mwaka | Makanisa ya MagharibiJumatano ya Majivu | Kanisa la KiorthodoksiJumatatu Safi |
|---|---|---|
| 2027 | 10 Februari 2027Jumatano | 15 Machi 2027Jumatatu |
| 2028 | 1 Machi 2028Jumatano | 28 Februari 2028Jumatatu |
| 2029 | 14 Februari 2029Jumatano | 19 Februari 2029Jumatatu |
| 2030 | 6 Machi 2030Jumatano | 11 Machi 2030Jumatatu |
| 2031 | 26 Februari 2031Jumatano | 24 Februari 2031Jumatatu |
Tarehe hufungua masomo ya siku hiyo katika kalenda ya Kiorthodoksi au ya Kikatoliki.
Tarehe za Kiorthodoksi ni kwa kalenda ya Juliasi, inayofuatwa na Makanisa ya Urusi, Serbia na Georgia na Mlima Athos: sikukuu zao zisizobadilika huangukia siku 13 baadaye katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria na mengine) huadhimisha Krismasi tarehe 25 Desemba; Pasaka na siku zinazoitegemea huhesabiwa sawa katika karibu Makanisa yote ya Kiorthodoksi.
Vifungu vya Biblia
Yoeli
12“Lakini hata sasa,” asema Bwana, “Nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote. Haraka, lia na omboleza.” 13Rarueni miyoyo yenu, si mavazi yenu tu, na kurudi kwa Bwana Mungu wenu. Kwa maana ni mwenye neema na mwenye huruma, si mwepesi wa hasira na wingi katika uaminifu wa agano, na angependa kugeuka kutokana na adhabu. 14Nani anajua? Labda angegeuka na kuwa na huruma, na kuacha baraka nyuma yake, sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji kwa Bwana, Mungu wenu? 15Piga tarumbeta huko Sayuni, itisha kwa ajili ya funga takatifu, na itisheni kusanyiko takatifu. 16Kusanyeni watu, wito kwa kusanyiko takatifu. Kusanya wazee, kukusanya watoto na watoto wachanga. Bwana arusi waweze kutoka nje ya vyumba vyao, na bibi arusi kutoka kwenye vyumba vyao. 17Basi makuhani, watumishi wa Bwana, waliao kati ya patakatifu na madhabahu. Wawaambie, Waitie watu wako, Ee Bwana, wala usitoe urithi wako kwa aibu, ili mataifa watawawale juu yao. Kwa nini wanapaswa kusema kati ya mataifa, “Yuko wapi Mungu wao?”
Mathayo
1Kisha Yesu aliongozwa na Roho mpaka jangwani ili ajaribiwe na ibilisi. 2Alipokuwa amefunga kwa siku arobaini mchana na usiku alipata njaa. 3Mjarabu akaja na akamwambia, “Kama wewe ni Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mkate.” 4Lakini Yesu alimjibu na kumwambia, “Imeandikwa, 'Mtu hataishi kwa mkate peke yake, bali kwa kila neno litokalo kinywani mwa Mungu.''' 5Kisha ibilisi akampeleka katika mji mtakatifu na kumweka mahali pa juu sana pa jengo la hekalu, 6na kumwambia,'' kama wewe ni Mwana wa Mungu, jirushe chini, kwa maana imeandikwa, 'Ataamuru malaika wake waje wakudake,' na, 'watakuinua kwa mikono yao, ili usijikwae mguu wako katika jiwe.” 7Yesu akamwambia, ''Tena imeandikwa, 'Usimjaribu Bwana Mungu wako.''' 8Kisha, ibilisi akamchukua na kumpeleka sehemu ya juu zaidi akamwonyesha falme zote za ulimwengu na fahari ya hizo zote. 9Akamwambia, “Nitakupa vitu vyote hivi ukunisujudia na kuniabudu.” 10Kisha Yesu akamwambia, “Nenda zako utoke hapa, Shetani! Kwa maana imeandikwa, 'Yakupasa kumwabudu Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake.'” 11Kisha ibilisi akamwacha, na tazama, malaika wakaja wakamtumikia.
Mathayo
1Zingatia kutotenda matendo ya haki mbele ya watu ili kujionyesha, vinginevyo hutapata thawabu kutoka kwa Baba aliye mbinguni. 2Hivyo basi unapotoa usipige tarumbeta na kujisifu mwenyewe kama wanafiki wanavyofanya katika masinagogi na katika mitaa, ili kwamba watu wawasifu. Kweli nawaambia, wamekwisha kupokea thawabu yao. 3Lakini wewe unapotoa, mkono wako wa kushoto usijue kinachofanywa na mkono wa kulia, 4ili kwamba zawadi yako itolewe kwa siri. Ndipo Baba yako aonaye sirini atakupatia thawabu yako. 5Na unapokuwa ukiomba, usiwe kama wanafiki, kwa kuwa wanapenda kusimama na kuomba kwenye masinagogi na kwenye kona za mitaani, ili kwamba watu wawatazame. Kweli nawaambia, wamekwishapokea thawabu yao. 6Lakini wewe, unapo omba, ingia chumbani. Funga mlango, na uombe kwa kwa Baba yako aliye sirini. Ndipo Baba yako aonaye sirini atakupatia thawabu yako. 16Zaidi ya yote, unapokuwa umefunga, usioneshe sura ya huzuni kama wanafiki wanavyofanya, kwa kuwa wanakunja sura zao ili kwamba watu wawatambue wamefunga. Kweli ninakuambia, wamekwisha kupokea thawabu yao. 17Lakini wewe, unapokuwa umefunga, paka mafuta kichwa chako na uoshe uso wako. 18Hivyo haitakuonesha mbele ya watu kuwa umefunga, lakini tu itakuwa kwa Baba yako aliye sirini. Na Baba yako aonaye sirini, atakupa thawabu yako. 19Usijitunzie hazina yako mwenyewe hapa duniani, ambapo nondo na kutu huharibu, ambapo wezi huvunja na kuiba. 20Badala yake, jitunzie hazina yako mwenyewe mbinguni, ambapo wala nondo wala kutu hawezi kuharibu, na ambapo wezi hawawezi kuvunja na kuiba. 21Kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo na moyo wako utakapokuwepo pia.
Katika sanaa
Kujaribiwa kwa KristoJuan de Flandes · karibu 1500/1504
Kujaribiwa kwa KristoLucas van Leyden · 1518
Yesu Achukuliwa na Roho Juu ya Mlima Mrefu (Jésus transporté par l'esprit sur une haute montagne)James Tissot · 1886–1894
Yesu Apelekwa Juu Kabisa ya Hekalu (Jésus porté sur le pinacle du Temple)James Tissot · 1886–1894
Malaika Wamtumikia Yesu (Jésus assisté par les anges)James Tissot · 1886–1894
Sikukuu nyingine
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki