Bible Explorer

Mwanzo › Biblia inasema nini › Mafanikio

Maisha na kazi

Biblia inasema nini kuhusu Mafanikio

Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (10), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.

Mit 16:3Kabidhi kwa Yehova kazi zako zote na mipango yako itafanikiwa.
Flp 4:13Ninaweza kufanya haya kwa kuwezeshwa na Yeye anitiaye nguvu.
Zab 37:4Kisha ufurahi mwenyewe katika Yahwe, naye atakupa matamanio ya moyo wako.
Yer 29:11Kwa maana mimi mwenyewe naijua mipangao niliyonayo kwa ajili yenu—hili ni tangazo la Yahwe—mipango kwa ajili ya amani na siyo kwa ajili ya mabaya, ili kuwapa ninyi tumaini na siku zenu za mwisho.
Kum 8:18Lakini mtamkumbuka akilini Yahwe Mungu wenu, kwa kuwa ni yeye awapae ninyi nguvu ya kupata utajiri, ili kwamba aweze kuanzisha agano lake aliloapa kwa baba zenu, kama ilivyo leo.
Yak 4:10Jinyenyekezeni wenyewe mbele za Bwana, na atawainua juu.
Yos 1:8Siku zote uuongee juu ya kitabu hiki cha sheria. Utakitafakari mchana na usiku ili kwamba uweze kutii yote yaliyoandikwa humo. Kisha utastawi na kufanikiwa.
Mit 3:5Mtegemee Yehova kwa moyo wako wote na wala usitegemee ufahamu wako mwenyewe,
1 Fal 2:3maamuzi yake, na maagizo ya maagano yake, uwe mwamngalifu kufanya yale yaliyoandikwa katika sheria za Musa, ili ufanikiwe katika yote utakayoyafanya, popote kule utakakokuwa,
Mt 16:26Je! Ni faida gani atakayopata mtu akipata dunia yote lakini akapoteza maisha yake? Je! Ni kitu gani atakachotoa mtu katika kubadilishana na maisha yake?

Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.

Vyanzo

Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0