Bible Explorer

Biblia › Zaburi › 100

ULB · Sura 100 / 150

Zaburi 100

1Zaburi ya shukrani. Mpigieni Yahwe kelele za furaha, enyi nchi yote.

2Mtumikieni Yahwe kwa furaha; njoni mbele zake mkiimba kwa furaha.

3Mjue kuwa Yahwe ni Mungu; alituumba, na sisi tu wake. Tu watu wake na kondoo wa malisho yake.

4Ingieni malangoni mwake kwa shukrani na nyuani mwake kwa kusifu. Mshukuruni yeye na litukuzeni jina lake.

5Maana Yahwe ni mwema; uaminifu wa agano lake wadumu milele na uaminifu wake vizazi na vizazi vyote.

Swahili Unlocked Literal Bible (ULB, 2019) · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 (maandiko bila mabadiliko; bila maelezo ya chini na vichwa) · eBible.org