Mwanzo › Biblia inasema nini › Uzee
Maisha na kazi
Biblia inasema nini kuhusu Uzee
Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (10), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.
Mit 16:31
Mvi ni taji ya utukufu; hupatikana kwa kuishi katika njia ya haki.Isa 46:4
Hata kwa njie wazee Mimi ndiye, mpaka mmeshapata mvi nitawachukua. Nimewaumba ninyi na nitawabeba ninyi; Nitwachukua nyie na nitawakomboa nyie.Mit 20:29
Utukufu wa watu vijana ni nguvu zao na fahari ya watu wazee ni mvi zao.Law 19:32
Ni lazima usimame mbele za mtu mwenye mvi na uheshimu uwepo wa mzee. Yakupasa umwegope Mungu wako. Mimi ndimi Yahweh.2 Kor 4:16
Hivyo hatukati tamaa. Japokuwa kwa nje tunachakaa, kwa ndani tunafanywa upya siku hadi siku.Ayu 12:12
Kwa wazee mna hekima; katika wingi wa siku mna ufahamu.Zab 71:18
Hakika, hata niwapo mzee na mvi kichwani, Mungu, usiniache mimi, kama ambavyo nimekuwa nikitanga nguvu yako kwa vizazi vijavyo, na uweza wako kwa yeyote ajaye.Zab 71:9
Usinitupe katika siku za miaka ya uzee wangu; usiniache wakati nguvu zangu zitakapoisha.Zab 92:14
Wao huzaa matunda hata uzeeni; hukaa safi na wenye afya,Mit 17:6
Wajukuu ni taji ya wazee na wazazi huleta heshima kwa watoto wao.Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.
Vyanzo
Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0