Bible Explorer

Biblia › Zaburi › 123

ULB · Sura 123 / 150

Zaburi 123

1Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu. Nakuinulia macho yangu, wewe uketiye mbinguni.

2Tazama, kama vile macho ya watumishi watazamapo kwenye mkono wa Bwana wao, na kama macho ya mjakazi yatazamapo mkono wa bibi yake, ndivyo hivyo macho yetu yanamtazama Yahwe mpaka atakapo tuhurumia.

3Ee Yahwe, utuhurumie, kwa maana tunadhalilishwa sana.

4Tumeshibishwa mzaha wa wenye kiburi na dharau ya wenye majivuno.

Swahili Unlocked Literal Bible (ULB, 2019) · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 (maandiko bila mabadiliko; bila maelezo ya chini na vichwa) · eBible.org