Mwanzo › Biblia inasema nini › Umoja
Mahusiano
Biblia inasema nini kuhusu Umoja
Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (10), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.
1 Kor 1:10
Sasa nawasihi kaka na dada zangu, kupitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba wote mkubali, na kwamba kusiwe na migawanyiko miongoni mwenu. Nawasihi kwamba muungane pamoja katika nia moja na katika kusudi moja.Zab 133:1
Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu, wa Daudi. Tazama, jinsi ilivyo vema na yakupendeza ndugu waishi pamoja, kwa umoja!Efe 4:3
Fanyeni bidii kuutunza umoja wa Roho katika kifungo cha amani.1 Pet 3:8
Hatimaye, ninyi nyote, muwe na nia moja, wenye huruma, upendo kama ndugu, wanyenyekevu, na wapole.2 Kor 13:11
Hatimaye, ndugu wa kiume na wa kike, furahini! fanyeni kazi kwa ajili ya urejesho, mtiwe moyo, kubalianeni ninyi kwa ninyi, muishi katika amani. Na Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi.Yn 17:23
Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili waweze kukamilishwa katika umoja; ili ulimwengu ujue kuwa hakika wewe ndiye uliyenituma, na kuwapenda, kama vile wewe ulivyonipenda, mimi.1 Kor 12:12
Kwa maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote ni vya mwili ule ule, vivyo hivyo na Kristo.Flp 2:2
Ikamilisheni furaha yangu kwa kunia mamoja mkiwa na upendo mmoja, mkiwa wamoja katika roho, na kuwa na kusudi moja.Rum 12:4–5
Kwa kuwa tuna viungo vingi katika mwili mmoja, lakini si viungo vyote vina kazi moja. Vivyo hivyo, sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo kila mmoja kwa mwenzake.Kol 3:14
Zaidi ya mambo haya yote, muwe na upendo, ambao ndio kigezo cha ukamilifu.Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.
Vyanzo
Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0