Bible Explorer

Biblia › Zaburi › 131

ULB · Sura 131 / 150

Zaburi 131

1Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu; wa Daudi. Yahwe, moyo wangu haujivuni wala macho yangu hayana kuburi. Sina matarajio makubwa kwa ajili yangu mwenyewe wala kujihofia kwa mambo ambayo yako juu ya uwezo wangu.

2Hakika nimejituliza na kuinyamazisha nafsi yangu; kama mtoto aliyeachishwa na mama yake, nafsi yangu ndani yangu iko kama mtoto aliye achishwa.

3Israeli, umtumainie Yahwe sasa na hata milele.

Swahili Unlocked Literal Bible (ULB, 2019) · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 (maandiko bila mabadiliko; bila maelezo ya chini na vichwa) · eBible.org