Bible Explorer

Biblia › Zaburi › 125

ULB · Sura 125 / 150

Zaburi 125

1Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu. Wale wamwaminio Yahwe ni kama mlima Sayuni, hautikisiki, wadumu milele.

2Kama milima inavyo izunguka Yerusalemu, hivyo ndivyo Yahwe anavyo wazunguka watu wake sasa na hata milele.

3Fimbo ya uovu haitatawala katika nchi ya wenye haki. Vinginevyo wenye haki wanaweza kukosea.

4Ee Yahwe, utende wema kwa wale walio wema na wale walio wanyoofu mioyoni mwao.

5Lakini kwa wale wanaogeukia njia zao za upotovu, Yahwe atawaondoa pamoja na watenda maovu. Amani iwe na Israeli.

Swahili Unlocked Literal Bible (ULB, 2019) · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 (maandiko bila mabadiliko; bila maelezo ya chini na vichwa) · eBible.org