Mwanzo › Sikukuu za mwaka wa kanisa › Majilio
Sikukuu za mwaka wa kanisa
Majilio
Wiki kabla ya Krismasi: katika makanisa ya Magharibi Majilio huanza Jumapili ya nne kabla ya Krismasi; katika Kanisa la Kiorthodoksi mfungo wa Kuzaliwa wa siku arobaini huanza tarehe 15 Novemba ya kalenda ya kanisa. Unabii na vifungu vya Injili vinavyosomwa wiki hizi, kwa ukamilifu.
Tarehe
| Mwaka | Makanisa ya MagharibiJumapili ya kwanza ya Majilio | Kanisa la KiorthodoksiMwanzo wa mfungo wa Kuzaliwa |
|---|---|---|
| 2026 | 29 Novemba 2026Jumapili | 28 Novemba 2026Jumamosi |
| 2027 | 28 Novemba 2027Jumapili | 28 Novemba 2027Jumapili |
| 2028 | 3 Desemba 2028Jumapili | 28 Novemba 2028Jumanne |
| 2029 | 2 Desemba 2029Jumapili | 28 Novemba 2029Jumatano |
| 2030 | 1 Desemba 2030Jumapili | 28 Novemba 2030Alhamisi |
Tarehe hufungua masomo ya siku hiyo katika kalenda ya Kiorthodoksi au ya Kikatoliki.
Tarehe za Kiorthodoksi ni kwa kalenda ya Juliasi, inayofuatwa na Makanisa ya Urusi, Serbia na Georgia na Mlima Athos: sikukuu zao zisizobadilika huangukia siku 13 baadaye katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria na mengine) huadhimisha Krismasi tarehe 25 Desemba; Pasaka na siku zinazoitegemea huhesabiwa sawa katika karibu Makanisa yote ya Kiorthodoksi.
Vifungu vya Biblia
Isaya
1''Faraja, faraja watu wangu,'' amesema Mungu. 2''Ongea kwa upole kwa Yerusalemu; na tangaza vita vimeisha, maana maovu yao yamesamehewa, maana alipokea mara mbili kutoka kwa mkono wa Yahwe kwa dhambi zao.'' 3Sauti inalia nje, ''Katika jangwa tengeneza njia ya Yahwe; njoosha njia ya Araba katika njia kuu ya Mungu.'' 4Kila bonde litanyanyuliwa juu, kila mlima na kilima kitasawazishwa; na aridhi ya mwinuko itasawazishwa, mahali palipokwaruzwa patakuwa na usawa; 5na utukufu wa Mungu utafunuliwa, na watu wote wataona kwa pamoja; maana mdomo wa Yahwe umezungumza. 6Sauti inasema, ''Lia.'' Jibu lingine, ''Kwa nini nilie?'' ''Mwili wote ni nyasi na maagano yaliyoaminika ni kama ua kwenye shamba. 7Nyasi zinanyauka na maua yanaperuka pale Yehwe atakapo puliza punzi yake juu yake; hakika ubinadamu ni nyasi. 8Nyasi hunyauka, maua hupepea, lakini neno la Yahwe litasimama daima.'' 9Nenda juu ya mlima mrefu, Sayuni, mbeba taarifa njema. waambie miji ya Yuda, ''Hapa ni Mungu wako!'' 10Angalia, Bwana Yahwe anakuja kama mpiganaji shujaa na jeshi imara linatawa juu yake. Ona, zawadi yako iko kwake, na wale walikombolewa wataenda mbele yake. 11Atalilisha kundi lake kama mchungaji, Atawakusanya kondoo katika jeshi lake, na kulichukua karibu na moyo wake, kwa upole atawongoza wake kuwauuguza watoto wao.
Isaya
1Miti itachipukia katika mizizi ya Yese, na matawi yanayotokana na mizizi yatazaa matunda. 2Na roho wa Bwana atashuka juu yake, roho wa hekima na maelewano, roho ya maelekezo na ukuu, roho ya maarifa na hofu ya Yahwe. 3Furaha yake itakuwa hofu ya Bwana; hatatoa hukumu kwa kile anachokiona, wala atatoa maamuzi kwa kile anachokisikia. 4Badala yake atawahukumu masikini kwa haki na atafanya maamuzi kwa usawa na unyenyekevu. Ataamurisha mgomo wa dunia kwa fimbo ya mdomo wake, na punzi ya midomo yake, atawauwa waovu. 5Haki itakuwa mkanda wa viuno kiuno chake kuzunguka mapaja yake. 6Mbwa mwitu atakaa pamoja na kondoo, na chui watalala chini pamoja na mtoto wa mbuzi, ndama, mtoto wa simba na ndama pamoja na ndama aliyenona. Mtoto mdogo atawaongoza wao. 7Ng'ombe na dubu watachungwa pamoja. Na watoto wao watalala pamoja. Simba atakula majani kama ng'ombe. 8Mtoto atacheza juu ya chimo la nyoka, na mtoto aliyeachwa ataweka mkono wake katika pango la nyoka. 9Hawataumizwa wala kuharibiwa kwenye mlima mtakatifu; kwa maana dunia itakuwa imejaa maarifa ya Yahwe, kama maji yajaavyo kwenye bahari. 10Siku hiyo mzizi wa Yese utasimama kama bendera ya watu. Taifa litamtafuta yeye nje, na mahali pake pakupumzikia patatukuka.
Marko
1Huu ni mwanzo wa injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu. 2Kama ilivyoandikwa na nabii Isaya, “Tazama, ninamtuma mjumbe wangu mbele yako, mmoja atakayetayarisha njia yako. 3Sauti ya mtu aitaye nyikani, “Ikamilisheni njia ya Bwana; zinyosheni njia zake”. 4Yohana alikuja, akibatiza nyikani na kuhubiri ubatizo wa toba kwa msamaha wa dhambi. 5Nchi yote ya Yudea na watu wote wa Yerusalemu walikwenda kwake. Walikuwa wakibatizwa naye katika mto Yordani, wakiungama dhambi zao. 6Yohana alikuwa anavaa vazi la manyoya ya ngamia na mkanda wa ngozi kiunoni mwake, na alikuwa anakula nzige na asali ya porini. 7Alihubiri na kusema, “Yupo mmoja anakuja baada yangu mwenye nguvu zaidi kuliko mimi, na sina hadhi hata ya kuinama chini na kufungua kamba za viatu vyake. 8Mimi niliwabatiza kwa maji, lakini yeye atawabatiza ninyi kwa Roho Mtakatifu.”
Luka
26Sasa, katika mwezi wa sita wa mimba ya Elizabeti, Mungu alimwambia malaika Gabrieli kwenda kwenye mji wa Galilaya uitwao Nazareti, 27kwa bikra aliyekuwa ameposwa na mwanaume ambaye jina lake lilikuwa Yusufu. Yeye alikuwa wa ukoo wa Daudi, na jina la bikra huyo lilikuwa Mariamu. 28Akaja kwake na akasema, “Salaam, wewe uliyepokea neema kuu! Bwana amependezwa nawe.” 29Lakini maneno ya malaika yalimchanganya na hakuelewa kwa nini malaika alisema salaam hii ya ajabu kwake. 30Malaika akamwambia, “Usiogope, Mariamu, maana umepata neema kutoka kwa Mungu. 31Na tazama, utabeba mimba katika tumbo lako na utazaa mwana. Nawe utamwita jina lake 'Yesu.' 32Atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Aliye Juu Sana. Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi baba yake. 33Atatawala juu ya ukoo wa Yakobo milele na ufalme wake hautakuwa na mwisho. 34Mariamu akamwambia malaika, hili litatokea kwa namna gani, maana sijawahi kulala na mwanaume yeyote? 35Malaika akajibu na akamwambia, “Roho Mtakatifu atakujia juu yako, na nguvu ya Aliye Juu Sana itakuja juu yako. Kwa hiyo, mtakatifu atakayezaliwa ataitwa Mwana wa Mungu. 36Na tazama, ndugu yako Elizabeti anaujauzito wa mwana kwenye umri wake wa uzee. Huu ni mwezi wa sita kwake, ambaye alikuwa anaitwa mgumba. 37Maana hakuna lisilowezekana kwa Mungu.” 38Mariamu akasema, “Tazama, mimi ni mtumishi wa kike wa Bwana. Acha iwe hivyo kwangu sawa sawa na ujumbe wako.” Kisha malaika akamwacha.
Luka
39Ndipo katika siku hizo Mariamu aliondoka na kwa haraka alikwenda katika nchi ya vilima, kwenye mji katika nchi ya Yudea. 40Alikwenda nyumbani mwa Zekaria na akamsalimia Elizabeti. 41Sasa, ilitokea kwamba Elizabeti aliposikia salamu ya Mariamu, mtoto tumboni mwake akaruka, na Elizabeti akajazwa na Roho Mtakatifu. 42Akapaza sauti yake na kusema kwa sauti kuu, “umebarikiwa wewe zaidi miongoni mwa wanawake, na mtoto aliyemo tumboni mwako amebarikiwa. 43Na imekuwaje kwangu kwamba, mama wa Bwana wangu ilipasa aje kwangu? 44Kwa kuwa tazama, iliposikika masikoni mwangu sauti ya kusalimia kwako, mtoto tumboni mwangu akaruka kwa furaha. 45Na amebarikiwe mwanamke yule ambaye aliamini ya kwamba ungetokea ukamilifu wa mambo yale aliyoambiwa kutoka kwa Bwana.” 46Mariamu akasema, nafsi yangu inamsifu Bwana, 47na roho yangu imefurahi katika Mungu Mwokozi wangu. 48Kwa maana ameiangalia hali ya chini ya mtumishi wake wa kike. Tazama, tangu sasa katika vizazi vyote wataniita mbarikiwa. 49Kwa maana yeye aliyemweza amefanya mambo makubwa kwangu, na jina lake ni takatifu. 50Rehema yake inadumu toka kizazi hata kizazi kwa wale wanao mheshimu yeye. 51Ameonesha nguvu kwa mkono wake; amewatawanya wale ambao walijivuna juu ya mawazo ya mioyo yao. 52Amewashusha chini wana wa wafalme toka katika viti vyao vya enzi na kuwainua juu walio na hali ya chini. 53Aliwashibisha wenye njaa kwa vitu vizuri, bali matajiri amewafukuza mikono mitupu. 54Ametoa msaada kwa Israeli mtumishi wake, ili kukumbuka kuonesha rehema 55(kama alivyosema kwa baba zetu) kwa Abrahamu na uzao wake milele.” 56Mariamu alikaa na Elizabeti yapata miezi mitatu hivi ndipo akarudi nyumbani kwake.
Katika sanaa
Kupashwa HabariJan van Eyck · karibu 1434/1436
Mariamu Amtembelea Elizabeti, pamoja na Mtakatifu Nikolao na Mtakatifu Antoni AbatiPiero di Cosimo · karibu 1489/1490
Kupashwa HabariGustave Doré · 1866
Kupashwa HabariDürer · karibu 1503–5
Mariamu Amtembelea ElizabetiDürer · karibu 1504
Kupashwa HabariLucas van Leyden · karibu 1516
Mariamu Amtembelea ElizabetiLucas van Leyden · 1520
Jani kutoka Kitabu cha Saa: Kupashwa Habari (recto)Mchoraji asiyejulikana wa Flanders · 1470–1479
Jani kutoka Kitabu cha Saa: Mariamu Amtembelea ElizabetiGuillaume Vrelant · karibu 1470–1480
Bishara kwa Mariamu (L'annonciation)James Tissot · 1886–1894
Mariamu Amtembelea Elizabeti (La visitation)James Tissot · 1886–1894
Wimbo wa Mariamu (Le magnificat)James Tissot · 1886–1894
Sikukuu nyingine
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki