Bible Explorer

Biblia › Zaburi › 82

ULB · Sura 82 / 150

Zaburi 82

1Zaburi ya Asafu. Mungu amesimama katika kusanyiko la mbinguni; katikati ya miungu anahukumu.

2Hata lini mtahukumu bila haki na kuonesha upendeleo kwa waovu? Selah

3Wateteeni maskini na yatima; dumisheni haki kwa aliyetaabishwa na fukara.

4Muokoeni maskini na muhitaji; watoeni mkononi mwa waovu.

5Hawajui wala hawaelewi; hutembea gizani; misingi yote ya nchi imebomoka.

6Mimi nilisema, “Ninyi ni miungu, na ninyi nyote wana wa Mungu aliye Juu.

7Hata hivyo mtakufa kama wanadamu na mtaanguka kama mmoja wa wakuu.”

8Uinuke, Ee Mungu, uihukumu nchi, maana unaurithi katika mataifa yote.

Swahili Unlocked Literal Bible (ULB, 2019) · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 (maandiko bila mabadiliko; bila maelezo ya chini na vichwa) · eBible.org