Bible Explorer

Biblia › Zaburi › 87

ULB · Sura 87 / 150

Zaburi 87

1Zaburi ya wana wa Kora; wimbo. Mji aliouanzisha umesimama juu ya mlima mtakatifu;

2Yahwe anapenda zaidi malango ya Sayuni kuliko mahema yote ya Yakobo.

3Mambo matukufu yamesemwa kwako, mji wa Mungu. Selah

4Ninataja Rahabu na Babeli kwa wafuasi wangu. Tazama, Filisti, na Tiro, pamoja na Ethiopia nao watasema, 'Huyu alizaliwa humo.'”

5Itasemwa juu ya Sayuni, “Kila mmoja wa hawa alizaliwa katika yeye; na yeye Aliye Juu atamuimarisha.

6Yahwe anaandika katika kitabau cha sensa ya mataifa, “Huyu alizaliwa humo.” Selah

7Hivyo waimbaji na wachezaji kwa pamoja waseme, “chemchem zangu zimo kwako.”

Swahili Unlocked Literal Bible (ULB, 2019) · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 (maandiko bila mabadiliko; bila maelezo ya chini na vichwa) · eBible.org