Bible Explorer

Biblia › Zaburi › 5

ULB · Sura 5 / 150

Zaburi 5

1Kwa kiongozi wa muziki; kwa vyombo vya upepo. Zaburi ya Daudi. Sikiliza nikuitapo, Yahweh; tazama kuugua kwangu.

2Sikiliza sauti yangu nikuitapo, Ee Mfalme wangu na Mungu wangu, kwa kuwa ni kwako Bwana naomba.

3Yahweh; sikia kilio changu asubuhi; na asubuhi nitaleta dua yangu kwako na kungoja kwa matarajio.

4Hakika wewe ni Mungu usiye kubaliana na uovu; watu waovu hawawezi kuwa wageni wako.

5Wenye kiburi hawata simama katika uwepo wako; wewe unawachukia wote wanaofanya maovu.

6Nawe utawaharibu waongo; Yahweh huwadharau vurugu na watu wadanganyifu.

7Lakini kwangu mimi, kwa sababu ya ukuu na uaminifu wa agano lako, nitakuja nyumbani mwako; na kwa heshima nitakuinamia mbele ya hekalu lako takatifu.

8Oh Bwana, uniongoze katika haki yako kwa sababu ya adui zangu; usawazishe njia yako mbele yangu.

9Kwa kuwa midomoni mwao hamna ukweli; utu wao wa ndani ni mwovu; makoo yao ni kaburi lililo wazi; husifu kinafiki kwa ulimi wao.

10Mungu, wafanye kuwa na hatia; mipango yao iwe kuanguka kwao! Kwa ajili ya makosa yao mengi uwatoe nje, kwa kuwa wamekuasi wewe.

11Bali wale wanao kukimbilia wafurahi; uwafanye wapige kelele kwa shangwe siku zote kwa sababu unawapigania; uwafanye wenye furaha ndani yako, wale walipendao jina lako.

12Kwa maana utawabariki wenye haki, Yahweh; utawazunguka kwa neema kama ngao.

Swahili Unlocked Literal Bible (ULB, 2019) · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 (maandiko bila mabadiliko; bila maelezo ya chini na vichwa) · eBible.org