ULB · Sura 70 / 150
Zaburi 70
1Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi; kuleta kumbukumbu. Uniokoe, Mungu! Yahwe, njoo haraka na unisaidie mimi.
2Wale wajaribuo kuchukua uhai wangu waaibishwe na kufedheheshwa; warudishwe nyuma na wasiheshimiwe, wale wafurahiao katika maumivu yangu.
3Warudishwe nyuma kwa sababu ya aibu yao, wale wasemao, “Aha, aha.”
4Wale wakutafutao wafurahi na kushangilia katika wewe; wale waupendao wokovu wako siku zote waseme, “Mungu asifiwe.”
5Lakini mimi ni maskini na muhitaji; harakisha kwangu, Mungu; wewe ni msaada wangu nawe huniokoa mimi. Yahwe, usichelewe.
Swahili Unlocked Literal Bible (ULB, 2019) · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 (maandiko bila mabadiliko; bila maelezo ya chini na vichwa) · eBible.org