ULB · Sura 54 / 150
Zaburi 54
1Kwa kiongozi wa muziki; kwenye vyombo vya nyuzi. Maschil ya Daudi; wakati Ziphites alipokuja na kumwambia Sauli, “Hivi Daudi hakujificha pamoja nasi?” Uniokoe, Mungu, kwa jina lako, na kwa nguvu zako unihukumu.
2Usikie maombi yangu, Mungu; uyategee sikio maneno ya mdomo wangu.
3Kwa maana wageni wameinuka dhidi yangu, na watu wasio na huruma wanaitafuta roho yangu; nao hawakumuweka Mungu mbele yao. Selah
4Tazama, Mungu ni msaidizi wangu; Bwana ndiye anisaidiaye.
5Naye atawalipizia uovu maadui zangu; katika uaminifu wako, uwaharibu!
6Nitakutolea dhabihu kwa moyo mkunjufu; nitalishukuru jina lako, Yahwe, kwa maana ni jema.
7Kwa kuwa yeye ameniokoa katika kila shida; macho yangu yamewatazama adui zangu yakiwa na ushindi.
Swahili Unlocked Literal Bible (ULB, 2019) · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 (maandiko bila mabadiliko; bila maelezo ya chini na vichwa) · eBible.org