Bible Explorer

Biblia › Zaburi › 134

ULB · Sura 134 / 150

Zaburi 134

1Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu. Njoni, mtukuzeni Yahwe, enyi nyote watumishi wa Yahwe, ninyi mnaotumika hekaluni mwa Yahwe wakati wa usiku.

2Inueni mikono yenu patakatifu pake na mtukuzeni Yahwe.

3Mungu na awabariki toka Sayuni, yeye aliye ziumba mbingu na nchi.

Swahili Unlocked Literal Bible (ULB, 2019) · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 (maandiko bila mabadiliko; bila maelezo ya chini na vichwa) · eBible.org